< Malachi Propheta 1 >

1 Onus verbi Domini ad Israel in manu Malachiae prophetae.
Tamko la neno la Bwana kwa Israeki kwa mkono wa Malaki.
2 Dilexi vos, dicit Dominus, et dixistis: In quo dilexisti nos? Nonne frater erat Esau Iacob, dicit Dominus, et dilexi Iacob,
“Nilikupenda, “asema Bwana. Lakini unasema, “kwa jinsi gani ulitupenda?” Esau siyo ndugu yake Yakobo?” asema Bwana. “Na bado nampenda Yakobo,
3 Esau autem odio habui? et posui Seir montes eius in solitudinem, et hereditatem eius in dracones deserti.
lakini nimemchukia Esau. nimeifanya milima yake kuwa ukiwa, na nimepafanya urithi wake kuwa makao ya mbweha wa jangwani.”
4 Quod si dixerit Idumaea: Destructi sumus, sed revertentes aedificabimus quae destructa sunt: Haec dicit Dominus exercituum: Isti aedificabunt, et ego destruam: et vocabuntur termini impietatis, et populus, cui iratus est Dominus usque in aeternum.
Kama Edomu husema, “Tumepigwa, lakini tutarudi na kujenga palipoharibiwa; “Bwana wa Majeshi asama hivi, “Watajenga lakini nitaiangusha chini; na wanaume watawaita 'Nchi ya uovu', na 'Watu ambao ambao Mungu ana hasira nao milele.”'
5 Et oculi vestri videbunt: et vos dicetis: Magnificetur Dominus super terminum Israel.
kwa macho yenu mtaona hili, na mtasema, “Bwana ni mkuu mbele ya mipaka ya Israel.”
6 Filius honorat patrem, et servus dominum suum: si ergo Pater ego sum, ubi est honor meus: et si Dominus ego sum, ubi est timor meus, dicit Dominus exercituum? ad vos, o sacerdotes, qui despicitis nomen meum, et dixistis: In quo despeximus nomen tuum?
mtoto amtiibaba yake, na mtumwa amtii bwana wake. ikiwa mimi, ni baba, iko wapi heshima yangu? na kama mimi ni bwana, iko wapi heshima yangu? Bwana wa majeshi asema hivi kwenu, makuhani, mnaodharau jina langu. lakini mnasema, 'tumeridharauje jina lako?
7 Offertis super altare meum panem pollutum, et dicitis: In quo polluimus te? In eo quod dicitis: Mensa Domini despecta est.
kwa kutoa mikate iliyonajisi madhabahuni kwangu. Na mnasema kuwa, 'Tumekuradhau kwa namna gani?' Kwa kusema hivyomeza ya Bwana imedharauliwa.
8 Si offeratis caecum ad immolandum, nonne malum est? et si offeratis claudum, et languidum, nonne malum est? offer illud duci tuo, si placuerit ei, aut si susceperit faciem tuam, dicit Dominus exercituum.
Mkitoa sadaka ya wanyama vipofu, hiyo siyo dhambi? na kama mkitoa vilema na wagonjwa, hiyo siyo dhambi? pelekeni hili kwa liwali; atawakubali au atainua nyuso zetu?” asema Bwana wa Majeshi.
9 Et nunc deprecamini vultum Dei ut misereatur vestri (de manu enim vestra factum est hoc) si quomodo suscipiat facies vestras, dicit Dominus exercituum.
Na sasa, mnajaribu kutafuta neema ya Mungu, ili kwamba awe mwema kwetu. “Na aina gani ya sadaka kwa sehemu yenu, ataziinua nyuso zenu? asema Bwana wa Majeshi.
10 Quis est in vobis, qui claudat ostia, et incendat altare meum gratuito? non est mihi voluntas in vobis, dicit Dominus exercituum: et munus non suscipiam de manu vestra.
Kama kungekuwa na mtu ambaye angefunga lango la Hekalu, ili kwamba kusewe na mto madhabahuni bure! lakini sina radhi na ninyi, “asema Bwana wa majeshi, “na sitaikubali sadaka yeyote kutoka katika mikono yenu.
11 Ab ortu enim solis usque ad occasum, magnum est nomen meum in Gentibus, et in omni loco sacrificatur, et offertur nomini meo oblatio munda: quia magnum est nomen meum in Gentibus, dicit Dominus exercituum.
Kutoka mawio ya jua mpaka machweo jina langu litakuwa kuu katikati ya mataifa; katika kila sehemu uvumba utatolewa katika jina langu, na pia sadaka safi. Kwa sababu jina langu likuwa kuu sana katikatik ya mataif,” asema Bwana wa majeshi.
12 Et vos polluistis illud in eo, quod dicitis: Mensa Domini contaminata est: et quod superponitur, contemptibilis est cum igne, qui illud devorat.
“lakini ninyi mnachafua mnaposema meza ya Bwana mnainajisi, na matunda yake, na chakula chake kudharauka.
13 Et dixistis: Ecce de labore, et exufflastis illud, dicit Dominus exercituum, et intulistis de rapinis claudum, et languidum, et intulistis munus: numquid suscipiam illud de manu vestra, dicit Dominus?
Na ninyi pia mwasema, 'jambo hili limetuchosha, nanyi mnalidharau, “asema Bwana wa majeshi. “Mmerudisha kilichokuwa kimechukuliwa na wanyama wa mwitu au vilema au walio wagonjwa; na ndicho mnaleta kuwa sadaka zenu! Je naweza kuikubali hii mikononi mwenu?” asema Bwana.
14 Maledictus dolosus, qui habet in grege suo masculum, et votum faciens immolat debile Domino: quia Rex magnus ego, dicit Dominus exercituum, et nomen meum horribile in Gentibus.
Alaniwe alye mdanganyifu, ambaye anaye mnyama dume katika kundi lake ana akaahidi kunitolea, lakini bado anatoa kwangu, mimi Bwana, ambayo ni kiujanja ujanja; kwa kuwa mimi ni mfalme mkuu,” asema Bwana wa Majeshi, “na jina langu litaogopwa katika mataifa.”

< Malachi Propheta 1 >