< Baebrania 11 >
1 Nambeambe imani yabile nga hakika yabile nayo mundu muda atarajia kilebe pulani kwa ujasiri. Ni hakika ya kilebe chabile bado bonekaniya.
Sasa imani ni hakika aliyo nayo mtu wakati atarajiapo kitu fulani kwa ujasiri. Ni hakika ya kitu ambacho bado hakijaonekana.
2 Kwa mana yee apindo bitu batithibitika kwa imani yabe.
Kwa sababu hii mababu zetu walithibitika kwa imani yao.
3 Kwa imani twatifahamu kwamba ulimwengu waumbilwe kwa amri ya Nnongo, ili kwamba chelo chatibonekaniya chatitengenezwa kwaa bonekana ni ilebe ambayo yabile yatibonekana. (aiōn )
Kwa imani tunafahamu kwamba ulimwengu uliumbwa kwa amri ya Mungu, ili kwamba kile kinachoonekana hakikutengenezwa kutokana na vitu ambavyo vilikuwa vinaonekana. (aiōn )
4 Ibile kwa mana ya imani kuwa Habili atikumtolea Nnongo sadaka ya kufaa kuliko kagapanga Kaini. Yaibile ni kwa mana yee atikusifiwa kuba mwene haki. Nnongo atikumsifu kwa mana ya zawadi yailetike. Kwa mana yoo, Habili bado abaya, ingawa atiwaa.
Ilikuwa kwa sababu ya imani kwamba Habili alimtolea Mungu sadaka ya kufaa kuliko alivyofanya Kaini. Ilikuwa ni kwa sababu hii kwamba alisifiwa kuwa mwenye haki. Mungu alimsifu kwa sababu ya zawadi alizoleta. Kwa sababu hiyo, Habili bado ananena, ingawa amekufa.
5 Yaibile kwa imani kuba Enoko apotwilwe nnani na abonike kwaa kiwo.”Abonekine kwaa, kwa mana Nnongo atikuntola” kwa mana yabayilwe nnani yake kuba atikumpendeza Nnongo kabla ya kuntola kunani.
Ilikuwa kwa imani kwamba Enoko alichukuliwa juu na hakuona mauti. “Hakuonekana, kwa sababu Mungu alimchukua” kwa vile ilinenwa juu yake kuwa alimpendeza Mungu kabla ya kuchukuliwa juu.
6 Ntopo imani yatiwezekana kwaa kumpendeza Nnongo, kwa mana ywaisa kwa Nnongo lazima aaminiye kuba Nnongo abile nkoti ni huapatia zawadi balo bankengamite.
Pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu, kwa kuwa ajaye kwa Mungu lazima aamini kwamba Mungu anaishi na kwamba huwapatia zawadi wale wamtafutao.
7 Yabile kwa imani kuba Nuhu, abile akanyilwe ni Nnongo husiana na makowe ambago yaibile kwaa yatibonekine kwa heshima ya Nnongo kachuchengya safina kwaajili ya kulopwa familia yake. Kwa kupanga yee, atikuihukumu dunia ni kuba mrithi ba haki yaisa petya imani.
Ilikuwa ni kwa imani kwamba Nuhu, akiwa ameonywa na Mungu kuhusiana na mambo ambayo hayakuwa yameonekana, kwa heshima ya ki Mungu alitengeneza safina kwa ajili ya kuiokoa familia yake. Kwa kufanya hivi, aliuhukumu ulimwengu na akawa mrithi wa haki ambayo huja kupitia imani.
8 Yaibile ni kwa imani kuwa Ibrahimu, paakemilwe alowa kueshimu no yendya pandu paapalikwa pokya kati urithi. Ayei bila yowa pandu gani pabile atiyenda.
Ilikuwa ni kwa imani kwamba Ibrahimu, alipoitwa alitii na kwenda mahali ambapo alipaswa kupokea kama urithi. Alitoka bila kujua mahali gani alikuwa anakwenda.
9 Yabile ni kwa imani yabile yatiitama mu'nnema ya ahadi kati mgeni. Atitama mu'lihema pamope ni Isaka ni Yakobo, barithi babenge ni ahadi yeyelo.
Ilikuwa ni kwa imani kwamba aliishi katika nchi ya ahadi kama mgeni. Aliishi katika mahema pamoja na Isaka na Yakobo, warithi wenzake wa ahadi ile ile.
10 Ayee nga sababu atitarajia kuupata mji ambao ywaubuni na kuuchenga alowa pangilwa Nnongo.
Hii ni kwa sababu alitarajia kuupata mji ambao mwenye kuubuni na mjenzi wake angelikuwa ni Mungu.
11 Yabile ni kwa imani panga Ibrahimu, na Sara mwene, wapokii ngupu ya tunga ndumbo ingawa babile apindo muno, kwa mana wamweni Nnongo kuwa mwaminifu, ywabile atiwaahidia mwana nnalome.
Ilikuwa ni kwa imani kwamba Ibrahimu, na Sara mwenyewe, walipokea nguvu ya kutunga mimba ingawa walikuwa wazee sana, kwa kuwa walimuona Mungu kuwa mwaminifu, ambaye aliwaahidia mtoto wa kiume.
12 Kwa eyo kae boka kwa mundu yolo yumo ywaabile atikaribia kiwo batibelekwa bana babalangika kwaa. Babile banyansima kati itobdo za kumaunde kati mbeyu ya mchanga katika fukwe ga bahari.
Kwa hiyo pia kutoka kwa mtu huyu mmoja ambaye alikuwa amekaribia kufa wakazaliwa watoto wasiohesabika. Walikuwa wengi kama nyota za angani na wengi kama mbegu za mchanga katika ufukwe wa bahari.
13 Aba bote bawile katika imani bila pokya ahadi, ila, babile baibweni ni kuikaribisha kwa kutalu, batibaya panga babile ageni na apitaji nnani ya nnema,
Hawa wote walikufa katika imani pasipo kupokea ahadi. Isipokuwa, wakiwa wameziona na kuzikaribisha kwa mbali, walikiri kwamba walikuwa wageni na wapitaji juu ya nchi.
14 Kwa balo balongela makowe kati aga babekite bayana kuwa waipala nchi yabe bene.
Kwa wale wasemao mambo kama haya wanaweka bayana kuwa wanatafuta nchi yao wenyewe.
15 Kwa kweli, kati babile bakiiwaza nchi ambayo babokite, babile na nafasi ya kerebuka.
Kwa kweli, kama wangekuwa wakiifikiria nchi ambayo kwayo walitoka, wangelikuwa na nafasi ya kurejea.
16 Lakini kati ya ibile, batamaniya nnema waubile bora, ambayo, ni ya kumaunde. Kwa eyo Nnongo abweni kwaa kiya kemelwa Nnongo wabe, kwa mana atiutayarisha nnema kwaajili yabe.
Lakini kama ilivyo, wanatamani nchi iliyo bora, ambayo, ni ya kimbingu. Kwa hiyo Mungu haoni aibu kuitwa Mungu wao, kwa kuwa ametayarisha mji kwa ajili yao.
17 Yabile ni kwa imani panga Ibrahimu baada ya jaribiwa, atimtoa Isaka. Nga nyoo, ywatipokya kwa puraha ahadi, alimtoa mwana wake mwene,
Ilikuwa ni kwa imani kwamba Ibrahimu baada ya kujaribiwa, alimtoa Isaka. Ndiyo, yeye ambaye alipokea kwa furaha ahadi, alimtoa mwanawe wa pekee,
18 ambaye nnani yake atilongelwa, “Boka kwa Isaka ubeleki wako walowa kemelwa.”
ambaye juu yake ilinenwa, “Kutoka kwa Isaka uzao wako utaitwa.”
19 Ibrahimu atangite panga Nnongo abile na uwezo wa kumfufua Isaka boka mu. kiwo, na kwa longela kwa lugha ya maumbo, atimpokya.
IbrahImU alijua kwamba Mungu alikuwa na uwezo wa kumfufua Isaka kutoka katika wafu, na kwa kuzungumza kwa lugha ya maumbo, alimpokea.
20 Yabile ni katika imani panga Isaka atimbariki Yakobo na Esau kuhusu makowe gaisa.
Ilikuwa ni kwa imani kwamba Isaka alimbariki Yakobo na Esau kuhusu mambo yajayo.
21 Ibile ni kwa imani panga Yakobo abile katika hali ya waa, atekumbarikiya kila yumo wa bana ba Yusufu. Yakobo aabudiya, kaegemeya nnani ya fimbo yake.
Ilikuwa ni kwa imani kwamba Yakobo alipokuwa katika hali ya kufa, alimbariki kila mmoja wa watoto wa Yusufu. Yakobo akaabudu, akiegemea juu ya fimbo yake.
22 Yabile ni kwa imani panga Yusufu muda wake wa mwisho ubile papipi, alongela nnani ya boka kwa bana ba Israel Misri na kabaagiza tola pamope nabo mifupa gake.
Ilikuwa ni kwa imani kwamba Yusufu wakati wake wa mwisho ulipokaribia, alinena juu ya kutoka kwa wana wa Israel Misri na akawaagiza kuchukua pamoja nao mifupa yake.
23 Ibile ni kwa imani panga Musa, paabelekilwe, atibikana kwaa muda wa miyei itatu na azazi bake kwa sababu bamweni kuwa ni mwana nchunu ywabile mzuri, na bayogopa kwaa amri ya mpwalume.
Ilikuwa ni kwa imani kwamba Musa, alipozaliwa, alifichwa kwa miezi mitatu na wazazi wake kwa sababu walimuona kuwa ni mtoto mchanga aliyekuwa mzuri, na hawakutishwa na amri ya mfalme.
24 Ibile ni kwa imani panga Musa paabile mundu mpindo, akani kukemwa mwana wa nwawa wa Farao.
Ilikuwa ni kwa imani kwamba Musa, alipokuwa mtu mzima, alikataa kuitwa mtoto wa binti Farao.
25 Badala yake, achawa shiriki mateso pamope ni bandu ba Nnongo badala ya puraika ni anasa za sambi kwa muda nchunu.
Badala yake, alichagua kushiriki mateso pamoja na watu wa Mungu badala ya kufurahia anasa za dhambi kwa kitambo.
26 Awazile kiya ya kunkengama Kristo kuwa ni utajiri nkolo kuliko hazina za Misri kwa mana atumbwi minyo katika zawadi muda wake woisa.
Alifikiri aibu ya kumfuata Kristo kuwa ni utajiri mkuu kuliko hazina za Misri kwa kuwa alikaza macho yake katika zawadi ya wakati wake ujao.
27 Ibile ni kwa imani panga Musa aboka Misri. Ahofia kwaa hasira ya mpwalume, kwa mana atipumilia kwa lolekeya kwa ywabonekana kwaa.
Ilikuwa ni kwa imani kwamba Musa alitoka Misri. Hakuhofia hasira ya Mfalme, kwa kuwa alivumilia kwa kutazama kwa asiyeonekana.
28 Ibile ni kwa imani panga aikamwi Pasaka na kunyunyiza mwai, ili panga mharibu wa mbeleki wa kwanza aweze kwaa kubakamwa wabeleki wa kwanza analome wa baisraeli.
Ilikuwa ni kwa imani kwamba aliishika pasaka na kunyunyiza damu, ili kwamba mharibu wa mzaliwa wa kwanza asiweze kuwagusa wazaliwa wa kwanza wa kiume wa waisrael.
29 Ibile ni kwa imani panga bapeta katika bahari ya shamu kati pannema nkavu. Muda bamisri batijaribu peta, balimezwa.
Ilikuwa ni kwa imani kwamba walipita katika bahari ya shamu kama katika nchi kavu. Wakati wamisri walipojaribu kupita, walimezwa.
30 Ibile ni kwa imani panga ukuta ba Yeriko utombwike pae, baada ya kuuzunguka kwa masoba saba,
Ilikuwa ni kwa imani kwamba ukuta wa Yeriko ulianguka chini, baada ya kuuzunguka kwa siku saba.
31 Ibile ni kwa imani panga Rahabu yolo kahaba aangamiya kwaa pamope ni balo babile kwaa atiifu, kwa sababu abile abapokii bapelelezi na kubahifadhi salama.
Ilikuwa ni kwa imani kwamba Rahabu yule kahaba hakuangamia pamoja na wale ambao hawakuwa watiifu, kwa sababu alikuwa amewapokea wapelelezi na kuwahifadhi salama.
32 Nibaye namani zaidi? Mana muda utosha kwaa longela ga Gideoni, Barak, Samsoni, Yeftha, Daudi, Samweli na manabii,
Na niseme nini zaidi? Maana muda hautoshi kusimulia ya Gideoni, Barak, Samsoni, Yeftha, Daudi, Samwel na za manabii,
33 ambao pitya imani batizishinda falme, bapangite haki, bapokya ahadi.
ambao kupitia imani walizishinda falme, walitenda haki, na wakapokea ahadi. Walizuia vinywa vya simba,
34 Baikanikya mikanwa ya imba, batizima ngupu ya mwoto, bakwepite ncha ya upanga, baponywa boka mu matamwe, babile mashujaa vitani, na catisababisha majeshi ga ageni kupiya.
walizima nguvu za moto, walikwepa ncha ya upanga, waliponywa kutoka katika magonjwa, walikuwa mashujaa vitani, na walisababisha majeshi wageni kukimbia.
35 Alwawa bapokii bandu ba kiwo babe kwa ndela ya ufufuo. Benge bateswile, bila yeketya kulekwa huru ili panga baweze pata uzoefu wa ufufuo ubile bora muno.
Wanawake walipokea wafu wao kwa njia ya ufufuo. Wengine waliteswa, bila kukubali kuachwa huru ili kwamba waweze kupata uzoefu wa ufufuo ulio bora zaidi.
36 Benge batiteswa kwa dhihaka na kwa kombwa, eloo, hata kwa tabilwa na kwa bekwa muligereza.
Wengine waliteswa kwa dhihaka na kwa vichapo, naam, hata kwa vifungo na kwa kutiwa gerezani.
37 Bapondwile maliwe. Batitekwanikwa ipande kwa misumeno. Batibulagwa kwa upanga. Batiyenda kwa ngozi ya ngondolo na ngozi ya mbuzi babile babapala, batiyendelya katika maumivu na mapangilwe yanoite kwaa.
Walipondwa mawe. Walikatwa vipande kwa misumeno. Waliuawa kwa upanga. Walikwenda kwa ngozi za kondoo na ngozi za mbuzi walikuwa wahitaji, wakiendelea katika maumivu na wakitendewa mabaya
38 (Ambayo ulimwengu wastahili kwaa kuwa nabo) batitanga tanga mmwitu, mukitombe, katika mapango na katika mashimo ga nnema.
(ambayo ulimwengu haukustahili kuwa nao), wakitangatanga nyikani, milimani, katika mapango na katika mashimo ya ardhini.
39 Ingawa bandu bote aba batiyeketiwa na Nnongo kwa sababu ya imani yabe, bapokya kwaa chaatiahidia.
Ingawa watu wote hawa walikubaliwa na Mungu kwa sababu ya imani yao, hawakupokea alichoahidi.
40 Nnongo atiyongolya kutupatia kilebe kibile bora. ili panga bila twenga baweza kwaa kamilishwa.
Mungu alitangulia kutupatia kitu kilichobora, ili kwamba bila sisi wasingeweza kukamilishwa.