< 1 Yohana 4 >

1 Apendwa, mumwaminiye kwaa kila roho, lakini muijaribu mubone mana yaboka kwa Nnongo, kwa sababu manabii wanyansima wa ubocho watitokea mu'dunia.
Wapendwa, msiiamini kila roho, lakini zijaribuni roho muone kama zinatokana na Mungu, kwa sababu manabii wengi wa uongo wametokea duniani.
2 Kwa lee mumtangite Roho wa Nnongo-kila roho yalowa baya kuwa Yesu Kristo atiisa katika yega ni ya Nnongo,
Kwa hili mtamjua Roho wa Mungu - kila roho itakayokiri kuwa Yesu Kristo amekuja katika mwili ni ya Mungu,
3 na kila roho yabaya kwaa Yesu ni Nnongo kwaa. Ayee ni roho ya mpinga Kristo, ambayo mupekania kuwa yaisa, nambeambe tayari ibile mu'dunia.
na kila roho isiyomkiri Yesu si ya Mungu. Hii ni roho ya mpinga kristo, ambayo mliyoisikia kuwa inakuja, na sasa tayari iko duniani.
4 Mwenga ni wa Nnongo, bana apendwa, na muyomwile washinda kwa sababu ywembe ywabile nkati yinu ni nkolo kuliko ywembe ywabile katika ulimwengu,
Ninyi ni wa Mungu, watoto wapendwa, na mmekwisha washinda kwa sababu yeye aliye ndani yenu ni mkuu kuliko yeye aliye katika ulimwengu.
5 Bembe ni ba ulimwengu, kwa eyo bakiba ni cha ulimwengu, na ulimwengu wabapekania.
Wao ni wa ulimwengu, kwa hiyo wanachokisema ni cha ulimwengu, na ulimwengu unawasikiliza.
6 Twenga ni wa Nnongo. Ywembe amtangite Nnongo aweza kutupekania. Ywembe ywabile kwaa na Nnongo aweza kwaa kutupekania. Katika yee tutangite roho waa kweli na roho wa ubocho.
Sisi ni wa Mungu. Yeye amjuaye Mungu hutusikiliza sisi. Yeye asiye wa Mungu hawezi kutusikiliza. Katika hili tunajua roho wa kweli na roho wa uongo.
7 Mwapendilwe, tupendane twenga kwa twenga, kwa elo lipendo lya Nnongo, na kila yumo ywampendae abelekilwe na Nnongo na kuntanga Nnongo.
Wapendwa, tupendane sisi kwa sisi, kwa vile upendo ni wa Mungu, na kila mmoja apendaye amezaliwa na Mungu na kumjua Mungu.
8 Ywembe ywampenda kwaa Nnongo amtangite kwaa, kwa mana Nnpngo ni upendo.
Yeye asiyependa hamjui Mungu, kwa sababu Mungu ni upendo.
9 Katika lee lipendo lya Nnongo lyatifunuliwa nkati yinu, panga Nnongo atintuma mwana wake wa pekee ulimwengu ili tutame pitya ywembe.
Katika hili pendo la Mungu lilifunuliwa miongoni mwetu, kwamba Mungu alimtuma Mwanae wa pekee ulimwenguni ili tuishi kupitia yeye.
10 Katika lipendo lee, ni panga kwaa twatimpenda Nnongo, lakini ywembe atitupenda twenga, no ntuma mwana wake awe fidia ya sambi yitu.
Katika hili pendo, si kwamba tulimpenda Mungu, lakini yeye alitupenda, na akamtuma Mwanawe awe fidia ya dhambi zetu.
11 Apendwa mana itei Nnongo atupendike twenga, yeyelo tupalikwa tupendane twenga ka twenga.
Wapendwa, ikiwa Mungu alitupenda sisi, vile vile tunapaswa kupendana sisi kwa sisi.
12 Ntopo hata yumo ywamweni Nnongo. Mana twapendana twenga kwa twenga, Nnongo atama nkati yitu.
Hakuna hata mmoja aliyemuona Mungu. Kama tukipendana sisi kwa sisi, Mungu anakaa ndani yetu na pendo lake limekamilika ndani yetu.
13 Katika lee tutangite kuwa twatama nkati yake na ywembe nkati yitu, kwa mana atupeileRoho wake.
Katika hili tunajua kuwa tunakaa ndani yake na yeye ndani yetu, kwa sababu ametupa Roho wake.
14 Na tuubweni na kuhushudia kuwa Tate attmtuma Mwana kuwa mkochopoli wa ulimwengu.
Na tumeona na kushuhudia kuwa Baba amemtuma Mwana kuwa mwokozi wa ulimwengu.
15 Kila ywabaya panga Yesu ni Mwana wa Nnongo, Nnongo atama nkati yake na ywembe nkati ya Nnongo.
Kila anayekiri kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu, Mungu anakaa ndani yake na yeye ndani ya Mungu.
16 Na tutangite na kuamini upendo abile nao Nnongo nkati yitu. Nnongo ni pendo, na ywembe atama nkati ya upendo atama nkati ya Nnongo, na Nnongo utama nkati yake.
Na tunajua na kuamini upendo alio nao Mungu ndani yetu. Mungu ni pendo, na yeye anayekaa ndani ya upendo anakaa ndani ya Mungu, na Mungu hukaa ndani yake.
17 Katika pendo lee liyomwike kamilika kati yitu, ili tuwe na ujasiri lisoba lya hukumu, kwa sababu mana ywembe abile, na twenga nga tubile ktika ulimwengu wolo.
Katika pendo hili limekwisha kamilishwa kati yetu, ili tuwe na ujasiri siku ya hukumu, kwa sababu kama yeye alivyo, na sisi ndivyo tulivyo katika ulimwenngu huu.
18 Ntopo hofu nkati ya pendo. Lakini pendo kamili huitupa hofu panja, kwa mana hofu huhusiana na hukumu. Lakini ywembe ywaogopeya akamilika kwaa katika lipendo.
Hakuna hofu ndani ya pendo. Lakini pendo kamili huitupa hofu nje, kwa sababu hofu huhusiana na hukumu. Lakini yeye aogopaye hajakamilishwa katika pendo.
19 Twapenda kwa mana Nnongo atitupenda kwanza.
Tunapenda kwa sababu Mungu alitupenda kwanza.
20 Mana itei yumo abaya, “Nampenda Nnongo” lakini anchukya nongowe, ywamweni, aweza kwaa kumpenda Nnongo ambae ywamwonea kwaa.
Ikiwa mmoja atasema, “Nampenda Mungu” lakini anamchukia ndugu yake, ni mwongo. Kwa sababu asiyempenda ndugu yake, anayemuona, hawezi kumpenda Mungu ambaye hajamuona.
21 Na yee nga amri tubile nayo boka kwake: Yeyote ywampendae Nnongo, apalikwa kumpenda nongowe pia.
Na hii ndiyo amri tuliyo nayo kutoka kwake: Yeyote ampendaye Mungu, anapaswa kumpenda ndugu yake pia.

< 1 Yohana 4 >