< Hiezechielis Prophetæ 9 >
1 Et clamavit in auribus meis voce magna, dicens: Appropinquaverunt visitationes urbis, et unusquisque vas interfectionis habet in manu sua.
Kisha akalia kwa sauti kubwa nikasikia kwenye masikio yangu, huku akisema, “Waache walinzi waje kwenye mji, kila mmoja na silaha yake ya uharibifu kwenye mkono wake.”
2 Et ecce sex viri veniebant de via portae superioris, quae respicit ad Aquilonem: et uniuscuiusque vas interitus in manu eius: vir quoque unus in medio eorum vestitus erat lineis, et atramentarium scriptoris ad renes eius: et ingressi sunt, et steterunt iuxta altare aereum:
Kisha tazama! watu wanne watakuja kutokea njia ya lango la juu linaloelekea kaskazini, kila mmoja na silaha yake ya kuchinjia kwenye mkono wake. Kulikuwa na mtu mmoja miongoni mwao alikuwa amevaa nguo ya kitani pamoja na kifaa cha uandishi ubavuni mwake. Hivyo waliingia na kusimama karibu na madhabahu ya shaba.
3 Et gloria Domini Israel assumpta est de cherub, quae erat super eum ad limen domus: et vocavit virum, qui indutus erat lineis, et atramentarium scriptoris habebat in lumbis suis.
Kisha utukufu wa Mungu wa Israeli ukapanda juu kutoka kwa kerubi ambapo ilikuwa kwenye kisingiti cha nyumba. Akamwita yule mtu aliyekuwa amevaa nguo ya kitani na kifaa cha uandishi ubavuni mwake.
4 Et dixit Dominus ad eum: Transi per mediam civitatem in medio Ierusalem: et signa thau super frontes virorum gementium, et dolentium super cunctis abominationibus, quae fiunt in medio eius.
Yahwe akamwambia, “Pita kati ya mji-kati ya Yerusalemu-na weka alama katika vipaji vya uso vya wale waliolemewa na kuona kuhusu machukizo yote yanafanyika kati ya mji.”
5 Et illis dixit, audiente me: Transite per civitatem sequentes eum, et percutite: non parcat oculus vester, neque misereamini.
Kisha akaongea na wengine kupitia kusikia kwangu, “Pita kwenye mji baada ya yeye na kuua. Msiache macho yenu yawe na huruma, na msiogope kuharibu
6 Senem, adolescentulum, et virginem, parvulos, et mulieres interficite usque ad internecionem: omnem autem, super quem videritis thau, ne occidatis, et a sanctuario meo incipite. Coeperunt ergo a viris senioribus, qui erant ante faciem domus.
iwe mzee, kijana, msichana, mtoto mdogo au wanawake. Waueni watu wote! Lakini msimkaribie mtu yeyote ambaye mwenye alama kwenye kichwa chake. Anzeni katika patakatifu pangu!” Hivyo wakaanza na wazee waliokuwa mbele ya nyumba.
7 Et dixit ad eos: Contaminate domum, et implete atria interfectis: egredimini. Et egressi sunt, et percutiebant eos, qui erant in civitate.
Akawaambia, “Najisi nyumba, na kujaza zio zake kwa waliokufa. Endeleeni!” Hivyo wakaenda na kuushambulia mji.
8 Et caede completa, remansi ego: ruique super faciem meam, et clamans aio: Heu, heu, heu Domine Deus: ergone disperdes omnes reliquias Israel, effundens furorem tuum super Ierusalem?
Walipokuwa wakiushambulia, nikajikuta mwenyewe na nikaangukia kwenye uso wangu na kulia kwa sauti na kusema, “Ee, Bwana Yahwe, utayaharibu mabaki yote ya Israeli wakati wa kumwaga ghadhabu yao juu ya Yerusalemu?”
9 Et dixit ad me: Iniquitas domus Israel, et Iuda, magna est nimis valde, et repleta est terra sanguinibus, et civitas repleta est aversione: dixerunt enim: Dereliquit Dominus terram, et Dominus non videt.
Akanambia, “Uovu wa nyumba ya Israeli na Yuda unaongezeka sana. Nchi imejaa damu na mji umejaa upotovu, tangu waliposema, 'Yahwe ameisahau nchi; na Yahwe haoni!'
10 Igitur et meus non parcet oculus, neque miserebor: viam eorum super caput eorum reddam.
Hivyo kisha, macho yangu hataangalia kwa huruma, na sintoacha kuwaharibu. Badala yake nitaileta juu ya vichwa vyao.”
11 Et ecce vir, qui erat indutus lineis, qui habebat atramentarium in dorso suo, respondit verbum, dicens: Feci sicut praecepisti mihi.
Tazama! yule mtu aliyekuwa amevaa nguo ya kitani aliyekuwa na kifaa cha uandishi kwa uapende wa ubavuni mwake. Alitoa taarifa na kusema, “Nimemaliza yale yote uliyoniamuru.”