< Lucam 22 >

1 adpropinquabat autem dies festus azymorum qui dicitur pascha
Basi Sikukuu ya Mkate Usiyotiwa Chachu ilikuwa imekaribia, ambayo inaitwa Pasaka.
2 et quaerebant principes sacerdotum et scribae quomodo eum interficerent timebant vero plebem
Makuhani wakuu na waandishi wakajadiliana namna ya kumuua Yesu, kwa sababu waliwaogopa watu.
3 intravit autem Satanas in Iudam qui cognominatur Scarioth unum de duodecim
Shetani akaingia ndani ya Yuda Iskariote, mmoja wa wale wanafunzi Kumi na mbili.
4 et abiit et locutus est cum principibus sacerdotum et magistratibus quemadmodum illum traderet eis
Yuda akaenda kujadiliana na wakuu wa makuhani na wakuu namna ambavyo atamkabidhi Yesu kwao.
5 et gavisi sunt et pacti sunt pecuniam illi dare
Walifurahi, na kukubaliana kumpa fedha.
6 et spopondit et quaerebat oportunitatem ut traderet illum sine turbis
Yeye aliridhia, na alitafuta fursa ya kumkabidhi Yesu kwao mbali na kundi la watu.
7 venit autem dies azymorum in qua necesse erat occidi pascha
Siku ya mikate isiyotiwa chachu ikafika, ambapo kondoo wa Pasaka lazima atolewe.
8 et misit Petrum et Iohannem dicens euntes parate nobis pascha ut manducemus
Yesu akawatuma Petro na Yohana, akasema, “Nendeni mkatuandalie chakula cha Pasaka ili tuje tukile.”
9 at illi dixerunt ubi vis paremus
Wakamuuliza, “Wapi unataka tuyafanyie hayo maandalizi?”
10 et dixit ad eos ecce introeuntibus vobis in civitatem occurret vobis homo amphoram aquae portans sequimini eum in domum in qua intrat
Akawajibu, “Sikilizeni, mtakapokuwa mmeingia mjini, mwanamume ambaye amebeba mtungi wa maji atakutana na ninyi. Mfuateni kwenye nyumba ambayo ataingia.
11 et dicetis patri familias domus dicit tibi magister ubi est diversorium ubi pascha cum discipulis meis manducem
Kisha mwambieni bwana wa nyumba, “Mwalimu anakwambia, “Kiko wapi chumba cha wageni, mahali ambapo nitakula Pasaka na wanafunzi wangu?”
12 et ipse vobis ostendet cenaculum magnum stratum et ibi parate
Atawaonyesha chumba cha ghorofani ambacho kiko tayari. Fanyeni maandalizi humo.”
13 euntes autem invenerunt sicut dixit illis et paraverunt pascha
Hivyo wakaenda, na wakakuta kila kitu kama alivyowaambia. Kisha wakaandaa chakula cha Pasaka.
14 et cum facta esset hora discubuit et duodecim apostoli cum eo
Muda ulipofika alikaa na wale mitume.
15 et ait illis desiderio desideravi hoc pascha manducare vobiscum antequam patiar
Kisha akawaambia, “Nina shauku kubwa ya kula sikukuu hii ya Pasaka na ninyi kabla ya kuteswa kwangu.
16 dico enim vobis quia ex hoc non manducabo illud donec impleatur in regno Dei
Kwa maana nawaambieni, sitakula tena mpaka itakapotimizwa katika ufalme wa Mungu.”
17 et accepto calice gratias egit et dixit accipite et dividite inter vos
Kisha Yesu akachukua kikombe, na alipokwisha kushukuru, akasema, “Chukueni hiki, na mgawane ninyi kwa ninyi.
18 dico enim vobis quod non bibam de generatione vitis donec regnum Dei veniat
Kwa maana nawaambia, sitakunywa tena mzao wa mzabibu, mpaka ufalme wa Mungu utakapokuja.”
19 et accepto pane gratias egit et fregit et dedit eis dicens hoc est corpus meum quod pro vobis datur hoc facite in meam commemorationem
Kisha akachukua mkate, na alipokwisha kushukuru, akaumega, na kuwapa, akisema, “Huu ni mwili wangu ambao umetolewa kwa ajili yenu. Fanyeni hivi kwa kunikumbuka mimi.”
20 similiter et calicem postquam cenavit dicens hic est calix novum testamentum in sanguine meo quod pro vobis funditur
Akachukua kikombe vivyo hivyo baada ya chakula cha usiku akisema, “Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu, ambayo imemwagika kwa ajili yenu.
21 verumtamen ecce manus tradentis me mecum est in mensa
Lakini angalieni. Yule anisalitie yuko pamoja nami mezani.
22 et quidem Filius hominis secundum quod definitum est vadit verumtamen vae illi homini per quem traditur
Kwa maana Mwana wa Adamu kwa kweli aenda zake kama ilivyokwisha amuliwa. Lakini ole kwa mtu yule ambaye kupitia yeye Mwana wa Adamu asalitiwa!”
23 et ipsi coeperunt quaerere inter se quis esset ex eis qui hoc facturus esset
Wakaanza kuulizana wao kwa wao, nani miongoni mwao ambaye angefanya jambo hili.
24 facta est autem et contentio inter eos quis eorum videretur esse maior
Kisha yakatokea mabishano katikati yao kwamba ni nani anaye dhaniwa kuwa mkuu kuliko wote.
25 dixit autem eis reges gentium dominantur eorum et qui potestatem habent super eos benefici vocantur
Akawaambia, “Wafalme wa watu wa mataifa wana ubwana juu yao, na wale mwenye mamlaka juu yao wanaitwa waheshimiwa watawala.
26 vos autem non sic sed qui maior est in vobis fiat sicut iunior et qui praecessor est sicut ministrator
Lakini haitakiwi kabisa kuwa hivi kwenu ninyi. Badala yake, acha yule ambaye ni mkubwa kati yenu awe kama mdogo. Na yule ambaye ni wa muhimu sana awe kama atumikaye.
27 nam quis maior est qui recumbit an qui ministrat nonne qui recumbit ego autem in medio vestrum sum sicut qui ministrat
Kwa sababu yupi mkubwa, yule akaaye mezani au yule anayetumika? Je si yule aketie mezani? Na mimi bado ni kati yenu kama atumikaye.
28 vos autem estis qui permansistis mecum in temptationibus meis
Lakini ninyi ndio ambao mmeendelea kuwa nami katika majaribu yangu.
29 et ego dispono vobis sicut disposuit mihi Pater meus regnum
Nawapa ninyi ufalme, kama vile Baba alivyonipa mimi ufalme,
30 ut edatis et bibatis super mensam meam in regno et sedeatis super thronos iudicantes duodecim tribus Israhel
kwamba mpate kula na kunywa mezani kwangu kwenye ufalme wangu. Na mtakaa kwenye viti vya enzi mkizihukumu kabila kumi na mbili za Israel.
31 ait autem Dominus Simon Simon ecce Satanas expetivit vos ut cribraret sicut triticum
Simoni, Simoni, fahamu kwamba, Shetani ameomba awapate ili awapepete kama ngano.
32 ego autem rogavi pro te ut non deficiat fides tua et tu aliquando conversus confirma fratres tuos
Lakini nimekuombea, kwamba imani yako isishindwe. Baada ya kuwa umerudi tena, waimarishe ndugu zako.”
33 qui dixit ei Domine tecum paratus sum et in carcerem et in mortem ire
Petro akamwambia, “Bwana, niko tayari kwenda na wewe gerezani na hata katika mauti.”
34 et ille dixit dico tibi Petre non cantabit hodie gallus donec ter abneges nosse me
Yesu akajibu, “Nakwambia, Petro, Jogoo hatawika leo, kabla hujanikana mara tatu kwamba unanijua.”
35 et dixit eis quando misi vos sine sacculo et pera et calciamentis numquid aliquid defuit vobis at illi dixerunt nihil
Kisha Yesu akawaambia, “Nilipowapeleka ninyi bila mfuko, kikapu cha vyakula, ua viatu, je mlipungukiwa na kitu?” Wakajibu “Hakuna.”
36 dixit ergo eis sed nunc qui habet sacculum tollat similiter et peram et qui non habet vendat tunicam suam et emat gladium
Kisha akawaambia, “Lakini sasa, kila mwenye mfuko, na auchukue pamoja na kikapu cha vyakula. Yule ambaye hana upanga imempasa auze joho lake anunue mmoja.
37 dico enim vobis quoniam adhuc hoc quod scriptum est oportet impleri in me et quod cum iniustis deputatus est etenim ea quae sunt de me finem habent
Kwa sababu nawaambia, yote ambayo yameandikwa kwa ajili yangu lazima yatimilike, 'Na alichukuliwa kama mtu ambaye anavunja torati.' Kwa sababu kile kilichotabiriwa kwa ajili yangu kinatimizwa.”
38 at illi dixerunt Domine ecce gladii duo hic at ille dixit eis satis est
Kisha wakasema, “Bwana, tazama! Hizi hapa panga mbili.” Na akawaambia”yatosha.”
39 et egressus ibat secundum consuetudinem in montem Olivarum secuti sunt autem illum et discipuli
Baada ya chakula cha usiku, Yesu aliondoka, kama ambavyo amekuwa akifanya mara kwa mara, akaenda mlima wa Mzeituni, na wanafunzi wakamfuata.
40 et cum pervenisset ad locum dixit illis orate ne intretis in temptationem
Walipofika, aliwaambia, “Ombeni kwamba msiingie majaribuni.”
41 et ipse avulsus est ab eis quantum iactus est lapidis et positis genibus orabat
Akaenda mbali na wao kama mrusho wa jiwe, akapiga magoti akaomba,
42 dicens Pater si vis transfer calicem istum a me verumtamen non mea voluntas sed tua fiat
akisema, “Baba, kama unataka, niondolee kikombe hiki. Lakini si kama nitakavyo mimi, lakini mapenzi yako yafanyike.”
43 apparuit autem illi angelus de caelo confortans eum et factus in agonia prolixius orabat
Kisha malaika kutoka mbinguni akamtokea, akamtia nguvu.
44 et factus est sudor eius sicut guttae sanguinis decurrentis in terram
Akiwa katika kuugua, akaomba kwa dhati zaidi, na jasho lake likawa kama matone makubwa ya damu yakidondoka chini.
45 et cum surrexisset ab oratione et venisset ad discipulos suos invenit eos dormientes prae tristitia
Wakati alipoamka kutoka katika maombi yake, alikuja kwa wanafunzi, na akawakuta wamelala kwa sababu ya huzuni yao,
46 et ait illis quid dormitis surgite orate ne intretis in temptationem
na akawauliza, “Kwanini mnalala? Amkeni muombe, kwamba msiingie majaribuni.”
47 adhuc eo loquente ecce turba et qui vocabatur Iudas unus de duodecim antecedebat eos et adpropinquavit Iesu ut oscularetur eum
Wakati alipokuwa bado akiongea, tazama, kundi kubwa la watu likatokea, na Yuda, mmoja wa mitume kumi na wawili akiwaongoza. Akaja karibu na Yesu ili ambusu,
48 Iesus autem dixit ei Iuda osculo Filium hominis tradis
lakini Yesu akamwambia, “Yuda, je unamsaliti Mwana wa Adamu kwa busu?”
49 videntes autem hii qui circa ipsum erant quod futurum erat dixerunt ei Domine si percutimus in gladio
Wakati wale waliokuwa karibu na Yesu walipoona hayo yanayotokea, wakasema, “Bwana, je tuwapige kwa upanga?”
50 et percussit unus ex illis servum principis sacerdotum et amputavit auriculam eius dextram
Kisha mmoja wao akampiga mtumishi wa kuhani mkuu, akamkata sikio lake la kulia.
51 respondens autem Iesus ait sinite usque huc et cum tetigisset auriculam eius sanavit eum
Yesu akasema, “hii inatosha. Na akagusa sikio lake, akamponya.
52 dixit autem Iesus ad eos qui venerant ad se principes sacerdotum et magistratus templi et seniores quasi ad latronem existis cum gladiis et fustibus
Yesu akasema kwa kuhani mkuu, na kwa wakuu wa hekalu, na kwa wazee waliokuja kinyume chake, “Je mnakuja kana kwamba mnakuja kupambana na mnyang'anyi, na marungu na mapanga?
53 cum cotidie vobiscum fuerim in templo non extendistis manus in me sed haec est hora vestra et potestas tenebrarum
Nilipokuwa pamoja nanyi siku zote kwenye hekalu, hamkuweka mikono yenu juu yangu. Lakini hii ni saa yako, na mamlaka ya giza.”
54 conprehendentes autem eum duxerunt ad domum principis sacerdotum Petrus vero sequebatur a longe
Wakamkamata, wakamuongoza, wakamleta nyumbani mwa kuhani mkuu. Lakini Petro akamfuatilia kwa mbali.
55 accenso autem igni in medio atrio et circumsedentibus illis erat Petrus in medio eorum
Baada ya kuwa wamewasha moto katika ule uwanda wa ndani na walipokwisha kukaa chini pamoja, Petro akakaa katikati yao.
56 quem cum vidisset ancilla quaedam sedentem ad lumen et eum fuisset intuita dixit et hic cum illo erat
Mtumishi mmoja wa kike akamuona Petro alipokuwa amekaa katika mwanga utokanao na moto, akamtazama akamwambia, “Huyu mtu pia alikuwa pamoja naye.”
57 at ille negavit eum dicens mulier non novi illum
Lakini Petro akakana, akasema, “mwanamke, mimi simjui.”
58 et post pusillum alius videns eum dixit et tu de illis es Petrus vero ait o homo non sum
Baada ya muda kidogo, mtu mwingine akamuona akasema “Wewe pia ni mmoja wao”. Lakini Petro akajibu, “Mwanaume, mimi siyo.”
59 et intervallo facto quasi horae unius alius quidam adfirmabat dicens vere et hic cum illo erat nam et Galilaeus est
Baada ya kama saa moja hivi, mwanaume mmoja akasisitiza akasema, “Kweli kabisa huyu mtu pia alikuwa pamoja naye, maana ni Mgalilaya.”
60 et ait Petrus homo nescio quod dicis et continuo adhuc illo loquente cantavit gallus
Lakini Petro akasema, “Mwanaume, sijui usemalo.” Na mara, wakati akiongea, jogoo akawika.
61 et conversus Dominus respexit Petrum et recordatus est Petrus verbi Domini sicut dixit quia priusquam gallus cantet ter me negabis
Akageuka, Bwana akamtazama Petro. Na Petro akalikumbuka neno la Bwana, pale alipomwambia, “Kabla ya jogoo kuwika leo, utanikana mimi mara tatu.”
62 et egressus foras Petrus flevit amare
Akienda nje, Petro akalia kwa uchungu mwingi.
63 et viri qui tenebant illum inludebant ei caedentes
Kisha wale wanaume waliokuwa wakimlinda Yesu, wakamdhihaki na kumpiga.
64 et velaverunt eum et percutiebant faciem eius et interrogabant eum dicentes prophetiza quis est qui te percussit
Baada ya kumfunika macho, wakamuuliza, wakisema, “Tabiri! Ni nani aliyekupiga?”
65 et alia multa blasphemantes dicebant in eum
Wakaongea mambo mengine mengi kinyume cha Yesu na kumkufuru yeye.
66 et ut factus est dies convenerunt seniores plebis et principes sacerdotum et scribae et duxerunt illum in concilium suum dicentes si tu es Christus dic nobis
Mara ilipokuwa asubuhi, wazee wa watu walikusanyika pamoja, wakuu wa makuhani na waandishi. Wakampeleka kwenye Baraza,
67 et ait illis si vobis dixero non creditis mihi
wakisema, “Kama wewe ni Kristo, tuambie.” Lakini yeye akawaambia, “Kama nikiwaambia, hamtaniamini,
68 si autem et interrogavero non respondebitis mihi neque dimittetis
na kama nikiwauliza hamtanijibu.”
69 ex hoc autem erit Filius hominis sedens a dextris virtutis Dei
Lakini kuanzia sasa na kuendelea, Mwana wa Adamu atakuwa amekaa mkono wa kuume wa nguvu ya Mungu.”
70 dixerunt autem omnes tu ergo es Filius Dei qui ait vos dicitis quia ego sum
Wote wakasema, “Kwa hiyo wewe ni Mwana wa Mungu?” Na Yesu akawaambia, “Ninyi mmesema mimi ndiye.”
71 at illi dixerunt quid adhuc desideramus testimonium ipsi enim audivimus de ore eius
Wakasema, “Kwa nini bado tunahitaji tena ushahidi? Kwa sababu sisi wenyewe tumesikia kutoka katika kinywa chake mwenyewe.”

< Lucam 22 >