< Deuteronomii 24 >

1 si acceperit homo uxorem et habuerit eam et non invenerit gratiam ante oculos eius propter aliquam foeditatem scribet libellum repudii et dabit in manu illius et dimittet eam de domo sua
Mwanamume akimchukua mke na kumuoa, na mke asipokubalika machoni pa mumewe kwa sababu kagundua jambo ambalo si jema kwake, basi anatakiwa amwandikie talaka, aiweke mkononi mwake, na kumfukuza nyumbani kwake.
2 cumque egressa alterum maritum duxerit
Akishaondoka nyumbani kwake, anaweza kwenda na kuwa mke wa mwanamume mwingine.
3 et ille quoque oderit eam dederitque ei libellum repudii et dimiserit de domo sua vel certe mortuus fuerit
Iwapo mume wa pili akamchukia na kumwandikia talaka, akaiweka mkononi mwake, na kumfukuza nyumbani kwake; au huyu mume wa pili akafariki, mwanamume aliyemchukua kuwa mke wake –
4 non poterit prior maritus recipere eam in uxorem quia polluta est et abominabilis facta est coram Domino ne peccare facias terram tuam quam Dominus Deus tuus tibi tradiderit possidendam
basi mume wa awali, yule aliyemfukuza mara ya kwanza, haruhusiwi kumchukua tena awe mke wake, baada ya yeye kuwa mchafu, kwa maana hiyo itakuwa ni chukizo kwa Yahwe. Hautakiwi kusababisha nchi iwe na hatia, nchi ambayo Yahwe Mungu wako anakupatia kama urithi.
5 cum acceperit homo nuper uxorem non procedet ad bellum nec ei quippiam necessitatis iniungetur publicae sed vacabit absque culpa domui suae ut uno anno laetetur cum uxore sua
Mwanamume atakapochukua mke mpya, hatakwenda vitani na jeshi, na wala hataamrishwa kwenda kwenye shughuli yoyote ya kulazimishwa; atakuwa huru kuwa nyumbani kwa mwaka mzima na atamfurahisha mke wake aliyemchukua.
6 non accipies loco pignoris inferiorem et superiorem molam quia animam suam adposuit tibi
Mwanamume yeyote hatachukua kinu wala jiwe la kinu kama dhamana, kwa maana hivyo itakuwa kuchukua Maisha ya mtu kama dhamana.
7 si deprehensus fuerit homo sollicitans fratrem suum de filiis Israhel et vendito eo accipiens pretium interficietur et auferes malum de medio tui
Iwapo mwanamume kakutwa kamteka mmoja wa kaka zake miongoni mwa watu wa Israeli, na kumtendea kama mtumwa na kisha kumuuza, huyo mwizi lazima afe; na utakuwa umeondoa uovu miongoni mwenu.
8 observa diligenter ne incurras in plagam leprae sed facies quaecumque docuerint te sacerdotes levitici generis iuxta id quod praecepi eis et imple sollicite
Kuwa mwangalifu kuhusu kiini chochote cha ukoma, ili kwamba uwe makini katika kuchunguza na kufuata kila agizo linalopewa kwako ambalo makuhani, Walawi, wanakufundisha; kama nilivyowaamuru, ili utekeleze.
9 mementote quae fecerit Dominus Deus vester Mariae in via cum egrederemini de Aegypto
Kumbukeni nini Yahwe Mungu wako alichomfanya Miriam ulipokuwa ukitoka Misri.
10 cum repetes a proximo tuo rem aliquam quam debet tibi non ingredieris domum eius ut pignus auferas
Utoapo mkopo wa aina yoyote kwa jirani yako, hautakiwi kwenda ndani ya nyumba yake kutafuta dhamana yake.
11 sed stabis foris et ille tibi proferet quod habuerit
Utasimama nje, na mwanamume aliyekopa kwako ataleta dhamana yake nje kwako.
12 sin autem pauper est non pernoctabit apud te pignus
Iwapo ni mtu maskini, hautakiwi kulala na dhamana yake ikiwa mikononi mwako.
13 sed statim reddes ei ante solis occasum ut dormiens in vestimento suo benedicat tibi et habeas iustitiam coram Domino Deo tuo
Hakika unapaswa kumrejeshea dhamana yake kabla jua halijazama, ili aweze kulala ndani ya vazi lake na akubariki; itakuwa utakatifu kwako mbele za Yahwe Mungu wako.
14 non negabis mercedem indigentis et pauperis fratris tui sive advenae qui tecum moratur in terra et intra portas tuas est
Hautakiwi kumuonea mtumishi wa kuajiriwa ambaye ni maskini na mhitaji, hata kama ni jamaa wa Israeli, au ni kati ya wageni mbao wamo katika nchi ndani ya malango ya mji wako;
15 sed eadem die reddes ei pretium laboris sui ante solis occasum quia pauper est et ex eo sustentat animam suam ne clamet contra te ad Dominum et reputetur tibi in peccatum
Kila siku unapaswa kumlipa mshahara wake; jua halipaswi kuzama kabla ya suala hili kutatuliwa, kwa maana ni maskini na anautegemea. Fanya hivi ili asilie dhidi yako kwa Yahwe, na kwamba isiwe ikawa dhambi ambayo umeitenda.
16 non occidentur patres pro filiis nec filii pro patribus sed unusquisque pro suo peccato morietur
Wazazi hawapaswi kuuwawa kwa niaba ya watoto wao, na wala watoto hawapaswi kuuawa kwa niaba ya wazazi wao. Badala yake, kila mtu anapaswa kuuwawa kwa dhambi yake mwenyewe.
17 non pervertes iudicium advenae et pupilli nec auferes pignoris loco viduae vestimentum
Haupaswi kutumia nguvu kuchukua haki inayomhusu mgeni au yatima, wala kuchukua vazi la mjane kama dhamana.
18 memento quod servieris in Aegypto et eruerit te Dominus Deus tuus inde idcirco praecipio tibi ut facias hanc rem
Badala yake, unapaswa ukumbuke ya kwamba ulikuwa mtumwa Misri, na kwamba Yahwe Mungu wako alikukomboa kutoka kule. Kwa hiyo ninakuagiza kutii amri hii.
19 quando messueris segetem in agro tuo et oblitus manipulum reliqueris non reverteris ut tollas eum sed advenam et pupillum et viduam auferre patieris ut benedicat tibi Dominus Deus tuus in omni opere manuum tuarum
Utakapovuna zao lako shambani mwako, na ukasahau kipande cha mbegu shambani, haupaswi kurudi na kukichukua; kinapaswa kuwa cha mgeni, cha yatima, au cha mjane, ili Yahwe Mungu wako akubariki katika kazi ya mikono yako.
20 si fruges colliges olivarum quicquid remanserit in arboribus non reverteris ut colligas sed relinques advenae pupillo ac viduae
Utakapotikisa mti wako wa mzeituni, haupaswi kupanda juu ya matawi tena; itakuwa kwa ajili ya mgeni, kwa yatima na kwa mjane.
21 si vindemiaveris vineam tuam non colliges remanentes racemos sed cedent in usus advenae pupilli ac viduae
Utakapokusanya mizabibu shambani mwako, haupaswi kukusanya masazo yake tena. Kinachobaki kitakuwa cha mgeni, cha yatima na cha mjane.
22 memento quod et tu servieris in Aegypto et idcirco praecipiam tibi ut facias hanc rem
Unatakiwa ukumbuke kuwa ulikuwa mtumwa katika nchi ya Misri; kwa hiyo nakuagiza kutii amri hii.

< Deuteronomii 24 >