< Proverbiorum 28 >

1 Fugit impius, nemine persequente: iustus autem quasi leo confidens, absque terrore erit.
Mtu mwovu hukimbia ingawa hakuna yeyote anayemfukuza, bali wenye haki ni wajasiri kama simba.
2 Propter peccata terrae multi principes eius: et propter hominis sapientiam, et horum scientiam quae dicuntur, vita ducis longior erit.
Wakati nchi inapokuwa na uasi, inakuwa na viongozi wengi, bali mwenye ufahamu na maarifa hudumisha utaratibu.
3 Vir pauper calumnians pauperes, similis est imbri vehementi, in quo paratur fames.
Mtu maskini amwoneaye yeye aliye maskini zaidi ni kama mvua ya dhoruba isiyosaza mazao.
4 Qui derelinquunt legem, laudant impium: qui custodiunt, succenduntur contra eum.
Wale waiachao sheria huwasifu waovu, bali wale waishikao sheria huwapinga.
5 Viri mali non cogitant iudicium: qui autem inquirunt Dominum, animadvertunt omnia.
Watu wabaya hawaelewi haki, bali wale wamtafutao Bwana wanaielewa kikamilifu.
6 Melior est pauper ambulans in simplicitate sua, quam dives in pravis itineribus.
Afadhali maskini ambaye mwenendo wake hauna lawama kuliko tajiri ambaye njia zake ni potovu.
7 Qui custodit legem, filius sapiens est: qui autem comessatores pascit, confundit patrem suum.
Yeye ashikaye sheria ni mwana mwenye ufahamu, bali rafiki wa walafi humwaibisha baba yake.
8 Qui coacervat divitias usuris et foenore liberali, in pauperes congregat eas.
Yeye aongezaye utajiri wake kwa riba kubwa mno hukusanya kwa ajili ya mwingine, ambaye atawahurumia maskini.
9 Qui declinat aures suas ne audiat legem, oratio eius erit execrabilis.
Kama mtu yeyote akikataa kusikia sheria, hata maombi yake ni chukizo.
10 Qui decipit iustos in via mala, in interitu suo corruet: et simplices possidebunt bona eius.
Yeye ambaye humwongoza mwenye haki kwenye mapito mabaya, ataanguka kwenye mtego wake mwenyewe, bali wasio na lawama watapokea urithi mwema.
11 Sapiens sibi videtur vir dives: pauper autem prudens scrutabitur eum.
Mtu tajiri anaweza kuwa na hekima machoni pake mwenyewe, bali mtu maskini mwenye ufahamu atamfichua.
12 In exultatione iustorum multa gloria est: regnantibus impiis ruinae hominum.
Mwenye haki ashindapo, kuna furaha kubwa, bali waovu watawalapo, watu hujificha.
13 Qui abscondit scelera sua, non dirigetur: qui autem confessus fuerit, et reliquerit ea, misericordiam consequetur.
Yeye afichaye dhambi zake hatafanikiwa, bali yeyote aziungamaye na kuziacha hupata rehema.
14 Beatus homo, qui semper est pavidus: qui vero mentis est durae, corruet in malum.
Amebarikiwa mtu ambaye siku zote humcha Bwana, bali yeye afanyaye moyo wake kuwa mgumu huangukia kwenye taabu.
15 Leo rugiens, et ursus esuriens, princeps impius super populum pauperem.
Kama simba angurumaye au dubu ashambuliaye, ndivyo alivyo mtu mwovu atawalaye wanyonge.
16 Dux indigens prudentia, multos opprimet per calumniam: qui autem odit avaritiam, longi fient dies eius.
Mtawala dhalimu hana akili, bali yeye achukiaye mapato ya udhalimu atafurahia maisha marefu.
17 Hominem, qui calumniatur animae sanguinem, si usque ad lacum fugerit, nemo sustinet.
Mtu mwenye kusumbuliwa na hatia ya kuua atakuwa mtoro mpaka kufa; mtu yeyote na asimsaidie.
18 Qui ambulat simpliciter, salvus erit: qui perversis graditur viis, concidet semel.
Yeye ambaye mwenendo wake hauna lawama hulindwa salama, bali yeye ambaye njia zake ni potovu ataanguka ghafula.
19 Qui operatur terram suam, satiabitur panibus: qui autem sectatur otium, replebitur egestate.
Yeye alimaye shamba lake atakuwa na chakula tele, bali yule afuataye mambo ya upuzi atakuwa na umaskini wa kumtosha.
20 Vir fidelis multum laudabitur: qui autem festinat ditari, non erit innocens.
Mtu mwaminifu atabarikiwa sana, bali yeye atamaniye kupata utajiri kwa haraka hataacha kuadhibiwa.
21 Qui cognoscit in iudicio faciem, non benefacit: iste et pro buccella panis deserit veritatem.
Kuonyesha upendeleo si vizuri, hata hivyo mtu atafanya kosa kwa kipande cha mkate.
22 Vir, qui festinat ditari, et aliis invidet, ignorat quod egestas superveniet ei.
Mtu mchoyo ana tamaa ya kupata utajiri, naye hana habari kuwa umaskini unamngojea.
23 Qui corripit hominem, gratiam postea inveniet apud eum magis quam ille, qui per linguae blandimenta decipit.
Yeye amkemeaye mtu mwishoni hupata kibali zaidi, kuliko mwenye maneno ya kusifu isivyostahili.
24 Qui subtrahit aliquid a patre suo, et a matre: et dicit hoc non esse peccatum, particeps homicidae est.
Yeye amwibiaye babaye au mamaye na kusema, “Si kosa,” yeye ni mwenzi wa yule aharibuye.
25 Qui se iactat, et dilatat, iurgia concitat: qui vero sperat in Domino, sanabitur.
Mtu mwenye tamaa huchochea fitina, bali yule amtegemeaye Bwana atafanikiwa.
26 Qui confidit in corde suo, stultus est: qui autem graditur sapienter, ipse laudabitur.
Yeye ajitumainiaye mwenyewe ni mpumbavu, bali yeye atembeaye katika hekima hulindwa salama.
27 Qui dat pauperi, non indigebit: qui despicit deprecantem, sustinebit penuriam.
Yeye ampaye maskini hatapungukiwa na kitu chochote, bali yeye awafumbiaye maskini macho hupata laana nyingi.
28 Cum surrexerint impii, abscondentur homines: cum illi perierint, multiplicabuntur iusti.
Wakati waovu watawalapo, watu huenda mafichoni, bali waovu wanapoangamia, wenye haki hufanikiwa.

< Proverbiorum 28 >