< 출애굽기 12 >
1 여호와께서 애굽 땅에서 모세와 아론에게 일러 가라사대
Yahweh akasema na Musa na Aruni katika nchi ya Misri. Alisema,
2 이 달로 너희에게 달의 시작 곧 해의 첫 달이 되게 하고
“Kwako wewe, mwezi huu utakuwa mwanzo wa miezi, mwezi wa kwanza wa mwaka kwako.
3 너희는 이스라엘 회중에게 고하여 이르라 이 달 열흘에 너희 매인이 어린 양을 취할지니 각 가족대로 그 식구를 위하여 어린 양을 취하되
Liambie kusanyiko la Israeli, 'Siku ya kumi mwezi huu kila mtu lazima achukuwe mwana kondoo au mbuzi mdogo wa kwake, kila familia ifanye hivi, mwana kondoo kwa kila nyumba.
4 그 어린 양에 대하여 식구가 너무 적으면 그 집의 이웃과 함께 수를 따라서 하나를 취하며 각 사람의 식량을 따라서 너희 어린 양을 계산할 것이며
Kama hiyo nyumba ni ndogo sana kwa mwana kondoo, mwanaume na jirani yake wachukuwe mwana kondoo au nyama ya mbuzi mdogo ambayo itatosha watu. Lazima iwe yatosha kwa kila mtu kula, kwaiyo lazima wachukuwe nyama ya kutosha kulisha wote.
5 너희 어린 양은 흠 없고 일년 된 수컷으로 하되 양이나 염소 중에서 취하고
Mwana kondoo wako au mbuzi wako mdogo lazima asiwe na upungufu, dume mwenye mwaka mmoja. Unaweza kuchukuwa mmoja wa kondoo au mbuzi.
6 이달 십사 일까지 간직하였다가 해질 때에 이스라엘 회중이 그 양을 잡고
Lazima umtunze mpaka siku ya kumi na nne ya huo mwezi. Kisha kusanyiko lote la Israeli lazima liwaue hawa wanyama jioni.
7 양을 먹을 집 문 좌우 설주와 인방에 바르고
Lazima uchukuwe baadhi ya damu na uweke kwenye sehemu mbili za mihimili ya milango na juu ya fremu za milango ambapo utalia hizo nyama.
8 그 밤에 그 고기를 불에 구워 무교병과 쓴 나물과 아울러 먹되
Lazima ule hizo nyama usiku, baada ya kuchoma kwenye moto. Kula na mkate ulio andaliwa kwa hamira, pamoja na mimea michungu.
9 날로나 물에 삶아서나 먹지 말고 그 머리와 정강이와 내장을 다 불에 구워 먹고
Usiile mbichi au imechemshwa kwenye maji. Badala yake, choma kwenye moto na kichwa chake, miguu na sehemu za ndani.
10 아침까지 남겨 두지 말며 아침까지 남은 것은 곧 소화하라
Usiache ata kidogo kubaki mpaka asubui. Lazima uchome chochote kilicho baki asubui.
11 너희는 그것을 이렇게 먹을지니 허리에 띠를 띠고 발에 신을 신고 손에 지팡이를 잡고 급히 먹으라 이것이 여호와의 유월절이니라
Hivi ndivyo wa paswa kula: ukiwa umefunga mkanda wako, umevaa viatu vyako, na gongo lako mkononi mwako. Lazima ule kwa haraka. Ni Pasaka ya Yahweh.
12 내가 그 밤에 애굽 땅에 두루 다니며 사람과 짐승을 무론하고 애굽 나라 가운데 처음 난 것을 다 치고 애굽의 모든 신에게 벌을 내리리라 나는 여호와로라
Yahweh anasema hili: Nitaenda katika nchi ya Misri usiku na kushambulia wazaliwa wote wa kwanza wa wanadamu na wanyama katika nchi ya Misri. Nitaleta pigo kwa miungu yote ya Misri. Mimi ni Yahweh.
13 내가 애굽 땅을 칠 때에 그 피가 너희의 거하는 집에 있어서 너희를 위하여 표적이 될지라 내가 피를 볼 때에 너희를 넘어가리니 재앙이 너희에게 내려 멸하지 아니하리라
Damu itakuwa ishara kwenye nyumba zenu ya kuja kwangu. Nitakapo ona damu, nitapita nitakapo shambulia nchi ya Misri. Ili pigo halitawajia na kuwaharibu.
14 너희는 이 날을 기념하여 여호와의 절기를 삼아 영원한 규례로 대대에 지킬지니라
Hii siku itakuwa kumbukumbu kwenu, ambayo lazima muadhimishe kama sherehe ya Yahweh. Itakuwa sheria kwenu pia, kwenye vizazi vyote vya watu wenu, ambayo mwapaswa kuadhimisha leo.
15 너희는 칠 일 동안 무교병을 먹을지니 그 첫날에 누룩을 너희 집에서 제하라 무릇 첫날부터 칠일까지 유교병을 먹는 자는 이스라엘에서 끊쳐지리라
Utakula mkate bila hamira wakati wa siku saba. Siku ya kwanza utaondoa hamira kwenye nyumba zenu. Yeyote atakaye kula mkate uliyotiwa chachu kwanzia siku ya kwanza mpaka siku ya saba, huyo mtu lazima akatwe kutoka Israeli.
16 너희에게 첫날에도 성회요 제칠일에도 성회가 되리니 이 두 날에는 아무 일도 하지 말고 각인의 식물만 너희가 갖출 것이니라
Siku ya kwanza kutakuwa na kusanyiko lililo tengwa kwa ajili yangu, na siku ya saba kutakuwa na kusanyiko kama hilo. Hakuna kazi itakayo fanywa hizi siku, zaidi ya kupika kila mmoja ale. Hiyo ndio kazi pekee itakayo fanywa na wewe.
17 너희는 무교절을 지키라 이 날에 내가 너희 군대를 애굽 땅에서 인도하여 내었음이니라 그러므로 너희가 영원한 규례를 삼아 이 날을 대대로 지킬지라
Lazima uadhimishe hii Sherehe ya Mkate Usiotiwa Chachu kwasababu ni siku hii ambayo nitawaleta watu wako, makundi yaliyo na silaha, kwa makundi yaliyo na silaha, kutoka nchi ya Misri. Lazima uadhimishe hii siku kwa vizazi vyote vya watu wako. Hii itakuwa sheria kwako.
18 정월에 그 달 십사일 저녁부터 이십일일 저녁까지 너희는 무교병을 먹을 것이요
Lazima ule mkate usiotiwa chachu kuanzia jioni ya siku ya kumi na nne ya mwezi wa kwanza wa mwaka, mpaka jioni ya siku ya ishirini na moja ya mwezi.
19 칠 일 동안은 누룩을 너희 집에 있지 않게 하라 무릇 유교물을 먹는 타국인이든지 본국에서 난 자든지 무론하고 이스라엘 회중에서 끊쳐지리니
Wakati wa hizi siku, nyumbani mwenu kusipatikane na hamira. Yeyote atakaye kula mkate ulio andaliwa na hamira lazima akatwe kutoka jamii ya Israeli, huyo mtu awe ni mgeni au mtu aliye zaliwa nchini mwenu.
20 너희는 아무 유교물이든지 먹지 말고 너희 모든 유하는 곳에서 무교병을 먹을지니라
Hautakula chochote kilicho andaliwa na hamira. Popote utapo ishi, lazima ule mkate usio na hamira.”'
21 모세가 이스라엘 모든 장로를 불러서 그들에게 이르되 너희는 나가서 너희 가족대로 어린 양을 택하여 유월절 양으로 잡고
Kisha Musa akawaita viongozi wote wa Israeli na kuwaambia, “Nendeni na mchague mwana kondoo au mbuzi watakao tosha kulisha familia zenu na muue mwana kondoo wa pasaka.
22 너희는 우슬초 묶음을 취하여 그릇에 담은 피에 적시어서 그 피를 문 인방과 좌우 설주에 뿌리고 아침까지 한 사람도 자기 집 문밖에 나가지 말라
Kisha chukua jani la hisopu na uchovye kwenye damu itakayo kuwa kwenye beseni. Paka damu iliyo kwenye beseni juu ya fremu ya mlango na kwenye mihimili miwili ya mlango. Hakuna ata mmoja atakaye toka nje ya mlango wake mpaka asubui.
23 여호와께서 애굽 사람을 치러 두루 다니실 때에 문 인방과 좌우 설주의 피를 보시면 그 문을 넘으시고 멸하는 자로 너희 집에 들어가서 너희를 치지 못하게 하실 것임이니라
Kwa kuwa Yahweh atapita kushambulia Wamisri. Atakapo ona damu juu ya fremu ya mlango na kwenye mihimili miwili ya mlango, atapita mlango wako na ata ruhusu mharibifu kuja nyumbani kwenu kuwashambulia.
24 너희는 이 일을 규례로 삼아 너희와 너희 자손이 영원히 지킬 것이니
Lazima uadhimishe hili tukio. Hili litakuwa daima sheria kwako na kwa uzao wenu.
25 너희는 여호와께서 허락하신 대로 너희에게 주시는 땅에 이를 때에 이 예식을 지킬 것이라
Utakapo ingia nchi Yahweh atakayo kupa, kama alivyo ahidi kufanya, lazima uadhimishe hili tendo la ibada.
26 이 후에 너희 자녀가 묻기를 이 예식이 무슨 뜻이냐 하거든
Watoto wako watakapo kuuliza, 'Hili tendo la ibada lina maana gani?'
27 너희는 이르기를 이는 여호와의 유월절 제사라 여호와께서 애굽 사람을 치실 때에 애굽에 있는 이스라엘 자손의 집을 넘으사 우리의 집을 구원하셨느니라 하라 하매 백성이 머리 숙여 경배하니라
kisha lazima useme, 'Ni sadaka ya Pasaka ya Yahweh, kwasababu Yahweh kapita nyumba za Waisraeli Misri alipo washambulia Wamisri. Aliweka nyumba zetu huru.”' Kisha watu wakamsujudia Yahweh.
28 이스라엘 자손이 물러가서 그대로 행하되 여호와께서 모세와 아론에게 명하신 대로 행하니라
Waisraeli wakaenda na kufanya kama Yahweh alivyo waamuru Musa na Aruni.
29 밤중에 여호와께서 애굽 땅에서 모든 처음 난 것 곧 위에 앉은 바로의 장자로부터 옥에 갇힌 사람의 장자까지와 생축의 처음 난것을 다 치시매
Ikawa usiku wa manane kuwa Yahweh akawashambulia wazaliwa wote wa kwanza wa nchi ya Misri, kuanzia mzaliwa wa kwanza wa Farao, aliye keti kiti chake cha enzi, mzaliwa wa kwanza wa mtu aliye gerezani na wazaliwa wote wa kwanza wa mifugo.
30 그 밤에 바로와 그 모든 신하와 모든 애굽 사람이 일어나고 애굽에 큰 호곡이 있었으니 이는 그 나라에 사망치 아니한 집이 하나도 없었음이었더라
Farao akaamka usiku - yeye, watumishi wake, na Wamisri. Palikuwa na kelele za maombolezo Misri, kwa kuwa hakukuwa na nyumba ambayo hamna mtu hakufa.
31 밤에 바로가 모세와 아론을 불러서 이르되 너희와 이스라엘 자손은 일어나 내 백성 가운데서 떠나서 너희의 말대로 가서 여호와를 섬기며
Farao akamuita Musa na Aruni usiku na kusema, “Inuka, tokeni miongoni mwa watu wangu, nyie pamoja na Waisraeli. Nenda, mmuabudu Yahweh, kama mlivyo sema mnataka kufanya.
32 너희의 말대로 너희의 양도 소도 몰아가고 나를 위하여 축복하라 하며
Chukuweni ng'ombe zenu na kondoo zenu, kama mlivyo sema, na muende, na pia mnibariki.”
33 애굽 사람들은 말하기를 우리가 다 죽은 자가 되도다 하고 백성을 재촉하여 그 지경에서 속히 보내려 하므로
Wamisri walikuwa na haraka ya kuwa ondoa nchini, kwa kuwa walisema, “Sisi ni watu tuliokufa.”
34 백성이 발교되지 못한 반죽 담은 그릇을 옷에 싸서 어깨에 메니라
Watu wakachukuwa ngano yao pasipo kuongeza hamira yeyote. Bakuli zao zakukandia ngano zilifungiwa kwenye nguo zao na kwenye mabega yao.
35 이스라엘 자손이 모세의 말대로 하여 애굽 사람에게 은금 패물과 의복을 구하매
Watu Waisraeli walifanya kama Musa alivyo waambia. Waliwaomba Wamisri vitu vya fedha, vitu vya dhahabu, na nguo.
36 여호와께서 애굽 사람으로 백성에게 은혜를 입히게 하사 그들의 구하는 대로 주게 하시므로 그들이 애굽 사람의 물품을 취하였더라
Yahweh aliwafanya Wamisri na shauku ya kuwapendeza Waisraeli. Hivyo Wamisri waliwapa chochote walicho waomba. Katika hili, Waisraeli waliwachukulia vingi Wamisri.
37 이스라엘 자손이 라암셋에서 발행하여 숙곳에 이르니 유아 외에 보행하는 장정이 육십만 가량이요
Waisraeli wakasafiri kutoka Ramesi kwenda Sakothi. Walikuwa na idadi ya wanaume 600, 000 kwa miguu, kuongezea kwa wanawake na watoto.
38 중다한 잡족과 양과 소와 심히 많은 생축이 그들과 함께하였으며
Mchanganyiko wa kundi la wasio Waisraeli pia walienda nao, pamoja na ng'ombe na kondoo, idadi kumbwa ya mifugo.
39 그들이 가지고 나온 발교되지 못한 반죽으로 무교병을 구웠으니 이는 그들이 애굽에서 쫓겨 남으로 지체할 수 없었음이며 아무 양식도 준비하지 못하였음이었더라
Walioka mikate na unga wa ngano wenye hamira walio utoa Misri. Ulikuwa hauna hamira kwasababu waliondolewa Misri na hawakuweza chelewa kuandaa chakula.
40 이스라엘 자손이 애굽에 거주한지 사백삼십 년이라
Waisraeli waliishi Misri kwa miaka 430.
41 사백삼십 년이 마치는 그 날에 여호와의 군대가 다 애굽 땅에서 나왔은즉
Baada ya miaka 430, siku hiyo hiyo, majeshi yote ya Yahweh yalio jiami waliondoka kutoka nchi ya Misri.
42 이 밤은 그들을 애굽 땅에서 인도하여 내심을 인하여 여호와 앞에 지킬 것이니 이는 여호와의 밤이라 이스라엘 자손이 다 대대로 지킬 것이니라
Huu ulikuwa usiku wakuwa macho, ili Yahweh awatoe kutoka nchi ya Misri. Huu ulikuwa usiku wa Yahweh wa kuadhimishwa na Waisraeli wote na watu wa vizazi vyao vyote.
43 여호와께서 모세와 아론에게 이르시되 유월절 규례가 이러하니라 이방 사람은 먹지 못할 것이나
Yahweh akamwambia Musa na Aruni, “Hii ni sheria ya Pasaka: hakuna mgeni anaye ruhusiwa kuila.
44 각 사람이 돈으로 산 종은 할례를 받은 후에 먹을 것이며
Walakini, kila mtumwa wa Misraeli, aliye nunuliwa kwa pesa, anaeza kula baada ya kutahiriwa.
Wageni na watumishi waajiriwa hawapaswi kula chakula chochote.
46 한 집에서 먹되 그 고기를 조금도 집 밖으로 내지 말고 뼈도 꺾지 말지며
Chakula chapaswa kuliwa ndani ya nyumba moja. Hauruhusiwi kubeba nyama yeyote nje ya nyumba, na hauruhusiwi kuvunja mfumba wowote.
Jamii zote za Israeli za paswa kuadhimisha sherehe.
48 너희와 함께 거하는 타국인이 여호와의 유월절을 지키고자 하거든 그 모든 남자는 할례를 받은 후에야 가까이하여 지킬지니 곧 그는 본토인과 같이 될 것이나 할례받지 못한 자는 먹지 못할 것이니라
Kama mgeni anaishi na wewe na anataka kuadhimisha Pasaka kwa Yahweh, ndugu zake wote wa kiume wapaswa kutahiriwa. Kisha anaeza kuja na kuadhimisha. Atakuwa kama watu walio zaliwa kwenye nchi. Walakini, hakuna mtu asiye tahiriwa anaruhusiwa kula chakula chochote.
49 본토인에게나 너희 중에 우거한 이방인에게나 이 법이 동일하니라 하셨으므로
Sheria hii hii itahusika kwa mzaliwa wa asili na mgeni anayeishi miongoni mwenu.”
50 온 이스라엘 자손이 이와 같이 행하되 여호와께서 모세와 아론에게 명하신 대로 행하였으며
Waisraeli wote walifanya kama Yahweh alivyo waamuru Musa na Aruni.
51 그 같은 날에 여호와께서 이스라엘 자손을 그 군대대로 애굽 땅에서 인도하여 내셨더라
Ikaja kuwa siku hiyo Yahweh akawaleta Israeli kutoka nchi ya Misri kwa makundi yalio jiami.