< Hebræos 7 >

1 hic enim Melchisedech rex Salem sacerdos Dei summi qui obviavit Abrahae regresso a caede regum et benedixit ei
Ilikuwa hivi Melkizedeki, mfalme wa Salemu, Kuhani wa Mungu aliye juu, aliyekutana na Abrahamu akirudi kutoka kuwaua wafalme na akambariki.
2 cui decimas omnium divisit Abraham primum quidem qui interpretatur rex iustitiae deinde autem et rex Salem quod est rex pacis
Abrahamu alimpa moja ya kumi ya kila kitu alichokuwa amekiteka. Jina lake “Melkizedeki “maana yake” mfalme wa haki” na pia “mflame wa Salemu” ambayo ni “mfalme wa amani.”
3 sine patre sine matre sine genealogia neque initium dierum neque finem vitae habens adsimilatus autem Filio Dei manet sacerdos in perpetuum
Hana baba, hana mama, hana wazazi, hana mwanzo wa siku wala mwisho wa maisha yake. Badala yake, anabakia kuhani milele, kama mwana wa Mungu.
4 intuemini autem quantus sit hic cui et decimam dedit de praecipuis Abraham patriarcha
Sasa fikiria jinsi huyu mtu alivyokuwa mkuu. Mzazi wetu Abrahamu alimpa moja ya kumi ya vitu vizuri alivyovichukua vitani.
5 et quidem de filiis Levi sacerdotium accipientes mandatum habent decimas sumere a populo secundum legem id est a fratribus suis quamquam et ipsi exierunt de lumbis Abrahae
Na hakika, ukoo wa Walawi waliopokea ofisi za kikuhani walikuwa na amri kutoka kwenye sheria kukusanya moja ya kumi kutoka kwa watu, ambayo ni, kutoka kwa Wairaeli wenzao, pamoja na kwamba wao, pia, ni ukoo kutoka kwa Abrahamu.
6 cuius autem generatio non adnumeratur in eis decimas sumpsit Abraham et hunc qui habebat repromissiones benedixit
Lakini Melkizedeki, ambaye hakuwa wa ukoo kutoka kwa Walawi, alipokea moja ya kumi kutoka kwa Abrahamu, na akambariki, yeye aliyekuwa na ahadi.
7 sine ulla autem contradictione quod minus est a meliore benedicitur
Hapo haikataliwi kwamba mtu mdogo hubarikiwa na mkubwa.
8 et hic quidem decimas morientes homines accipiunt ibi autem contestatus quia vivit
Kwa jambo hili mtu apokeaye moja ya kumi atakufa siku moja, lakini kwa jambo jingine mmoja aliyepokea moja ya kumi kwa Abrahamu ikaelezwa kama anayeishi.
9 et ut ita dictum sit per Abraham et Levi qui decimas accipit decimatus est
Na kwa namna ya kuzungumza, Lawi aliyepokea moja ya kumi, pia alilipa moja ya kumi kwa Abrahamu,
10 adhuc enim in lumbis patris erat quando obviavit ei Melchisedech
kwa sababu Lawi alikuwa katika viuno vya baba yake Abrahamu wakati Melkizedeki alipokutana na Abrahamu.
11 si ergo consummatio per sacerdotium leviticum erat populus enim sub ipso legem accepit quid adhuc necessarium secundum ordinem Melchisedech alium surgere sacerdotem et non secundum ordinem Aaron dici
Sasa kama ukamilifu uliwezekana kupitia ukuhani wa Lawi, (hivyo chini yake watu hupokea sheria), kulikuwa na hitaji gani zaidi kwa kuhani mwingine kuinuka baada ya mfumo wa Melkizedeki, na siyo kuitwa baada ya mpangilio wa Haruni?
12 translato enim sacerdotio necesse est ut et legis translatio fiat
Kwa hiyo ukuhani ukibadilika, hapana budi sheria nayo kubadilika.
13 in quo enim haec dicuntur de alia tribu est de qua nullus altario praesto fuit
Kwa mmoja ambaye mambo haya yalisemwa kuhusu kabila jingine, kutoka kwake hakuna aliyehudumu madhabahuni.
14 manifestum enim quod ex Iuda ortus sit Dominus noster in qua tribu nihil de sacerdotibus Moses locutus est
Sasa ni wazi kwamba Bwana wetu alitoka katika Yuda, kabila ambalo Musa hakutaja kuhusu makuhani.
15 et amplius adhuc manifestum est si secundum similitudinem Melchisedech exsurgit alius sacerdos
Na haya tusemayo ni wazi hasa ikiwa kuhani mwingine atatokea kwa mfano wa Melkizedeki.
16 qui non secundum legem mandati carnalis factus est sed secundum virtutem vitae insolubilis
Kuhani huyu mpya siyo mmoja ambaye amekuwa kuhani juu ya msingi wa sheria zinazohusiana na uzao wa mtu, lakini katika msingi wa nguvu ya maisha yasiyoweza kuharibika.
17 contestatur enim quoniam tu es sacerdos in aeternum secundum ordinem Melchisedech (aiōn g165)
Hivyo maandiko yanashuhudia kuhusu yeye: “Wewe ni kuhani milele baada ya mfumo wa Melkizedeki.” (aiōn g165)
18 reprobatio quidem fit praecedentis mandati propter infirmitatem eius et inutilitatem
Kwa kuwa amri iliyotangulia iliwekwa pembeni kwa sababu ilikuwa dhaifu na haifai.
19 nihil enim ad perfectum adduxit lex introductio vero melioris spei per quam proximamus ad Deum
Hivyo sheria haikufanya chochote kikamilifu. Isipokuwa, kulikuwa na ujasiri mzuri kwa hayo tunamsogelea Mungu.
20 et quantum est non sine iureiurando alii quidem sine iureiurando sacerdotes facti sunt
Na Ujasiri huu mzuri haukutokea pasipo kuzungumzia kiapo, kwa hili makuhani wengine hawakuchukua kiapo chochote.
21 hic autem cum iureiurando per eum qui dixit ad illum iuravit Dominus et non paenitebit tu es sacerdos in aeternum (aiōn g165)
Lakini Mungu alichukua kiapo wakati aliposema kuhusu Yesu, “Bwana ameapa na hatabadilisha mawazo yake.' wewe ni kuhani milele.” (aiōn g165)
22 in tantum melioris testamenti sponsor factus est Iesus
Kwa hili Yesu pia amekuja kuwa dhamana ya agano bora.
23 et alii quidem plures facti sunt sacerdotes idcirco quod morte prohiberentur permanere
Kwa hakika, kifo huzuia makuhani kuhudumu milele. Hii ni kwa sababu walikuwapo makuhani wengi, mmoja baada ya mwingine.
24 hic autem eo quod maneat in aeternum sempiternum habet sacerdotium (aiōn g165)
Lakini kwa sababu Yesu anaishi milele, ukuhani wake haubadiliki. (aiōn g165)
25 unde et salvare in perpetuo potest accedentes per semet ipsum ad Deum semper vivens ad interpellandum pro eis
Kwa hiyo yeye pia anaweza kwa ukamilifu kukamilisha kuwaokoa wanaomkaribia Mungu kupitia kwake, kwa kuwa yeye anaishi daima kwa kuomba kwa ajili yao.
26 talis enim decebat ut nobis esset pontifex sanctus innocens inpollutus segregatus a peccatoribus et excelsior caelis factus
Kwa hiyo kuhani mkuu wa namna hii anastahili kwetu. Asiye na dhambi, hatia, msafi, aliyetengwa kutoka kwa wenye dhambi, na amekuwa juu kuliko mbingu.
27 qui non habet cotidie necessitatem quemadmodum sacerdotes prius pro suis delictis hostias offerre deinde pro populi hoc enim fecit semel se offerendo
Yeye hakuwa na uhitaji, mfano wa makuhani wakuu, kutoa dhabihu kila siku, kwanza kwa dhambi yake mwenyewe, na baadaye kwa dhambi za watu. Alifanya hivi mara moja kwa wote, alipojitoa yeye mwenyewe.
28 lex enim homines constituit sacerdotes infirmitatem habentes sermo autem iurisiurandi qui post legem est Filium in aeternum perfectum (aiōn g165)
Kwa sheria huwateua watu dhaifu kuwa makuhani wakuu, lakini neno la kiapo, lililokuja baada ya sheria, alimteua Mwana, aliyefanywa kuwa mkamilifu milele. (aiōn g165)

< Hebræos 7 >