< Exodus 34 >

1 Ac deinceps: Præcide, ait, tibi duas tabulas lapideas instar priorum, et scribam super eas verba, quæ habuerunt tabulæ quas fregisti.
Yahweh akamwabia Musa, “Kata mbao mbili za mawe kama zile za awali. Nitaandika kwenye hizi mbao za mawe maneno yaliyo kuwa kwenye mbao za mawe za mwanzo, mbao za mawe ulizo zivunja.
2 Esto paratus mane, ut ascendas statim in montem Sinai, stabisque mecum super verticem montis.
Kuwa tayari asubui na uje Mlima Sinai, na uje mbele zangu juu ya mlima.
3 Nullus ascendat tecum, nec videatur quispiam per totum montem: boves quoque et oves non pascantur e contra.
Hakuna atakaye kuja nawe. Usiruhusu mtu yeyote aonekana popote kwenye mlima. Hakuna kundi la mifugo wanao ruhusiwa ata kula mbele ya mlima.”
4 Excidit ergo duas tabulas lapideas, quales antea fuerant: et de nocte consurgens ascendit in montem Sinai, sicut præceperat ei Dominus, portans secum tabulas.
Hivyo Musa akakata mbao mbili za mawe kama za mwanzo, na akaamka asubui mapema na kwenda juu ya Mlima Sinai, kama Yahweh alivyo muelekeza. Musa alibeba mbao za mawe mikononi mwake.
5 Cumque descendisset Dominus per nubem, stetit Moyses cum eo, invocans nomen Domini.
Yahweh akaja chini katika wingu na akasima mbele za Musa, na akatamka jina “Yahweh.”
6 Quo transeunte coram eo, ait: Dominator Domine Deus, misericors et clemens, patiens et multæ miserationis, ac verax,
Yahweh akapita kwake na kukiri, “Yahweh, Yahweh, Mungu ni wa rehema na wa neema, sio mwepesi wa hasira, na anadumu katika uwaminifu wa agano na uadilifu,
7 qui custodis misericordiam in millia; qui aufers iniquitatem, et scelera, atque peccata, nullusque apud te per se innocens est; qui reddis iniquitatem patrum filiis, ac nepotibus in tertiam et quartam progeniem.
ukishika uaminifu wa agano kwa vizazi maelfu, ukisamehe maasi, makosa, na dhambi. Lakini hamsafishi mwenye hatia. Ataleta adhabu ya dhambi za baba kwa watoto wao na watoto wa watoto wao, kwa kizazi cha tatu na hadi cha nne.”
8 Festinusque Moyses, curvatus est pronus in terram, et adorans
Musa haraka akainamisha kichwa chake kwenye ardhi na kuabudu.
9 ait: Si inveni gratiam in conspectu tuo, Domine, obsecro ut gradiaris nobiscum (populus enim duræ cervicis est) et auferas iniquitates nostras atque peccata, nosque possideas.
Kisha akasema, “Kama sasa nimepata upendeleo machoni pako, Bwana wangu, tafadhali nenda pamoja nasi, kwa kuwa hawa watu ni wa korofi. Samehe maasi yetu na dhambi zetu, na utuchukuwe kama urithi wako.”
10 Respondit Dominus: Ego inibo pactum videntibus cunctis: signa faciam quæ numquam visa sunt super terram, nec in ullis gentibus, ut cernat populus iste, in cujus es medio, opus Domini terribile quod facturus sum.
Yahweh akasema, “Ona, ninakaribu kufanya agano. Mbele za watu wako, nitafanya maajabu ambayo hayajawai kufanywa duniani kote wala kwenye taifa lote. Watu wote miongoni mwako wataona matendo yangu, kwa kuwa ni kitu cha hofu ninacho fanya kwako.
11 Observa cuncta quæ hodie mando tibi: ego ipse ejiciam ante faciem tuam Amorrhæum, et Chananæum, et Hethæum, Pherezæum quoque, et Hevæum, et Jebusæum.
Tii amri zangu leo. Ninawaondoa mbele yako Waamori, Wakanani, Wahivi, Wahiti, Waperizi, Wahivi, na Wayebusi.
12 Cave ne umquam cum habitatoribus terræ illius jungas amicitias, quæ sint tibi in ruinam:
Kuwa mwanglifu usifanye agano na wakazi wa nchi unayo kwenda, au wata kuwa mtego kwako.
13 sed aras eorum destrue, confringe statuas, lucosque succide:
Badala yake, lazima uvunje madhabahu zao, ponda nguzo zao za mawe, na kukata nguzo zao za Ashera.
14 noli adorare deum alienum. Dominus zelotes nomen ejus; Deus est æmulator.
Kwa kuwa wewe haupaswi kumuabudu mungu mwingine, maana Yahweh, ambaye jina lake ni Uwivu, ni Mungu wa uwivu.
15 Ne ineas pactum cum hominibus illarum regionum: ne, cum fornicati fuerint cum diis suis, et adoraverint simulacra eorum, vocet te quispiam ut comedas de immolatis.
Hivyo kuwa mwangalifu usifanye agano na wakazi wa nchi, kwa kuwa wanajifanyia ukahaba kwa miungu yao, na wanatoa dhabihu kwa miungu yao. Kisha mmoja wao ata kukaribisha na wewe utakula baadhi ya dhabihu zake,
16 Nec uxorem de filiabus eorum accipies filiis tuis: ne, postquam ipsæ fuerint fornicatæ, fornicari faciant et filios tuos in deos suos.
na kisha utachukuwa baadhi ya mabinti zake kwa wanao, na mabinti wake watafanya ukahaba kwa miungu yao, na watafanya wanao kufanya ukahaba kwa miungu yao.
17 Deos conflatiles non facies tibi.
Usifanye Miungu ya chuma ya kuyayusha.
18 Solemnitatem azymorum custodies. Septem diebus vesceris azymis, sicut præcepi tibi, in tempore mensis novorum: mense enim verni temporis egressus es de Ægypto.
Laziam ushike Sherehe ya Mkate Usiotiwachachu. Kama nilivyo kuamuru, lazima ule mkate usio na hamira kwa siku saba kwa muda uliotengwa wa mwezi wa Abibu, maana nikatika mwezi wa Abibu ulitoka Misri.
19 Omne quod aperit vulvam generis masculini, meum erit. De cunctis animantibus, tam de bobus, quam de ovibus, meum erit.
Wazaliwa wote ni mwangu, ata mzaliwa wa kwanza wa kiume wa mifugo, yote ya ng'ombe na kondoo.
20 Primogenitum asini redimes ove: sin autem nec pretium pro eo dederis, occidetur. Primogenitum filiorum tuorum redimes: nec apparebis in conspectu meo vacuus.
Lazima umnunue tena mzaliwa kwanza wa punda kwa kondoo, lakini usipo mnunua tena, kisha uivunje shingo yake. Lazima ununue tena wazaliwa wa kwanza wote wa wanao. Hakuna ata mmoja atakye kuja kwangu mikono mitupu.
21 Sex diebus operaberis; die septimo cessabis arare et metere.
Utafanya kazi kwa siku sita, lakini siku ya saba utapumzika. Ata wakati wakilimo na wa mavuno, lazima upumzike.
22 Solemnitatem hebdomadarum facies tibi in primitiis frugum messis tuæ triticeæ, et solemnitatem, quando redeunte anni tempore cuncta conduntur.
Lazima uadhimishe Sherehe ya Majuma kwa mazao ya kwanza ya mavuno ya ngano, na lazima uadhimishe Sherehe ya Makusanyo mwisho wa mwaka.
23 Tribus temporibus anni apparebit omne masculinum tuum in conspectu omnipotentis Domini Dei Israël.
Mara tatu kwa mwaka wanaume wenu wote watajitokeza kwa Bwana Yahweh, Mungu wa Israeli.
24 Cum enim tulero gentes a facie tua, et dilatavero terminos tuos, nullus insidiabitur terræ tuæ, ascendente te, et apparente in conspectu Domini Dei tui ter in anno.
Kwa kuwa nitaondoa mataifa mbele yenu na kutanua mipika. Hakuna atakaye tamani kuwa na ardhi yenu kama yao utakapo toka mbele za Yahweh mara tatu kwa mwaka.
25 Non immolabis super fermento sanguinem hostiæ meæ: neque residebit mane de victima solemnitatis Phase.
Hautatoa damu ya dhabihu yangu na hamira yeyote, wala nyama yeyote kutoka dhabihu za Sherehe ya Pasaka kubaki hadi asubui.
26 Primitias frugum terræ tuæ offeres in domo Domini Dei tui. Non coques hædum in lacte matris suæ.
Lazima ulete matunda ya kwanza yalio bora kutoka nyumbani kwako. Usimchemshe mbuzi mtoto katika maziwa ya mama yake.”
27 Dixitque Dominus ad Moysen: Scribe tibi verba hæc, quibus et tecum et cum Israël pepigi fœdus.
Yahweh akamwabia Musa, “Andika chini haya maneno, kwa kuwa nimejiahidi haya maneno niliyo yasema, na nimefanya agano kwako na Israeli.”
28 Fuit ergo ibi cum Domino quadraginta dies et quadraginta noctes: panem non comedit, et aquam non bibit, et scripsit in tabulis verba fœderis decem.
Musa alikuwa huko na Yahweh kwa siku arobaini na usiku; hakula chakula chochote wala kunywa maji yeyote. Aliandika katika mbao maneno ya agano, Amri kumi.
29 Cumque descenderet Moyses de monte Sinai, tenebat duas tabulas testimonii, et ignorabat quod cornuta esset facies sua ex consortio sermonis Domini.
Musa alipo shuka chini ya Mlima Sinai na mbao mbili za agano za ushuhuda mikononi mwake, hakujua kuwa ngozi ya kuwa uso wake ulikuwa wa'ngaa akizungumza na Mungu.
30 Videntes autem Aaron et filii Israël cornutam Moysi faciem, timuerunt prope accedere.
Wakati Aruni na Waisraeli walipo muona Musa, ngozi ya uso wake ulikuwa wa ng'aa, na waliogopa kuja karibu yake.
31 Vocatique ab eo, reversi sunt tam Aaron, quam principes synagogæ. Et postquam locutus est ad eos,
Lakini Musa aliwaita, na Aruni na viongozi wa jamii wakaja kwake. Kisha Musa akasema nao.
32 venerunt ad eum etiam omnes filii Israël: quibus præcepit cuncta quæ audierat a Domino in monte Sinai.
Baada ya haya, watu wote wa Israeli wakaja kwa Musa, na akawambia amri zote Yahweh alizo mpa katika Mlima Sinai.
33 Impletisque sermonibus, posuit velamen super faciem suam.
Musa alipo maliza kuzungumza nao, alifunika uso wake kwa kitambaa.
34 Quod ingressus ad Dominum, et loquens cum eo, auferebat donec exiret, et tunc loquebatur ad filios Israël omnia quæ sibi fuerant imperata.
Wakati Musa alipoenda mbele za Yahweh kusema naye, aliondoa kitambaa, hadi alipo toka. Alipo toka, aliwaambia Waisraeli alicho amriwa kusema.
35 Qui videbant faciem egredientis Moysi esse cornutam, sed operiebat ille rursus faciem suam, siquando loquebatur ad eos.
Waisraeli walipo muona Musa ana'ngaa uso, alirudisha kitambaa tena usoni mpaka alipokuwa anaenda kuongea na Yahweh.

< Exodus 34 >