< Ii Samuelis 22 >
1 Locutus est autem David Domino verba carminis huius, in die qua liberavit eum Dominus de manu omnium inimicorum suorum, et de manu Saul.
Daudi akamwimbia Yahwe maneno ya wimbo huu siku ile Yahwe alipomwokoa katika mkono wa adui zake wote na katika mkono wa Sauli.
2 et ait: Dominus petra mea, et robur meum, et salvator meus.
Akaomba hivi, “Yahwe ni mwamba wangu, ngome yangu, aliyeniokoa.
3 Deus fortis meus sperabo in eum: scutum meum, et cornu salutis meae: elevator meus, et refugium meum: salvator meus, de iniquitate liberabis me.
Mungu ni mwamba wangu. Yeye ni kimbilio langu. Ngao yangu, pembe ya wokovu wangu, ngome yangu na kimbilio langu, aniokoaye na mabaya yote.
4 Laudabilem invocabo Dominum: et ab inimicis meis salvus ero.
Nitamwita Yahwe, astahiliye kutukuzwa, nami nitaokolewa kutoka kwa adui zangu.
5 Quia circumdederunt me contritiones mortis: torrentes Belial terruerunt me.
Maana mawimbi ya mauti yalinizunguka, mafuriko ya maji ya uharibifu yakanishinda.
6 Funes inferni circumdederunt me: praevenerunt me laquei mortis. (Sheol )
Vifungo vya kuzimu vilinizunguka; kamba za mauti zikaninasa. (Sheol )
7 In tribulatione mea invocabo Dominum, et ad Deum meum clamabo: et exaudiet de templo sancto suo vocem meam, et clamor meus veniet ad aures eius.
Katika shida yangu nalimwita Yahwe; nilimwita Mungu wangu; akaisikia sauti yangu katika hekalu lake, na kilio changu cha msaada kikafika masikioni mwake.
8 Commota est et contremuit terra: fundamenta montium concussa sunt, et conquassata, quoniam iratus est eis.
Ndipo nchi ilipotikisika na kutetemeka. Misingi ya mbingu ikatetemeka na kutikiswa, kwa kuwa Mungu alikasirika.
9 Ascendit fumus de naribus eius, et ignis de ore eius vorabit: carbones succensi sunt ab eo.
Moshi ukatoka katika pua yake, na miale ya moto ikatoka katika kinywa chake. Makaa yakawashwa nayo.
10 Inclinavit caelos, et descendit: et caligo sub pedibus eius.
Alizifungua mbingu akashuka, na giza totoro lilikuwa chini ya miguu yake.
11 Et ascendit super cherubim, et volavit: et lapsus est super pennas venti.
Alipanda juu ya kerubi na kuruka. Alionekana katika mawingu ya upepo.
12 Posuit tenebras in circuitu suo latibulum: cribrans aquas de nubibus caelorum.
Naye akalifanya giza kuwa hema kumzunguka, akakusanya mawingu makubwa ya mvua angani.
13 Prae fulgore in conspectu eius, succensi sunt carbones ignis.
Makaa ya moto yalidondoka mbele zake kutoka katika radi.
14 Tonabit de caelo Dominus: et excelsus dabit vocem suam.
Yahwe alishuka kutoka katika mbingu. Aliyejuu alipiga kelele.
15 Misit sagittas et dissipavit eos: fulgur, et consumpsit eos.
Alipiga mishale na kuwatawanya adui zake—miale ya radi na kuwasambaratisha.
16 Et apparuerunt effusiones maris, et revelata sunt fundamenta orbis ab increpatione Domini, ab inspiratione spiritus furoris eius.
Kisha njia za maji zikaonekana; misingi ya dunia ikawa wazi katika kilio cha vita ya Yahweh, katika sauti za pumzi ya pua zake.
17 Misit de coelo, et assumpsit me: et extraxit me de aquis multis.
Kutoka juu alifika chini; akanishikilia! Aliniondoa katika vilindi vya maji.
18 Liberavit me ab inimico meo potentissimo, et ab his qui oderant me: quoniam robustiores me erant.
Aliniokoa kutoka kwa adui zangu wenye nguvu, kwao walionichukia, kwa maana walikuwa na nguvu sana kwangu.
19 Praevenit me in die afflictionis meae, et factus est Dominus firmamentum meum.
Walikuja kinyume changu siku ya shida yangu, lakini Yahwe alikuwa msaada wangu.
20 Et eduxit me in latitudinem: liberavit me, quia complacui ei.
Pia aliniweka mahali panapo nafasi. Aliniokoa kwa kuwa alipendezwa nami.
21 Retribuet mihi Dominus secundum iustitiam meam: et secundum munditiam manuum mearum reddet mihi.
Yahwe amenituza kwa kipimo cha haki yangu; amenirejesha kwa kiwango cha usafi wa mikono yangu.
22 Quia custodivi vias Domini, et non egi impie, a Deo meo.
Kwa maana nimezishika njia za Yahwe na sijafanya uovu kwa kugeuka kutoka kwa Mungu.
23 Omnia enim iudicia eius in conspectu meo: et praecepta eius non amovi a me.
Kwa kuwa maagizo yake yote ya haki yamekuwa mbele yangu; kwa kuwa sheria zake, sikujiepusha nazo.
24 Et ero perfectus cum eo: et custodiam me ab iniquitate mea.
Nimekuwa bila hatia mbele zake pia, na nimejiepusha na dhambi.
25 Et restituet mihi Dominus secundum iustitiam meam: et secundum munditiam manuum mearum, in conspectu oculorum suorum.
Kwa hiyo Yahwe amenirejesha kwa kiasi cha uadilifu wangu, kwa kipimo cha usafi wangu mbele zake.
26 Cum sancto sanctus eris: et cum robusto perfectus.
Kwa mwaminifu, unajionesha kuwa mwaminifu; kwake asiye na hatia; unajionesha kuwa hauna hatia.
27 Cum electo electus eris: et cum perverso perverteris.
Kwa usafi unajionesha kuwa msafi, lakini kwa wakaidi unajionesha kuwa mkaidi.
28 Et populum pauperem salvum facies: oculisque tuis excelsos humiliabis.
Unaokoa walioteswa, lakini macho yako ni kinyume cha wenye kiburi, unawashusha chini.
29 Quia tu lucerna mea Domine: et tu Domine illuminabis tenebras meas.
Kwa maana wewe ni taa yangu, Yahwe. Yahwe huangaza katika giza langu.
30 In te enim curram accinctus: in Deo meo transiliam murum.
Maana kwa ajili yake ninaweza kupita vipingamizi; kwa msaada wa Mungu wangu naweza kuruka juu ya ukuta.
31 Deus, immaculata via eius, eloquium Domini igne examinatum: scutum est omnium sperantium in se.
Maana njia za Mungu ni kamilifu. Neno la Yahwe ni safi. Yeye ni ngao yao wanaomkimbilia.
32 Quis est Deus praeter Dominum: et quis fortis praeter Deum nostrum?
Maana ni nani aliye Mungu isipokuwa Yahwe? Na ni nani aliyemwamba isipokuwa Mungu?
33 Deus qui accinxit me fortitudine: et complanavit perfectam viam meam.
Mungu ni kimbilio langu, na umwongoza katika njia yake mtu asiye na hatia.
34 Coaequans pedes meos cervis, et super excelsa mea statuens me.
Huifanya myepesi miguu yangu kama kurungu na kuniweka katika vilima virefu.
35 Docens manus meas ad praelium, et componens quasi arcum aereum brachia mea.
Huifundisha mikono yangu kwa vita, na viganja vyangu kupinda upinde wa shaba.
36 Dedisti mihi clypeum salutis tuae: et mansuetudo mea multiplicavit me.
Umenipa ngao ya wokovu wako, na matakwa yako yamenifanya mkuu.
37 Dilatabis gressus meos subtus me: et non deficient tali mei.
Umeitengenezea miguu yangu nafasi chini yangu, hivyo miguu yangu haikujikwaa.
38 Persequar inimicos meos, et conteram: et non convertar donec consumam eos.
Niliwafuatia adui zangu na kuwaangamiza. Sikurudi nyuma hadi walipoangamizwa.
39 Consumam eos et confringam, ut non consurgant: cadent sub pedibus meis.
Niliwararua na kuwasambaratisha; hawawezi kuinuka. Wameanguka chini ya miguu yangu.
40 Accinxisti me fortitudine ad praelium: incurvasti resistentes mihi subtus me.
Unaweka nguvu ndani yangu kama mkanda kwa vita; unawaweka chini yangu wanaoinuka kinyume changu.
41 Inimicos meos dedisti mihi dorsum: odientes me, et disperdam eos.
Ulinipa migongo ya shingo za adui zangu; niliwaangamiza kabisa wale wanaonichukia.
42 Clamabunt, et non erit qui salvet, ad Dominum, et non exaudiet eos.
Walilia kwa msaada, lakini hakuna aliyewaokoa; walimlilia Yahwe, lakini hakuwajibu.
43 Delebo eos ut pulverem terrae: quasi lutum platearum comminuam eos atque confringam.
Niliwaponda katika vipande kama mavumbi juu ya ardhi, niliwakanyaga kama matope mitaani.
44 Salvabis me a contradictionibus populi mei: custodies me in caput Gentium: populus, quem ignoro, serviet mihi.
Umeniokoa pia kutoka katika mashutumu ya watu wangu. Umeniweka kama kichwa cha mataifa. Watu nisiowajua wananitumikia.
45 Filii alieni resistent mihi, auditu auris obedient mihi.
Wageni walishurutishwa kuniinamia. Mara waliposikia kuhusu mimi, walinitii.
46 Filii alieni defluxerunt, et contrahentur in angustiis suis.
Wageni walikuja wakitetemeka kutoka katika ngome zao.
47 Vivit Dominus, et benedictus Deus meus: et exaltabitur Deus fortis salutis meae.
Yahwe anaishi! Mwamba wangu atukuzwe. Mungu na ainuliwe, mwamba wa wokovu wangu.
48 Deus qui das vindictas mihi, et deiicis populos sub me.
Huyu ndiye Mungu anilipiaye kisasi, awawekaye watu chini yangu.
49 Qui educis me ab inimicis meis, et a resistentibus mihi elevas me: a viro iniquo liberabis me:
Uniweka huru mbali na adui zangu. Hakika, uliniinua juu yao walioinuka kinyume changu. Uliniokoa kutoka kwa watu wenye ghasia.
50 Propterea confitebor tibi Domine in gentibus: et nomini tuo cantabo.
Kwa hiyo nitakushukuru, Yahwe, kati ya mataifa; nitaliimbia sifa jina lako.
51 Magnificans salutes regis sui, et faciens misericordiam christo suo David, et semini eius in sempiternum.
Mungu hutoa ushindi mkuu kwa mfalme wake, na uonesha uaminifu wake wa kiagano kwa mtiwa mafuta wake, kwa Daudi na uzao wake daima.”