< Nehemiæ 1 >
1 Verba Nehemiæ filii Helchiæ. Et factum est in mense Casleu, anno vigesimo, et ego eram in Susis castro.
Maneno ya Nehemia mwana wa Hakalia Ikawa, katika mwezi wa Kisleu, katika mwaka wa ishirini, nilikuwa katika mji mkuu wa Sushani,
2 Et venit Hanani unus de fratribus meis, ipse et viri ex Iuda: et interrogavi eos de Iudæis, qui remanserant, et supererant de captivitate, et Ierusalem.
mmoja wa ndugu zangu, Hanani, alikuja pamoja na watu wengine kutoka Yuda, nami nikawauliza kuhusu Wayahudi waliopona, Wayahudi waliosalia waliokuwa huko, na kuhusu Yerusalemu.
3 Et dixerunt mihi: Qui remanserunt, et relicti sunt de captivitate ibi in provincia, in afflictione magna sunt, et in opprobrio: et murus Ierusalem dissipatus est, et portæ eius combustæ sunt igni.
Wakaniambia, “Wale waliokuwa katika mkoa ule waliookoka katika kifungo wapo katika shida kubwa na aibu kwa sababu ukuta wa Yerusalemu umebomolewa na milango yake imeteketezwa kwa moto.”
4 Cumque audissem verba huiuscemodi, sedi, et flevi, et luxi diebus multis: ieiunabam, et orabam ante faciem Dei cæli.
Na mara tu niliposikia maneno haya, nikakaa na kulia, na kwa siku niliendelea kuomboleza na kufunga na kuomba mbele ya Mungu wa mbinguni.
5 Et dixi: Quæso Domine Deus cæli fortis, magne atque terribilis, qui custodis pactum et misericordiam cum his qui te diligunt, et custodiunt mandata tua:
Ndipo nikasema, “Wewe ndiwe Bwana, Mungu wa mbinguni, Mungu uliye mkuu na kushangaza, unayetimiza agano na upendo wa kudumu pamoja na wale wanaokupenda na kushika amri zake.
6 fiant aures tuæ auscultantes, et oculi tui aperti ut audias orationem servi tui, quam ego oro coram te hodie nocte et die pro filiis Israel servis tuis: et confiteor pro peccatis filiorum Israel, quibus peccaverunt tibi: ego, et domus patris mei peccavimus,
Sikiliza maombi yangu na fungua macho yako, ili uisikie sala ya mtumishi wako kwamba sasa nasali mbele yako mchana na usiku kwa ajili ya watu wa Israeli watumishi wako. Mimi ninakiri dhambi za watu wa Israeli, ambazo tumefanya dhidi yako. Wote mimi na nyumba ya baba yangu tumefanya dhambi.
7 vanitate seducti sumus, et non custodivimus mandatum tuum, et ceremonias, et iudicia quæ præcepisti Moysi famulo tuo.
Tumefanya uovu sana juu yako, na hatukuzingatia amri, sheria, na hukumu ambazo ulimwamuru mtumishi wako Musa.
8 Memento verbi, quod mandasti Moysi servo tuo, dicens: Cum transgressi fueritis, ego dispergam vos in populos:
Tafadhali kumbuka neno ulilomuamuru mtumishi wako Musa, 'mkitenda pasipo uaminifu, nitawatawanya kati ya mataifa,
9 et si revertamini ad me, et custodiatis præcepta mea, et faciatis ea; etiamsi abducti fueritis ad extrema cæli, inde congregabo vos, et reducam in locum, quem elegi ut habitaret nomen meum ibi.
lakini mkirudi kwangu na kufuata amri zangu na kuzifanya, ingawa watu wako walienea chini ya mbingu za mbali, Nami nitawakusanya kutoka huko na kuwaleta mahali pale nilipopachagua ili kulifanya jina langu.'
10 Et ipsi servi tui, et populus tuus: quos redemisti in fortitudine tua magna, et in manu tua valida.
Sasa wao ni watumishi wako na watu wako, ambao uliwaokoa kwa nguvu yako kubwa na kwa mkono wako wenye nguvu.
11 Obsecro Domine, sit auris tua attendens ad orationem servi tui, et ad orationem servorum tuorum, qui volunt timere nomen tuum: et dirige servum tuum hodie, et da ei misericordiam ante virum hunc. Ego enim eram pincerna regis.
Bwana, naomba, sikiliza sasa maombi ya watumishi wako na sala ya watumishi wako ambao hufurahia kuheshimu jina lako. Sasa unifanikishe mimi mtumishi wako leo, na unijalie rehema mbele ya mtu huyu.” Nilikuwa mnyweshaji wa mfalme.