< Matendo ga Mitume 8 >

1 Sauli abile mu'makubaliano ya kiwo chake, lisoba lee nga atumbwile kuwatesa kinyume cha likanisa lyalibile Yerusalemu; na baaminio bote batawanyika katika majigambo ga Yudea na Samaria, ila mitume.
Sauli alikuwa kwenye makubaliano ya kifo chake. siku hiyo ndipo alipoanza kuwatesa kinyume cha kanisa lililokuwa Yerusalemu; na waaminio wote waliotawanyika katika majimbo ya Yudea na Samaria, isipokuwa mitume.
2 Bandu bacha'Nnongo balimsika Stephano na kupanga maombolezo makolo nnani yake.
Watu wachamungu walimzika Stefano na kufanya maombolezo makubwa juu yake.
3 Lakini Sauli atilidhuru muno likanisa. Ayenda mu'nyumba kwa nyumba na kubaburuza panja anwawa na analome, na kuwabeka muligereza.
Lakini Sauli alilidhuru sana kanisa. Alikwenda nyumba kwa nyumba na kuwaburuza nje wanawake na waume, na kuwatupia gerezani.
4 Baaminio ambao babile batitawanyika bado balihubili neno.
waaminio ambao walikuwa wametawanyika bado walilihubiri neno.
5 Filipo atiuluka katika mji wa Samaria na kuntangaza Kristo kolyo.
Filipo akashuka katika mji wa Samaria na akamtangaza Kristo huko.
6 Baada ya bandu kugayowa na kubona ishara azipangite Filipo; babekite umakini nnani yake chalo chaakibaya.
Baada ya makutano kusikia na kuona ishara alizofanya Filipo; wakaweka umakini juu ya kile alichosema.
7 Boka po bandu banyansima bayowine, nchela achafu bakibatoka bandu huku wakilela kwa lilobe likolo, na benge batipooza na iwete baponile.
Kutoka hapo watu wengi waliosikia, pepo wachafu waliwatoka watu huku wakilia kwa sauti kubwa, na wengi waliopooza na viwete waliponywa.
8 Na pabile na puraha ngolo katika mji.
Na kulikuwa na furaha kubwa katika mji.
9 Lakini pabile na mundu yumo katika mji wolo lina lyake Simon, ambaye akipanga bwabe, ambao atiutumya kubashangaza bandu ba litaifa lya Samaria, muda abaya kuwa ywembe ni mundu wa muhimu.
Lakini palikuwa na mtu mmoja katika mji ule jina lake Simon, ambaye alikuwa akifanya uchawi; ambao aliutumia kuwashangaza watu wa taifa la Samaria, wakati akisema kuwa yeye ni mtu wa muhimu.
10 Basamalia bote tangu nchunu hata mkolo kamsikiliza; babaya;”mundu yolo ni yelo ngupu ya Nnongo ambaye ni kolo.”
Wasamaria wote tangu mdogo hata mkubwa, wakamsikiliza; wakasema;”mtu huyu ni ile nguvu ya Mungu ambayo ni kuu.”
11 Bamsikiliza, kwa maana atibashangaza muda mrefu kwa bwabe wake.
Wakamsikiliza, kwa maana amewashangaza muda mrefu kwa uchawi wake.
12 Lakini muda pabaaminiya kuwa Filipo ahubiri nnani ya ufalme wa Nnongo na nnani ya lina lya Yesu Kristo, batiabatiza, analome kwa alwawa.
Lakini wakati walipoamini kuwa Filipo alihubiri juu ya ufalme wa Mungu na juu ya jina la Yesu Kristo, walibatizwa, wanaume kwa wanawake.
13 Na Simoni mwene aaminiya, baada ya kubatizwa, aliendelea kuwa na Filipo; abweni ishara na miujiza yaibile ikipangika, atishangala.
Na Simoni mwenyewe aliamini: baada ya kubatizwa, aliendelea kuwa na Filipo; alipoona ishara na miujiza iliyokuwa ikitendeka, alishangaa.
14 Mundu mitume ba Yerusalemu bayowine kuwa Samaria yapokya neno lya Nnongo, baatuma Petro na Yohana.
Wakati mitume wa Yerusalemu waliposikia kuwa Samaria imepokea neno la Mungu, wakawatuma Petro na Yohana.
15 Muda babile bauluka kabalobya; panga wamokee Roho Mtakatifu.
Wakati walipokuwa wakishuka wakawaombea; kwamba wampokee Roho Mtakatifu.
16 Mpaka muda woo, Roho Mtakatifu abile amshukia kwaa hata yumo wabe; babile batibatizwa kwa lina lya Ngwana Yesu.
Mpaka muda huo, Roho Mtakatifu alikuwa hajawashukia hata mmoja wao; walikuwa tu wamebatizwa kwa jina la Bwana Yesu.
17 Petro na Yohana baabekeya maboko, na bembe bampokya Roho Mtakatifu
Ndipo Petro na Yohana wakawawekea mikono, nao wakampokea Roho Mtakatifu.
18 Muda Simoni abweni Roho Mtakatifu atitolewa pitya kuwekewa maboko na mitume; apala kuwapeya mbanje,
Wakati Simoni alipoona kwamba Roho Mtakatifu ametolewa kupitia kuwekewa mikono na mitume; akataka kuwapa pesa,
19 Kabaya, “Munipei ayee ngupu, ili kila ywanimbekya maboko apokee Roho Mtakatifu.”
Akasema, “Nipeni hii nguvu, ili kila nitakayemwekea mikono apokee Roho Mtakatifu.”
20 Lakini Petro ammakiye; mbanje yako pamope na wenga ipotee kutalu, kwa sababu utangite kuwa karama ya Nnongo yapatikana kwa mbanje.
Lakini Petro akamwambia; pesa yako pamoja na wewe ipotelee mbali, kwa sababu umedhani kuwa karama ya Mungu inapatikana kwa pesa.
21 Ubile kwaa na sehemu katika likowe lee, kwa sababu mwoyo wako ni mnyoofu kwaa nnongi ya Nnongo.
Hauna sehemu katika jambo hili, kwa sababu moyo wako si mnyoofu mbele za Mungu.
22 Nga nyo bai tubu maovu yako na kunloba Nnongo labda walowa samehewa fikra ya mwoyo wako.
Hivyo basi tubu maovu yako na kumwomba Mungu labda utasamehewe fikra za moyo wako.
23 Kwa maana nibona ubile katika sumu ya uchungu na kifungo cha sambi.”
Kwa maana naona uko katika sumu ya uchungu na kifungo cha dhambi.”
24 Simoni kanyangwa na kubaya, Munlobe Ngwana kwa ajili yango, kwa mana makowe gote yamuyabaya yaweza pangika kwango.
Simoni akajibu na kusema, “Mwombeni Bwana kwa ajili yangu, kwa kuwa mambo yote mliyozungumza yaweza kunitokea.
25 Muda Petro na Yohana babile batishuhudia na kuhubiri neno lya Ngwana, batikerebuka Yerusalemu kwa ndela yoo; batihubiri injili katika vijiji vyanyansima vya Basamaria.
Wakati Petro na Yohana walipokuwa wameshuhudia na kuhubiri neno la Bwana, walirudi Yerusalemu kwa njia hiyo; walihubiri injili katika vijiji vingi vya Wasamaria.
26 Bai malaika ba Ngwana kalongela na Filipo no baya, “Angza na uyende kusini katika ndela ya'iyenda pae ya Yerusalemu kuelekea Gaza.” (Ndela yee ibile katika lijangwa).
Basi malaika wa Bwana akanena na Filipo na kusema, “Angaza na uende kusini katika njia iendayo chini ya Yerusalemu kuelekea Gaza.” ( Njia hii iko katika jangwa).
27 Kaangaza na yenda. Linga, pabile na mundu wa Ethiopia, towashi abile na mamlaka kolo pae ya kandase; malkia ba Ethiopia. Ywatibekwa nnani ya hazina yake yote, ni ywembe abile ayenda Yerusalemu kuabudu.
Akaangaza na kwenda. Tazama, kulikuwa na mtu wa Ethiopia, towashi mwenye mamlaka kuu chini ya kandase; malkia wa Ethiopia. Aliyewekwa juu ya hazina yake yote; naye alikuwa amekwenda Yerusalemu kuabudu.
28 Abile akerebuka atami mu'gari yake kasoma chuo cha nabii Isaya.
Alikuwa akirejea ameketi garini mwake akisoma chuo cha nabii Isaya.
29 Roho kalongela na Filipo, “Sogea papipi na gari lee ukengamane nalo.
Roho akasema na Filipo, “Sogea karibu na gari hili ukashikamane nalo.
30 “Nga nyo Filipo kayenda mbio, atimsika kasoma katika chuo cha nabii Isaya, kabaya, Je utangite cha ukisomile?”
“Hivyo Filipo akaenda mbio, akamsikia akisoma katika chuo cha nabii Isaya; akasema, Je unafahamu unachosoma?”
31 Muethiopia kabaya, “Naweza kinamani bila ongozwa na mundu?” Kamsihi Filipo apande garini na atami pamope ni ywembe.
Muethiopia akasema, “nitawezaje mtu asiponiongoza?” Akamsihi Filipo apande garini na kuketi pamoja naye.
32 Nambeambe lifungu lya maandiko lyalibile atilisoma Muethiopia ni lee; Ationgozwa kati ngondolo kuyenda machinjioni chinjwa; na mana ngondolo atinyamaza kimya, afungua kwaa nkano wake:
Sasa fungu la maandiko alilokuwa akisoma Muethiopia ni hili; Aliongozwa kama kondoo kwenda machinjioni kuchinjwa; na kama kondoo alinyamaza kimya, hakufungua kinywa chake:
33 Kwa huzunikiya kwake hukumu yake itiondolewa: Nyai ywaeleza kizazi chake? maisha yake yationdolewa katika nchi.”
Kwa kuhuzunishwa kwake hukumu yake iliondolewa: Nani ataeleza kizazi chake? maisha yake yameondolewa katika nchi.”
34 Ayoo towashi kannaluya Filipo, no baya, “Nakuloba, ni nabii yupi ambaye ilongelwa habari yake, ni kuhusu ywembe, au za mundu ywenge”?
Hivyo towashi akamwuliza Filipo, na kusema, “nakuomba, ni nabii yupi ambaye anaongelewa habari zake, ni kuhusu yeye, au za mtu mwingine”?
35 Filipo atumbwi kulongela, atumbwile kwa liandiko lee la Isaya kumhubiria habari ya Yesu.
Filipo alianza kuongea, alianza kwa andiko hili la Isaya kumhubiria habari za Yesu.
36 Babile mundela, baika pabile na mase,'towashi kabaya, “Linga, pabile na mase pano namani chakengama nibatizwe kwaa?”
Wakiwa njiani, wakafika penye maji,' towashi akasema, “Tazama, pana maji hapa nini kinazuia nisibatizwe?,
37 maneno aga, “Nga nyo Muethopia kanyangwa “naaminiya panga Yesu Kristo ni Mwana wa Nnongo,” gabile kwaa mu'maandiko ga kale) nga Muethiopia kaamuru gari lisimame.
maneno haya, “Hivyo Muethiopia akajibu “naamini kwamba Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu,” hayamo kwenyemaandiko ya kale). Ndipo Muethiopia akaamuru gari lisimame.
38 Batiyenda nkati ya maji, pamope Filipo na towashi, Filipo kambatiza.
Walikwenda ndani ya maji, pamoja Filipo na towashi, Filipo akambatiza.
39 Muda babokite mu'mase, Roho wa Ngwana yatimpeleka Filipo kutalu; towashi amweni kwaa, kayenda mu'ndela yake kashangilia.
Wakati walipotoka kwenye maji, Roho wa Bwana ikampeleka Filipo mbali; towashi hakumwona, akaenda njia yake akishangilia.
40 Lakini Filipo katokea Azoto. Apeta katika nkoa wolo kuhubiri injili katika miji yote mpaka paaikite Kaisaria.
Lakini Philipo akatokea Azoto. Alipita katika mkoa ule na kuhubiri injili katika miji yote mpaka alipofika Kaisaria.

< Matendo ga Mitume 8 >