< Apocalypsis 7 >

1 post haec vidi quattuor angelos stantes super quattuor angulos terrae tenentes quattuor ventos terrae ne flaret ventus super terram neque super mare neque in ullam arborem
Baada ya haya niliona malaika wanne wamesimama kwenye kona nne za dunia, wamezuia pepo nne za nchi kwa nguvu ili kwamba pasiwe na upepo unaovuma katika nchi, juu ya bahari au dhidi ya mti wowote.
2 et vidi alterum angelum ascendentem ab ortu solis habentem signum Dei vivi et clamavit voce magna quattuor angelis quibus datum est nocere terrae et mari
Nikaona malaika mwingine akija kutoka mashariki, aliyekuwa na muhuri wa Mungu aliye hai. Akalia kwa sauti kuu kwa malaika wanne ambao walipewa ruhusa ya kudhuru nchi na bahari:
3 dicens nolite nocere terrae neque mari neque arboribus quoadusque signemus servos Dei nostri in frontibus eorum
“Msiidhuru nchi, bahari, au miti mpaka tutakapokuwa tumekwishaweka muhuri katika paji za vichwa vya watumishi wa Mungu wetu.”
4 et audivi numerum signatorum centum quadraginta quattuor milia signati ex omni tribu filiorum Israhel
Nikasikia idadi ya wale waliotiwa muhuri: 144, 000, ambao walitiwa muhuri kutoka kila kabila ya watu wa Israel:
5 ex tribu Iuda duodecim milia signati ex tribu Ruben duodecim milia ex tribu Gad duodecim milia
12, 000 kutoka katika kabila ya Yuda walitiwa muhuri, 12, 000 kutoka katika kabila ya Rubeni, 12, 000 kutoka katika kabila ya Gadi.
6 ex tribu Aser duodecim milia ex tribu Nepthalim duodecim milia ex tribu Manasse duodecim milia
12, 000 kutoka katika kabila ya Asheri, 12, 000 kutoka katika kabila ya Naftali, 12, 000 kutoka katika kabila ya Manase.
7 ex tribu Symeon duodecim milia ex tribu Levi duodecim milia ex tribu Issachar duodecim milia
12, 000 kutoka kabila ya Simioni, 12, 000 kutoka kabila ya Lawi, 12, 000 kutoka kabila ya Isakari,
8 ex tribu Zabulon duodecim milia ex tribu Ioseph duodecim milia ex tribu Beniamin duodecim milia signati
12, 000 kutoka kabila ya Zebuloni, 12, 000 kutoka kabila ya Yusufu, na 12, 000 kutoka kabila ya Benyamini walitiwa muhuri.
9 post haec vidi turbam magnam quam dinumerare nemo poterat ex omnibus gentibus et tribubus et populis et linguis stantes ante thronum et in conspectu agni amicti stolas albas et palmae in manibus eorum
Baada ya mambo haya nilitazama, na kulikuwa na umati mkubwa ambao hapana mtu angeweza kuuhesabu - kutoka kila taifa, kabila, jamaa, na lugha - wamesimama mbele ya kiti cha enzi na mbele ya Mwanakondoo. Walikuwa wamevaa kanzu nyeupe na wana matawi ya mitende mikononi mwao,
10 et clamabant voce magna dicentes salus Deo nostro qui sedet super thronum et agno
na walikuwa wakiita kwa sauti ya juu: “Wokovu ni kwa Mungu ambaye ameketi katika kiti cha enzi, na kwa Mwanakondoo!”
11 et omnes angeli stabant in circuitu throni et seniorum et quattuor animalium et ceciderunt in conspectu throni in facies suas et adoraverunt Deum
Malaika wote waliokuwa wamesimama kuzunguka kiti cha enzi na kuwazunguka wale wazee pamoja na wenye uhai wanne, wakainama chini ardhini na wakaweka nyuso zao juu ya ardhi mbele ya kiti cha enzi na wakamwabudu Mungu,
12 dicentes amen benedictio et claritas et sapientia et gratiarum actio et honor et virtus et fortitudo Deo nostro in saecula saeculorum amen (aiōn g165)
wakisema, “Amina! Sifa, utukufu, hekima, shukurani, heshima, uwezo na nguvu viwe kwa Mungu wetu milele na milele! Amina!” (aiōn g165)
13 et respondit unus de senioribus dicens mihi hii qui amicti sunt stolis albis qui sunt et unde venerunt
Kisha mmoja wa wale wazee akaniuliza, “hawa ni akina nani waliovaa kanzu nyeupe, na wametoka wapi?
14 et dixi illi domine mi tu scis et dixit mihi hii sunt qui veniunt de tribulatione magna et laverunt stolas suas et dealbaverunt eas in sanguine agni
Nikamwambia, “Bwana mkubwa, unajua wewe,” na akaniambia, “Hawa ni wale waliotoka katika dhiki kuu. Wamezifua kanzu zao na kuzifanya nyeupe kwa damu ya Mwanakondoo.
15 ideo sunt ante thronum Dei et serviunt ei die ac nocte in templo eius et qui sedet in throno habitabit super illos
Kwa sababu hii, wako mbele ya kiti cha enzi cha Mungu, na wanamwabudu yeye usiku na mchana katika hekalu lake. Yeye aliye keti juu ya kiti cha enzi atasambaza hema yake juu yao.
16 non esurient neque sitient amplius neque cadet super illos sol neque ullus aestus
Hawataona njaa tena, wala kiu tena. Jua halitawachoma, wala joto la kuunguza.
17 quoniam agnus qui in medio throni est reget illos et deducet eos ad vitae fontes aquarum et absterget Deus omnem lacrimam ex oculis eorum
Kwa kuwa Mwanakondoo aliye katikati ya kiti cha enzi atakuwa mchungaji wao, na atawaongoza katika chemchemi ya maji ya uzima, na Mungu atafuta kila chozi katika macho yao.”

< Apocalypsis 7 >