< 역대하 31 >
1 이 모든 일이 마치매 거기 있는 이스라엘 무리가 나가서 유다 여러 성읍에 이르러 주상을 깨뜨리며 아세라 목상을 찍으며 유다와 베냐민과 에브라임과 므낫세 온 땅에서 산당과 단을 제하여 멸하고 이스라엘 모든 자손이 각각 그 본성 기업으로 돌아갔더라
Sasa wakati haya yote yalipokwisha, watu wote wa Israeli waliokuwepo pale wakaenda huko kwenye mji wa Yuda na wakazivunja vipande vipande nguzo za mawe na wakazikata nchi za maashera, na wakazibomoa sehemu za juu na madhabahu katika Yuda yote na Benyamini, na katika Efraimu na Manase, hadi walipoziharibu zote. Kisha watu wote wa Israeli wakarudi, kila mtu kwenye mali zake na kwenye mji wake.
2 히스기야가 제사장들과 레위 사람들의 반차를 정하고 각각 그 직임을 행하게 하되 곧 제사장들과 레위 사람들로 번제와 화목제를 드리며 여호와의 영문에서 섬기며 감사하며 찬송하게 하고
Hezekia akayapanga makundi ya makuhani na Walawi wakajipanaga kwa makundi yao, kila mtu akapangwa katika kazi yake, wote makuhani na Walawi. Aliwapanga wafanye sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani, kuhudumu, kutoa shukrani, na kusifu katika malango ya hekalu la Yahwe.
3 또 자기 재산 중에서 얼마를 정하여 여호와의 율법에 기록된 대로 번제 곧 조석 번제와 안식일과 초하루와 절기의 번제에 쓰게 하고
Pia akawapanga katika sehemu ya mfalme kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa kutoka katika mali zake, hiyo ni kwa ajili ya, sadaka za kuteketezwa za asubuhi na jioni, na sadaka za kuteketezwa kwa ajili ya siku za Sabato, mwezi mpya, na sikukuu zisizobadilika, kama ilivyokuwa imeandikwa katika sheria ya Yahwe.
4 또 예루살렘에 거한 백성을 명하여 제사장들과 레위 사람들의 응식을 주어 저희로 여호와의 율법을 힘쓰게 하라 한지라
Vilevile, akawaamuru watu walioishi Yerusalemu kutoa fungu kwa ajili ya makuhani na Walawi, ili kwamba wawe makini katika kuitii sheria ya Yahwe.
5 왕의 명령이 내리자 곧 이스라엘 자손이 곡식과 포도주와 기름과 꿀과 밭의 모든 소산의 처음 것을 풍성히 드렸고 또 모든 것의 십일조를 많이 가져왔으며
Mapema mara baada ya amri kutolewa, watu wa Israeli kwa ukarimu wakatoa malimbuko ya nafaka, divai mpya, mafuta. asali, na kila kitu kutoka kwenye mavuno ya shamba. Wakaleta ndani fungu la kumi la kila kitu; ambavyo vilikuwa kiasi kikubwa sana.
6 유다 여러 성읍에 거한 이스라엘과 유다 자손도 소와 양의 십일조를 가져왔고 또 그 하나님 여호와께 구별하여 드릴 성물의 십일조를 가져왔으며 그것을 쌓아 더미를 이루었는데
Watu wa Israeli na Yuda ambao waliishi katika mji wa Yuda pia wakaleta zaka za ng'ombe na kondoo, na zaka za vitu vitakatifu amabavyo vilikuwa vimewekwa wakfu kwa Yahwe Mungu wao, na wakavifunga katika marundo.
Ilikuwa mwezi wa tatu wakati walipoanza kufunga michango yao katika marundo, na wakamaliza mwezi wa saba.
8 히스기야와 방백들이 와서 더미를 보고 여호와를 송축하고 그 백성 이스라엘을 위하여 축복하니라
Hezekia na viongozi walipokuja na kuyaona marundo, wakambariki Yahwe na watu wake Israeli.
9 히스기야가 그 더미에 대하여 제사장들과 레위 사람들에게 물으니
Kisha Hezekia akawauliza makuhani na Walawi kuhusu marundo.
10 사독의 족속 대제사장 아사랴가 대답하여 가로되 백성이 예물을 여호와의 전에 드리기 시작함으로부터 우리가 족하게 먹었으나 남은 것이 많으니 이는 여호와께서 그 백성에게 복을 주셨음이라 그 남은 것이 이렇게 많이 쌓였나이다
Azaria, kuhani mkuu, wa nyumba ya Zadoki, akamjibu na akasema, “Tangu watu walipoanza kuleta matoleo katika nyumba ya Yahwe, tumekula na tulikuwa navyo vya kutosha, tulibakiza vingi, kwa maana Yahwe amewabariki watu wake. kilichokuwa kimebaki ni kiasi kikubwa hiki hapa.”
11 그 때에 히스기야가 명하여 여호와의 전 안에 방을 예비하라 한고로 드디어 예비하고
Kisha Hezekia akaagiza vyumba vya kuhifadhia viandaliwe katika nyumba ya Yahwe, na wakaviandaa.
12 성심으로 그 예물과 십일조와 구별한 물건을 갖다 두고 레위 사람 고나냐는 그 일을 주관하고 그 아우 시므이는 버금이 되며
Kisha kwa uaminifu wakayaleta ndani matoleo, zaka, na vitu ambavyo ni vya Yahwe. Konania, Mlawi, alikuwa meneja mkuu wa hivyo vitu, na Shimei, ndu yake, alikuwa wa pili kwake.
13 여히엘과 아사시야와 나핫과 아사헬과 여리못과 요사밧과 엘리엘과 이스마가와 마핫과 브나야는 고나냐와 그 아우 시므이의 수하에서 보살피는 자가 되니 이는 히스기야 왕과 하나님의 전을 관리하는 아사랴의 명한 바며
Yehieli, Azaria, Nahathi, Asaheli, na Yerimothi, Yazabadi, Elieli, Ismakia, Mahathi, na Benania walikuwa wasimamizi chini ya mkono wa Konania na Shimei ndu yake, kwa uteuzi wa Hezekia, mfalme, na Azaria mwanagalizi mkuu wa nyumba ya Mungu.
14 동문지기 레위 사람 임나의 아들 고레는 즐거이 하나님께 드리는 예물을 맡아 여호와께 드리는 것과 모든 지성물을 나눠 주며
Kore mwana wa Imna Mlawi, bawabu katika mlango wa mashariki, alikuwa juu ya sadaka za hiari za Mungu, msimamizi wa kugawa sadaka kwa Yahwe na sadaka takatifu kuliko zote.
15 그 수하의 에덴과 미냐민과 예수아와 스마야와 아마랴와 스가냐는 제사장의 성읍들에 있어서 직임을 맡아 그 형제에게 반차대로 무론대소하고 나눠 주되
Chini yake walikuwepo Edeni, Miniamini, Yoshua, Shemai, Amaaria, na Shekania, katika miji ya makuhani. Wakazijaza ofisi za uaminifu, ili kutoa sadaka hizi kwa ndugu zao fungu kwa fungu, kwa wote walio muhimu na wasiomuhimu.
16 삼 세 이상으로 족보에 기록된 남자 외에 날마다 여호와의 전에 들어가서 그 반차대로 직임에 수종드는 자들에게 다 나눠 주며
Pia wakatoa kwa wale wanaume wenye umri wa miaka mitatu na kuendelea, amabao walikuwa wameandikwa kataika kaitatu cha babu zao walioiingia nyumba ya Yahwe, kwa mujibu wa ratiba ya kila siku, kuifanya kazi katika ofisi zao na zamu zao. (Mandishi ya kale yanasema hivi: “badala ya wanaume wa umri wa miaka mitatu na kuendelea”, wanaume wa mika thelathini na kuendelea.”).
17 또 그 족속대로 족보에 기록된 제사장들에게 나눠 주며 이십 세 이상부터 그 반차대로 직임을 맡은 레위 사람들에게 나눠 주며
Waliwaganya makuhani kwa mujibu wa kumbu kumbu za babu zao, na hivyo hivyo kwa Walawi wenye umri wa miaka ishirini na zaidi, kwa mujibu wa ofisi zao na zamu zao.
18 또 그 족보에 기록된 온 회중의 어린 아이와 아내와 자녀들에게 나눠 주었으니 이 회중은 성결하고 충실히 그 직분을 다하는 자며
Waliwajumuisha watoto wao wadogo wote, wake zao, wana wao, na binti zao, katika jamii yote, kwa maana walikuwa waaminifu katika kujitunza wenye watakatifu.
19 각 성읍에서 녹명된 사람이 있어 성읍 가까운 들에 거한 아론 자손 제사장들에게도 나눠 주되 제사장들의 모든 남자와 족보에 기록된 레위 사람들에게 나눠 주었더라
Kwa maana makuhani, uzao wa Haruni, amabao walikuwa katika mashamba ya vijiji wakimilikiwa na miji yao, au katika kila mji, palikuwa na watu walioteuliwa kwa majina kutoa mafungu kwa ajili ya wanaume miongoni mwa makuhani, na kwa wote waliokuwa wameorodheshwa katika kumbukumbu za babu zao kuwa miongoni mwa Walawi.
20 히스기야가 온 유다에 이같이 행하되 그 하나님 여호와 보시기에 선과 정의와 진실함으로 행하였으니
Hezekia alifanya haya katika Yuda yote. Akakamilisha kilichokuwa chema, haki, na uaminifu mbele za Yahwe Mungu wake.
21 무릇 그 행하는 모든 일 곧 하나님의 전에 수종드는 일에나 율법에나 계명에나 그 하나님을 구하고 일심으로 행하여 형통하였더라
Katika kila jambo ambalo alianzisha katika ibada ya nyumba ya Mungu, sheria, na zile amri, kumtafuta Mungu, alikifanya kwa moyo wake wote, na alifanikiwa.