< 창세기 41 >

1 만 이년 후에 바로가 꿈을 꾼즉 자기가 하숫가에 섰는데
Ikawa mwishoni mwa miaka miwili mizima Farao akaota ndoto.
2 보니 아름답고 살찐 일곱 암소가 하수에서 올라와 갈밭에서 뜯어먹고
Tazama, alikuwa amesimama kando ya Nile. Tazama, ng'ombe saba wakatoka katika mto Nile, wakupendeza na wanene, na wakajilisha katika nyasi.
3 그 뒤에 또 흉악하고 파리한 다른 일곱 암소가 하수에서 올라와 그 소와 함께 하숫가에 섰더니
Tazama, ng'ombe wengine saba wakatoka katika Nile baada yao, wasiopendeza na wamekondeana. Wakasimama ukingoni mwa mto kando ya wale ng'ombe wengine.
4 그 흉악하고 파리한 소가 그 아름답고 살찐 일곱 소를 먹은지라 바로가 곧 깨었다가
Kisha wale ng'ombe wasiopendeza na waliokonda wakawala wale waliokuwa wanapendeza na walionenepa.
5 다시 잠이 들어 꿈을 꾸니 한 줄기에 무성하고 충실한 일곱 이삭이 나오고
Kisha Farao akaamka. Kisha akalala na kuota mara ya pili. Tazama, masuke saba ya nafaka yalichipua katika mche mmoja, mema na mazuri.
6 그 후에 또 세약하고 동풍에 마른 일곱 이삭이 나오더니
Tazama, masuke saba, membamba na yaliyokaushwa na upepo wa mashariki, yakachipua baada yake.
7 그 세약한 일곱 이삭이 무성하고 충실한 일곱 이삭을 삼킨지라 바로가 깬즉 꿈이라
Masuke membamba yakayameza yale masuke saba mema yote. Farao akaamka, na, tazama, ilikuwa ni ndoto tu.
8 아침에 그 마음이 번민하여 보내어 애굽의 술객과 박사를 모두 불러 그들에게 그 꿈을 고하였으나 그것을 바로에게 해석하는 자가 없었더라
Ikawa wakati wa asubuhi roho yake ikafadhaika. Akatuma na kuwaita waganga na wenye hekima wote wa Misri. Farao akawasimlia ndoto zake, lakini hakuna aliyeweza kumtafsiria Farao.
9 술 맡은 관원장이 바로에게 고하여 가로되 내가 오늘날 나의 허물을 추억하나이다
Kisha mkuu wa wanyweshaji akamwambia Farao, “Leo ninayafikiri makosa yangu.
10 바로께서 종들에게 노하사 나와 떡 굽는 관원장을 시위대장의 집에 가두셨을 때에
Farao aliwakasirikia watumishi wake, na kutuweka kifungoni katika nyumba ya kapteni wa walinzi, mkuu wa waokaji na mimi.
11 나와 그가 하룻밤에 꿈을 꾼즉 각기 징조가 있는 꿈이라
Tuliota ndoto usiku huo mmoja, yeye na mimi. Kila mmoja aliota kwa kadili ya tafsiri yake.
12 그곳에 시위대장의 종된 히브리 소년이 우리와 함께 있기로 우리가 그에게 고하매 그가 우리의 꿈을 풀되 그 꿈대로 각인에게 해석하더니
Pamoja nasi kulikuwa na kijana Mwebrania, mtumishi wa kapteni wa walinzi. Tulimwambia na akatutafsiria ndoto zetu. Alitutafsiria kila mmoja wetu kulingana na ndoto yake.
13 그 해석한 대로 되어 나는 복직하고 그는 매여 달렸나이다
Ikawa kama alivyotutafsiria, ndivyo ilivyokuwa. Farao alinirudisha katika nafasi yangu, lakini akamtundika yule mwingine.”
14 이에 바로가 보내어 요셉을 부르매 그들이 급히 그를 옥에서 낸지라 요셉이 곧 수염을 깎고 그 옷을 갈아 입고 바로에게 들어오니
Ndipo Farao alipotuma na kumwita Yusufu. Kwa haraka wakamtoa gerezani. Akajinyoa mwenyewe, akabadili mavazi yake, na akaingia kwa Farao.
15 바로가 요셉에게 이르되 내가 한 꿈을 꾸었으나 그것을 해석하는 자가 없더니 들은즉 너는 꿈을 들으면 능히 푼다더라
Farao akamwambia Yusufu, “Nimeoda ndoto, lakini hakuna wa kuitafsiri. Lakini nimesikia kuhusu wewe, kwamba unaposikia ndoto unaweza kuitafsiri.”
16 요셉이 바로에게 대답하여 가로되 이는 내게 있는 것이 아니라 하나님이 바로에게 평안한 대답을 하시리이다
Yusufu akamjibu Farao, kusema, “Siyo katika mimi. Mungu atamjibu Farao kwa uhakika.”
17 바로가 요셉에게 이르되 내가 꿈에 하숫가에 서서
Farao akamwambia Yusufu, “Katika ndoto yangu, tazama, nilisimama katika ukingo wa Nile.
18 보니 살지고 아름다운 일곱 암소가 하숫가에 올라와 갈밭에서 뜯어 먹고
Tazama, ng'ombe saba wakatoka ndani ya Nile, wanene na wakuvutia, nao wakajilisha katika nyasi.
19 그 뒤에 또 약하고 심히 흉악하고 파리한 일곱 암소가 올라오니 그같이 흉악한 것들은 애굽 땅에서 내가 아직 보지 못한 것이라
Tazama, ng'ombe wengine saba wakapanda baada yao, dhaifu, wabaya, na wembaba. Sijawao kuona wabaya kama hao katika nchi yote ya Misri.
20 그 파리하고 흉악한 소가 처음의 일곱 살찐 소를 먹었으며
Wale ng'ombe wembamba na wabaya wakawala wale ng'ombe saba na wanene.
21 먹었으나 먹은듯하지 아니하여 여전히 흉악하더라 내가 곧 깨었다가
Walipokuwa wamemaliza kuwala wote, haikujulikana kama walikuwa wamewala, kwani walibaki wabaya kama mwanzo. Kisha nikaamka.
22 다시 꿈에 보니 한 줄기에 무성하고 충실한 일곱 이삭이 나오고
Niliona katika ndoto yangu, na tazama, masuke saba yakatoka katika bua moja, jema na limejaa.
23 그 후에 또 세약하고 동풍에 마른 일곱 이삭이 나더니
Tazama, masuke saba zaidi, yaliyonyauka, membamba na yamekaushwa na upepo wa mashariki, yakachipua baada yake.
24 그 세약한 이삭이 좋은 일곱 이삭을 삼키더라 내가 그 꿈을 술객에게 말하였으나 그것을 내게 보이는 자가 없느니라
Yale masuke membamba yakayameza masuke saba mema. Niliwaambia waganga ndoto hizi, lakini hakuna aliyeweza kunielezea.”
25 요셉이 바로에게 고하되 바로의 꿈은 하나이라 하나님이 그 하실 일을 바로에게 보이심이니이다
Yusufu akamwambia Farao, “Ndoto za Farao ni moja. Mungu amemwambia Farao kuhusu jambo analokwenda kulifanya.
26 일곱 좋은 암소는 일곱 해요 일곱 좋은 이삭도 일곱 해니 그 꿈은 하나이라
Wale ng'ombe saba wema ni miaka saba, na masuke saba mema ni miaka saba. Ndoto ni moja.
27 그 후에 올라온 파리하고 흉악한 일곱 소는 칠년이요 동풍에 말라 속이 빈 일곱 이삭도 일곱 해 흉년이니
Na wale ng'ombe saba wembamba na wabaya waliokuja baadaye ni miaka saba, na pia masuke saba membamba yaliyokaushwa na upepo wa mashariki itakuwa miaka saba ya njaa.
28 내가 바로에게 고하기를 하나님이 그 하실 일로 바로에게 보이신다 함이 이것이라
Hilo ni jambo nililomwambia Farao. Mungu amemfunulia Farao jambo analokwenda kulifanya.
29 온 애굽 땅에 일곱 해 큰 풍년이 있겠고
Tazama, miaka saba yenye utele mwingi inakuja katika nchi yote ya Misri.
30 후에 일곱 해 흉년이 들므로 애굽 땅에 있던 풍년을 다 잊어버리게 되고 이 땅이 기근으로 멸망되리니
Na miaka saba ya njaa itakuja baada yake, na utele wote katika nchi ya Misri utasahaulika, na njaa itaiaribu nchi.
31 후에 든 그 흉년이 너무 심하므로 이전 풍년을 이 땅에서 기억하지 못하게 되리이다
Utele hautakumbukwa katika nchi kwa sababu ya njaa itakayofuata, kwa kuwa itakuwa kali sana.
32 바로께서 꿈을 두 번 겹쳐 꾸신 것은 하나님이 이 일을 정하셨음이라 속히 행하시리니
Kwamb ndoto ilijirudia kwa Farao sababu ni kwamba jambo hili limeanzishwa na Mungu, na Mungu atalitimiza hivi karibuni.
33 이제 바로께서는 명철하고 지혜있는 사람을 택하여 애굽 땅을 치리하게 하시고
Basi Farao atafute mtu mwenye maharifa na busara, na kumweka juu ya nchi ya Misri.
34 바로께서는 또 이같이 행하사 국중에 여러 관리를 두어 그 일곱 해 풍년에 애굽 땅의 오분의 일을 거두되
Farao na afanye hivi: achague wasimamizi juu ya nchi. Na wachukue sehemu ya tano ya mazao ya Misri katika miaka saba ya shibe.
35 그 관리로 장차 올 풍년의 모든 곡물을 거두고 그 곡물을 바로의 손에 돌려 양식을 위하여 각 성에 적치하게 하소서
Na wakusanye chakula chote cha hii miaka myema ijayo na kuitunza nafaka chini ya mamlaka ya Farao, kwa chakula kutumika katika miji. Wakiifadhi.
36 이와 같이 그 곡물을 이 땅에 저장하여 애굽 땅에 임할 일곱 해 흉년을 예비하시면 땅이 이 흉년을 인하여 멸망치 아니하리이다
Chakula kitakuwa matumizi ya nchi kwa miaka saba ya njaa itakayokuwa katika nchi ya Misri. Kwa njia hii nchi haitaaribiwa na njaa.”
37 바로와 그 모든 신하가 이 일을 좋게 여긴지라
Ushauri huu ukawa mwema machoni pa Farao na machoni pa watumishi wake wote.
38 바로가 그 신하들에게 이르되 이와 같이 하나님의 신에 감동한 사람을 우리가 어찌 얻을 수 있으리요 하고
Farao akawambia watumishi wake, “Je tunaweza kumpata mtu kama huyu, ambaye ndani yake kuna Roho wa Mungu?”
39 요셉에게 이르되 하나님이 이 모든 것을 네게 보이셨으니 너와 같이 명철하고 지혜있는 자가 없도다
Hivyo Farao akamwambia Yusufu, “Kwa vile Mungu amekuonesha yote haya, hakuna mtu mwenye ufahamu na busara kama wewe.
40 너는 내 집을 치리하라 내 백성이 다 네 명을 복종하리니 나는 너보다 높음이 보좌뿐이니라
Utakuwa juu ya nyumba yangu, watu wangu watatawaliwa kwa kadili ya neno lako. Katika kiti cha enzi peke yake mimi nitakuwa mkuu kuliko wewe.”
41 바로가 또 요셉에게 이르되 내가 너로 애굽 온 땅을 총리하게 하노라 하고
Farao akamwambia Yusufu, “Tazama, nimekuweka juu ya nchi yote ya Misri.”
42 자기의 인장 반지를 빼어 요셉의 손에 끼우고 그에게 세마포 옷을 입히고 금사슬을 목에 걸고
Farao akavua pete yake ya mhuri kutoka katika mkono wake na kuiweka katika mkono wa Yusufu. Akamvika kwa mavazi ya kitani safi, na kuweka mkufu wa dhahabu shingoni mwake.
43 자기에게 있는 버금 수레에 그를 태우매 무리가 그 앞에서 소리 지르기를 엎드리라 하더라 바로가 그로 애굽 전국을 총리하게 하였더라
Akataka apandishwe katika kibandawazi cha pili alichokuwa nacho. Watu wakapiga kelele mbele yake, “Pigeni magoti.” Farao akamweka juu ya nchi yote ya Misri.
44 바로가 요셉에게 이르되 나는 바로라 애굽 온 땅에서 네 허락 없이는 수족을 놀릴 자가 없으리라 하고
Farao akamwambia Yusufu, “Mimi ni Farao, mbali na wewe, hakuna mtu atakayeinua mkono wake au mguu wake katika nchi ya Misri.”
45 그가 요셉의 이름을 사브낫바네아라 하고 또 온 제사장 보디베라의 딸 아스낫을 그에게 주어 아내를 삼게 하니라 요셉이 나가 애굽 온 땅을 순찰하니라
Farao akamwita Yusufu jina la Zafenathi Panea.” Akampa Asenathi, binti wa Potifera kuhani wa On, kuwa mke wake. Yusufu akaenda juu ya nchi yote ya Misri.
46 요셉이 애굽왕 바로 앞에 설 때에 삼십 세라 그가 바로 앞을 떠나 애굽 온 땅을 순찰하니
Yusufu alikuwa na umri wa miaka thelathini aliposimama mbele ya Farao, mfalme wa Misri. Yusufu akatoka mbele ya Farao, na kwenda katika nchi yote ya Misri.
47 일곱 해 풍년에 토지 소출이 심히 많은지라
Katika miaka saba ya shibe nchi ilipozaa kwa wingi.
48 요셉이 애굽 땅에 있는 그 칠년 곡물을 거두어 각성에 저축하되 각성 주위의 밭의 곡물을 그 성중에 저장하매
Akakusanya chakula chote cha miaka saba iliyokuwako katika nchi ya Misri na kukiweka chakula katika miji. Akaweka katika kila mji chakula cha mashamba yaliyokizunguka.
49 저장한 곡식이 바다 모래 같이 심히 많아 세기를 그쳤으니 그 수가 한이 없음이었더라
Yusufu akahifadhi nafaka kama mchanga wa bahari, kingi kiasi kwamba akaacha kuhesabu, kwa sababu kilikuwa hakihesabiki.
50 흉년이 들기 전에 요셉에게 두 아들을 낳되 곧 온 제사장 보디베라의 딸 아스낫이 그에게 낳은지라
Kabla miaka ya njaa kuingia Yusufu akapata wana wawili, ambao Asenathi, binti wa Potifera kuhani wa On, alimzalia.
51 요셉이 그 장자의 이름을 므낫세라 하였으니 하나님이 나로 나의 모든 고난과 나의 아비의 온 집 일을 잊어버리게 하셨다 함이요
Yusufu akamwita mzaliwa wake wa kwanza Manase, kwani alisema, “Mungu amenisahaurisha shida zangu zote na nyumba yote ya baba yangu.”
52 차자의 이름을 에브라임이라 하였으니 하나님이 나로 나의 수고 한 땅에서 창성하게 하셨다 함이었더라
Akamwita mwanawe wa pili Efraimu, kwani alisema, Mungu amenipa uzao katika nchi ya mateso yangu.”
53 애굽 땅에 일곱 해 풍년이 그치고
Miaka saba ya shibe iliyokuwa katika nchi ya Misri ikafika mwisho.
54 요셉의 말과 같이 일곱 해 흉년이 들기 시작하매 각국에는 기근이 있으나 애굽 온 땅에는 식물이 있더니
Miaka saba ya njaa ikaanza, kama alivyokuwa amesema Yusufu. Kulikuwa na njaa katika nchi zote, lakini katika nchi yote ya Misri kulikuwa na chakula.
55 애굽 온 땅이 주리매 백성이 바로에게 부르짖어 양식을 구하는지라 바로가 애굽 모든 백성에게 이르되 요셉에게 가서 그가 너희에게 이르는 대로 하라 하니라
Nchi yote ya Misri ilipokuwa na njaa, watu wakapiga kelele kwa Farao kwa ajili ya chakula. Farao akawambia Wamisri wote, “Nendeni kwa Yusufu na mfanye atakavyosema.”
56 온 지면에 기근이 있으매 요셉이 모든 창고를 열고 애굽 백성에게 팔새 애굽 땅에 기근이 심하며
Njaa ilikuwa juu ya uso wote wa nchi. Yusufu akafungua ghala zote na kuuza chakula kwa Wamisri. Njaa ilikuwa kali sana katika nchi ya Misri.
57 각국 백성도 양식을 사려고 애굽으로 들어와 요셉에게 이르렀으니 기근이 온 세상에 심함이었더라
Dunia yote ikaja Misri kununua nafaka kutoka kwa Yusufu, kwani njaa ilikuwa kali katika dunia yote.

< 창세기 41 >