< Matendo ga Mitume 22 >

1 “Alongo na tate bango, muupekanie utetezi wango wanalowa kuupanga kwinu nambea, mbe.”
“Ndugu na baba zangu, sikilizeni utetezi wangu nitakaofanya kwenu sasa.”
2 Kipenga sa bandu pakiyowine Paulo akilongela nabo kiebrania, batinyamaza. Kabaya.
Makutano walipo sikia Paulo akiongea nao kwa kiebrania, wakanyamaza. Akasema,
3 “Nenga na myahudi, nibelekwile mji wa Tarso eneo lya Kilikia, ila niipatike elimu katika mji wolo, mu'magolo ga Gamalieli. Natifundishwa lingana na ndela sahihi ya saliya ya tate bitu. Nenga nibile na bidii ya Nnongo, kati mwenga mwabote mwamubile leno.
“Mimi ni myahudi, nimezaliwa mji wa Tarso eneo la Kilikia, ila nilipata elimu katika mji huu, miguuni pa Gamalieli. Nilifundishwa kulingana na njia sahihi za sheria za baba zetu. Mimi ninabidii ya Mungu, kama ninyi nyote mlivyo leo.
4 Natibatesa kwa ndela yee mpaka kubulagwa, natibakamwa analome na alwawa na kubatupa mu'ligereza.
Niliwatesa kwa njia hii hadi kufa; nikawafunga wanaume na wanawake na kuwatupa gerezani.
5 Hata kuhani nkolo na apindo bote baweza kutoa ushahidi panga natipokya barua boka kwabe kwa ajili ya alongo babile Dameski, kwango nenga kusafiri kuyenda kolyo. Ibile nialete bandu Yerusalemu kwa ndela yee ili batabilwe no adhibiwa.
Hata kuhani mkuu na wazee wote wanaweza kutoa ushahidi kwamba nilipokea barua kutoka kwao kwa ajili ya ndugu walio Dameski, kwangu mimi kusafiri kwenda huko. Ilikuwa niwalete watu Yerusalemu wa njia ile ili wafungwe na kuadhibiwa.
6 Itokea panga panibile nikisafiri no karibia Dameski, majira ya mutwekati ghafla bweya nkolo uisile boka kumaunde natumbwa kuniangaza.
Ilitokea kwamba pale nilipokua nikisafiri nakaribia Dameski, majira ya mchana ghafla nuru kuu ikatokea mbinguni ikaanza kuniangaza.
7 Natitomboka pae na kupekaniya lilobe lyabaya,'Sauli, Sauli kwa mwanja namani waniudhi?'
Nikaanguka chini na kusikia sauti ikiniambia, 'Sauli, Sauli kwanini unaniudhi?'
8 Nkayangwa,'wenga wa nyai, Ngwana?' Kanibakiya,'Nenga na Yesu Mnazareti, ambaye wenga waniudhi.'
Nikajibu, 'wewe ni nani, Bwana?' Akaniambia, 'Mini ni Yesu Mnazareti, ambaye wewe unaniudhi.'
9 Balo babile na nenga baibweni bweya, ila bayowine kwa lilobe lya yolo ywalongela na nenga.
Wale waliokuwa na mimi waliiona nuru, ila hawakusikia sauti ya yule alie ongea na mimi.
10 Nikabaya,'Nipange namani, Ngwana?' Ngwana kanibakiya,'Yema na ujingye Dameski; kolyo walowa bakiwa kila kilebe chaupalikwa kukipanga.'
Nikasema, 'Nifanye nini, Bwana?' Bwana akaniambia, 'Simama na uingie Dameski; huko utaambiwa kila kitu unachopaswa kufanya.'
11 Naweza kwaa kubona kwa mana ya mwangaza wa bweya wolo, bga nibokite Dameski kwa kuongozwa na maboko ga balo babile na nenga.
Sikuweza kuona kwa sababu ya muangaza wa nuru ile, ndipo nikaenda Dameski kwa kuongozwa na mikono ya wale waliokuwa na mimi.
12 Kolyo natikwembana na mundu ywakemelwa Anania, ywabile mundu ywaikamwa saliya na mwene kuheshimika nnongi ya Bayahudi bote batami kolyo.
Huko nikakutana na mtu aitwaye Anania, alikuwa mtu aliyeshika sheria na mwenye kuheshimika mbele ya Wayahudi wote walioishi huko.
13 Kaisa kwango, na ayemi nnongi yango, no baya,'nongo wango Sauli, upate kuona.'Kwa muda wowolo natibona.
Akaja kwangu, akasimama mbele yangu, na kusema, 'Ndugu yangu Sauli, upate kuona.'Kwa muda ule ule nikamuona.
14 Akabaya,'Nnongo wa tate yitu atikuchawa wenga upate kugatanga mapenzi gake, kumwona yolo ywabile na haki, na kuiyowa lilobe yaiboka mu'nkanwa wake.
Akasema, 'Mungu wa baba zetu amekuchagua wewe upate kujua mapenzi yake, kumuona yule mwenyehaki, na kusikia sauti itokayo kwenye kinywa chake.
15 Kwa mana walowa pangika shahidi kwake kwa bandu bote nnani ya uyabonekeya na kugapekaniya.
Kwa sababu utakuwa shahidi kwake kwa watu wote juu ya uliyoyaona na kusikia.
16 Bai nambeambe kwa namani wasubiri? Amka, ubatizwe, ukaoshe dhambi yako, ukilikema lina lyake.'
Basi sasa kwa nini unasubiri? Amka, ubatizwe, ukaoshe dhambi zako, ukiliita jina lake.'
17 Baada ya kukerebuka Yerusalemu, na panibile nikisali nkati ya lihekalu, ikatokea panga nipeilwe maono.
Baada ya kurejea Yerusalemu, na nilipokuwa nikisali ndani ya hekalu, ikatokea kwamba nikapewa maono.
18 Namweni kanibakiya,'Hima na utoke Yerusalemu haraka, kwa sababu balowa kuuyeketya kwaa ushuhuda wako kuhusu nenga.'
Nikamuona akiniambia, 'Hima na utoke Yerusalemu haraka, kwa sababu hawatakubali ushuhuda wako kuhusu mimi.'
19 Nikabaya,'Ngwana, bembe bene batangite kuwa natibafunga muligereza na kuwakombwa balo baaminiya katika lisinagogi.
Nikasema, 'Bwana, wao wenyewe wanajua niliwafunga gerezani na kuwapiga wale waliokuamini katika kila sinagogi.
20 Na myai ya Stephano shahidi wako yatimwagwa, Nenga pia nibile nayemile papipi na kuyeketya na nibile nalinda ngobo ya balo babile bakimulaga.'
Na damu ya Stefano shahidi wako ilipomwagwa, Mimi pia nilikuwa nimesimama karibu na kukubali na nilikuwa nalinda nguo za wale waliomwua.'
21 Lakini atinibakiya, “Uyende kwa sababu nenga nalowa kukutuma uyende mbale kwa bandu ba mataifa.”'
Lakini aliniambia, 'Enenda, kwa sababu mimi nitakutuma uende mbali kwa watu wa mataifa.”'
22 Bandu batinruhusu alongele nnani ya neno lee. Lakini badae patilipaza lilobe no baya, mwondoe mundu yolo katika nnema”kwa sababu ni sahihi kwaa atame.”
Watu wakamruhusu aongee juu ya neno hili. Lakini baadaye walipaza sauti na kusema, “mwondoe mtu huyu katika nchi: kwa sababu sio sahihi aishi.”
23 Pababile bakipaza lilobe, na kutupa ngobo yabe na kutupa mavumbi nnani,
Walipokuwa wakipaza sauti, na kutupa mavazi yao na kutupa mavumbi juu,
24 jemedari nkolo atiamuru Paulo aletwe mu'ngome. Atiamuru analuywe huku akikombwa mijeredi, ili ywembe mwene atange kwa namani babile babile bakikombwa ndoti ya naman yelo.
jemedari mkuu akaamuru Paulo aletwe ngomeni. Akaamuru aulizwe huku anapigwa mijeledi, ili yeye mwenyewe ajue kwa nini walikuwa wanampigia kelele namna ile.
25 Hata pababile batimfunga kwa kamba, Paulo ammakiye yolo akida ywayemile papipi ni ywembe, “Je! ni haki kwinu kunkombwa ywabile Mrumi na bado ahukumilwa kwaa?”
Hata walipokuwa wamemfunga kwa kamba, Paulo akamwambia yule akida aliye simama karibu naye, “Je! ni haki kwenu kumpiga mtu aliye Mrumi na bado hajahukumiwa?”
26 Yolo akida paayowine maneno aga, kayenda kwa jemedari nkolo na kummakiya, abaya, “Upala kupanga namani? Kwa maana mundu yolo mrumi.”
Yule akida aliposikia maneno haya, akaenda kwa jemedari mkuu na kumwambia, akisema, “Unataka kufanya nini? Kwa maana mtu huyu ni mrumi.”
27 Jemedari nkolo kaisa na kummakiya, “Nibakiye, je wenga ni raia ba Rumi?” Paulo kabaya, “Eloo.”
Jemedari mkuu akaja na kumwambia, “Niambie, je wewe ni raia wa Rumi?” Paulo akasema, “Ndiyo.”
28 Jemedari kayangwa, “Kwo pitya kiasi kikoro cha pesa nga nilipata uraia.” Lakini Paulo kammakiya, “Nenga na mrumi wa kubelekwa.”
Jemedari akamjibu, “Ni kupitia kiasi kikubwa cha pesa ndipo nilipata uraia.” Lakini Paulo akamwambia, “Mimi ni mrumi wa kuzaliwa.”
29 Bai balo babile tayari kuyenda kumuuliza kuboka na kumwacha wakati wowolo. Na jemedari niywembe atiyogopa, paayowine kuwa Paulo ni Mrumi, na kwa sababu amtabile
Basi wale waliokuwa tayari kwenda kumuuliza wakaondoka na kumwacha wakati huo huo. Na jemedari naye akaogopa, alipojua kuwa Paulo ni Mrumi, na kwa sababu amemfunga.
30 Lisoba lyanyaibele, jemedari nkolo apala kutanga ukweli kuhusu mashtaka ga Bayahudi dhidi ya Paulo. Nga nyoo atimfungua vifungo vyake ni kuamuru akolo ba makuhani na baraza lyote bakwembane. Kanneta Paulo pae, ni kumbeka katikati yabe.
Siku iliyofuatayo, jemedari mkuu alitaka kujua ukweli kuhusu mashtaka ya Wayahudi dhidi ya Paulo. Hivyo akamfungua vifungo vyake akaamuru wakuu wa makuhani na baraza lote wakutane. Akamleta Paulo chini, na kumweka katikati yao.

< Matendo ga Mitume 22 >