< Micha Propheta 2 >

1 [Væ qui cogitatis inutile, et operamini malum in cubilibus vestris! In luce matutina faciunt illud, quoniam contra Deum est manus eorum.
Ole wao wale wanao wanaokusudia mabaya, kwa wale wanaokusudia kwenye vitanda vyao kufanya maovu. Katika asubuhi wanayafanya kwa sababu wana nguvu.
2 Et concupierunt agros, et violenter tulerunt: et rapuerunt domos, et calumniabantur virum, et domum ejus: virum, et hæreditatem ejus.
Wanatamani mashamba na kuyapunguza; wanazitamani nyumba na kuzichukua. Wanadhulumu mtu na nyumba yake, mtu na urithi wake.
3 Idcirco hæc dicit Dominus: Ecce ego cogito super familiam istam malum, unde non auferetis colla vestra, et non ambulabitis superbi: quoniam tempus pessimum est.
Kwa hiyo Yahwe asema hivi, “Tazama, nakaribia kuleta janga dhidi ya huu ukoo, ambalo hamtazitoa shingo zenu. Hamtatembea kwa kiburi, kwa kuwa itakuwa wakati wa uovu.
4 In die illa sumetur super vos parabola, et cantabitur canticum cum suavitate, dicentium: Depopulatione vastati sumus; pars populi mei commutata est: quomodo recedet a me, cum revertatur, qui regiones nostras dividat?
Katika siku hiyo maadui zako wataimba wimbo kuhusu wewe, na kuomboleza kwa maombolezo ya huzuni. Wataimba, 'Sisi Waisraeli tumeangamizwa kabisa; Yahwe hubadilisha eneo la watu wangu. Je ataliondoaje kutoka kwangu? Huwagawia mshamba yetu kusaliti.”'
5 Propter hoc non erit tibi mittens funiculum sortis in cœtu Domini.
Kwa hiyo, ninyi watu matajiri hamtakuwa uzao kugawanya eneo kwa kupiga kura katika mkutano wa Yahwe.
6 Ne loquamini loquentes; non stillabit super istos, non comprehendet confusio.
“Msitabiri,” wanasema. “Hawatayatabiri haya mambo; lawama hazitakuja.”
7 Dicit domus Jacob: Numquid abbreviatus est spiritus Domini, aut tales sunt cogitationes ejus? nonne verba mea bona sunt cum eo qui recte graditur?
Je litasemwa kweli, nyumba ya Yakobo, “je Roho ya Yahwe? Je haya ni matendo yake kweli?” Maneno yangu hayafai kwa kila mmoja atembeaye kwa unyoofu?
8 et e contrario populus meus in adversarium consurrexit. Desuper tunica pallium sustulistis: et eos qui transibant simpliciter convertistis in bellum.
Hivi karibuni watu wangu wameinuka kama adui. Mmelivua joho, nguo, kutoka wale wapitao wasioshutumiwa, kama maaskari kurudi kutoka kwenye vita kwa kile wakifikiriacho ni salama.
9 Mulieres populi mei ejecistis de domo deliciarum suarum; a parvulis earum tulistis laudem meam in perpetuum.
Mnawaendesha wanawake wangu kwa watu wangu kutoka kwenye nyumba nzuri; mnachukua baraka kutoka kwa watoto wao wadogo daima.
10 Surgite, et ite, quia non habetis hic requiem: propter immunditiam ejus corrumpetur putredine pessima.
Inukeni na muondoke, kwa kuwa hii sio sehemu ambayo mnaweza kuishi, kwa sababu ya unajisi wake; imeangamizwa kwa maangamizo kabisa.
11 Utinam non essem vir habens spiritum, et mendacium potius loquerer! Stillabo tibi in vinum et in ebrietatem; et erit super quem stillatur populus iste.
Kama mtu akija kwenu katika roho ya uongo na kudanganya na kusema, “Nitatabiri kwenu kuhusu mvinyo na kilevi kikali,” angeweza kufikiriwa kuwa nabii kwa ajili ya hawa watu.
12 Congregatione congregabo, Jacob, totum te; in unum conducam reliquias Israël: pariter ponam illum quasi gregem in ovili, quasi pecus in medio caularum: tumultuabuntur a multitudine hominum.
Nitawaleta pamoja wote hakika, Yakobo. Hakika nitawakusanya mabaki ya Israeli. Nitawaleta pamoja kama kondoo katika zizi, kama kundi la wanyama katika malisho. Kutakuwa na kelele kwasababu ya wingi wa watu.
13 Ascendet enim pandens iter ante eos: divident, et transibunt portam, et ingredientur per eam: et transibit rex eorum coram eis, et Dominus in capite eorum.]
Mtu avunjaye hufungua njia zao kwa ajili yao kwenda mbele yao. Wamebomoa kupitia lango na kutoka nje; mfalme wao atapita mbele yao. Yahwe atakuwa mbele yao.

< Micha Propheta 2 >