< Romanos 16 >
1 Commendo autem vobis Phoeben sororem nostram, quae est in ministerio Ecclesiae, quae est in Cenchris:
Namkabidhi kwenu Fibi dada yetu, ambaye ni mtumishi wa kanisa ambalo liko Kenkrea,
2 ut eam suscipiatis in Domino digne sanctis: et assistatis ei in quocumque negotio vestri indiguerit: etenim ipsa quoque astitit multis, et mihi ipsi.
ili kwamba mnaweza kumpokea katika Bwana. Fanyeni hivi katika kicho cha thamani cha waumini, na msimame pamoja naye katika jambo lolote atakalokuwa na uhitaji nalo. Maana yeye mwenyewe amekuwa mhudumu wa wengi, na kwa ajili yangu mwenyewe.
3 Salutate Priscam, et Aquilam adiutores meos in Christo Iesu;
Msalimu Priska na Akila, watenda kazi pamoja nami katika Kristo Yesu,
4 (qui pro anima mea suas cervices supposuerunt: quibus non solus ego gratias ago, sed et cunctae ecclesiae Gentium)
ambao kwa maisha yangu waliyahatarisha maisha yao wenyewe. Ninatoa shukrani kwao, na siyo tu mimi, bali pia kwa makanisa yote ya mataifa.
5 et domesticam Ecclesiam eorum. Salutate Ephaenetum dilectum mihi, qui est primitivus Ecclesiae Asiae in Christo Iesu.
Lisalimie kanisa ambalo liko nyumbani kwao. Msalimie Epanieto mpendwa wangu, ambaye ni mzaliwa wa kwanza wa Kristo katika Asia.
6 Salutate Mariam, quae multum laboravit in nobis.
Msalimie Mariamu ambaye ametenda kazi kwa bidii kwa ajili yenu.
7 Salutate Andronicum, et Iuliam cognatos, et concaptivos meos: qui sunt nobiles in Apostolis, qui et ante me fuerunt in Christo.
Msalimie Androniko na Yunia, jamaa zangu, na wafungwa pamoja nami. Ni wa muhimu miongoni mwa mitume, ambao pia walitangulia kumjua Kristo kabla yangu.
8 Salutate Ampliatum dilectissimum mihi in Domino.
Msalimie Ampliato, mpendwa wangu katika Bwana.
9 Salutate Urbanum adiutorem nostrum in Christo Iesu, et Stachyn dilectum meum.
Msalimie Urbano, mtenda kazi pamoja nami katika Kristo, na Stakisi mpendwa wangu.
10 Salutate Apellen probum in Christo.
Msalimie Apele, mwenye kukubaliwa katika Kristo. Wasalimie wote ambao walio katika nyumba ya Aristobulo.
11 Salutate eos, qui sunt ex Aristoboli domo. Salutate Herodionem cognatum meum. Salutate eos, qui sunt ex Narcissi domo, qui sunt in Domino.
Nisalimie Herodioni, jamaa yangu. Nisalimie wote walio katika nyumba ya Narkiso, ambao wako katika Bwana.
12 Salutate Tryphaenam, et Tryphosam: quae laborant in Domino. Salutate Persidem charissimam, quae multum laboravit in Domino.
Nisalimie Trifaina na Trifosa, wanaotenda kazi kwa bidii katika Bwana. msalimie Persisi mpendwa, ambaye ametenda kazi zaidi kwa Bwana,
13 Salutate Rufum electum in Domino, et matrem eius, et meam.
Nisalimie Rufo, aliyechaguliwa katika Bwana na mama yake na wangu.
14 Salutate Asyncritum, Phlegontem, Hermam, Patrobam, Hermen: et qui cum eis sunt, fratres.
Msalimie Asinkrito, Flegon, Herme, Patroba, Herma, na ndugu wote walio pamoja nao.
15 Salutate Philologum, et Iuliam, Nereum, et sororem eius, et Olympiadem, et omnes, qui cum eis sunt, sanctos.
Nisalimie Filologo naYulia, Nerea na dada yake, na Olimpa, na waumini wote walio pamoja nao.
16 Salutate invicem in osculo sancto. Salutant vos omnes Ecclesiae Christi.
Nisalimie kila mmoja kwa busu takatifu. Makanisa yote katika Kristo yawasalimu.
17 Rogo autem vos fratres, ut observetis eos, qui dissensiones, et offendicula praeter doctrinam, quam vos didicistis, faciunt, et declinate ab illis.
Sasa nawasihi, ndugu, kutafakari juu ya hao ambao wanasababisha mgawanyiko na vipingamizi. Wanakwenda kinyume na mafundisho ambayo mmekwisha kujifunza. Geukeni mtoke kwao.
18 Huiuscemodi enim Christo Domino nostro non serviunt, sed suo ventri: et per dulces sermones, et benedictiones seducunt corda innocentium.
Kwa maana watu kama hawa hawamtumikii Kristo Bwana, bali matumbo yao wenyewe. Kwa maneno yao laini na pongezi za uongo wanadanganya mioyo ya wasio na hatia.
19 Vestra enim obedientia in omnem locum divulgata est. Gaudeo igitur in vobis. Sed volo vos sapientes esse in bono, et simplices in malo.
Kwa mfano wa utii wenu mwamfikia kila mmoja. Kwa hiyo, nafurahi juu yenu, lakini nawataka ninyi mwe na busara katika hali ya wema, na kutokuwa na hatia mbele ya uovu.
20 Deus autem pacis conterat Satanam sub pedibus vestris velociter. Gratia Domini nostri Iesu Christi vobiscum.
Mungu wa amani hatakawia kumwangamiza shetani chini ya nyayo zenu. Neema ya Bwana Yesu Kristo iwe pamoja nanyi.
21 Salutat vos Timotheus adiutor meus, et Lucius, et Iason, et Sosipater cognati mei.
Timotheo, mtendakazi pamoja nami, awasalimu, na Lukio, Yasoni na Sospeter, jamaa zangu.
22 Saluto vos ego Tertius, qui scripsi epistolam, in Domino.
Mimi, Tertio, niliyeuandika waraka huu, nawasalimu katika jina la Bwana.
23 Salutat vos Caius hospes meus, et universa Ecclesia. Salutat vos Erastus archarius civitatis, et Quartus, frater.
Gayo, aliyenitunza na kwa kanisa lote, lawasalimu. Erasto, mtunza hazina wa mji, awasalimu, pamoja na Kwarto aliye ndugu.
24 Gratia Domini nostri Iesu Christi cum omnibus vobis. Amen.
(Zingatia: Katika nakala halisi za kwanza, mstari huu haupo. Tazama Warumi 16: 20. “Neema ya Bwana Yesu Kristo ikae nanyi nyote. Amina.”)
25 Ei autem, qui potens est vos confirmare iuxta Evangelium meum, et praedicationem Iesu Christi, secundum revelationem mysterii temporibus aeternis taciti, (aiōnios )
Sasa kwake yeye aliye na uwezo kufanya msimame kulingana na injili na mafundisho ya Yesu Kristo, kulingana na ufunuo wa siri iliyofichwa kwa muda mrefu, (aiōnios )
26 (quod nunc patefactum est per Scripturas Prophetarum secundum praeceptum aeterni Dei, ad obeditionem fidei) in cunctis Gentibus cogniti, (aiōnios )
lakini sasa imekwisha funuliwa na kufanywa kujulikana na maandiko ya unabii kulingana na amri ya Mungu wa milele, kwa utii wa imani miongoni mwa mataifa yote? (aiōnios )
27 soli sapienti Deo, per Iesum Christum, cui honor, et gloria in saecula saeculorum. Amen. (aiōn )
Kwa Mungu pekee mwenye hekima, kupitia Yesu Kristo, kuwe na utukufu milele yote. Amina (aiōn )