< Psalmorum 16 >
1 Tituli inscriptio, ipsi David. [Conserva me, Domine, quoniam speravi in te.
Unilinde, Mungu, kwa kuwa nakimbilia kwako kwa ajili ya usalama.
2 Dixi Domino: Deus meus es tu, quoniam bonorum meorum non eges.
Nami ninasema kwa Yahwe, “Wewe ni Bwana wangu; wema wangu ni bure pasipo wewe.
3 Sanctis qui sunt in terra ejus, mirificavit omnes voluntates meas in eis.
Kama kwa watakatifu walioko duniani, ndio walio bora; furaha yangu yote iko kwao.
4 Multiplicatæ sunt infirmitates eorum: postea acceleraverunt. Non congregabo conventicula eorum de sanguinibus, nec memor ero nominum eorum per labia mea.
Taabu yao itaongezeka, wale watafutao miungu mingine. Sitamimina sadaka ya damu kwa miungu yao. Wala kuyainua majina yao kwa midomo yao.
5 Dominus pars hæreditatis meæ, et calicis mei: tu es qui restitues hæreditatem meam mihi.
Yahwe, wewe ni sehemu ya chaguo langu na kikombe changu. Unaishikilia kesho yangu.
6 Funes ceciderunt mihi in præclaris; etenim hæreditas mea præclara est mihi.
Mistari iliyo pimwa imelelazwa mahari pa kufurahisha kwa ajili yangu; hakika urithi ufurahishao ni wangu.
7 Benedicam Dominum qui tribuit mihi intellectum; insuper et usque ad noctem increpuerunt me renes mei.
Nitakubariki Yahwe, wewe unishauliye; hata wakati wa usiku akili zangu za nielekeza.
8 Providebam Dominum in conspectu meo semper: quoniam a dextris est mihi, ne commovear.
Nimemuweka Yahwe mbele yangu kila wakati, ili nisitikisike kutoka mkono wake wa kuume.
9 Propter hoc lætatum est cor meum, et exsultavit lingua mea; insuper et caro mea requiescet in spe.
Kwa hiyo moyo wangu unafuraha, utukufu wangu washangilia. Hakika nitaishi katika usalama.
10 Quoniam non derelinques animam meam in inferno, nec dabis sanctum tuum videre corruptionem. (Sheol )
Kwa kuwa hautaiacha roho yangu kuzimuni. Wewe hautamuacha mwaminifu wako kuliona shimo. (Sheol )
11 Notas mihi fecisti vias vitæ; adimplebis me lætitia cum vultu tuo: delectationes in dextera tua usque in finem.]
Wewe hunifundisha njia ya maisha; furaha tele inakaa katika uwepo wako; furaha inakaa katika mkono wako wa kuume milele!”