< Hebræos 10 >

1 Umbram enim habens lex futurorum bonorum, non ipsam imaginem rerum: per singulos annos eisdem ipsis hostiis, quas offerunt indesinenter, numquam potest accedentes perfectos facere:
Kwa vile sheria ni kivuli cha mambo mema yajayo, si yale yaliyo halisi. Sheria kamwe haiwezi kuwakamilisha wale ambao wanaomkaribia Mungu kwa njia ya dhabihu zilezile ambazo makuhani waliendelea kutoa mwaka baada ya mwaka.
2 alioquin cessassent offerri: ideo quod nullam haberent ultra conscientiam peccati, cultores semel mundati:
Au vinginevyo dhabihu hizo zisingeweza kukoma kutolewa? Kwa kigezo hicho waabuduo, wakiwa wamesafishwa mara moja, wasingelikuwa na utambuzi zaidi wa dhambi.
3 sed in ipsis commemoratio peccatorum per singulos annos fit.
Bali katika dhabihu hizo kuna ukumbusho wa dhambi zilizotendwa mwaka baada ya mwaka.
4 impossibile enim est sanguine taurorum et hircorum auferri peccata.
Kwa kuwa haiwezekani kwa damu ya mafahari na mbuzi kuziondoa dhambi.
5 Ideo ingrediens mundum dicit: Hostiam, et oblationem noluisti: corpus autem aptasti mihi:
Wakati Kristo alipokuja duniani, alisema, “Hamkutamani matoleo au dhabihu, badala yake, mliandaa mwili kwa ajili yangu.
6 holocaustomata pro peccato non tibi placuerunt.
Hamkuwa na thamani katika matoleo yote ya kuteketezwa au dhabihu kwa ajili ya dhambi.
7 Tunc dixi: Ecce venio: in capite libri scriptum est de me: Ut faciam, Deus, voluntatem tuam.
Kisha nilisema, “Ona, hapa ninayafanya mapenzi yako, Mungu, kama ilivyoandikwa kunihusu mimi katika gombo”.
8 Superius dicens: Quia hostias, et oblationes, et holocaustomata pro peccato noluisti, nec placita sunt tibi, quae secundum legem offeruntur,
Alisema kama ilivyo semwa hapo juu: “Hamkutamani dhabihu, matoleo, au sadaka ya kuteketezwa kwa ajili ya dhambi, wala hukuona furaha ndani yake” dhabihu ambazo zinatolewa kulingana na sheria.
9 tunc dixi: Ecce venio, ut faciam, Deus, voluntatem tuam: aufert primum, ut sequens statuat.
Kisha alisema, “Ona, niko hapa kufanya mapenzi yako”. Ameweka pembeni taratibu zilizo za awali ili kuimarisha zile za pili.
10 In qua voluntate sanctificati sumus per oblationem corporis Iesu Christi semel.
Katika taratibu za pili, tumekwisha tengwa kwa Mungu kwa mapenzi yake kupitia kujitoa kwa mwili wa Yesu Kristo mara moja kwa nyakati zote.
11 Et omnis quidem sacerdos praesto est quotidie ministrans, et easdem saepe offerens hostias, quae numquam possunt auferre peccata:
Ni kweli, kila kuhani husimama kwa huduma siku kwa siku, akitoa dhabihu ile ile, ambayo, kwa vyovyote, kamwe isingeweza kuziondoa dhambi.
12 hic autem unam pro peccatis offerens hostiam, in sempiternum sedet in dextera Dei,
Lakini baada ya Kristo kutoa dhabihu mara moja kwa dhambi milele yote, aliketi mkono wa kuume wa Mungu,
13 de cetero expectans donec ponantur inimici eius scabellum pedum eius.
akisubiri mpaka maadui zake watiwe chini na kufanywa kiti kwa ajili ya miguu yake.
14 Una enim oblatione, consummavit in sempiternum sanctificatos.
Kwa kuwa kwa njia ya toleo moja amewakamilisha milele wale ambao wametengwa kwa Mungu.
15 Contestatur autem nos et Spiritus sanctus. Postquam enim dixit:
Na Roho Mtakatifu pia ashuhudia kwetu. Kwa kuwa kwanza alisema,
16 Hoc autem testamentum, quod testabor ad illos post dies illos, dicit Dominus: Dabo leges meas in cordibus eorum, et in mentibus eorum superscribam eas:
“Hili ni agano nitakalofanya pamoja nao baada ya siku hizo; asema Bwana: nitaweka sheria zangu ndani ya mioyo yao, na nitaziandika katika akili zao”.
17 et peccatorum, et iniquitatum eorum iam non recordabor amplius.
Kisha alisema, “Hawatazikumbuka tena dhambi na matendo yao mafu”.
18 Ubi autem horum remissio: iam non est oblatio pro peccato.
Sasa mahali palipo na msamaha kwa hawa, hakuna tena dhabihu yoyote kwa ajili ya dhambi.
19 Habentes itaque fratres fiduciam in introitu sanctorum in sanguine Christi,
Kwa hiyo, ndugu, tunao ujasiri wa kuingia mahali patakatifu zaidi kwa damu ya Yesu.
20 quam initiavit nobis viam novam, et viventem per velamen, id est, carnem suam,
Hiyo ni njia ambayo ameifungua kwa ajili yetu kwa njia ya mwili wake, mpya na hai inayopitia kwenye pazia.
21 et sacerdotem magnum super domum Dei:
Na kwa sababu tunaye kuhani mkuu juu ya nyumba ya Mungu,
22 accedamus cum vero corde in plenitudine fidei, aspersi corda a conscientia mala, et abluti corpus aqua munda,
na tumkaribie na moyo wa kweli katika utimilifu wa uhakika wa imani tukiwa na mioyo iliyonyunyiziwa safi kutoka uovu wa dhamiri na kuwa na miili yetu iliyooshwa kwa maji safi.
23 teneamus spei nostrae confessionem indeclinabilem, (fidelis enim est qui repromisit),
Basi na tushikilie kwa uthabiti katika ungamo la ujasiri wa tumaini letu, bila ya kugeuka, kwa sababu Mungu aliyeahidi ni mwaminifu.
24 et consideremus invicem in provocationem charitatis, et bonorum operum:
Na tuzidi kutafakari namna ya kumtia moyo kila mmoja kupenda na matendo mema.
25 non deserentes collectionem nostram, sicut consuetudinis est quibusdam, sed consolantes, et tanto magis quanto videritis appropinquantem diem.
Na tusiache kukusanyika pamoja, kama wafanyavyo wengine. Badala yake, kutiana moyo kila mmoja zaidi na zaidi, kama muonavyo siku inakaribia.
26 Voluntarie enim peccantibus nobis post acceptam notitiam veritatis, iam non relinquitur pro peccatis hostia,
Kama tukifanya makusudi kuendelea kutenda dhambi baada ya kuwa tumepokea elimu ya ukweli, Dhabihu nyingine ya dhambi haisalii tena.
27 terribilis autem quaedam expectatio iudicii, et ignis aemulatio, quae consumptura est adversarios.
Badala yake, kuna tarajio pekee la hukumu ya kutisha, na ukali wa moto ambao utawateketeza maadui wa Mungu.
28 Irritam quis faciens legem Moysi, sine ulla miseratione duobus vel tribus testibus moritur:
Yeyote ambaye ameikataa sheria ya Musa hufa bila rehema mbele ya ushuhuda wa mashahidi wawili au watatu.
29 quanto magis putatis deteriora mereri supplicia qui filium Dei conculcaverit, et sanguinem testamenti pollutum duxerit, in quo sanctificatus est, et spiritui gratiae contumeliam fecerit?
kiwango gani zaidi cha adhabu unafikiri kinamstahiri kilammoja ambaye amemdharau mwana wa Mungu, yeyote aliyeitendea damu ya agano kama kitu kisicho kitakatifu, damu ambayo kwayo aliiweka wakfu kwa Mungu - yeyote ambaye amemtukana Roho wa neema?
30 Scimus enim qui dixit: Mihi vindictam, et ego retribuam. Et iterum: Quia iudicabit Dominus populum suum.
Kwakuwa tunajua mmoja ambaye aliyesema, “Kisasi ni changu, nitalipa”. Na tena, “Bwana atawahukumu watu wake”.
31 Horrendum est incidere in manus Dei viventis.
Ni jambo la kuogofya mtu kuangukia katika mikono ya Mungu aliye hai!
32 Rememoramini autem pristinos dies, in quibus illuminati, magnum certamen sustinuistis passionum:
Lakini kumbuka siku zilizopita, baada ya kutiwa kwenu nuru, ni jinsi gani mliweza kuvumilia maumivu makali.
33 et in altero quidem opprobriis, et tribulationibus spectaculum facti: in altero autem socii taliter conversantium effecti.
Mlikuwa mmewekwa wazi katika dhihaka ya matukano na mateso, na mlikuwa washiriki pamoja na wale waliopitia mateso kama hayo.
34 Nam et vinctis compassi estis, et rapinam bonorum vestrorum cum gaudio suscepistis, cognoscentes vos habere meliorem, et manentem substantiam.
Kwa kuwa mlikuwa na moyo wa huruma kwa hao waliokuwa wafungwa, na mlipokea kwa furaha adhabu ya urithi wenu, mkijua kwamba ninyi wenyewe mlikuwa na urithi bora na wa kudumu milele.
35 Nolite itaque amittere confidentiam vestram, quae magnam habet remunerationem.
Kwa hiyo msiutupe ujasiri wenu, ulio na zawadi kuu.
36 Patientia enim vobis necessaria est: ut voluntatem Dei facientes, reportetis promissionem.
Kwa kuwa mnahitaji uvumilivu, ili kwamba mpate kupokea ambacho Mungu amekiahidi, baada ya kuwa mmekwisha yatenda mapenzi yake.
37 Adhuc enim modicum aliquantulumque, qui venturus est, veniet, et non tardabit.
Kwa kuwa baada ya kitambo kidogo, mmoja anayekuja, atakuja hakika na hatakawia.
38 iustus autem meus ex fide vivit. quod si subtraxerit se, non placebit animae meae.
Mwenye haki wangu ataishi kwa imani. Kama atarudi nyuma, sitapendezwa naye.”
39 Nos autem non sumus subtractionis filii in perditionem, sed fidei in acquisitionem animae.
Lakini sisi si kama wale warudio nyuma kwa kuangamia. Badala yake, sisi ni baadhi ya wale tulio na imani ya kuzilinda roho zetu.

< Hebræos 10 >