< I Paralipomenon 25 >

1 igitur David et magistratus exercitus secreverunt in ministerium filios Asaph et Heman et Idithun qui prophetarent in citharis et psalteriis et cymbalis secundum numerum suum dedicato sibi officio servientes
Daudi na viongozi wa wafanyakazi wa hema la kuabudia walichaguliwa kwa kazi baadhi walikuwa wana wa Asafu, Hemani, na Yeduthuni. Wanaume hawa walitabiri kwa vinubi, vifaa vya uzi, na upatu. Hii ni orodha ya wanaume walioifanya hii kazi:
2 de filiis Asaph Zacchur et Ioseph et Nathania et Asarela filii Asaph sub manu Asaph prophetantis iuxta regem
Kutoka wana wa Asafu: Zakuri, Yosefu, Nethania, na Asharela, wana wa Asafu, chini ya mwongozo wa Asafu, ambaye alitabiri chini ya uwangalizi wa mfalme.
3 porro Idithun filii Idithun Godolias Sori Iesaias et Sabias et Matthathias sex sub manu patris sui Idithun qui in cithara prophetabat super confitentes et laudantes Dominum
Kutoka wana wa Yeduthuni: Gedalia, Zeri, Yeshaia, Shimei, Hashabia, na Matithia, sita kwa ujumla, chini ya mwongozo wa baba yao Yeduthuni, ambaye alipiga kinubi kwa kutoa shukurani na kumsifu Yahweh.
4 Heman quoque filii Heman Bocciau Matthaniau Ozihel Subuhel et Ierimoth Ananias Anani Elietha Geddelthi et Romemthiezer et Iesbacasa Mellothi Othir Mazioth
Kutoka wana wa Hemani: Bukia, Matania, Uzieli, Shebueli, na yerimothi, Hanania, Hanani, Eliatha, Gidalti, Romamti Ezeri, yoshibekasha, Mallothi, Hothiri, na Mahaziothi.
5 omnes isti filii Heman videntis regis in sermonibus Dei ut exaltaret cornu deditque Deus Heman filios quattuordecim et filias tres
Hawa wote walikuwa wana wa Hemani mfalme wa manabii. Mungu alimpa Hemani wana kumi na nne na mabinti watatu kwa ajili ya kumpa heshima.
6 universi sub manu patris sui ad cantandum in templo Domini distributi erant in cymbalis et psalteriis et citharis in ministeria domus Domini iuxta regem Asaph videlicet et Idithun et Heman
Hawa wote walikuwa chini ya mwongozo wa baba yao. Walikuwa ni waimbaji katika nyumba ya Yahweh, pamoja na upatu na vifaa vya uzi walivyohudumu katika nyumba ya Mungu. Asafu, Yeduthuni, na Hemani walikuwa chini ya uwangalizi wa mfalme.
7 fuit autem numerus eorum cum fratribus suis qui erudiebant canticum Domini cuncti doctores ducenti octoginta octo
Wao na kaka zao walikuwa na uwelewa na walifundishwa kutengeneza muziki kwa Yahweh walikuwa na idadi ya 288.
8 miseruntque sortes per vices suas ex aequo tam maior quam minor doctus pariter et indoctus
Walirusha kura kwa majukumu yao, wote sawa, sawa kwa vijana na kwa wazee, kwa walimua na kwa wanafunzi.
9 egressaque est sors prima Ioseph qui erat de Asaph secunda Godoliae ipsi et filiis eius et fratribus duodecim
Sasa kuhusu wana wa Asafu: kura ya kwanza iliangukia katika familia ya Yusufu; ya pili iliangukia katika familia ya Gedalia, idadi ya watu kumi na mbili;
10 tertia Zacchur filiis et fratribus eius duodecim
ya tatu iliangukia kwa Zakuri, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
11 quarta Isari filiis et fratribus eius duodecim
ya nne iliangukia kwa Izri, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
12 quinta Nathaniae filiis et fratribus eius duodecim
ya tano iliangukia kwa Nethania, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
13 sexta Bocciau filiis et fratribus eius duodecim
ya sita iliangukia kwa Bukia, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
14 septima Israhela filiis et fratribus eius duodecim
ya saba iliangukia kwa Yesharela, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
15 octava Isaiae filiis et fratribus eius duodecim
ya nane iliangukia kwa Yeshaia, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
16 nona Matthaniae filiis et fratribus eius duodecim
ya tisa iliangukia kwa Matania, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
17 decima Semeiae filiis et fratribus eius duodecim
ya kumi iliangukia kwa Shimei, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
18 undecima Ezrahel filiis et fratribus eius duodecim
ya kumi na moja iliangukia kwa Azareli, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
19 duodecima Asabiae filiis et fratribus eius duodecim
ya kumi na mbili iliangukia kwa Hashabia, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
20 tertiadecima Subahel filiis et fratribus eius duodecim
ya kumi na tatu iliangukia kwa Shubaeli, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
21 quartadecima Matthathiae filiis et fratribus eius duodecim
ya kumi na nne iliangukia kwa Matithia, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
22 quintadecima Ierimoth filiis et fratribus eius duodecim
ya kumi na tano iliangukia kwa Yeromothi, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
23 sextadecima Ananiae filiis et fratribus eius duodecim
ya kumi na sita iliangukia kwa Hanania, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
24 septimadecima Iesbocasae filiis et fratribus eius duodecim
ya kumi na saba iliangukia kwa Yoshibekasha, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
25 octavadecima Anani filiis et fratribus eius duodecim
ya kumi na nane iliangukia kwa Hanani, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
26 nonadecima Mellothi filiis et fratribus eius duodecim
ya kumi na tisa iliangukia kwa Malothi, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
27 vicesima Eliatha filiis et fratribus eius duodecim
ya ishirini iliangukia kwa Eliatha, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
28 vicesima prima Othir filiis et fratribus eius duodecim
ya ishirini na moja iliangukia kwa Hothiri, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
29 vicesima secunda Godollathi filiis et fratribus eius duodecim
ya ishirini na mbili iliangukia kwa Gidalti, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
30 vicesima tertia Maziuth filiis et fratribus eius duodecim
ya ishirini na tatu iliangukia kwa Mahaziothi, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
31 vicesima quarta Romamthiezer filiis et fratribus eius duodecim
ya ishirini na nne iliangukia kwa Romamti Eza, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili.

< I Paralipomenon 25 >