< Corinthios I 5 >

1 omnino auditur inter vos fornicatio et talis fornicatio qualis nec inter gentes ita ut uxorem patris aliquis habeat
Tumesikia taarifa kuwa kuna zinaa miongoni mwenu, aina ya zinaa ambayo haipo hata katikati ya watu wa Mataifa. Tuna taarifa kwamba mmoja wenu analala na mke wa baba yake.
2 et vos inflati estis et non magis luctum habuistis ut tollatur de medio vestrum qui hoc opus fecit
Nanyi mwajisifu! Badala ya kuhuzunika? Yule aliyefanya hivyo anapaswa kuondolewa miongoni mwenu.
3 ego quidem absens corpore praesens autem spiritu iam iudicavi ut praesens eum qui sic operatus est
Ingawa sipo pamoja nanyi kimwili lakini nipo nanyi kiroho, nimekwisha mhukumu yeye aliyefanya hivi, kama vile nilikuwepo.
4 in nomine Domini nostri Iesu Christi congregatis vobis et meo spiritu cum virtute Domini Iesu
Mnapokutanika pamoja katika jina la Bwana wetu Yesu, na roho yangu ipo pale kama kwa nguvu za Bwana wetu Yesu, nimekwisha mhukumu mtu huyu.
5 tradere huiusmodi Satanae in interitum carnis ut spiritus salvus sit in die Domini Iesu
Nimekwisha kumkabidhi mtu huyu kwa Shetani ili kwamba mwili wake uharibiwe, ili roho yake iweze kuokolewa katika siku ya Bwana.
6 non bona gloriatio vestra nescitis quia modicum fermentum totam massam corrumpit
Majivuno yenu si kitu kizuri. Hamjui chachu kidogo huharibu donge zima?
7 expurgate vetus fermentum ut sitis nova consparsio sicut estis azymi etenim pascha nostrum immolatus est Christus
Jisafisheni ninyi wenyewe chachu ya kale, ili kwamba muwe donge jipya, ili kwamba mwe mkate usiochachuliwa. Kwa kuwa, Kristo, Mwana Kondoo wetu wa pasaka amekwisha kuchinjwa.
8 itaque epulemur non in fermento veteri neque in fermento malitiae et nequitiae sed in azymis sinceritatis et veritatis
Kwa hiyo tusherekee karamu si kwa chachu ya kale, chachu ya tabia mbaya na uovu. Badala yake, tusherekee na mkate usiotiwa chachu wa unyenyekevu na kweli.
9 scripsi vobis in epistula ne commisceamini fornicariis
Niliandika katika barua yangu kuwa msichangamane na wazinzi.
10 non utique fornicariis huius mundi aut avaris aut rapacibus aut idolis servientibus alioquin debueratis de hoc mundo exisse
Sina maana wazinzi wa dunia hii, au na wenye tamaa au wanyang'anyi au waabudu sanamu kwa kukaa mbali nao, basi ingewapasa mtoke duniani.
11 nunc autem scripsi vobis non commisceri si is qui frater nominatur est fornicator aut avarus aut idolis serviens aut maledicus aut ebriosus aut rapax cum eiusmodi nec cibum sumere
Lakini sasa nawaandikia kutojichanganya na yeyote anayeitwa kaka au dada katika Kristo, lakini anaishi katika uzinzi au ambaye ni mwenye kutamani, au mnyang'anyi, au mwabudu sanamu, au mtukanaji au mlevi. Wala msile naye mtu wa namna ile.
12 quid enim mihi de his qui foris sunt iudicare nonne de his qui intus sunt vos iudicatis
Kwa hiyo nitajihusishaje kuwahukumu walio nje ya Kanisa? Badala yake, ninyi hamkuwahukumu walio ndani ya kanisa?
13 nam eos qui foris sunt Deus iudicabit auferte malum ex vobis ipsis
Lakini Mungu anawahukumu walio nje. “Mwondoeni mtu mwovu miongoni mwenu”

< Corinthios I 5 >