< Timotheum Ii 2 >

1 tu ergo fili mi confortare in gratia quae est in Christo Iesu
Kwa hiyo, wewe mwanangu, utiwe nguvu katika neema iliyondani ya Kristo Yesu.
2 et quae audisti a me per multos testes haec commenda fidelibus hominibus qui idonei erunt et alios docere
Na mambo uliyoyasikia kwangu miongoni mwa mashahidi wengi, uyakabidhi kwa watu waaminifu ambao wataweza kuwafundisha wengine pia.
3 labora sicut bonus miles Christi Iesu
Shiriki mateso pamoja nami, kama askari mwema wa Kristo Yesu.
4 nemo militans inplicat se negotiis saecularibus ut ei placeat cui se probavit
Hakuna askari atumikae wakati huo huo akijihusisha na shughuli za kawaida za maisha haya, ili kwamba ampendeze ofisa wake mkuu.
5 nam et qui certat in agone non coronatur nisi legitime certaverit
Pia kama mtu akishindana kama mwanariadha, hatapewa taji asiposhindana kwa kufuata kanuni.
6 laborantem agricolam oportet primum de fructibus accipere
Ni Muhimu kwamba mkulima mwenye bidii awe wa kwanza kupokea mgao wa mazao yake.
7 intellege quae dico dabit enim tibi Dominus in omnibus intellectum
Tafakari kuhusu nisemacho, kwa maana Bwana atakupa uelewa katika mambo yote.
8 memor esto Iesum Christum resurrexisse a mortuis ex semine David secundum evangelium meum
Mkumbuke Yesu Kristo, kutoka uzao wa Daudi, ambaye alifufuliwa kutoka kwa wafu. Hii ni kulingana na ujumbe wangu wa Injili,
9 in quo laboro usque ad vincula quasi male operans sed verbum Dei non est alligatum
ambao kwa sababu ya huo ninateswa hata kufungwa minyororo kama mhalifu. Lakini neno la Mungu halifungwi kwa minyororo.
10 ideo omnia sustineo propter electos ut et ipsi salutem consequantur quae est in Christo Iesu cum gloria caelesti (aiōnios g166)
Kwa hiyo, navumilia mambo yote kwa ajili ya wale ambao Mungu amekwishawachagua, ili kwamba nao pia waupate wokovu ulio katika Kristo Yesu pamoja na utukufu wa milele. (aiōnios g166)
11 fidelis sermo nam si conmortui sumus et convivemus
Usemi huu ni wakuaminika: “Ikiwa tumekufa pamoja naye, tutaishi pamoja naye pia,
12 si sustinemus et conregnabimus si negabimus et ille negabit nos
kama tukivumilia, tutatawala pamoja naye pia, kama tukimkana yeye, naye pia atatukana sisi.
13 si non credimus ille fidelis manet negare se ipsum non potest
kama hatutakuwa waaminifu, yeye atabaki kuwa mwaminifu, maana hawezi kujikana mwenyewe.”
14 haec commone testificans coram Domino noli verbis contendere in nihil utile ad subversionem audientium
Endelea kuwakumbusha juu ya mambo haya. Waonye mbele za Mungu waache kubishana kuhusu maneno. Kwa sababu hakuna manufaa katika jambo hili. Kutokana na hili kuna uharibifu kwa wale wanaosikiliza.
15 sollicite cura te ipsum probabilem exhibere Deo operarium inconfusibilem recte tractantem verbum veritatis
Fanya bidii kujionesha kuwa umekubalika kwa Mungu kama mtenda kazi asiye na sababu ya kulaumiwa. Litumie neno la kweli kwa usahihi.
16 profana autem inaniloquia devita multum enim proficient ad impietatem
Jiepushe na majadiliano ya kidunia, ambayo huongoza kwa zaidi na zaidi ya uasi.
17 et sermo eorum ut cancer serpit ex quibus est Hymeneus et Philetus
Majadiliano yao yatasambaa kama donda ndugu. Miongoni mwao ni Himenayo na Fileto.
18 qui a veritate exciderunt dicentes resurrectionem iam factam et subvertunt quorundam fidem
Hawa ni watu walioukosa ukweli. Wanasema ya kuwa ufufuo tayari umishatokea. Wanapindua imani ya baadhi ya watu.
19 sed firmum fundamentum Dei stetit habens signaculum hoc cognovit Dominus qui sunt eius et discedat ab iniquitate omnis qui nominat nomen Domini
Hata hivyo, msingi imara wa Mungu unasimama, wenye uandishi huu, “Bwana anawajua walio wake, na kila alitajaye jina la Bwana ni lazima ajitenge na udhalimu.”
20 in magna autem domo non solum sunt vasa aurea et argentea sed et lignea et fictilia et quaedam quidem in honorem quaedam autem in contumeliam
Kwenye nyumba ya kitajiri, siyo kwamba vimo vyombo vya dhahabu na shaba tu. Pia kuna vyombo vya miti na udongo. Baadhi ya hivi ni kwa ajili ya matumizi ya heshima na baadhi yake ni kwa matumizi yasiyo ya heshima.
21 si quis ergo emundaverit se ab istis erit vas in honorem sanctificatum et utile Domino ad omne opus bonum paratum
Ikiwa mtu atajitakasa mwenyewe kutoka kwenye matumizi yasiyo ya heshima, yeye ni chombo chenye kuheshimika. Ametengwa maalumu, mwenye manufaa kwa Bwana, na ameandaliwa kwa kila kazi njema.
22 iuvenilia autem desideria fuge sectare vero iustitiam fidem caritatem pacem cum his qui invocant Dominum de corde puro
Zikimbie tamaa za ujanani. Ukifuata haki, imani, upendo na amani pamoja na wale wamwitao Bwana kwa moyo safi.
23 stultas autem et sine disciplina quaestiones devita sciens quia generant lites
Lakini ukatae upumbavu na maswali ya kipuuzi. Kwani unajua ya kuwa huzaa ugomvi.
24 servum autem Domini non oportet litigare sed mansuetum esse ad omnes docibilem patientem
Mtumishi wa Bwana hapaswi kugombana, badala yake inampasa kuwa mpole kwa watu wote, awezaye kufundisha, na mvumilivu.
25 cum modestia corripientem eos qui resistunt nequando det illis Deus paenitentiam ad cognoscendam veritatem
Ni lazima awaelimishe kwa upole wale wampingao. Yamkini Mungu aweze kuwapatia toba kwa kuifahamu kweli.
26 et resipiscant a diaboli laqueis a quo capti tenentur ad ipsius voluntatem
Waweze kupata ufahamu tena na kuepuka mtego wa Shetani, baada ya kuwa wametekwa na yeye kwa ajili ya mapenzi yake.

< Timotheum Ii 2 >