< 열왕기상 6 >

1 이스라엘 자손이 애굽 땅에서 나온지 사백팔십 년이요 솔로몬이 이스라엘 왕이 된지 사년 시브월 곧 이월에 솔로몬이 여호와를 위하여 전 건축하기를 시작하였더라
Kwa hiyo Sulemani akaanza kulijenga hekalu. Hii ilikuwa mwaka wa 480 baada ya wana wa Israeli kutoka katika nchi ya Misri, katika mwaka wa nne wa utawala wa Sulemani huko Israeli, katika mwezi wa Ziv, ambao ndio mwezi wa pili.
2 솔로몬 왕이 여호와를 위하여 건축한 전은 장이 육십 규빗이요 광이 이십 규빗이요 고가 삼십 규빗이며
Hekalu ambalo mfalme Sulemani alimjengea BWANA lilikuwa na urefu wa mita 27, na upana wa mita 9, na kimo cha mita 13. 5.
3 전의 성소 앞 낭실의 장은 전의 광과 같이 이십 규빗이요 그 광은 전 앞에서부터 십 규빗이며
Na ukumbi uliokuwa mbele ya hekalu ulikuwa na urefu wa mita 9 na upana wa mita 4. 5 sawa na upana wa sehemu kuu ya hekalu.
4 전을 위하여 붙박이 교창을 내고
Lile hekalu alilitengenezea madirisha ambayo fremu zake kwa nje yalifanya yaonekane membamba kuliko ile sehemu ya ndani.
5 또 전의 벽 곧 성소와 지성소의 벽에 연접하여 돌아가며 다락들을 건축하되 다락마다 돌아가며 골방들을 만들었으니
Na ukuta wa nyumba aliuzungushia vyumba kuzunguka pande zake, kushikamana na vyumba vya nje na vya ndani ya hekalu. Akajenga vyumba katika pande zote.
6 하층 다락의 광은 다섯 규빗이요 중층 다락의 광은 여섯 규빗이요 제삼층 다락의 광은 일곱 규빗이라 전의 벽 바깥으로 돌아가며 턱을 내어 골방 들보들로 전의 벽에 박히지 않게 하였으며
Kile chumba cha chini kilikuwa na upana wa mita 2. 3, kile cha kati kilikuwa na upana wa mita 2. 8. na kile cha tatu kilikuwa na upana wa mita 3. 2. upande wa nje akaupunguza ukuta wa nyumba pande zote, ili boriti zisishikamane ukutani mwa nyumba.
7 이 전은 건축할 때에 돌을 뜨는 곳에서 치석하고 가져다가 건축하였으므로 건축하는 동안에 전 속에서는 방망이나 도끼나 모든 철 연장 소리가 들리지 아니하였으며
Hekalu lilijengwa kwa mawe yaliyokuwa yamechongwa chimboni. Hakuna nyundo, wala shoka au chombo chochote cha chuma kilisikika wakati hekalu lilipokuwa likjengwa.
8 중층 골방의 문은 전 오른편에 있는데 나사모양 사닥다리로 말미암아 하층에서 중층에 오르고 중층에서 제삼층에 오르게 하였더라
Upande wa kusini wa hekalu kulikuwa na lango la chini, ambalo mtu hupanda kwa madaraja mpaka juu kwenye chumba cha kati, na kutoka chumba cha kati hadi chumba cha tatu.
9 전의 건축이 마치니라 그 전은 백향목 서까래와 널판으로 덮었고
Kwa hiyo Sulemani akalijenga hekalu mpaka akalimaliza, akalifunika hekalu kwa boriti na mbao za mwerezi.
10 또 온 전으로 돌아가며 고가 다섯 규빗 되는 다락방을 건축하되 백향목 들보로 전에 연접하게 하였더라
Akajenga vyumba vya pembeni mwa hekalu, kila upande mita 2. 3 kwenda juu. Navyo vikaunganishwa na hekalu kwa mbao za mierezi.
11 여호와의 말씀이 솔로몬에게 임하여 가라사대
Neno la BWANA likamjia Sulemani, likisema,
12 네가 이제 이 전을 건축하니 네가 만일 내 법도를 따르며 내 율례를 행하며 나의 모든 계명을 지켜 그대로 행하면 내가 네 아비 다윗에게 한 말을 네게 확실히 이룰 것이요
“Kuhusu hili hekalu ambalo unajenga, kama utatatembea katika maagizo yangu na kuhukumu kwa haki, na kutunza amri zangu na kuishi kwa hizo, ndipo ntakapozithibitisha ahadi zangu na wewe ambazo niliziahidi kwa baba yako Daudi.
13 내가 또한 이스라엘 자손 가운데 거하며 내 백성 이스라엘을 버리지 아니하리라 하셨더라
Nitaishi kati ya watu wa Israeli nami sitawatupa.”
14 솔로몬이 전 건축하기를 마치고
Kwa hiyo Sulemani akalijenga hekalu mpaka akalimaliza.
15 백향목 널판으로 전의 안 벽 곧 전 마루에서 천장까지의 벽에 입히고 또 잣나무 널판으로 전 마루를 놓고
Kisha akajenga kuta za ndani za hekalu kwa mbao za mwerezi. Kuanzia sakafu ya hekalu hadi boriti za juu, kwa ndani akazifunika kwa miti, na akaifunika sakafu kwa mbao za miberoshi.
16 또 전 뒤편에서부터 이십 규빗 되는 곳에 마루에서 천장까지 백향목 널판으로 가로막아 전의 내소 곧 지성소를 만들었으며
Alijenga mita 9 ndani ya hekalu kwa mbao za miberoshi kutoka sakafuni hadi juu. Hiki ni chumba cha ndani, cha patakatifu sana.
17 내소 앞에 있는 외소 곧 성소의 장이 사십 규빗이며
Ule ukumbu mkuu, ulikuwa mahali pakatifu amabao ulikuwa mbele ya patakatifu sana, ulikuwa wa mita 18. hapo kulikwa na mbao za mwerezi ndani ya hekalu, zilizokuwa zimechongwa kwa sura ya vibuyu na maua yaliyochanua.
18 전 안에 입힌 백향목에는 박과 핀 꽃을 아로새겼고 모두 백향목이라 돌이 보이지 아니하며
Zote zilikuwa za mierezi kwa ndani. Hapakuonekana chochote ndani kilichokuwa kimetengenezwa kwa mawe.
19 여호와의 언약궤를 두기 위하여 전 안에 내소를 예비하였는데
Sulemani alitengeneza kile chumba cha ndani kwa lengo la kuweka sanduku la agano la BWANA.
20 그 내소의 속이 장이 이십 규빗이요 광이 이십 규빗이요 고가 이십 규빗이라 정금으로 입혔고 백향목 단에도 입혔더라
Kile chumba cha ndani kilikuwa na upana wa mita 9, na kimo cha mita 9. Sulemani alizifunika kuta kwa dhabahu na madhabahu aliifunika kwa mbao za mierezi.
21 솔로몬이 정금으로 외소 안에 입히고 내소 앞에 금사슬로 건너지르고 내소를 금으로 입히고
Sulemani alifunika ndani ya hekalu kwa dhahabu safi na akaweka mikufu ya dhahabu iliyopita mbele ya chumba cha ndani, na kulifunika eneo la mbele kwa dhabahu.
22 온 전을 금으로 입히기를 마치고 내소에 속한 단의 전부를 금으로 입혔더라
Akalisakafia kwa dhahabu eneo lote la ndani mpaka akamaliza hekalu lote. Pia akalisakafia kwa dhahabu madhahabu yote ya chumba cha ndani.
23 내소 안에 감람목으로 두 그룹을 만들었는데 그 고가 각각 십 규빗이라
Sulemani akatengeneza makerubi mawili kwa mbao za mizeituni, kila moja lilikuwa na kimo cha mita 4. 5 kwa ajili ya chumba cha ndani.
24 한 그룹의 이 날개는 다섯 규빗이요 저 날개도 다섯 규빗이니 이 날개 끝으로부터 저 날개 끝까지 십 규빗이며
Bawa moja la kerubi wa kwanza lilikuwa na urefu wa mita 2. 3. Kwa hiyo kutoka ncha ya bawa moja hadi ncha ya bawa lingine kulikuwa na umbali wa mita 4. 5. Yule
25 다른 그룹도 십 규빗이니 그 두 그룹은 한 척수, 한 모양이요
kerubi mwingine naye alikuwa na bawa lenye kipimo cha mita 4. 5 Makerubi hawa walikuwa wanafanana kwa umbo na kwa vipimo.
26 이 그룹의 고가 십 규빗이요 저 그룹도 일반이라
Kimo cha kerubi mmoja kilikuwa mita 4. 5 na yule wa pili alikuwa hivyo hivyo.
27 솔로몬이 내소 가운데 그룹을 두었으니 그룹들의 날개가 폐었는데 이 그룹의 날개는 이 벽에 닿았고 저 그룹의 날개는 저 벽에 닿았으며 두 날개는 전의 중앙에서 서로 닿았더라
Sulemani aliwaweka hao kerubi kwenye chumba cha patakatifu sana. Bawa moja la kerubi lilikuwa limeenea kiasi kwamba bawa moja liligusa ukuta huu na bawa la yule wa pili nalo liligusa ukuta wa upande mwingine. Hayo mabawa yalikuwa yanakutana katikati ya chumba cha patakatifu sana.
28 저가 금으로 그룹에 입혔더라
Sulemani aliwafunika hao kerubi kwa dhahabu.
29 내외소 사면 벽에는 모두 그룹들과 종려와 핀 꽃 형상을 아로새겼고
Akazinakshi kuta zote kwa sura za makerubi, miti ya mitende, na maua yaliyochanua, kwa vyumba vya nje na vya ndani.
30 내외 전 마루에는 금으로 입혔으며
Sulemani akalisakafia hekalu kwa dhahabu, kwa vyumba vyote vya ndani na vya nje.
31 내소에 들어가는 곳에는 감람목으로 문을 만들었는데 그 문 인방과 문설주는 벽의 오분지 일이요
Sulemani akatengeneza milango ya mbao za mizeituni kwenye lango la kuingia ndani. Aliweka vizingiti na miimo kwenye pande tano.
32 감람목으로 만든 그 두 문짝에 그룹과 종려와 핀 꽃을 아로새기고 금으로 입히되 곧 그룹들과 종려에 금으로 입혔더라
Kwa hiyo akatengeneza na milango miwili ya mizeituni, na akainakshi kwa makerubi, na mitende, na maua yaliyochanua. Akasakafia kwa dhahabu na akatandaza dhahabu kwenye makerubi na kwenye mitende.
33 또 외소의 문을 위하여 감람목으로 문설주를 만들었으니 곧 벽의 사분지 일이며
Kwa njia hii, akalitengenezea hekalu miimo miwili ya mbao za mizeituni yenye pande nne
34 그 두 문짝은 잣나무라 이 문짝도 두 짝으로 접게 되었고 저 문짝도 두 짝으로 접게 되었으며
na milango miwili ya mbao za mierezi. Zile mbao mbili za mlango mmoja zilikuwa zikijikunja na mbao mbili za mlango wa pili nazo zilikuwa zikijikunja pia.
35 그 문짝에 그룹들과 종려와 핀 꽃을 아로새기고 금으로 입히되 그 새긴데 맞게 하였고
Akazinakshi kwa makerubi, mitende, na maua yaliyochanua, na pia akazisakafia kwa dhahabu juu ya zile nakshi.
36 또 다듬은 돌 세 켜와 백향목 두꺼운 판자 한 켜로 둘러 안뜰을 만들었더라
Akalijengs Korido la ndani kwa safu tatu za mawe ya kuchongwa na safu moja ya mhimili wa mierezi.
37 제사년 시브월에 여호와의 전 기초를 쌓았고
Msingi wa hekalu ulijengwa katika mwaka wa nne, wa mwezi wa Ziv.
38 제십일년 불월 곧 팔월에 그 설계와 식양대로 전이 다 필역되었으니 솔로몬이 전을 건축한 동안이 칠 년이었더라
Mwaka wa kumi na moja mwezi wa Buli, ambao ndio mwezi wa nane, sehemu zote za hekalu zilimalizika na sharti zake zote. Sulemani alilijenga hekalu kwa miaka saba.

< 열왕기상 6 >