< Liber Numeri 9 >

1 Locutus est Dominus ad Moysen in deserto Sinai anno secundo, postquam egressi sunt de Terra Aegypti, mense primo dicens:
BWANA akanena na Musa katika katika jangwa la Sinai, mwezi wa kwanza wa mwaka wa pili baada ya kutoka katika nci ya Misri. Akasema,
2 Faciant filii Israel Phase in tempore suo,
“Wana wa Israeli wataikumbuka Pasaka katika wakati wake kila mwaka.
3 quartadecima die mensis huius ad vesperam, iuxta omnes ceremonias et iustificationes eius.
Siku ya kumi na nne ya mwezi huu, muda wa jioni, utaikumbuka Pasaka kila mwaka kwa muda uliopanggwa. Lazima uikumbuke, fuata taratibu zake zote na utii sheria zake zote zinazohusiana na tukio hilo.
4 Praecepitque Moyses filiis Israel ut facerent Phase.
Kwa hiyo, Musa akawaambia wana wa Isareli kuwa wataishika sikukuu ya Pasaka.
5 Qui fecerunt tempore suo: quartadecima die mensis ad vesperam in monte Sinai. Iuxta omnia quae mandaverat Dominus Moysi, fecerunt filii Israel.
Kwa hiyo wakaishika sikuu ya Pasaka katika mwezi wa kwanza, wakati wa jioni wa siku ya kumi na nne ya mwezi katika jangwa la Sinai. Wana wa Israeli walitii kila kitu ambacho BWANA alimwamuru Musa kukifanya.
6 Ecce autem quidam immundi super anima hominis, qui non poterant facere Phase in die illo, accedentes ad Moysen et Aaron,
Kulikuwa na watu fulani walionajisika kwa sababu ya maiti ya mtu. Hawakuweza kuishika Pasaka siku hiyo. Kwa hiyo walikwenda kwa Musa na Haruni siku hiyohiyo.
7 dixerunt eis: Immundi sumus super anima hominis. quare fraudamur ut non valeamus oblationem offerre Domino in tempore suo inter filios Israel?
Wakamwambia Musa, “Sisi tumenajisika kwa sababu ya maiti ya mtu. Kwa nini basi unatutaka tuendelee kutoa sadaka kwa BWANA kwa wakati wa mwaka uliopangwa kwa wana wa Israeli?”
8 Quibus respondit Moyses: State ut consulam quid praecipiat Dominus de vobis.
Naye Musa akawaambia, “Subirini nimsikilize BWANA ataniambia nini juu Yenu.”
9 Locutusque est Dominus ad Moysen, dicens:
BWANA akanena na Musa, akamwambia,
10 Loquere filiis Israel: Homo qui fuerit immundus super anima, sive in via procul in gente vestra, faciat Phase Domino
“Nena na wana wa Israeli, uwaambie, 'kama mmoja wenu au mwana wa uzao wenu amenajisika kwa sababu ya maiti, au ana safari ndefu, bado anaweza kuishika Pasaka ya BWANA.
11 in mense secundo, quartadecima die mensis ad vesperam: cum azymis et lactucis agrestibus comedent illud:
Wataishika Pasaka siku ya kumi na nne ya mwezi wa pili wakati wa jioni. Wataila kwa mikate isyotiwa chahcu na mboga chungu.
12 non relinquent ex eo quippiam usque mane, et os eius non confringent, omnem ritum Phase observabunt.
Wasiiache mpaka jioni, au kuvunja mifupa yake. Watafuata taratibu zote za Pasaka.
13 Si quis autem et mundus est, et in itinere non fuit, et tamen non fecit Phase, exterminabitur anima illa de populis suis, quia sacrificium Domino non obtulit tempore suo: peccatum suum ipse portabit.
Lakini mtu yeyote asiye najisi na hayuko safarini, na akashindwa kuishika Pasaka, huyo mtu lazima aondolewe kati ya watu wake kwa sababu hakutoa sadaka ambayo BWANA huitaka kwa wakati wa mwaka uliopangwa. Huyo mtu lazima aibebe dhambi yake.
14 Peregrinus quoque et advena si fuerint apud vos, facient Phase Domino iuxta ceremonias et iustificationes eius. Praeceptum idem erit apud vos tam advenae quam indigenae.
Kama mtu mgeni anayeishi kati yenu na akaishika, Pasaka kwa heshima ya BWANA, ataishika na kufanya amri zote, na kutii taratibu zake. Utakuwa na sheria hizohizo kwa wageni na kwa wote waliaozaliwa katika nchi.
15 Igitur die qua erectum est tabernaculum, operuit illud nubes. A vespere autem super tentorium erat quasi species ignis usque mane.
Na siku hiyo ambayo masikani iliposimamishwa, wingu lilifunika masikani, ile hema ya amari ya agano. Ilipokuwa jioni wingu lilkuwa juu ya masikani. Lilionekana kama moto mpaka asubuhi.
16 sic fiebat iugiter: per diem operiebat illud nubes, et per noctem quasi species ignis.
Liliendelea hivyohivyo. Lile wingu lilifunika masikani na kuonekana kama moto wakati wa usiku.
17 Cumque ablata fuisset nubes, quae tabernaculum protegebat, tunc proficiscebantur filii Israel: et in loco ubi stetisset nubes, ibi castrametabantur.
Na kila wingu lilipochukuliwa kutoka kwenye hema, wana wa Isareli waliendelea na safari yao. Na kila wingu liliposimama, watu waliweka kambi.
18 Ad imperium Domini proficiscebantur, et ad imperium illius figebant tabernaculum. Cunctis diebus quibus stabat nubes super tabernaculum, manebant in eodem loco:
Wana wa Israrli walisafiri kwa amri ya BWANA, na kwa amri yake waliweka kambi. Wakati wingu liliposimama juu ya masikani, nao walikaa kwenye kambi zao.
19 et si evenisset ut multo tempore maneret super illud, erant filii Israel in excubiis Domini, et non proficiscebantur
Na wingu lilipobaki kwenye masikani kwa siku nyingi, wana wa Israeli walitakiwa kutii maelekezo ya BWANA na kusitisha safari yao.
20 quot diebus fuisset nubes super tabernaculum. Ad imperium Domini erigebant tentoria, et ad imperium illius deponebant.
Wakati mwingine wingu lilibaki kwa siku chache tu kwenye masikani. Kwa mazingira kama hayo walilazimika kutii amri ya BWANA - waliweka kambi na kisha kuendelea na safari tena kwa amri yake.
21 Si fuisset nubes a vespere usque mane, et statim diluculo tabernaculum reliquisset, proficiscebantur: et, si post diem et noctem recessisset, dissipabant tentoria.
Wakati mwingine wingu lilikuwepo kambini kuanzia jioni mpaka asubuhi. Na wingu liliponyanyuliwa asubuhi, walisafiri. Kama liliendelea kwa mchana wote na kwa usiku wote, ni pale tu wingu liliponyanyuliwa ndipo walipoendelea na safari.
22 Si vero biduo aut uno mense vel longiori tempore fuisset super tabernaculum, manebant filii Israel in eodem loco, et non proficiscebantur: statim autem ut recessisset, movebant castra.
Hata kama wingu lilibaki kwenye masikini kwa siku mbili, kwa mwezi mmoja, au kwa mwaka mmoja, ili mradi tu limebaki pale, wana wa Israeli walibaki kwenye kambi zao na kusitisha safari. Lakini pale wingu liliponyanyuliwa, walianza safari yao.
23 Per verbum Domini figebant tentoria, et per verbum illius proficiscebantur: erantque in excubiis Domini iuxta imperium eius per manum Moysi.
Walifanya kambi kwa amri ya BWANA, na walisafiri kwa amri yake. Walitii amri ya BWANA iliyotolewa kupitia kwa Musa

< Liber Numeri 9 >