< Ii Paralipomenon 34 >

1 Octo annorum erat Josias cum regnare cœpisset, et triginta et uno anno regnavit in Jerusalem.
Yosia alikuwa na umri wa miaka kumi na nane alipoanza kutawala; alitawala miaka thelathini na moja katika Yerusalemu.
2 Fecitque quod erat rectum in conspectu Domini, et ambulavit in viis David patris sui: non declinavit neque ad dextram, neque ad sinistram.
Alifanya yaliyohaki katika macho ya Yahwe, na alitembea katiaka njia za Daudi babu yake, ha hakugeuka mbali iwe kulia au kushoto.
3 Octavo autem anno regni sui, cum adhuc esset puer, cœpit quærere Deum patris sui David: et duodecimo anno postquam regnare cœperat, mundavit Judam et Jerusalem ab excelsis, et lucis, simulacrisque et sculptilibus.
Kwa maana ndani ya miaka minane ya ya utawala wake, alipokuwa bado kijana, alianza kumtafuta Mungu wa Daudi, babu yake. Katika miaka ishirini, alianza kuisafisha Yuda na Yerusalemu kutoka sehemu za juu, vituo vya Maashera, na sanamu za kuchonga na sanamu za chuma ya kuyeyushwa.
4 Destruxeruntque coram eo aras Baalim, et simulacra quæ superposita fuerant, demoliti sunt: lucos etiam et sculptilia succidit atque comminuit, et super tumulos eorum qui eis immolare consueverant, fragmenta dispersit.
Watu wakazivunja madhabahu za Baali katika uwepo wake; akazibomoa nguzo za Maashera na na zile sanamu za kuchonga, na sanamu za chuma ya kuyeyushwa katika vipande hadi zikawa mavumbi. Akayasamabaza mavumbi juu ya makaburi ya wale ambao walizitolea sadaka.
5 Ossa præterea sacerdotum combussit in altaribus idolorum, mundavitque Judam et Jerusalem.
Akaichoma mifupa ya makuhani wao juu ya madhabahu zao. Katika namna hii, akaisafisha Yuda na Yerusalemu.
6 Sed et in urbibus Manasse, et Ephraim, et Simeon, usque Nephthali, cuncta subvertit.
Alifanya hivyo hivyo katika miji ya Manase, Efraimu, na Simeoni, sehemu zote hadi Neftali, na katika maeneo yaliyoizunguka.
7 Cumque altaria dissipasset, et lucos et sculptilia contrivisset in frustra, cunctaque delubra demolitus esset de universa terra Israël, reversus est in Jerusalem.
Alizivunja madhabahu, akayapiga Maashera, na sanamu za kuchonga kuwa unga, na kuzisambaratisha madhabahu zote za uvumba katika nchi yote ya Israeli; kisha akarudi Yerusalemu.
8 Igitur anno octavodecimo regni sui, mundata jam terra et templo Domini, misit Saphan filium Eseliæ, et Maasiam principem civitatis, et Joha filium Joachaz a commentariis, ut instaurarent domum Domini Dei sui.
Sasa katika kipindi cha miaka ishirini ya utawala wake, baada ya Yosia kuisafisha nchi na hekalu, alimtuma Shafani mwana wa Azali, Manaseya, akida wa mji, na Yoa mwana wa Yoahazi katibu, kuikarabati nyumba ya Yahwe Mungu wake.
9 Qui venerunt ad Helciam sacerdotem magnum: acceptamque ab eo pecuniam quæ illata fuerat in domum Domini, et quam congregaverant Levitæ, et janitores de Manasse, et Ephraim, et universis reliquiis Israël, ab omni quoque Juda, et Benjamin, et habitatoribus Jerusalem,
Wakaenda kwa Hilkia, kuhani mkuu, na wakakabidhi kwake fedha ambazo zilikuwa zimeletwa kwenye nyumbaa ya Mungu, ambazo Walawi, walinzi wa milingo, walikuwa wamekusanya kutoka Manase na Efraimu, kutoka kwa masalia wote wa Israeli, kutoka Yuda yote na Benyamini, na kutoka kwa wakaaji wa Yerusalemu.
10 tradiderunt in manibus eorum qui præerant operariis in domo Domini, ut instaurarent templum, et infirma quæque sarcirent.
Wakaikabidhi ile fedha kwa watu waliosimamia kazi ya hekalu la Yahwe. Watu wale wakawalipa wafanya kazi walioilikarabati na kulijenga tena hekalu.
11 At illi dederunt eam artificibus et cæmentariis, ut emerent lapides de lapicidinis, et ligna ad commissuras ædificii, et ad contignationem domorum quas destruxerant reges Juda.
Wakawalipa maseremala na wajenzi kwa ajili ya kununulia mawe ya kuchonga na mbao kwa ajili ya kuungia, na kutengeneza boriti za nyumba amabazo baadha ya wafalme wa Yuda waliziacha zikachakaa.
12 Qui fideliter cuncta faciebant. Erant autem præpositi operantium Jahath et Abdias de filiis Merari, Zacharias et Mosollam de filiis Caath, qui urgebant opus: omnes Levitæ scientes organis canere.
Watu waliifanya kazi kwa uaminifu. Wasimamizi wao Yahathi na Obadia, Walawi, wa wana wa Merari; na Zekaria na Meshulamu, kutoka kwa wana wa Wakohathi. Walawi wengine, wote kati ya wale waliokuwa wanamziki wazuri sana, kwa ukaribu waliwaelekeza watendakazi.
13 Super eos vero qui ad diversos usus onera portabant, erant scribæ, et magistri de Levitis, janitores.
Walawi hawa walikuwa viongoziz wa wale waliobeba vifaa vya ujenzi na watu wengine wote waliofanya kazi kwa namna yoyote ile. Pia palikuwa na Walawi ambao walikuwa makatibu, watawala na walinda lango.
14 Cumque efferrent pecuniam quæ illata fuerat in templum Domini, reperit Helcias sacerdos librum legis Domini per manum Moysi.
Walipoileta fedha ambayo ilikuwa imeletwa kwenye nyumba ya Yahwe, Hilkia yule kuhani akakiokota kitabu cha sheri ya Yahwe ambacho kilikuwa kimetolewa kupitia Musa.
15 Et ait ad Saphan scribam: Librum legis inveni in domo Domini: et tradidit ei.
Hilkia akamwambia Shafani yule mwandishi, “Nimekiokota kitabu cha sheria katika nyumba ya Yahwe”. Hilikia akakileta kitabu kwa Shefani.
16 At ille intulit volumen ad regem, et nuntiavit ei, dicens: Omnia quæ dedisti in manu servorum tuorum, ecce complentur.
Shefani akakipelek kitabu kwa mfalme, na pia akatoa taarifa kwake, akisema, “Watumishi wako wanafanya kila kitu walichokabidhiwa.
17 Argentum quod repertum est in domo Domini, conflaverunt, datumque est præfectis artificum, et diversa opera fabricantium.
Waliitoa feedha yote amabayo ilionekana katika nyumba ya Yahwe, na waliikabidhi katika mikono ya wasimamizi na watendakazi.”
18 Præterea tradidit mihi Helcias sacerdos hunc librum. Quem cum rege præsente recitasset,
Shefani mwandishi akamwambia mfalme.” Hilkia kuhani amenipa kitabu.” Kisha Shefani akamsomea mfalme katika hicho kitabu.
19 audissetque ille verba legis, scidit vestimenta sua:
Ikawa kwamba mfalme alipokuwa ameyasikia maneno ya sheria, aliyararua mavazi yake.
20 et præcepit Helciæ, et Ahicam filio Saphan, et Abdon filio Micha, Saphan quoque scribæ, et Asaæ servo regis, dicens:
Mflme akawaamuru Hilkia, Ahikamu mwana wa Shafani, Abdoni mwana wa Mika, Shafani mwaandishi, na Asaya, mtumishi wake, akisema,
21 Ite, et orate Dominum pro me, et pro reliquiis Israël et Juda, super universis sermonibus libri istius, qui repertus est: magnus enim furor Domini stillavit super nos, eo quod non custodierint patres nostri verba Domini ut facerent omnia quæ scripta sunt in isto volumine.
“Nendeni mkaulize mapenzi ya Yahwe kwa ajili yangu, na kwa wale waliobaki katika Israeli na Yuda, kwa sababu ya maneno ya kitabu ambacho kimeokotwa. Kwa maani ni kikuu, kwa sababu babu zetu hawakuyasikiliza maneno ya kitabu hiki ili kuyatii yote yaliyokuwa yameandikwa ndani yake”. (Badala ya “ambayo yamemiminwa juu yetu”, baadhi ya matoleo yanasema “ambayo yamemulikwa zidi yetu”).
22 Abiit ergo Helcias, et hi qui simul a rege missi fuerant, ad Oldam prophetidem, uxorem Sellum filii Thecuath filii Hasra custodis vestium, quæ habitabat in Jerusalem in Secunda: et locuti sunt ei verba quæ supra narravimus.
Kwa hiyo Hilkia, na wale ambao mfalme alikuwa amewaamuru, wakaenda kwa Hulda nabii wa kike, mke wa Shalumu mwana wa Tohathi mwana wa Hasra, mtunza mavazi (aliishi katika Yerusalemu katika wilaya ya pili), na walizungumza naye katika namna hii.
23 At illa respondit eis: Hæc dicit Dominus Deus Israël: Dicite viro qui misit vos ad me:
Akasema kwao, “Hivi ndivyo Yahwe, Mungu wa Israeli, anasema: Mwambie mtu aliyewatuma kwangu,
24 Hæc dicit Dominus: Ecce ego inducam mala super locum istum et super habitatores ejus, cunctaque maledicta quæ scripta sunt in libro hoc, quem legerunt coram rege Juda.
Hivi ndivyo Yahwe anasema: Ona, niko karibu kuleta maafa juu ya sehemu hii na wakaaaji wake, laana zote zilizoandikwa katika kitabu walichokisoma mbele ya mfalme wa Yuda.
25 Quia dereliquerunt me, et sacrificaverunt diis alienis, ut me ad iracundiam provocarent in cunctis operibus manuum suarum, idcirco stillabit furor meus super locum istum, et non extinguetur.
Kwa sababu wamenisahau na wametoa sadaka za uvumba kwa miungu mingine, ili kwamba waniweke katika hasira kwa matendo yote waliyofanya — kwa hiyo hasira yangu itamiminwa juu ya hii sehemu, na haitazimishwa. (Badala ya “ambayo yamemiminwa juu yetu”, baadhi ya matoleo yana “amabyo yamemlikwa zidi yetu”.)
26 Ad regem autem Juda, qui misit vos pro Domino deprecando, sic loquimini: Hæc dicit Dominus Deus Israël: Quoniam audisti verba voluminis,
Lakini kwa mfalme wa Yuda, aliyewatuma kumuuliza Yahwe alichopaswa kufanya, hivi ndivyo mtakavyosema kwake, 'Yahwe, Mungu wa Israeli anasema hivi: Kuhusu maneno uliyosika,
27 atque emollitum est cor tuum, et humiliatus es in conspectu Dei super his quæ dicta sunt contra locum hunc et habitatores Jerusalem, reveritusque faciem meam scidisti vestimenta tua, et flevisti coram me: ego quoque exaudivi te, dicit Dominus.
kwa sababu moyo wako ulipondeka, na ulijinyenyekeza mbele yangu ulipoyasikia maneno yake zidi ya sehemu hii na wakaaji wake, na kwa sababu umejinyenyekeza mwenyewe mbele zangu, pia nimekusikiliza —hili ni azimio la Yahwe—
28 Jam enim colligam te ad patres tuos, et infereris in sepulchrum tuum in pace: nec videbunt oculi tui omne malum quod ego inducturus sum super locum istum, et super habitatores ejus. Retulerunt itaque regi cuncta quæ dixerat.
ona, nitakukusanya kwa mababu zako. Utakusanywa katika kaburi lako kwa amani, na macho yako hayataona maafa yoyoye nitakayoleta juu ya sehemu hii na wakaaji wake”. Wale watu wakarudisha ujumbe huu kwa mfalme.
29 At ille convocatis universis majoribus natu Juda et Jerusalem,
Mfalme akatuma wajumbe na kuwakusanya wazee wote wa Yuda na Yerusalemu.
30 ascendit in domum Domini, unaque omnes viri Juda et habitatores Jerusalem, sacerdotes et Levitæ, et cunctus populus a minimo usque ad maximum. Quibus audientibus in domo Domini, legit rex omnia verba voluminis:
Kisha mfalme akaenda kwenye nyumba ya Yahwe, na watu wote wa Yuda wakaaji wa Yerusalemu, na makuhani, Walawi, na watu wote, kuanzia wakubwa hadi wadogo. Kisha akasoma mbele zao maneno yote ya kitabu cha Agano kilichokuwa kimeokotwa katika nyumba ya Yahwe.
31 et stans in tribunali suo, percussit fœdus coram Domino ut ambularet post eum, et custodiret præcepta, et testimonia, et justificationes ejus in toto corde suo, et in tota anima sua, faceretque quæ scripta sunt in volumine illo, quod legerat.
Mfalme aksimama katika sehemu yake na kufanya aganao mbele za Yahwe, kutembea mbele za Yahwe, na kuzishika amri zake, taratibu zake, na sheria zake, kwa moyo wake wote na roho yake yote, kuyatii maneno ya agano yaliyokuwa yameandikwa katika agano ambayo yalikuwa yameandikwa katika kitabu hiki.
32 Adjuravit quoque super hoc omnes qui reperti fuerant in Jerusalem et Benjamin: et fecerunt habitatores Jerusalem juxta pactum Domini Dei patrum suorum.
Aliwasababisha wote walioonekana katika Yerusalemu na Benyamini kusimama kwa agano. Wakaaji wa Yerusalemu wakatembea kwa agano la Mungu, Mungu wa babu zao.
33 Abstulit ergo Josias cunctas abominationes de universis regionibus filiorum Israël: et fecit omnes qui residui erant in Israël, servire Domino Deo suo. Cunctis diebus ejus non recesserunt a Domino Deo patrum suorum.
Yosia akapeleka mbali mambo yote ya machukizo kutoka kwenye nchi iliyomilikiw na watu wa Israeli. Akamfanya kila mtu katika Israeli amwabudu Yahwe, Mungu wao. Kwa maisha siku zake zote, hawakugeka mbali kwa kutomfuata Yahwe, Mungu wa mababu zao.

< Ii Paralipomenon 34 >