< Corinthios I 4 >
1 sic nos existimet homo ut ministros Christi et dispensatores mysteriorum Dei
Hivi ndivyo mtu atuhesabu sisi, kama watumishi wa Kristo na mawakili wa siri za kweli za Mungu.
2 hic iam quaeritur inter dispensatores ut fidelis quis inveniatur
Katika hili, kinachotakiwa kwa uwakili ni kwamba wawe wa kutumainiwa.
3 mihi autem pro minimo est ut a vobis iudicer aut ab humano die sed neque me ipsum iudico
Lakini kwangu mimi ni kitu kidogo sana kuwa ninahukumiwa na ninyi au hukumu ya kibinadamu. Kwa kuwa sijihukumu hata mimi mwenyewe.
4 nihil enim mihi conscius sum sed non in hoc iustificatus sum qui autem iudicat me Dominus est
Sijihukumu mimi mwenyewe, hii haina maana kuwa mimi ni mwenye haki. Ni Bwana anihukumuye.
5 itaque nolite ante tempus iudicare quoadusque veniat Dominus qui et inluminabit abscondita tenebrarum et manifestabit consilia cordium et tunc laus erit unicuique a Deo
Kwa hiyo, msitamke hukumu juu ya lolote kabla ya wakati, kabla ya kuja kwa Bwana. Atayaleta nuruni mambo yaliyofichika gizani na kufunua makusudi ya mioyo. Ndipo kila mmoja atapokea sifa yake kutoka kwa Mungu.
6 haec autem fratres transfiguravi in me et Apollo propter vos ut in nobis discatis ne supra quam scriptum est unus adversus alterum infletur pro alio
Sasa, kaka na dada zangu, mimi mwenyewe na Apolo nimetumia kanuni hizi kwa ajili yenu. Ili kwamba kutoka kwetu mnaweza kujifunza maana ya usemi, “Usiende zaidi ya kilivyoandikwa.” Hii ni kwamba hakuna mmoja wenu ajivunaye juu ya mwingine.
7 quis enim te discernit quid autem habes quod non accepisti si autem accepisti quid gloriaris quasi non acceperis
Maana ni nani aonaye tofauti kati yenu na mwingine? Ni nini ulicho nacho hukukipokea bure? Kama umekwisha kupokea bure, kwa nini mnajivuna kama hamkufanya hivyo?
8 iam saturati estis iam divites facti estis sine nobis regnastis et utinam regnaretis ut et nos vobiscum regnaremus
Tayari mnavyo vyote ambavyo mngetaka! Tayari mmekuwa na utajiri! Mmeanza kutawala-na kwamba mnamiliki zaidi yetu sisi! Kweli, nawatakia umililki mwema ili kwamba tumiliki pamoja nanyi.
9 puto enim Deus nos apostolos novissimos ostendit tamquam morti destinatos quia spectaculum facti sumus mundo et angelis et hominibus
Kwa hiyo ninadhani Mungu ametuweka sisi mitume kama kutuonyesha wa mwisho katika mustari wa maandamano na kama watu waliohukumiwa kuuawa. Tumekuwa kama tamasha kwa ulimwengu, kwa malaika na kwa wanadamu.
10 nos stulti propter Christum vos autem prudentes in Christo nos infirmi vos autem fortes vos nobiles nos autem ignobiles
Sisi ni wajinga kwa ajili ya Kristo, lakini ninyi ni wenye hekima katika Kristo. Tu wanyonge, lakini ninyi mna nguvu. Mnaheshimiwa, lakina sisi tunadharauliwa.
11 usque in hanc horam et esurimus et sitimus et nudi sumus et colaphis caedimur et instabiles sumus
Hata saa hii tuna njaa na kiu, hatuna nguo, tuna mapigo, na tena hatuna makazi.
12 et laboramus operantes manibus nostris maledicimur et benedicimus persecutionem patimur et sustinemus
Tunafanya kazi kwa bidii, kwa mikono yetu wenyewe. Tunapodharauliwa, twabariki. Wakati tunapoteswa, twavumilia.
13 blasphemamur et obsecramus tamquam purgamenta huius mundi facti sumus omnium peripsima usque adhuc
Tunapotukanwa, twarudisha kwa upole. Tumekuwa, na tu bado tunahesabiwa kuwa kama kukataliwa na dunia na takataka kwa mambo yote.
14 non ut confundam vos haec scribo sed ut filios meos carissimos moneo
Siandiki mambo haya kuwaaibisha ninyi, lakini kuwarudi ninyi kama watoto wangu niwapendao.
15 nam si decem milia pedagogorum habeatis in Christo sed non multos patres nam in Christo Iesu per evangelium ego vos genui
Hata kama mna waalimu makumi elfu katika Kristo, hamna baba wengi. Kwa kuwa nimekuwa baba yenu katika Yesu Kristo kupitia injili.
16 rogo ergo vos imitatores mei estote
Hivyo ninawasihi mniige mimi.
17 ideo misi ad vos Timotheum qui est filius meus carissimus et fidelis in Domino qui vos commonefaciat vias meas quae sunt in Christo sicut ubique in omni ecclesia doceo
Hiyo ndiyo sababu nilimtuma kwenu Timotheo, mpendwa wangu na mtoto mwaminifu katika Bwana. Atawakumbusheni njia zangu katika Kristo, kama ninavyofundisha kila mahali na kila kanisa.
18 tamquam non venturus sim ad vos sic inflati sunt quidam
Sasa baadhi yenu wanajisifu, wakitenda kana kwamba sitakuja kwenu.
19 veniam autem cito ad vos si Dominus voluerit et cognoscam non sermonem eorum qui inflati sunt sed virtutem
Lakini nitakuja kwenu kitambo, kama Bwana akipenda. Ndipo nitajua si maneno yao tu wanaojisifu, lakini nitaona nguvu zao.
20 non enim in sermone est regnum Dei sed in virtute
Kwa kuwa ufalme wa Mungu hauwi katika maneno bali katika nguvu.
21 quid vultis in virga veniam ad vos an in caritate et spiritu mansuetudinis
Mnataka nini? Nije kwenu na fimbo au kwa upendo na katika roho ya upole?