< Corinthios I 8 >
1 de his autem quae idolis sacrificantur scimus quia omnes scientiam habemus scientia inflat caritas vero aedificat
Sasa kuhusu vyakula vilivyotolewa sadaka kwa sanamu: tunajua ya kwamba “sisi sote tuna maarifa.” Maarifa huleta majivuno, bali upendo hujenga.
2 si quis se existimat scire aliquid nondum cognovit quemadmodum oporteat eum scire
Ikiwa mtu yeyote anadhani kwamba anajua jambo fulani, mtu huyo bado hajui kama impasavyo kujua.
3 si quis autem diligit Deum hic cognitus est ab eo
Lakini ikiwa mmoja wapo akimpenda Mungu, mtu huyo anajulikana naye.
4 de escis autem quae idolis immolantur scimus quia nihil est idolum in mundo et quod nullus Deus nisi unus
Basi kuhusu kula vyakula vilivyotolewa sadaka kwa sanamu: twajua kuwa “sanamu si kitu katika dunia hii,” na ya kuwa hakuna Mungu ila mmoja tu.”
5 nam et si sunt qui dicantur dii sive in caelo sive in terra siquidem sunt dii multi et domini multi
Kwa maana kuna wengi waitwao miungu ikiwa ni mbinguni au duniani, kama vile walivyo “miungu na mabwana wengi.”
6 nobis tamen unus Deus Pater ex quo omnia et nos in illum et unus Dominus Iesus Christus per quem omnia et nos per ipsum
“Ijapokuwa kwetu kuna Mungu mmoja tu ambaye ni Baba, vitu vyote vimetoka kwake, nasi tunaishi kwake, na Bwana mmoja Yesu Kristo, ambaye kwake vitu vyote vimekuwapo, na kwa yeye sisi tupo.”
7 sed non in omnibus est scientia quidam autem conscientia usque nunc idoli quasi idolothytum manducant et conscientia ipsorum cum sit infirma polluitur
Hata hivyo, ujuzi huu haupo ndani ya kila mmoja. Badala yake, wengine walishiriki ibada za sanamu hapo zamani, na hata sasa wanakula vyakula hivi kana kwamba ni kitu kilichotolewa sadaka kwa sanamu. Dhamiri zao zimepotoshwa kwa kuwa ni dhaifu.
8 esca autem nos non commendat Deo neque si non manducaverimus deficiemus neque si manducaverimus abundabimus
Lakini chakula hakitatuthibitisha sisi kwa Mungu. Sisi sio wabaya sana kama tusipo kula, wala wema sana ikiwa tutakula.
9 videte autem ne forte haec licentia vestra offendiculum fiat infirmibus
Lakini iweni makini ya kwamba uhuru wenu usiwe sababu ya kumkwaza aliye dhaifu katika imani.
10 si enim quis viderit eum qui habet scientiam in idolio recumbentem nonne conscientia eius cum sit infirma aedificabitur ad manducandum idolothyta
Hebu fikiri kwamba mtu amekuona, wewe uliye na ujuzi, unakula chakula katika hekalu la sanamu. Dhamiri yake mtu huyo haitathibitika hata yeye naye ale vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu?
11 et peribit infirmus in tua scientia frater propter quem Christus mortuus est
Kwa hiyo kwa sababu ya ufahamu wako wa ukweli juu ya asili ya sanamu, kaka au dada yako aliye dhaifu, ambaye pia Kristo alikufa kwa ajili yake, anaangamizwa.
12 sic autem peccantes in fratres et percutientes conscientiam eorum infirmam in Christo peccatis
Hivyo, unapofanya dhambi dhidi ya kaka na dada zako na kuzijeruhi dhamiri zao zilizo dhaifu, mnatenda dhambi dhidi ya Kristo.
13 quapropter si esca scandalizat fratrem meum non manducabo carnem in aeternum ne fratrem meum scandalizem (aiōn )
Kwa hiyo, ikiwa chakula kinasababisha kumkwaza kaka au dada, sitakula nyama kamwe, ili nisimsababishe kaka au dada yangu kuanguka. (aiōn )