< 에스더 9 >
1 아달월 곧 십이월 십삼일은 왕의 조명을 행하게 된 날이라 유다인의 대적이 저희를 제어하기를 바랐더니 유다인이 도리어 자기를 미워하는 자를 제어하게 된 그 날에
Sasa katika mwezi wa kumi na mbili, siku ya kumi na tatu ambayo ni siku ya Adari, siku ambayo adui wa Wayahudi walitarajia kutekeleza sheria ya mfalme na kupata nguvu dhidi ya Wayahudi. Badala yake Wayahudi wakapata nguvu dhidi ya adui zao.
2 유다인들이 아하수에로 왕의 각 도, 각 읍에 모여 자기를 해하고자 하는 자를 죽이려 하니 모든 민족이 저희를 두려워하여 능히 막을 자가 없고
Wayahudi wote wakakusanyika katika miji yao katika majimbo yote ya Mfalme Ahusiero, kutia mikono juu ya wale waliokusudia ubaya. Hakuna aliye kuwa tayari kusimama zao kwa sababu hofu yao ilikuwa imewaangukia watu wote.
3 각 도 모든 관원과 대신과 방백과 왕의 사무를 보는 자들이 모르드개를 두려워하므로 다 유다인을 도우니
Wakuu wote wa majimbo, maakida na magavana, na watawala wa mfalme, waliwasaidia Wayahudi kwa kuwa hofu ya Modekai ilikuwa imewaangukia.
4 모르드개가 왕궁에서 존귀하여 점점 창대하매 이 사람 모르드개의 명성이 각 도에 퍼지더라
Kwa kuwa Modekai alikuwa mkuu katika nyumba ya mfalme, na umaarufu wake ukasambaa katika majimbo yote, kwa kuwa Modekai alikuwa akifanyika mkuu.
5 유다인이 칼로 그 모든 대적을 쳐서 도륙하고 진멸하고 자기를 미워하는 자에게 마음대로 행하고
Wayahudi wakawavamia maadi zao kwa upanga, wakiwatenda vibaya kama walivyokuwa wamekusudiwa mabaya dhidi yao Wakawatenda kama walivyo ona vyema machoni pao.
6 유다인이 또 도성 수산에서 오백 인을 죽이고 멸하고
Katika ngome ya mji wa Shushani pekee jumla ya maadui waliouawa na na kuharibiwa na Wayahudi ni wanaume mia tano.
Miongoni mwa waliouawa ni pamoja na Parishandatha, Dalphoni, Aspatha,
Poratha, Adalia, Aridatha,
Parimashita, Arisai, Aridai, Vaizatha,
10 곧 함므다다의 손자요 유다인의 대적 하만의 열 아들을 죽였으나 그 재산에는 손을 대지 아니하였더라
na wana kumi wa Hamani, mwana wa Hammedatha, adui wa Wayahudi. Lakini hawakuchua mateka yoyote.
11 그 날에 도성 수산에서 도륙한 자의 수효를 왕께 고하니
Idadi ya wale waliouawa siku hiyo katika mji wa Shushani, ilifikishwa kwa Mfalme Ahusiero.
12 왕이 왕후 에스더에게 이르되 유다인이 도성 수산에서 이미 오백 인을 죽이고 멸하고 또 하만의 열 아들을 죽였으니 왕의 다른 도에서는 어떠하였겠느뇨 이제 그대의 소청이 무엇이뇨 곧 허락하겠노라 그대의 요구가 무엇이뇨 또한 시행하겠노라
Mfalme akamwambia malkia Esta. Mfalme akamwambia Malkia Esta, “Wayahudi wameua wanaume mia tano katika mji wa Shushani, wakiwemo wana kumi wa Hamani adui wa Wayahudi. Je wamefanya nini katika majimbo mengine? Na sasa haja yako ni nini? Utapewa. Ombi lako ni nini?”
13 에스더가 가로되 왕이 만일 선히 여기시거든 수산에 거하는 유다인으로 내일도 오늘날 조서대로 행하게 하시고 하만의 열 아들의 시체를 나무에 달게 하소서
Esta akamjibu, “Mfalme kama ikikupendeza, ruhusu Wayuadi walio katika mji wa Shushani wapige mbiu hii na kesho, na miili ya watoto wa Hamani itundikwe juu ya miti.”
14 왕이 그대로 행하기를 허락하고 조서를 내리니 하만의 열 아들의 시체가 달리니라
Mfalme akaamuru ombi la Esta litekelezwe. Mbiu ilipigwa katika mji wa Shushani, na wana kumi wa Hamani wakatundikwa juu ya miti.
15 아달월 십사일에도 수산에 있는 유다인이 모여 또 삼백 인을 수산에서 도륙하되 그 재산에는 손을 대지 아니하였고
Wayahudi katika mji wa Shushani walisanyika pamoja siku ya kumi na nne ya mwezi wa Adari, na kuwaua maadui zao mia tatu katika mji wa Shushani, lakini hawakugusa nyara zao.
16 왕의 각 도에 있는 다른 유다인들이 모여 스스로 생명을 보호하여 대적들에게서 벗어나며 자기를 미워하는 자 칠만 오천 인을 도륙하되 그 재산에는 손을 대지 아니하였더라
Na Wayahudi katika majimbo mengine wakakusanyika ili kujilinda na wakapata faraja kutoka kwa maadui na wakawaua maadui zao elfu sabini na tano, lakini hawakugusa mikono yao kwa vitu vya thamani wale waliouwawa.
17 아달월 십삼일에 그 일을 행하였고 십사일에 쉬며 그 날에 잔치를 베풀어 즐겼고
Katika siku ya kumi na tatu ya mwezi wa Adari, Wayahudi wakapumzika katika siku ya kumi na nne, wakapumzika siku hiyo ya karamu na furaha.
18 수산에 거한 유다인은 십삼일과 십사일에 모였고 십오일에 쉬며 이 날에 잔치를 베풀어 즐긴지라
Lakini Wayahudi walioishi katika mji wa Shushani wakaja pamoja siku ya kumi na tatu na ya kumi na nne. Na siku ya kumi na tano wakapumzika na wafanya karamu na kufurahia.
19 그러므로 촌촌의 유다인 곧 성이 없는 고을 고을에 거하는 자들이 아달월 십사일로 경절을 삼아 잔치를 베풀고 즐기며 서로 예물을 주더라
Hii ndiyo sababu Wayahudi wa vijijini, wanaishi maeneo ya vijijini, huadhimisha siku ya kumi na nne ya mwezi wa Adari kama siku ya furaha na karamu na siku ambayo hutumiana zawadi kwa kila mmoja.
20 모르드개가 이 일을 기록하고 아하수에로 왕의 각 도에 있는 모든 유다인에게 무론 원근하고 글을 보내어 이르기를
Modekai akaweka mambo haya na akatuma nyaraka kwa Wayahudi wote waliokuwa katika utawala wa Mfalme Ahusiero,
21 한 규례를 세워 해마다 아달월 십사일과 십오일을 지키라
akiwataka kuazimisha siku ya kumi na nne na kumi na tano ya mwezi wa Adari kila mwaka.
22 이 달 이 날에 유다인이 대적에게서 벗어나서 평안함을 얻어 슬픔이 변하여 기쁨이 되고 애통이 변하여 길한 날이 되었으니 이 두 날을 지켜 잔치를 베풀고 즐기며 서로 예물을 주며 가난한 자를 구제하라 하매
Hizi zilikuwa ndizo siku ambazo Wahudi walipata faraja kutoka kwa maadui zao na wakati huu ndio wakati ambao huzuni ya Wayahudi iligeuzwa kuwa furaha, na kutoka kwa maombolezo hadi kwenye pumziko. Walipaswa kuzifanya siku za karamu na furaha, na kutumiana zawadi ya chakula, na zawadi kwa masikini.
23 유다인이 자기들의 이미 시작한 대로 또는 모르드개의 보낸 글대로 계속하여 행하였으니
Wayahudi wakaendelea na maadhimisho wakifanya kile ambacho Modekai alikuwa amewaandikia.
24 곧 아각 사람 함므다다의 아들 모든 유다인의 대적 하만이 유다인을 진멸하기를 꾀하고 부르 곧 제비를 뽑아 저희를 죽이고 멸하려 하였으나
Na wakati huo Modekai mwana wa Hammedatha mwagagi, adui wa Wayahudi aliyekuwa amepanga njama ya kuwaangamiza Wayahudi, na kwa kupiga Puri (yaani akapiga kura) ili kuwaangamiza kabisa.
25 에스더가 왕의 앞에 나아감을 인하여 왕이 조서를 내려 하만이 유다인을 해하려던 악한 꾀를 그 머리에 돌려 보내어 하만과 그 여러 아들을 나무에 달게 하였으므로
Lakini Mfalme Ahusiero alipopata taarifa ya mpango mbaya huu alioupanga Modekai dhidi ya Wayahudi, aliagiza kwa nyaraka afanyiwe Modekai mwenyewe, na kwamba yeye na wana wake wanyongwe juu ya miti.
26 무리가 부르의 이름을 좇아 이 두 날을 부림이라 하고 유다인이 이 글의 모든 말과 이 일에 보고 당한 것을 인하여
Hivyo Wayahudi wakaziita siku hizi Purimu, kutokana na jina Puri. Kwa sababu ya mambo yote yaliyo kuwa yameandika katika barua, na mambo yote ambayo walikuwa wameyaona kwa macho yao, na yale yalikuwa yamewapata,
27 뜻을 정하고 자기와 자손과 자기와 화합한 자들이 해마다 그 기록한 정기에 이 두 날을 연하여 지켜 폐하지 아니하기로 작정하고
Wayahudi wakapokea jukumu na desturi mpya. Desturi hii iwe kwa ajili yao, watoto wao, na kila ambaye aliyeungana nao. Na itakuwa kwamba maadhimisho haya watayafanya kwa kila mwaka. Wataadhimisha kwa namna fulani na nyakati hizo hizo kila mwaka.
28 각 도, 각 읍, 각 집에서 대대로 이 두 날을 기념하여 지키되 이 부림일을 유다인 중에서 폐하지 않게 하고 그 자손 중에서도 기념함이 폐하지 않게 하였더라
Siku hizi zilipaswa kuadhimishwa katika kila kizazi, kila familia, kila jimbo na kwa kila mji. Wayahudi hawa na watoto wao hawakuacha kuadhimisha siku hizi za Purimu, ili kwamba wasizisahau.
29 아비하일의 딸 왕후 에스더와 유다인 모르드개가 전권으로 글을 쓰고 부림에 대한 이 둘째 편지를 굳이 지키게 하되
Malkia Esta na Modekai wakaandika kwa mamlaka yote na kuthibitisha barua hii ya pili kuhusu Purimu.
30 화평하고 진실한 말로 편지를 써서 아하수에로의 나라 일백이십칠 도에 있는 유다 모든 사람에게 보내어
Barua zilipelekwa katika majimbo 127 ya mfalme Ahusiero, zikiwatakia Wayahudi wote amani na kweli.
31 정한 기한에 이 부림일을 지키게 하였으니 이는 유다인 모르드개와 왕후 에스더의 명한 바와 유다인이 금식하며 부르짖은 것을 인하여 자기와 자기 자손을 위하여 정한 바가 있음이더라
Na kuthibitisha siku za Purimu sawa sawa na maelekezo ya Modekai na Esta yaliyowataka Wayahudi waadhimishe. Wayahudi wakatii maagizo kwa ajili yao na uzao wao, kama walivyotii siku za kufunga na kuomboleza.
32 에스더의 명령이 이 부림에 대한 일을 견고히 하였고 그 일이 책에 기록되었더라
Agizo la Esta likahakikisha sheria hizi kuhusu Purimu, na ikaandikwa katika kitabu.