< 레위기 14 >

1 여호와께서 모세에게 일러 가라사대
Yahwe alizungumza na Musa, akisema,
2 문둥 환자의 정결케 되는 날의 규례는 이러하니 곧 그 사람을 제사장에게로 데려갈 것이요
“Hii itakuwa sheria kwaajili ya mtu aliyekufa kwenye siku ya utakaso. Lazima aletwe kwa kuhani.
3 제사장은 진에서 나가서 진찰할지니 그 환자에게 있던 문둥병 환처가 나았으면
Kuhani atakwenda nje ya kambi kumchunguza mtu kuona kama madhara ya ugonjwa wa ngozi yameponywa.
4 제사장은 그를 위하여 명하여 정한 산 새 두마리와, 백향목과, 홍색실과, 우슬초를 가져오게 하고
Ndipo kuhani ataamuru kwamba mtu mwenye kutakaswa lazima achukue ndege safi wawili, waliohai, mti wa mwerezi, kitani nyekundu na hisopo.
5 제사장은 또 명하여 그 새 하나는 흐르는 물 위 질그릇 안에서 잡게 하고
Kuhani atamwamuru kuua moja ya hao ndege juu ya maji safi yaliyo kwenye chungu cha udongo.
6 다른 새는 산대로 취하여 백향목과, 홍색실과, 우슬초와 함께 가져다가 흐르는 물 위에서 잡은 새 피를 찍어
Ndipo kuhani atamchukua ndege aliyehai na mti wa mwerezi, na kitani nyekundu na hisopo, na vyote hivi, pamoja na ndege aliyehai atavichovya kwenye damu ya ndege aliyechinjiwa kwenye maji safi.
7 문둥병에서 정결함을 받을 자에게 일곱번 뿌려 정하다 하고 그 산 새는 들에 놓을지며
Ndipo kuhani atanyunyiza maji haya mara saba juu ya mtu anayetakaswa katika ugonjwa, na ndipo kuhani atamtangaza kuwa msafi. Ndipo kuhani atamwachia ndege aliyehai katika eneo wazi.
8 정결함을 받는 자는 그 옷을 빨고 모든 털을 밀고 물로 몸을 씻을 것이라 그리하면 정하리니 그 후에 진에 들어올 것이나 자기 장막 밖에 칠일을 거할 것이요
Mtu aliyetakaswa atafua nguo zake, atanyoa nywele zake zote, ataoga kwa maji, na ndipo atakuwa safi. Baada ya hayo lazima aje kwenye kambi, lakini ataishi nje ya hema lake kwa siku saba.
9 칠일만에 그 모든 털을 밀되 머리털과 수염과 눈썹을 다 밀고 그 옷을 빨고 몸을 물에 씻을 것이라 그리하면 정하리라
Katika siku ya saba lazima anyoe nywele za kichwa chake, na lazima pia anyoe ndevu zake na nyusi. Lazima anyoe nywele zake zote, na lazima afue nguo zake na aoge kwenye maji; ndipo atakuwa safi.
10 제 팔일에 그는 흠 없는 어린 수양 둘과 일년 된 흠 없는 어린 암양 하나와 또 고운 가루 에바 십분 삼에 기름 섞은 소제물과 기름 한 록을 취할 것이요
Katika siku ya nane lazima achukue dume wa wana kondoo wawili wasio na lawama, mwana kondoo jike wa mwaka mmoja asiye na lawama, na tatu ya kumi ya efa ya unga safi uliochanganywa mafuta kama sadaka ya nafaka, na kipimo kimoja cha mafuta.
11 정결케 하는 제사장은 정결함을 받을 자와 그 물건들을 회막 문 여호와 앞에 두고
Kuhani ambaye amemtakasa mtu atamsimamisha mtu ambaye aliyemtakasa, pamoja na vile vitu, mbele ya Yahwe mahali pa kuingilia kwenye hema ya mkutano.
12 어린 수양 하나를 취하여 기름 한 록과 아울러 속건제로 드리되 여호와 앞에 흔들어 요제를 삼고
Kuhani atachukua mmoja wa wanakondoo dume na kumtoa kama sadaka ya hatia, pamoja na kipimo cha mafuta; atavitikisa kwa sadaka ya kutikiswa mbele ya Yahwe.
13 그 어린 수양은 거룩한 장소 곧 속죄제와 번제 희생 잡는 곳에서 잡을 것이며 속건 제물은 속죄 제물과 일례로 제사장에게 돌릴지니 이는 지극히 거룩한 것이니라
Lazima aue mwana kondoo dume mahali ambapo wanapochinjia sadaka ya dhambi na sadaka ya kuteketezwa, katika eneo la hema, sababu sadaka ya dhambi ni ya kuhani, kama afanyavyo sadaka ya hatia, kwasababu ni takatifu zaidi.
14 제사장은 그 속건제 희생의 피를 취하여 정결함을 받을 자의 우편 귓부리와, 우편 손 엄지가락과, 우편 발 엄지가락에 바를 것이요
Kuhani atachukua baadhi ya damu ya sadaka ya hatia na kuiweka kwenye ncha ya sikio la kulia la mtu yule wa kutakaswa, katika dole gumba la kulia, katika dole la mguu wa kulia.
15 제사장은 또 그 한 록의 기름을 취하여 자기 좌편 손바닥에 따르고
Ndipo kuhani atachukua mafuta kutoka chombo na kuyamimina katika kiganja cha mkono wake wa kushoto, na kuzamisha kidole chake katika mafuta hayo yaliyo kwenye mkono wa kushoto,
16 우편 손가락으로 좌편 손의 기름을 찍어 그 손가락으로 그것을 여호와 앞에 일곱번 뿌릴 것이요
na kunyunyiza baadhi ya mafuta kwa kidole mara saba mbele za Yahwe.
17 손에 남은 기름은 제사장이 정결함을 받는 자의 우편 귓부리와, 우편 손 엄지가락과, 우편 발 엄지가락 곧 속건제 희생의 피 위에 바를 것이며
kuhani ataweka mafuta yaliyobaki kwenye mkono wake kwenye ncha ya sikio la kulia la mtu wa kutakaswa, juu ya dole gumba la mkono wa kulia, na katika dole kubwa la mguu wa kulia. Lazima aweke mafuta haya juu ya damu kutoka kwenye sadaka ya hatia.
18 오히려 그 손에 남은 기름은 제사장이 그 정결함을 받는 자의 머리에 바르고 여호와 앞에서 제사장은 그를 위하여 속죄하고
Kama kwa mafuta yaliyosalia kwamba katika mkono wa kuhani, atayaweka juu ya kichwa cha mtu ambaye atakaswaye, na kuhani atafanya utakaso kwaajili yake mbele za Yahwe.
19 또 제사장은 속죄제를 드려 그 부정함을 인하여 정결함을 받으려는 자를 위하여 속죄하고 그 후에 번제 희생을 잡을 것이요
Ndipo kuhani atatoa sadaka ya dhambi na kufanya upatanisho kwaajili yake atakaswaye kwa sababu ya kutokuwa safi kwake, na badaye ataua sadaka ya kuchomwa.
20 제사장은 그 번제와 소제를 단에 드려 그를 위하여 속죄할 것이라 그리하면 그가 정결하리라!
Ndipo kuhani atatoa sadaka ya kuteketezwa na sadaka ya nafaka juu ya madhabahu. Kuhani atafanya upatanisho kwaajili ya mtu huyo, na ndipo atakuwa safi.
21 그가 가난하여 이에 힘이 미치지 못하면 그는 흔들어 자기를 속할 속건제를 위하여 어린 수양 하나와 소제를 위하여 고운 가루 에바 십분 일에 기름 섞은 것과 기름 한 록을 취하고
Kwa namna hiyo, kama mtu ni masikini na hawezi kumudu matoleo haya, ndipo anaweza kuchukua kondoo mmoja dume kama sadaka ya hatia ya kutikiswa, kufanya upatanisho kwaajili yake mwenyewe, na moja ya kumi ya efa ya unga safi uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka, na chombo cha mafuta,
22 그 힘이 미치는 대로 산비둘기 둘이나 집비둘기 새끼 둘을 취하되 하나는 속죄 제물로, 하나는 번제물로 삼아
pamoja na njiwa wawili au kinda mbili za njiwa, ambao anaweza kupata; ndege mmoja atakuwa sadaka ya dhambi na mwingine sadaka ya kuteketezwa.
23 제 팔일에 그 결례를 위하여 그것들을 회막 문 여호와 앞 제사장에게로 가져갈 것이요
Katika siku ya nane lazima awalete kwa kuhani kwaajili ya utakaso, pakuigilia katika hema ya mkutano, mbele ya Yahwe.
24 제사장은 속건제 어린 양과 기름 한 록을 취하여 여호와 앞에 흔들어 요제를 삼고
Kuhani atachukua mwana kondoo kwaajili ya sadaka, na atachukua pamoja na kiasi cha mafuta ya mzeituni, na ataviinua juu kama anaviwasilisha kwa Yahwe.
25 속건제의 어린 양을 잡아서 제사장은 그 속건제 희생의 피를 취하여 정결함을 받을 자의 우편 손 엄지 가락과, 우편 발 엄지가락에 바를 것이요
Atamuua mwana kondoo kwaajili ya sadaka ya hatia, na atachukua baadhi ya ya damu ya sadaka ya hatia na kuiweka juu ya ncha ya sikio la kulia la yule wakutakaswa, juu ya dole gumba la mkono wake wa kulia, na kwenye dole kubwa la mguu, wa kulia.
26 제사장은 그 기름을 자기 좌편 손바닥에 따르고
Ndipo kuhani atamimina baadhi ya mafuta katika kiganja cha mkono wake wa kushoto,
27 우편 손가락으로 좌편 손의 기름을 조금 찍어 여호와 앞에 일곱번 뿌릴 것이요
na atanyunyiza kwa kidole chake cha kulia baadhi ya mafuta ambayo yako kwenye mkono wa kushoto mara saba mbele za Yahwe.
28 그 손의 기름은 제사장이 정결함을 받을 자의 우편 귓부리와, 우편 손 엄지가락과, 우편 발 엄지가락 곧 속건제 희생의 피를 바른 곳에 바를 것이며
Ndipo kuhani ataweka kiasi cha mafuta ambayo yako kwenye mkono wake kwenye ncha ya sikio la yule mtu wa kutakaswa, katika dole gumba lake la mkono wa kulia, na dole kubwa la mguu wa kulia, maeneo yale yale ambayo kaweka damu ya sadaka ya hatia.
29 또 그 손에 남은 기름은 제사장이 그 정결함을 받는 자의 머리에 발라 여호와 앞에서 그를 위하여 속죄할 것이며
Ataweka mafuta yaliyobaki yaliyo mkononi mwake juu ya yule wakutakaswa, kufanya upatanisho kwaajili yake mbele za Yahwe.
30 그는 힘이 미치는 대로 산비둘기 하나나 집비둘기 새끼 하나를 드리되
Lazima atoe sadaka ya njiwa au makinda ya njiwa, yale ambayo mtu ameweza kupata -
31 곧 그 힘이 미치는 것의 하나는 속죄제로, 나는 소제와 함께 번제로 드릴 것이요, 제사장은 정결함을 받을 자를 위하여 여호와 앞에 속죄할지니
moja kama ya sadaka ya dhambi na nyingine kama sadaka ya kuteketezwa, pamoja na sadaka ya nafaka. Ndipo kuhani atafanya upatanisho kwaajili ya yule ambaye atatakaswa mbele za Yahwe.
32 문둥병 환자로서 그 결례에 힘이 부족한 자의 규례가 이러하니라
Hii ni sheria kwaajili ya mtu kwake kuna athari za ugonjwa wa ngozi, ambaye hawezi kumudu kiwango cha sadaka kwaajili ya utakaso wake.”
33 여호와께서 모세와 아론에게 일러 가라사대
Yahwe alizungumza na Musa na Haruni, akisema,
34 내가 네게 기업으로 주는 가나안 땅에 너희가 이른 때에 내가 너희 기업의 땅에서 어느 집에 문둥병 색점을 발하게 하거든
“Wakati mtakuja katika nchi ya Kanaani ambayo nimewapa kama miliki, na kama naweka ukungu unaenea ndani ya nyumba katika nchi ya miliki yenu,
35 그 집 주인은 제사장에게 와서 고하기를 무슨 색점이 집에 생겼다 할 것이요
ndipo yeye ambaye anamiliki nyumba ile lazima aje na kumwambia kuhani. Lazima aseme 'Inaonekana kwangu kuna kitu fulani kama ukungu ndani ya nyumba yangu.'”
36 제사장은 그 색점을 보러 가기 전에 그 가장 집물에 부정을 면케하기 위하여 명하여 그 집을 비게 한 후에 들어가서 그 집을 볼지니
Ndipo kuhani ataamuru kwamba watoe vitu vyote ndani kabla hajaenda ndani kuona uthibitisho wa ukungu, kiasi kwamba hakuna ndani ya nyumba kitakachofanywa najisi. Badaye kuhani lazima aende ndani kuona humo ndani.
37 그 색점을 볼 때에 그 집 벽에 푸르거나 붉은 무늬의 색점이 있어 벽보다 우묵하면
Yeye lazima achunguze ukungu kuona kama umo katika kuta za nyumba, na kuona ikiwa kunaonekana ukijani au wekundu katika bonde za mwonekano wa kuta.
38 제사장은 그 집 문으로 나와 그 집을 칠일 동안 폐쇄하였다가
Kama nyumba inao ukungu, ndipo kuhani atatoka nje ya nyuma na kufunga mlango wa nyumba kwa siku saba.
39 칠일만에 또 와서 살펴볼 것이요 그 색점이 벽에 퍼졌으면
Ndipo kuhani atarudi tena katika siku ya saba na kuichunguza kuona kama ukungu umeenea katika kuta za nyumba.
40 그는 명하여 색점 있는 돌을 빼어 성 밖 부정한 곳에 버리게 하고
Kama hivyo, ndipo kuhani ataamuru kwamba wayaondoe mawe ambayo ukungu umepatikana na yatupwe katika sehemu najisi nje ya mji.
41 또 집안 사면을 긁게 하고 그 긁은 흙을 성 밖 부정한 곳에 쏟아버리게 할 것이요
Yeye atataka kuta zote za ndani ya nyumba zikwanguliwe, na lazima achukue vitu vilivyochafuliwa na hivyo vilivyokwanguliwa nje ya mji na kuvitupa kwenye eneo lisilosafi.
42 그들은 다른 돌로 그 돌을 대신하며 다른 흙으로 집에 바를지니라
Lazima wayachukue mawe mengine na kuyaweka katika sehemu ya mawe yaliyoondolewa, na lazima watumie udongo mpya kupigia lipu nyumba.
43 돌을 빼며 집을 긁고 고쳐 바른 후에 색점이 집에 복발하거든
Kama ukungu unakuja tena na unaingia katika nyumba ambayo mawe yameondolewa na kuta zimekwanguliwa na kupigwa lipu upya,
44 제사장은 또 와서 살펴볼 것이요 그 색점이 만일 집에 퍼졌으면 악성 문둥병인즉 이는 부정하니
ndipo kuhani lazima aje aingie ndani na kuchunguza nyumba kuona kama ukungu umeenea ndani ya nyumba. Kama hivyo, huo ni ukungu mbaya, na nyumba ni najisi.
45 그는 그 집을 헐고 돌과 그 재목과 그 집의 모든 흙을 성 밖 부정한 곳으로 내어갈 것이며
Nyumba hiyo lazima iangushwe chini. Hayo mawe, mbao, na lipu yote ndani ya nyumba lazima vibebwe kupelekwa nje ya mji kwenye sehemu najisi.
46 그 집을 폐쇄한 날 동안에 들어가는 자는 저녁까지 부정할 것이요
Kwa nyongeza, yeyote anaenda ndani ya nyumba wakati imefungwa atakuwa najisi mpaka jioni.
47 그 집에서 자는 자는 그 옷을 빨 것이요 그 집에서 먹는 자도 그 옷을 빨 것이니라
Na yeyote aliyelala ndani ya nyumba lazima afue nguo zake, na yeyote aliyekula ndani ya nyumba lazima afue nguo zake.
48 그 집을 고쳐 바른 후에 제사장이 들어가 살펴 보아서 색점이 집에 퍼지지 아니하였으면 이는 색점이 나은 것이니 제사장은 그 집을 정하다 하고
Kama kuhani akaingia hiyo kuichunguza kuona ikiwa ukungu umeenea katika nyumba baada ya nyumba kupigwa lipu, ndipo, kama ukungu umetoweka, ataitangaza nyumba hiyo kuwa ni safi.
49 그는 그 집을 정결케 하기 위하여 새 두마리와, 백향목과, 홍색실과, 우슬초를 취하고
Ndipo kuhani lazima achukue ndege wawili kuitakasa nyumba, na mti wa mwelezi, na sufu nyekundu, na hisopo.
50 그 새 하나를 흐르는 물 위 질그릇 안에서 잡고
Atamuua ndege mmojawapo katika maji masafi kwenye dumu la udongo.
51 백향목과, 우슬초와, 홍색실과, 산새를 가져다가 잡은 새의 피와 흐르는 물을 찍어 그 집에 일곱번 뿌릴 것이요
Atachukua mti wa mwerezi, hisopo, sufu nyekundu na ndege aliyehai, na kuvichovya kwenye damu ya ndege aliyekufa, kwenye maji safi, na kunyunyizia nyumba mara saba.
52 그는 새의 피와, 흐르는 물과, 산새와, 백향목과, 우슬초와, 홍색실로 집을 정결케 하고
Ataitakasa nyumba kwa damu ya ndege na maji safi, pamoja na ndege aliyehai, mti wa mwerezi, hisopo, na sufu nyekundu. Lakini atamwachia ndege aliyehai aende nje ya mji mashambani.
53 그 산새는 성 밖 들에 놓아 그 집을 위하여 속할 것이라 그리하면 정결하리라!
Kwa njia hii lazima afanye upatanisho kwaajili ya nyumba, na itakuwa safi.
54 이는 각종 문둥병 환처에 대한 규례니 곧 옴과
Hii ni sheria kwa aina zote za athari ya ugonjwa wa ngozi na vitu vyote vinavyosababisha ugonjwa kama huo, na kwaajili ya kuwashwa,
55 의복과 가옥의 문둥병과
na kwa ukungu kwenye mavazi na nyumba,
56 붓는 것과 피부병과 색점의
kwaajili ya uvimbe, kwaajili ya vipele, madoa,
57 언제는 부정하고 언제는 정함을 가르치는 것이니 문둥병의 규례가 이러하니라
kutambua wakati wowote tatizo hili ni najisi au lini limetakaswa. Hii ni sheria kwaajili ya athari za ugonjwa wa ukungu.

< 레위기 14 >