< Leviticus 12 >
1 Locutusque est Dominus ad Moysen, dicens:
Yahweh akamwambia Musa,
2 Loquere filiis Israël, et dices ad eos: Mulier, si suscepto semine pepererit masculum, immunda erit septem diebus juxta dies separationis menstruæ.
“zungumza na watu wa Israeli, uwaambie, 'endapo mwanamke anakuwa mjamzito na kujifungua mtoto wa kiume, naye atakuwa najisi kwa muda wasiku saba, ni kama tu vile anavyokuwa najisi katika siku za kipindi chake kwa mwezi.
3 Et die octavo circumcidetur infantulus:
Katika siku ya nane nyama ya govi la mtoto mvulana itatahiriwa.
4 ipsa vero triginta tribus diebus manebit in sanguine purificationis suæ. Omne sanctum non tanget, nec ingredietur in sanctuarium, donec impleantur dies purificationis suæ.
Kisha utakaso wa mama wa kutokwa damu yake utaendelea kwa muda wa siku tatu. Haimpasi kugusa kitu chochote kilicho kitakatifu au kukaribia eneo la hema mpaka zitakapomalizika siku za kutakaswa kwake.
5 Sin autem feminam pepererit, immunda erit duabus hebdomadibus juxta ritum fluxus menstrui, et sexaginta sex diebus manebit in sanguine purificationis suæ.
Lakini kama atajifungua mtoto wa kike, naye atakuwa najisi kwa mud wa majuma mawili, kama alivyo wakati wa kipindi chake. Kisha utakaso wa mama utaendelea kwa siku sitini sita.
6 Cumque expleti fuerint dies purificationis suæ, pro filio sive pro filia, deferet agnum anniculum in holocaustum, et pullum columbæ sive turturem pro peccato, ad ostium tabernaculi testimonii, et tradet sacerdoti,
Siku za kutakaswa kwake zitakapoisha, kwa ajili ya mwana au binti, atalazimika kuleta kwa kuhani mwana-kondoo wa mwaka mmoja kuwa sadaka ya kuteketezwa, na kinda la njiwa au huwa kuwa sadaka ya dhambi, mbele ya ingilio la hema la kukutania,
7 qui offeret illa coram Domino, et orabit pro ea, et sic mundabitur a profluvio sanguinis sui: ista est lex parientis masculum aut feminam.
Kisha atawatoa mbele za Yahweh na kufanya sadaka ya upatanisho kwa ajili yake, naye atatakaswa kutokana kutiririka kwa damu yake. Hii ndiyo sheria kuhusu mwanamke aifunguaye ama mtoto wa kiume au wa kike.
8 Quod si non invenerit manus ejus, nec potuerit offerre agnum, sumet duos turtures vel duos pullos columbarum, unum in holocaustum, et alterum pro peccato: orabitque pro ea sacerdos, et sic mundabitur.
Na kama hana uwezo wa kutoa mwana-kondoo, naye ataleta makinda mawili ya njiwa ua hua, mmoja kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa na mwingine kuwa sadaka ya dhambi, naye kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake; naye atakuwa safi.”