< Psalmorum 102 >

1 Oratio pauperis, cum anxius fuerit, et in conspectu Domini effuderit precem suam. Domine, exaudi orationem meam, et clamor meus ad te veniat.
Sikia maombi yangu, Ee Yahwe; sikia kulia kwangu kwako.
2 Non avertas faciem tuam a me: in quacumque die tribulor, inclina ad me aurem tuam; in quacumque die invocavero te, velociter exaudi me.
Usiufiche uso wako mbali nami wakati wa shida. Unisikilize. Nikuitapo, unijibu upesi.
3 Quia defecerunt sicut fumus dies mei, et ossa mea sicut cremium aruerunt.
Kwa maana siku zangu zinapita kama moshi, na mifupa yangu kama moto.
4 Percussus sum ut fœnum, et aruit cor meum, quia oblitus sum comedere panem meum.
Moyo wangu umeumizwa na niko kama majani yaliyo kauka. Ninasahau kula chakula chochote.
5 A voce gemitus mei adhæsit os meum carni meæ.
Kwa muendelezo wa kuugua kwangu, nimekonda sana.
6 Similis factus sum pellicano solitudinis; factus sum sicut nycticorax in domicilio.
Niko kama mwali wa jangwani; nimekuwa kama bundi magofuni.
7 Vigilavi, et factus sum sicut passer solitarius in tecto.
Ninalala macho kama shomoro faraghani, pekeyake juu ya paa.
8 Tota die exprobrabant mihi inimici mei, et qui laudabant me adversum me jurabant:
Adui zangu wananilaumu mchana kutwa; wale wanao nidhihaki hutumia jina langu katika laana.
9 quia cinerem tamquam panem manducabam, et potum meum cum fletu miscebam,
Ninakula majivu kama mkate na kuchanganya kinywaji changu kwa machozi.
10 a facie iræ et indignationis tuæ: quia elevans allisisti me.
Kwa sababu ya hasira yako kali, umeniinua juu kunitupa chini.
11 Dies mei sicut umbra declinaverunt, et ego sicut fœnum arui.
Siku zangu ni kama kivuli kanachofifia, na ninanyauka kama majani.
12 Tu autem, Domine, in æternum permanes, et memoriale tuum in generationem et generationem.
Lakini wewe, Yahwe, unaishi milele, na kumbukumbu lako ni kwa vizazi vyote.
13 Tu exsurgens misereberis Sion, quia tempus miserendi ejus, quia venit tempus:
Wewe utasimama na kuirehemu Sayuni. Sasa ni wakati wa mkurehemu yeye. Wakati ulio teuliwa umefika.
14 quoniam placuerunt servis tuis lapides ejus, et terræ ejus miserebuntur.
Maana watumishi wako wameyaridhia mawe yake pendwa na kuyaonea huruma mavumbi ya magofu yake.
15 Et timebunt gentes nomen tuum, Domine, et omnes reges terræ gloriam tuam:
Mataifa wataliheshimu jina lako, Yahwe, na wafalme wote wa nchi watauheshimu utukufu wako.
16 quia ædificavit Dominus Sion, et videbitur in gloria sua.
Yahwe ataijenga tena Sayuni na ataonekana katika utukufu wake.
17 Respexit in orationem humilium et non sprevit precem eorum.
Wakati huo, atajibu maombi ya fukara; hatayakataa maombi yao.
18 Scribantur hæc in generatione altera, et populus qui creabitur laudabit Dominum.
Hii itaandikwa kwa ajili ya vizazi vijavyo, na watu ambao bado hawajazaliwa watamsifu Yahwe.
19 Quia prospexit de excelso sancto suo; Dominus de cælo in terram aspexit:
Maana ametazama chini toka mahali pa juu patakatifu;
20 ut audiret gemitus compeditorum; ut solveret filios interemptorum:
Toka mbinguni Yahwe ameiangalia nchi, ili kusikia kuugua kwa wafungwa, kuwafungua waliohukumiwa kufa.
21 ut annuntient in Sion nomen Domini, et laudem ejus in Jerusalem:
Kisha watu watalitangaza jina la Yahwe katika Sayuni na sifa zake katika Yerusalemu
22 in conveniendo populos in unum, et reges, ut serviant Domino.
pindi mataifa na falme watakapokusanyika pamoja kumtumikia Yahwe.
23 Respondit ei in via virtutis suæ: Paucitatem dierum meorum nuntia mihi:
Amechukua nguvu zangu katikati ya siku zangu za kuishi, amezifupisha siku zangu.
24 ne revoces me in dimidio dierum meorum, in generationem et generationem anni tui.
Nilisema, “Mungu wangu, usinichukue katikati ya siku zangu; wewe uko hapa hata kizazi chote.
25 Initio tu, Domine, terram fundasti, et opera manuum tuarum sunt cæli.
Tangu zama za kale wewe uliiweka nchi mahali pake; mbingu ni kazi ya mikono yako.
26 Ipsi peribunt, tu autem permanes; et omnes sicut vestimentum veterascent. Et sicut opertorium mutabis eos, et mutabuntur;
Mbingu na nchi zitaangamia lakini wewe utabaki; zitachakaa kama mavazi; utaziondoa kama watu waondoavyo mavazi yaliyo chakaa, nazo hazitaonekana tena.
27 tu autem idem ipse es, et anni tui non deficient.
Lakini wewe ni yuleyule, na miaka yako haitakuwa na mwisho.
28 Filii servorum tuorum habitabunt, et semen eorum in sæculum dirigetur.
Watoto wa watumishi wako wataendelea kuishi, na uzao wao utaishi katika uwepo wako.

< Psalmorum 102 >