< 역대상 29 >
1 다윗 왕이 온 회중에게 이르되 내 아들 솔로몬이 홀로 하나님의 택하신 바 되었으나 오히려 어리고 연약하고 이 역사는 크도다 이 전은 사람을 위한 것이 아니요 여호와 하나님을 위한 것이라
Mfalme Daudi akasema kwa kusanyiko lote, “Sulemani mwanangu, ambaye mwenyewe Mungu amemchagu, bado nimdogo na hana uzoefu, na jukumu ni kubwa. Maana hekalu sio kwa ajili ya watu bali la Mungu.
2 내가 이미 내 하나님의 전을 위하여 힘을 다하여 예비하였나니 곧 기구를 만들 금과 은과 놋과 철과 나무며 또 마노와 박을 보석과 꾸밀 보석과 채석과 다른 보석들과 화반석이 매우 많으며
Hivyo nimefanya kwa ubora wangu kutoa kwa ajili ya hekalu la Mungu. Nina toa dhahabu kwa vitu vya kujengwa na dhahabu, fedha kwa vitu vya kujengwa na fedha, shaba kwa vitu vya kujengwa na shaba, nishati kwa vitu vya kujengwa na nishati, na mbao kwa vitu vya kujengwa na mbao. Pia nina toa mawe ya shohamu, mawe ya kupangwa, mawe ya upambaji wandani ya rangi mbali mbali - kila haina ya mawe ya thamani - na marimari kwa wingi.
3 성전을 위하여 예비한 이 모든 것 외에도 내 마음에 내 하나님의 전을 사모하므로 나의 사유의 금, 은으로 내 하나님의 전을 위하여 드렸노니
Sasa, kwasababu ya mapenzi yangu kwa nyumba ya Mungu, Ninatoa hazina yangu binafsi ya dhahabu na fedha. Ninafanya hivi kwa nyongeza kwa yote niliyofanya katika hekalu takatifu:
4 곧 오빌의 금 삼천 달란트와 천은 칠천 달란트라 모든 전 벽에 입히며
talanta za dhahabu elfu tatu kutoka Ofiri, na talanta elfu saba za fedha zilizotakasika, ili kufunika kuta za majengo.
5 금, 은 그릇을 만들며 공장의 손으로 하는 모든 일에 쓰게 하였노니 오늘날 누가 즐거이 손에 채워 여호와께 드리겠느냐
Ninachangia dhahabu kwa vitu vya kujengwa na dhahabu, na fedha kwa vitu vya kujengwa na fedha, na kazi zote zinazotakiwa kufanywa na wajenzi. Nani mwingine anataka kuchangia kwa Yahweh leo na kujitoa kwake?”
6 이에 모든 족장과 이스라엘 모든 지파 어른과 천부장과 백부장과 왕의 사무 감독이 다 즐거이 드리되
Kisha sadaka za hiari zilitolewa na viongozi wa mababu wa familia zao, viongozi wa makabila ya Israeli, wakuu wa maelfu na mamia, na waamuzi waliojuu ya kazi ya mfalme.
7 하나님의 전 역사를 위하여 금 오천 달란트와 금 다릭 일만과 은 일만 달란트와 놋 일만 팔천 달란트와 철 십만 달란트를 드리고
Walitoa kwa ajili ya huduma ya nyumba ya Mungu talanta elfu tano na darkoni elfu kumi za dhahabu, talanta elfu kumi za fedha, talanta elfu nane za fedha, na talanta za chuma 100, 000.
8 무릇 보석이 있는 자는 게르손 사람 여히엘의 손에 부쳐 여호와의 전 곳간에 드렸더라
Haao walio na mawe ya thamani waliyatoa katika Hazina ya nyumba Yahweh, chini ya usimamizi wa Yehieli, mzao wa Gerishoni.
9 백성이 자기의 즐거이 드림으로 기뻐하였으니 곧 저희가 성심으로 여호와께 즐거이 드림이며 다윗 왕도 기쁨을 이기지 못하여 하니라
Watu walifurahi kwa ajili ya hizi sadaka za hiari, kwasababu walitoa kwa moyo wao wote kwa Yahweh. Mfalme Daudi pia alifurahi sana.
10 다윗이 온 회중 앞에서 여호와를 송축하여 가로되 우리 조상 이스라엘의 하나님 여호와여 주는 영원히 송축을 받으시옵소서
Daudi alimbariki Yahweh mbele ya kusanyiko lote. Alisema, “Na uabudiwe, Yahweh, Mungu wa Israeli babu wetu, milele na milele.
11 여호와여 광대하심과 권능과 영광과 이김과 위엄이 다 주께 속하였사오니 천지에 있는 것이 다 주의 것이로소이다 여호와여 주권도 주께 속하였사오니 주는 높으사 만유의 머리심이니이다
Kwako, Yahweh, kuna ukuu, nguvu, utukufu, ushindi, na enzi. Kwa kuwa yote yalio mbinguni na duniani ni yako. Kwako ni ufalme, Yahweh, na umetukuzwa kama mtawala juu ya vyote.
12 부와 귀가 주께로 말미암고 또 주는 만유의 주재가 되사 손에 권세와 능력이 있사오니 모든 자를 크게 하심과 강하게 하심이 주의 손에 있나이다
Utajiri na heshima utoka kwako, unatawala juu ya watu wote. Mkononi mwako kuna nguvu na uwezo. Unao uweza na nguvu ya kuwafanya watu kuwa mkuu na kumpa uweza yeyote.
13 우리 하나님이여 이제 우리가 주께 감사하오며 주의 영화로운 이름을 찬양하나이다
Kisha sasa, Mungu wetu, tunakushukuru na kusifu jina lako tukufu.
14 나와 나의 백성이 무엇이관대 이처럼 즐거운 마음으로 드릴 힘이 있었나이까 모든 것이 주께로 말미암았사오니 우리가 주의 손에서 받은 것으로 주께 드렸을 뿐이니이다
Lakini mimi ni nani, na watu wangu ni nani, tustahili kutoa kwa hiari hivi vitu? Kweli, vitu vyote vya toka kwako, na tumerudisha kwako vilivyo vyako.
15 주 앞에서는 우리가 우리 열조와 다름이 없이 나그네와 우거한 자라 세상에 있는 날이 그림자 같아서 머무름이 없나이다
Kwa kuwa sisi ni wageni na wasafiri mbele zako, mababu zetu wote walikuwa. Siku zetu katika dunia ni kama kivuli, na hakuna tumaini la kubaki duniani.
16 우리 하나님 여호와여 우리가 주의 거룩한 이름을 위하여 전을 건축하려고 미리 저축한 이 모든 물건이 다 주의 손에서 왔사오니 다 주의 것이니이다
Yahweh Mungu wetu, utajiri wote tulio kusanya kujenga hekalu kwa kuheshimu jina lako - watoka kwako na ni wako.
17 나의 하나님이여 주께서 마음을 감찰하시고 정직을 기뻐하시는 줄 내가 아나이다 내가 정직한 마음으로 이 모든 것을 즐거이 드렸사오며 이제 내가 또 여기 있는 주의 백성이 주께 즐거이 드리는 것을 보오니 심히 기쁘도소이다
Ninajua, Mungu wangu, unachunguza moyo na wapendezwa na unyofu. Kwangu mimi, kwa unyofu wa moyo wangu nimetoa kwa hiari vitu vyote, na sasa natazama kwa furaha watu walio hapa wakitoa tunu kwako.
18 우리 열조 아브라함과 이삭과 이스라엘의 하나님 여호와여 주께서 이것을 주의 백성의 심중에 영원히 두어 생각하게 하시고 그 마음을 예비하여 주께로 돌아오게 하옵시며
yahweh, Mungu wa Ibrahimu, Isaka, na Israeli - mababu zetu - hifadhi hili katika fikra za watu wako. Elekeza mioyo yao kwako.
19 또 내 아들 솔로몬에게 정성된 마음을 주사 주의 계명과 법도와 율례를 지켜 이 모든 일을 행하게 하시고 내가 위하여 예비한 것으로 전을 건축하게 하옵소서
Mjalie Sulemani mwanangu moyo wa shauku wakutii amri zako, shuhuda za agano lako, na maagizo yako, na kutekeleza mipango hii yote ya kujenga nyumba niliyoiandaa.”
20 다윗이 온 회중에게 이르되 너희는 너희 하나님 여호와를 송축하라 하매 회중이 그 열조의 하나님 여호와를 송축하고 머리를 숙여 여호와와 왕에게 절하고
Daudi akasema kwa kusanyiko lote, “Sasa mbariki Yahweh Mungu wenu.” Kusanyiko lote likambariki Yahweh, Munug wa mababu zao, wakainamisha vichwa vyao na kumuabudu Yahweh na kusujudu mbele za mfalme.
21 이튿날 여호와께 제사를 드리고 또 번제를 드리니 수송아지가 일천이요 수양이 일천이요 어린 양이 일천이요 또 그 전제라 온 이스라엘을 위하여 풍성한 제물을 드리고
Kwa siku iliyo fuata, wakatoa dhabiu kwa Yahweh na kumtolea sadaka ya kuteketeza. Walitoa sadaka ya ng'ombe elfu moja, kondoo elfu moja, na wana kondoo elfu moja, pamoja na sadaka zao za vinywaji na dhabihu tele kwa Israeli yote.
22 이 날에 무리가 크게 기뻐하여 여호와 앞에서 먹으며 마셨더라 무리가 다윗의 아들 솔로몬으로 다시 왕을 삼아 기름을 부어 여호와께 돌려 주권자가 되게 하고 사독에게도 기름을 부어 제사장이 되게 하니라
Siku ile, walikunywa na kula mbele za Yahweh kwa furaha tele. Walimfanya Sulemani, mwana wa Daudi, mfalme mara ya pili, na kumpaka mafuta ya mamlaka ya Yahweh kuwa mfalme. Pia walimpaka Zadoki mafuta kuwa mfalme.
23 솔로몬이 여호와께서 주신 위에 앉아 부친 다윗을 이어 왕이 되어 형통하니 온 이스라엘이 그 명령을 순종하며
Kisha Sulemani akaketi kwenye kiti cha enzi cha Yahweh kama mfalme baada ya Daudi baba yake. Alifanikiwa, na Israeli yote ikamtii.
24 모든 방백과 용사와 다윗 왕의 여러 아들이 솔로몬 왕에게 복종하니
Viongozi wote, wanajeshi, na Mfalme Daudi wanae wakaonyesha utii kwa Mfalme Sulemani.
25 여호와께서 솔로몬으로 이스라엘 무리의 목전에 심히 존대케 하시고 또 왕의 위엄을 주사 그 전 이스라엘 모든 왕보다 뛰어나게 하셨더라
Yahweh alimheshimu sana Sulemani na kumkirimia nguvu kubwa kuliko mfalme yeyote aliyetangulia kabla yake Israeli.
26 이새의 아들 다윗이 온 이스라엘의 왕이 되어
Daudi mwana wa Yese alitawala Israeli yote.
27 이스라엘을 치리한 날짜는 사십 년이라 헤브론에서 칠 년을 치리하였고 예루살렘에서 삼십삼 년을 치리하였더라
Daudi alikuwa mfalme wa Israeli kwa miaka arobaini. Alitawala kwa miaka saba Hebroni na miaka thelathini na tatu Yerusalemu.
28 저가 나이 많아 늙도록 부하고 존귀하다가 죽으매 그 아들 솔로몬이 대신하여 왕이 되니라
Alikufa katika umri mzuri mkubwa, baada ya kufurahia maisha marefu, utajiri na heshima. Sulemani mwanae alitawala baada yake.
29 다윗 왕의 시종 행적이 선견자 사무엘의 글과 선지자 나단의 글과 선견자 갓의 글에 다 기록되고
Mafanikio ya mfalme Daudi yameandikwa katika historia ya Samweli nabii, katika historia ya Nathani nabii, na katika historia ya Gadi nabii.
30 또 저의 왕 된 일과 그 권세와 저와 이스라엘과 온 세상 열국의 지난 시사가 다 기록되니라
Yalio ekwa kwenye kumbukumbu ni matendo ya utawala wake, mafanikio yake na mambo yalio mdhuru, Israeli, na falme zote za nchi zingine.