< 역대상 7 >
1 잇사갈의 아들들은 돌라와, 부아와, 야숩과, 시므론 네 사람이며
Wana wa Isakari walikuwa: Tola, Pua, Yashubu na Shimroni; wote ni wanne.
2 돌라의 아들들은 웃시와, 르바야와, 여리엘과, 야매와, 입삼과, 스므엘이니 다 그 아비 돌라의 집 족장이라 대대로 용사더니 다윗 때에 이르러는 그 수효가 이만 이천 육백명이었더라
Wana wa Tola walikuwa: Uzi, Refaya, Yerieli, Yahmai, Ibsamu na Shemueli waliokuwa viongozi wa jamaa zao. Wakati wa utawala wa Mfalme Daudi, wazao wa Tola walioorodheshwa kama wapiganaji katika ukoo wao walikuwa watu 22,600.
3 웃시의 아들은 이스라히야요 이스라히야의 아들들은 미가엘과, 오바댜와, 요엘과, 잇시야 다섯 사람이 모두 족장이며
Mwana wa Uzi alikuwa: Izrahia. Wana wa Izrahia walikuwa: Mikaeli, Obadia, Yoeli na Ishia. Wote hawa watano walikuwa wakuu wao.
4 저희와 함께한 자는 그 보계와 종족대로 능히 출전할만한 군대가 삼만 육천인이니 이는 그 처자가 많은 연고며
Kulingana na ukoo wa jamaa zao, walikuwa na watu hodari wa vita wapatao 36,000, kwa sababu walikuwa na wanawake na watoto wengi.
5 그 형제 잇사갈의 모든 종족은 다 큰 용사라 그 보계대로 계수하면 팔만 칠천인이었더라
Jamaa ya watu waliokuwa wapiganaji hodari kutoka koo zote za Isakari, kama ilivyoorodheshwa katika ukoo wao, jumla yao walikuwa 87,000.
6 베냐민의 아들들은 벨라와, 베겔과, 여디아엘 세 사람이며
Wana watatu wa Benyamini walikuwa: Bela, Bekeri na Yediaeli.
7 벨라의 아들들은 에스본과, 우시와, 웃시엘과, 여리못과, 이리 다섯 사람이니 다 그 집의 족장이요 큰 용사라 그 보계대로 계수하면 이만 이천 삼십 사인이며
Wana wa Bela walikuwa: Esboni, Uzi, Uzieli, Yeremothi na Iri; walikuwa viongozi wa jamaa zao; wote ni watano. Watu wapiganaji walioorodheshwa katika ukoo wao walikuwa 22,034.
8 베겔의 아들들은 스미라와, 요아스와, 엘리에셀과, 엘료에내와, 오므리와, 여레못과, 아비야와, 아나돗과, 알레멧이니 베겔의 아들들은 이러하며
Wana wa Bekeri walikuwa: Zemira, Yoashi, Eliezeri, Elioenai, Omri, Yeremothi, Abiya, Anathothi na Alemethi. Hawa wote walikuwa wana wa Bekeri.
9 저희는 다 그 집의 족장이요 큰 용사라 그 자손을 보계대로 계수하면 이만 이백인이며
Orodha ya ukoo wao iliyoandikwa viongozi wa jamaa zao walikuwa wapiganaji 20,200.
10 여디아엘의 아들은 빌한이요 빌한의 아들들은 여우스와, 베냐민과, 에훗과, 그나아나와, 세단과, 다시스와, 아히사할이니
Mwana wa Yediaeli alikuwa: Bilhani. Wana wa Bilhani walikuwa: Yeushi, Benyamini, Ehudi, Kenaana, Zethani, Tarshishi na Ahishahari.
11 이 여디아엘의 아들들은 그 집의 족장이요 큰 용사라 그 자손 중에 능히 출전할만한 자가 일만 칠천 이백인이며
Hawa wana wote wa Yediaeli walikuwa viongozi wa jamaa zao. Kulikuwako wanaume wapiganaji 17,200 waliokuwa tayari kwenda vitani.
12 일의 아들은 숩빔과, 훔빔이요 아헬의 아들은 후심이더라
Washupimu na Wahupimu walikuwa wazao wa Iri. Wahushimu walikuwa wazao wa Aheri.
13 납달리의 아들들은 야시엘과, 구니와, 예셀과, 살룸이니 이는 빌하의 손자더라
Wana wa Naftali walikuwa: Yahzieli, Guni, Yeseri na Shalumu; hao walikuwa wazao wa Bilha.
14 므낫세의 아들들 그 처의 소생은 아스리엘이요 그 첩 아람 여인의 소생은 길르앗의 아비 마길이니
Wana wa Manase walikuwa: Asirieli alikuwa mzao wake kutokana na suria wake wa Kiaramu. Huyu suria akamzaa Makiri baba wa Gileadi.
15 마길은 훔빔과 숩빔의 누이 마아가라 하는 이에게 장가들었더라 므낫세의 둘째 아들의 이름은 슬로브핫이니 슬로브핫은 딸들만 낳았으며
Makiri akatwaa mke kutoka miongoni mwa Wahupimu na Washupimu. Jina la dada yake aliitwa Maaka. Mwana wa pili wa Makiri aliitwa Selofehadi, ambaye alikuwa na wasichana tu.
16 마길의 아내 마아가는 아들을 낳아 그 이름을 베레스라 하였으며 그 아우는 이름이 세레스며 세레스의 아들은 울람과 라겜이요
Maaka mkewe Makiri akamzaa mwana aliyemwita Pereshi. Jina la nduguye lilikuwa Shereshi. Wana wa Pereshi walikuwa Ulamu na Rakemu.
17 울람의 아들은 브단이니 이는 다 길르앗의 자손이라 길르앗은 마길의 아들이요 므낫세의 손자며
Mwana wa Ulamu alikuwa: Bedani. Hawa ndio waliokuwa wana wa Gileadi mwana wa Makiri, mwana wa Manase.
18 그 누이 함몰레겟은 이스홋과, 아비에셀과, 말라를 낳았고
Dada yake aliyeitwa Hamolekethi aliwazaa Ish-Hodi, Abiezeri na Mahla.
19 스미다의 아들은 아히안과, 세겜과, 릭히와, 아니암이더라
Wana wa Shemida walikuwa: Ahiani, Shekemu, Liki na Aniamu.
20 에브라임의 아들은 수델라요 그 아들은 베렛이요 그 아들은 다핫이요 그 아들은 엘르아다요 그 아들은 다핫이요
Wana wa Efraimu walikuwa: Shuthela, ambaye alimzaa Beredi, Beredi akamzaa Tahathi, Tahathi akazaa Eleada, Eleada akamzaa Tahathi,
21 그 아들은 사밧이요 그 아들은 수델라며 저가 또 에셀과 엘르앗을 낳았더니 저희가 가드 토인에게 죽임을 당하였으니 이는 저희가 내려가서 가드 사람의 짐승을 빼앗고자 하였음이라
Tahathi akamzaa Zabadi, na Zabadi akamzaa Shuthela. Ezeri na Eleadi waliuawa na wenyeji wa Gathi walipokuwa wamekwenda huko kuwanyangʼanya mifugo yao.
22 그 아비 에브라임이 위하여 여러 날 슬퍼하므로 그 형제가 와서 위로하였더라
Baba yao Efraimu akawaombolezea kwa siku nyingi, na jamaa zake wakaja kumfariji.
23 그 후에 에브라임이 그 아내와 동침하였더니 아내가 잉태하여 아들을 낳으니 그 집이 재앙을 받았으므로 그 이름을 브리아라 하였더라
Kisha akakutana kimwili na mke wake tena, naye akachukua mimba, akamzalia mwana. Akamwita Beria, kwa sababu ya misiba iliyoipata nyumba yake.
24 에브라임의 딸은 세에라니 저가 아래 윗 벧호론과 우센세에라를 세웠더라
Beria alikuwa na binti jina lake Sheera. Huyu ndiye aliijenga miji ya Beth-Horoni ya Juu na Beth-Horoni ya Chini, pamoja na Uzen-Sheera.
25 브리아의 아들들은 레바와, 레셉이요 레셉의 아들은 델라요 그 아들은 다한이요
Beria akamzaa pia Refa, naye Refa akamzaa Reshefu, Reshefu akamzaa Tela, Tela akamzaa Tahani,
26 그 아들은 라단이요 그 아들은 암미훗이요 그 아들은 엘리사마요
Tahani akamzaa Ladani, Ladani akamzaa Amihudi, Amihudi akamzaa Elishama,
27 그 아들은 눈이요 그 아들은 여호수아더라
Elishama akamzaa Nuni, Nuni akamzaa Yoshua.
28 에브라임 자손의 산업과 거처는 벧엘과 그 향리요 동에는 나아란이요 서에는 게셀과 그 향리며 또 세겜과 그 향리니 아사와 그 향리까지며
Nchi zao na makazi yao yalijumuisha Betheli na vijiji vilivyouzunguka, Naarani ilikuwa upande wa mashariki, Gezeri pamoja na vijiji vyake upande wa magharibi, pia Shekemu na vijiji vyake hadi kufikia Aya na vijiji vyake.
29 또 므낫세 자손의 지경에 가까운 벧스안과 그 향리와 다아낙과 그 향리와 므깃도와 그 향리와 돌과 그 향리라 이스라엘의 아들 요셉의 자손이 이 여러 곳에 거하였더라
Katika mipaka ya Manase walikuwepo Beth-Shani, Taanaki, Megido na Dori pamoja na vijiji vyake. Wana wa Yosefu mwana wa Israeli waliishi katika miji hii.
30 아셀의 아들들은 임나와, 이스와와, 이스위와, 브리아요 저희의 매제는 세라며
Wana wa Asheri walikuwa: Imna, Ishva, Ishvi na Beria. Dada yao alikuwa Sera.
31 브리아의 아들들은 헤벨과, 말기엘이니 말기엘은 비르사잇의 아비며
Wana wa Beria walikuwa: Heberi na Malkieli, aliyekuwa baba yake Birzaithi.
32 헤벨은 야블렛과, 소멜과, 호담과 저희의 매제 수아를 낳았으며
Heberi akawazaa Yafleti, Shomeri na Hothamu, na Shua dada yao.
33 야블렛의 아들들은 바삭과, 빔할과, 아스왓이니 야블렛의 아들은 이러하며
Wana wa Yafleti walikuwa: Pasaki, Bimhali na Ashvathi. Hawa walikuwa wana wa Yafleti.
34 소멜의 아들들은 아히와, 로가와, 호바와, 아람이요
Wana wa Shemeri walikuwa: Ahi, Roga, Yehuba na Aramu.
35 그 아우 헬렘의 아들들은 소바와, 임나와, 셀레스와, 아말이요
Wana wa Helemu ndugu yake walikuwa: Sofa, Imna, Sheleshi na Amali.
36 소바의 아들들은 수아와, 하르네벨과, 수알과, 베리와, 이므라와
Wana wa Sofa walikuwa: Sua, Harneferi, Shuali, Beri, Imra,
37 베셀과, 홋과, 사마와, 실사와, 이드란과, 브에라요
Bezeri, Hodu, Shama, Shilsha, Ithrani na Beera.
38 예델의 아들들은 여분네와, 비스바와, 아라요
Wana wa Yetheri walikuwa: Yefune, Pispa na Ara.
39 울라의 아들들은 아라와, 한니엘과, 리시아니
Wana wa Ula walikuwa: Ara, Hanieli na Risia.
40 이는 다 아셀의 자손으로 족장이요 뽑힌 큰 용사요 방백의 두목이라 출전할만한 자를 그 보계대로 계수하면 이만 육천인이었더라
Hawa wote ndio waliokuwa wazao wa Asheri, viongozi wa jamaa zao, watu bora, mashujaa walio hodari na viongozi maarufu. Idadi ya watu waliokuwa tayari kwa vita, kama ilivyoorodheshwa katika ukoo wao, walikuwa 26,000.