< Matendo ga Mitume 27 >
1 Paiamuliwe panga tupalikwa tunasafiri kwa mase kuyenda Italia, watimkabidhi Paulo na afungwa benge kwa afisa yumo wa jeshi lya Kiroma ywakemelwa Julio, wa Kikosi cha Agustani.
2 Tukapanda meli boka Adrmitamu, ambayo ibile itisafiri kandokando ya pwani ya Asia. Nga nyo tujingii mubahari. Aristaka boka Thesalonike ya Makedonia kayenda pamope natwee.
3 Lisoba lya nyaibele tuikite katika mji wa Sidoni, ambapo Julio atimpangia kwa ukarimu na atibaruhusu kuyenda kwa rafiki zake kupokya ukarimu wabe.
4 Boka po twayenda mu'bahari tukasafiri kuzunguka kisiwa cha Kipto ambacho kibile kimeukinga mbepo, kwa mana mbepo ubile ukitukabili.
5 Baada ya kuwa tumesafiri katika mase yabile papipi na Kilikia na Pamfilia, twaisa Mira, mji wa Lisia.
6 Palo yolo afisa wa jeshi lya Kiroma, akaikuta meli boka Alexandria ambayo ibile itisafiri kuelekea Italia. Akatupandisha ndani yake.
7 Baada ya kusafiri mbolembole kwa masoba ganyansima na hatimaye tuikite kwa taabu karibu na Kinidas, mbepo waruhusu kwaa kae kuelekea ndela yoo, nga nyoo tukasafiri kandokando ya kivuli cha Krete tukiukenga mbepo, mkabala na Salmone.
8 Twatisafiri kandokando ya pwani kwa ugumu, mpaka tuikite mahali pakemelwa Fari Haveni ambayo ibile papipi na mji wa Lasi.
9 Tutweti muda mwingi muno, na muda wa mfungo wa Ayahudi ubile umepita pia, nambeambe ibile ni hatari kuyendelea kusafiri. Nga nyo Paulo atitukanikiya,
10 no baya, “Alalome nibweni safari ambayo twapala kuitola ywalowa kuwa na madhara na hasara yanyansima, ni kwamizigo kichake kwaa na meli, lakini pia maisha yitu.”
11 Lakini afisa yumo wa jeshi la Kiroma atimpekaniya muno ngwana wake na mmiliki wa meli, kuliko makowe ambayo galongelwa na Paulo.
12 Kwa sababu bandari ibile kwaa sehemu rahisi tama kipindi sa mbepo, mabaharia banyansima batisauri tusafiri boka palo, ili kwa namna yoyote tukiweza kuika mji wa Foinike, tutame palo kipindi sa mbepo, Foinike ni bandari kolyo Krete, na itilinga kaskazini na kusini mashariki.
13 Mbepo ya kusini pautumbwile kuvuma mbolembole, mabaharia bapatike chelo ambacho babile bakihitaji. Bating'oa nanga na kusafiri kandokando ya Krete papipi na pwani.
14 Lakini baada ya muda mwipi mbepo nkali, waukemelwa wa kaskazini mashariki, utumbwile kutukombwa boka ng'ambo ya kisiwa.
15 Muda meli yatilemewa na kushindwa kuikabili mbepo, twatikubaliana na hali yee, tukasafiri nao.
16 Tukabutuka pitya wolo upande ubile utiukenga mbepo wa kisiwa kikemelwa Kauda; na kwa taabu muno twatifanikiwa kuuokoa mtumbwi.
17 Baada ya kuwa tumeivuta, balitumia kamba kuifunga meli. Batiyogopa panga tungeweza kuyenda katika eneo lya mchanga wanyansima wa Syiti, nga nyo batiulua nanga na batiendeshwa kandokando.
18 Tukombwile kwa nguvu muno na dhoruba, nga nyo lisoba lyanyaibele mabaharia batumbwile kutupa miziogo boka mu'meli.
19 Lisoba lya tatu, mabaharia batumbwile kuyatoa mase kwa maboko gabe bene.
20 Muda ambao liumu na ndondwa yatuangazia kwaa masoba ganyansima, bado dhoruba ngolo itukombwile, na matumaini panga twalowa lopolelwa yatiboka.
21 Baada ya kuwa batiyenda muda mrefu bila chakulya, nga Paulo ayemi katikati ya mabaharia kabaya, “Alalome, mpalikwa kunipekaniya, na kana tuiboite nanga boka Krete, ili kupata madhara aga na hasara.
22 Nambeambe naafariji panga mube na mwoyo, kwa sababu pabile kwaa na upotevu wa maisha kati yinu, ila hasara ya meli.
23 Kwa mana kilo chakipitike malaika wa Nnongo, ambaye yolo Nnongo nenga ni wake, na ambaye namwabudia kae-malaika bake ayemi pembeni yango
24 no baya, “Kana uyogope Paulo. Lazima uyemi nnongi ya Kaisari, linga, Nnongo katika wema wake akupeile aba bote ambao wasafiri pamope nawenga.
25 Nga nyo, alalome, mujipe mwoyo, kwa sababu namwaminiya Nnongo, panga ipalika kati yaanibakiye.
26 Lakini lazima tuumie kwa kukombwa katika baadhi ya visiwa.”
27 Pauikite kilo ya komi na ncheche, patubile tukiyendeshwa kolyo na kolyo mu'bahari ya Adratik, kati kilo ya manane nyoo, mabaharia batifikiri panga batikaribia nchi kavu.
28 Balitumia milio kupima kina cha mase na kupata mita thelathini na sita, baada ya muda mwipi bapema bapatike mita ishirini na saba.
29 Batiyogopa kwanza twaweza kugonga miamba, nha nyo bakaulua nanga ncheche boka katika sehemu ya kuwekea nanga no kuloba panga bwamba uise mapema.
30 Balo mabaharia batiipala namna ya kuitelekeza yelo meli na balizishusha majini boti njunu na kulopwa maisha, na bapangite kuwa wanatupa nanga boka sehemu ya nnongi ya boti.
31 Lakini Paulo kambakiya yolo askari wa jeshi la Kiroma na balo askari, “Muweza kwaa kuilopwa ila aba bandu babakia mu'meli.”
32 Boka po balo askari bakatike kamba na yelo boti ilekitwe itolwe na mase.
33 Muda mwanga wa bwamba paubile utijitokeza, Paulo atibasihi bote angalau balyee kisunu. Kabaya, “Ayee nga lisoba lya komi na ncheche mwalenda bila kulyaa, mwalyaa kwaa kilebe.
34 Nga nyo nawasihi mtole chakulya kisunu, kwa sababu yee ni kwaajili ya tama kwinu; na ntopo hata nywili yimo ya ntwe winu yalowa potea.
35 Paayomwile baya nyoo, atitola mkate na kumshukuru Nnongo nnongi ya minyo ga kila mundu. Boka po kaetekwana mkate no tumbwa lyaa.
36 Boka po bote batiwa mwoyo na bembe batola chakulya.
37 Tubile bandu 276 nkati ya meli.
38 Paayomwile lyaa pakayukwita, baipangite meli nyepesi kwa kutupa ngano nkati ya mase.
39 Paibile mutwekati, paibweni kwaa nchi kavu, lakini babweni sehemu ya nchi kavu yaijingya mumase yaibile na mchanga wanyansima. batilongela kati baweza kuiendesha meli kuelekea palo.
40 Nga nyoo batizilegeza nanga bazilekite mumase. Katika muda wowolo batizilegeza kamba za tanga na kuiinua sehemu ya nnongi kuelekea katika mbepo, nga nyo batielekea katika iyo sehemu yabile na mchanga wanyansima.
41 Lakini baisile mahali ambapo mikondo ibele ya mase itikwembana, na meli ikaelekya mchangani. Na yelo sehemu ya nnongi ikakwama palo na iweza kwaa boka, lakini sehemu ya mbele uya meli itumbwile kutekwanika kwa sababu ya ukale wa mawimbi.
42 Mpango wa balo askari ubile ni kuwabulaga wafungwa, ili panga ntopo ywaweza ogelea na kutoroka.
43 Lakini yolo askari wa jeshi la Kiroma apala kumwokoa Paulo, nga nyo akausimamisha mpango wabe; na akaamuru balo ambao baweza kuogelea baruke boka melini kwanza bayende nchi kavu.
44 Boka po alalome benge balowa kunkengama, benge nnani ya ipande ya mbao na benge nnani ya ilebe yenge boka mu'meli. Kwa ndela yee ipangike panga bote twalowa ika salama nchi kavu.