< 잠언 26 >

1 미련한 자에게는 영예가 적당하지 아니하니 마치 여름에 눈오는 것과 추수 때에 비오는 것 같으니라
Kama theluji wakati wa joto au mvua kwenye mavuno, ndivyo mpumbavu asivyostahili heshima.
2 까닭 없는 저주는 참새의 떠도는 것과 제비의 날아가는 것 같이 이르지 아니하느니라
Kama shorowanda hurukaruka na kumeza wadudu wakati wa kuruka, ndivyo ilivyo laana isiyostahili haishuki.
3 말에게는 채찍이요 나귀에게는 자갈이요 미련한 자의 등에는 막대기니라
Mjeledi ni kwa ajili ya farasi, hatamu kwa ajili ya punda na fimbo ni kwa ajili mgongo wa wapumbavu.
4 미련한 자의 어리석은 것을 따라 대답하지 말라 두렵건대 네가 그와 같을까 하노라
Usimjibu mpumbavu na kujiunga katika upumbavu wake, au utakuwa kama yeye.
5 미련한 자의 어리석은 것을 따라 그에게 대답하라 두렵건대 그가 스스로 지혜롭게 여길까 하노라
Mjibu mpumbavu na jiunge katika upumbavu wake, ili asiweze kuwa na busara katika macho yake mwenyewe.
6 미련한 자 편에 기별하는 것은 자기의 발을 베어 버림이라 해를 받느니라
Anayetuma ujumbe kwa mkono wa mpumbavu huikata miguu yake mwenyewe na kunywa vurugu.
7 저는 자의 다리는 힘 없이 달렸나니 미련한 자의 입의 잠언도 그러하니라
Miguu ya kiwete inayoning'ia chini ni kama mithali kwenye kinywa cha wapumbavu.
8 미련한 자에게 영예를 주는 것은 돌을 물매에 매는 것과 같으니라
Kujaribisha jiwe kwenye kombeo ni sawa na kumpa heshima mpumbavu.
9 미련한 자의 입의 잠언은 술 취한 자의 손에 든 가시나무 같으니라
Mwiba unaochoma kwenye mkono wa mlevi ni kama mithali kwenye kinywa cha wapumbavu.
10 장인이 온갖 것을 만들지라도 미련한 자를 고용하는 것은 지나가는 자를 고용함과 같으니라
Mpiga mishale anayejeruhi kila mtu ni kama mtu anayemwajiri mpumbavu au kila mtu anayepita karibu yake.
11 개가 그 토한 것을 도로 먹는 것 같이 미련한 자는 그 미련한 것을 거듭 행하느니라
Kama mbwa anavyorudia matapishi yake, ndivyo alivyo mpumbavu anayerudia upuuzi wake.
12 네가 스스로 지혜롭게 여기는 자를 보느냐 그보다 미련한 자에게 오히려 바랄 것이 있느니라
Je unamwona mtu mwenye busara katika macho yake mwenyewe? Mpumbavu anamatumaini zaidi kuliko yeye.
13 게으른 자는 길에 사자가 있다 거리에 사자가 있다 하느니라
Mtu mvivu husema “Kuna simba kwenye barabara! Kuna simba katikati ya njia kuu!”
14 문짝이 돌쩌귀를 따라서 도는 것 같이 게으른 자는 침상에서 구으느니라
Kama mlango unavyogeuka kwenye bawaba zake, ndivyo alivyo mtu mvivu kwenye kitanda chake.
15 게으른 자는 그 손을 그릇에 넣고도 입으로 올리기를 괴로와하느니라
Mtu mvivu hutia mkono wake kwenye sufuria na bado hana nguvu kuunyanyua kwenda kwenye kinywa chake.
16 게으른 자는 선히 대답하는 사람 일곱보다 자기를 지혜롭게 여기느니라
Mtu mvivu ni mwenye hekima kwenye macho yake mwenyewe kuliko watu saba wenye ufahamu.
17 길로 지나다가 자기에게 상관없는 다툼을 간섭하는 자는 개 귀를 잡는 자와 같으니라
Kama mtu anayeshikilia masikio ya mbwa, ndivyo alivyo mpitajia anayepata hasira kwenye ugomvi ambao si wake.
18 횃불을 던지며 살을 쏘아서 사람을 죽이는 미친 사람이 있나니
Kama mtu mwendawazimu anayetupa mishale,
19 자기 이웃을 속이고 말하기를 내가 희롱하였노라 하는 자도 그러하니라
ndivyo alivyo ambaye humdanganya jirani yake na kusema, “Je sikuwa naongea utani?”
20 나무가 다하면 불이 꺼지고 말장이가 없어지면 다툼이 쉬느니라
Kwa kukosa kuni, moto huzimika; na pale pasipo na mmbea ugomvi hukoma.
21 숯불 위에 숯을 더하는 것과 타는 불에 나무를 더하는 것 같이 다툼을 좋아하는 자는 시비를 일으키느니라
Mkaa ni kwa kuwasha makaa na kuni kwa ajili ya moto, ndivyo alivyo mtu mgomvi kwa kuwasha ugomvi.
22 남의 말하기를 좋아하는 자의 말은 별식과 같아서 뱃 속 깊은 데로 내려가느니라
Maneno ya mmbea ni kama chembe tamu; nazo zinashuka chini kwenye sehemu za ndani ya mwili.
23 온유한 입술에 악한 마음은 낮은 은을 입힌 토기니라
Kioo kinachofunika chombo cha udongo ni kama midomo inayoungua na moyo mbaya.
24 감정있는 자는 입술로는 꾸미고 속에는 궤휼을 품나니
Yule ambaye huwachukia wengine huficha hisia zake kwa midomo na hufunika uongo ndani yake mwenyewe.
25 그 말이 좋을지라도 믿지 말 것은 그 마음에 일곱 가지 가증한 것이 있음이라
Ataongea kwa huruma, lakini usimwamini, maana kuna machukizo saba kwenye moyo wake.
26 궤휼로 그 감정을 감출지라도 그 악이 회중 앞에 드러나리라
Ingawa chuki zake zimefunikwa kwa udanganyifu, uovu wake utakuwa wazi katika kusanyiko.
27 함정을 파는 자는 그것에 빠질 것이요 돌을 굴리는 자는 도리어 그것에 치이리라
Anayechimba shimo atatumbukia ndani yake na jiwe litamsaga yule anayelisukuma.
28 거짓말하는 자는 자기의 해한 자를 미워하고 아첨하는 입은 패망을 일으키느니라
Ulimi wa uongo huchukia watu unaowajeruhi na kinywa cha uongo husogeza karibu uharibifu.

< 잠언 26 >