< Iohannis Iii 1 >

1 senior Gaio carissimo quem ego diligo in veritate
Mzee, kwa Gayo mpenzi, ninayempenda katika kweli.
2 carissime de omnibus orationem facio prospere te ingredi et valere sicut prospere agit anima tua
Mpendwa, nakuombea ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya njema, kama vile roho yako inavyofanikiwa.
3 gavisus sum valde venientibus fratribus et testimonium perhibentibus veritati tuae sicut tu in veritate ambulas
Maana nilifurahi sana wakati nilipoambiwa na ndugu waliokuja na kutoa ushuhuda juu ya kweli yako, kama vile unavyoenenda katika kweli.
4 maiorem horum non habeo gratiam quam ut audiam filios meos in veritate ambulantes
Sina furaha kubwa zaidi ya hii, kusikia kwamba watoto wangu wanatembea katika kweli.
5 carissime fideliter facis quicquid operaris in fratres et hoc in peregrinos
Mpendwa, unaenenda kwa uaminifu unapowahudumia ndugu na wageni,
6 qui testimonium reddiderunt caritati tuae in conspectu ecclesiae quos bene facies deducens digne Deo
ambao wametoa ushuhuda wa upendo wako mbele ya kanisa. Unafanya vizuri kuwasafirisha katika safari zao kwa namna ambayo inampendeza Mungu.
7 pro nomine enim profecti sunt nihil accipientes a gentibus
Kwa sababu kwa ajili ya Jina, walienda bila kuchukua kitu chochote kutoka kwa watu wa Mataifa.
8 nos ergo debemus suscipere huiusmodi ut cooperatores simus veritatis
Hivyo, tunatakiwa kuwakaribisha watu kama hawa, ili tuwe watenda kazi wenza kwa ajili ya kweli.
9 scripsissem forsitan ecclesiae sed is qui amat primatum gerere in eis Diotrepes non recipit nos
Nililiandikia kusanyiko jambo fulani, lakini Diotrofe, anayependa kuwa wa kwanza miongoni mwao, hakubaliani na sisi.
10 propter hoc si venero commoneam eius opera quae facit verbis malignis garriens in nos et quasi non ei ista sufficiant nec ipse suscipit fratres et eos qui cupiunt prohibet et de ecclesia eicit
Hivyo, kama nikija nitayakumbuka matendo yake anayoyafanya, jinsi anavyosema maneno mabaya kinyume nasi. Hajaridhika na matendo haya, yeye mwenyewe hawapokei ndugu. Hata huwakataza wengine ambao wanatamani kuwakaribisha hao ndugu na kuwafukuza watoke kwenye kusanyiko.
11 carissime noli imitari malum sed quod bonum est qui benefacit ex Deo est qui malefacit non vidit Deum
Mpenzi, usiige kilicho kibaya, bali iga kilicho chema. Yeye atendaye mema ni wa Mungu; na yeye atendaye mabaya hajamwona Mungu.
12 Demetrio testimonium redditur ab omnibus et ab ipsa veritate et nos autem testimonium perhibemus et nosti quoniam testimonium nostrum verum est
Demetrio ameshuhudiwa na wote na kweli yenyewe. sisi pia ni mashahidi, na unajua kuwa ushahuhuda wetu ni wa kweli.
13 multa habui scribere tibi sed nolui per atramentum et calamum scribere tibi
Ninayo mambo mengi ya kukuandikia, lakini sipendi kukuandikia kwa kalamu na wino.
14 spero autem protinus te videre et os ad os loquemur pax tibi salutant te amici saluta amicos per nomen
Bali ninatarajia kukuona hivi karibuni, na tutaongea nawe ana kwa ana. Amani iwe pamoja nawe. Marafiki wanakusalimu. Wasalimu marafiki kila mmoja kwa jina lake.

< Iohannis Iii 1 >