< Psalmorum 81 >
1 in finem pro torcularibus Asaph exultate Deo adiutori nostro iubilate Deo Iacob
Mwimbieni Mungu aliye nguvu yetu kwa sauti; pigeni kelele za furaha kwa Mungu wa Yakobo.
2 sumite psalmum et date tympanum psalterium iucundum cum cithara
Imbeni wimbo na pigeni matari, kinubi chenye sauti nzuri pamoja na kinanda.
3 bucinate in neomenia tuba in insigni die sollemnitatis nostrae
Pigeni panda mwandamo wa mwezi, katika siku ya mbalamwezi, mwanzoni mwa sikukuu.
4 quia praeceptum Israhel est et iudicium Dei Iacob
Kwa kuwa ni agizo kwa Israeli, amri iliyotolewa na Mungu wa Yakobo.
5 testimonium in Ioseph posuit illud cum exiret de terra Aegypti linguam quam non noverat audivit
Aliitoa kama maelekezo kwa Yusufu alipoenda katika nchi ya Misri, ambako nilisikia sauti ambayo sikuweza kuitambua:
6 devertit ab oneribus dorsum eius manus eius in cofino servierunt
“Niliutua mzigo kutoka mabegani mwake; mikono yake ilipumzishwa kubeba kikapu.
7 in tribulatione invocasti me et liberavi te exaudivi te in abscondito tempestatis probavi te apud aquam Contradictionis diapsalma
Katika dhiki yako uliniita, nami nikakusaidia; nilikujibu kutoka katika wingu jeusi la radi. Nilikujaribu kwenye maji ya Meriba. (Selah)
8 audi populus meus et contestabor te Israhel si audias me
Sikilizeni, watu wangu, nami nitawaonya, Israeli, kama tu ugalinisikiliza!
9 non erit in te deus recens nec adorabis deum alienum
Lazima kati yenu kusiwepo na mungu wa kigeni; haupaswi kumwabudu mungu wa kigeni.
10 ego enim sum Dominus Deus tuus qui eduxi te de terra Aegypti dilata os tuum et implebo illud
Mimi ni Yahwe niliyekutoa katika nchi ya Misri, fungua sana kinywa chako, nami nitakijaza.
11 et non audivit populus meus vocem meam et Israhel non intendit mihi
Lakini watu wangu hawakusikiliza maneno yangu; Israeli hawakunitii.
12 et dimisi illos secundum desideria cordis eorum ibunt in adinventionibus suis
Nikawaacha waende katika katika njia yao wenyewe ya ukaidi ili kwamba waweze kufanya kinachoonekana sahihi kwao.
13 si populus meus audisset me Israhel si in viis meis ambulasset
Oh, laiti watu wangu wangenisikiliza mimi; oh, watu wangu wangelitembea katika njia yangu.
14 pro nihilo forsitan inimicos eorum humiliassem et super tribulantes eos misissem manum meam
Kisha ningewatiisha adui zao haraka na kugeuzia mkono wangu dhidi ya watesi wao.
15 inimici Domini mentiti sunt ei et erit tempus eorum in saeculo
Wale wanaomchukia Yahwe katika hofu na waanguke chini mbele zake! Wawe wanyonge milele.
16 et cibavit illos ex adipe frumenti et de petra melle saturavit illos
Ningewalisha Israeli kwa ngano bora; Ningewatosheleza kwa asali itokayo mwambani.”