< 열왕기하 9 >

1 선지자 엘리사가 선지자의 생도 중 하나를 불러 이르되 너는 허리를 동이고 이 기름병을 손에 가지고 길르앗 라못으로 가라
Nabii Elisha akamwita mmoja wa watoto wa manabii na kumwambia, “Vaa kwa kwa safari, halafu chukua hii chupa ndogo ya mafuta kwenye mikono yako na uende Romoth Geliadi.
2 거기 이르거든 님시의 손자 여호사밧의 아들 예후를 찾아 들어가서 그 형제 중에서 일어나게 하고 데리고 골방으로 들어가서
Wakati utakapofika, mtafute Yehu mwana wa Yehoshafati mwana wa Nimshi, na uende ukaingie na kumfanya ainuke kutoka miongoni mwa rafiki zake, na ukampeleke katika chumba cha ndani.
3 기름병을 가지고 그 머리에 부으며 이르기를 여호와의 말씀이 내가 네게 기름을 부어 이스라엘 왕을 삼노라 하셨느니라 하고 곧 문을 열고 도망하되 지체치 말지니라
Kisha chukua ile chupa ya mafuta na imiminie kwenye kichwa chake na kusema, 'Yahwe anasema hivi: “Nimekumiminia mafuta uwe mfalme juu ya Israeli. “Halafu fungua mlango, na kukimbia; usichelewe.”
4 그 소년 곧 소년 선지자가 드디어 길르앗 라못으로 가니라
Basi yule kijana, yule nabii kijana, akaenda Romoth Geliadi.
5 저가 이르러 보니 군대 장관들이 앉았는지라 소년이 가로되 `장관이여 내가 당신에게 할 말씀이 있나이다' 예후가 가로되 `우리 모든 사람중에 뉘게 하려느냐' 가로되 `장관이여 당신에게니이다'
Wakati alipofika, kumbe, wale manahodha wa lile jeshi walikuwa wamekaa. Hivyo yule nabii kijana akasema, “Nimekuja mara moja naneno kwako, nahodha.” Yehu akajibu, “kwa yupi katika sisi?” Yule nabii kijana akajibu, “Kwako nahodha.”
6 예후가 일어나 집으로 들어가니 소년이 그 머리에 기름을 부으며 이르되 `이스라엘 하나님 여호와의 말씀이 내가 네게 기름을 부어 여호와의 백성 곧 이스라엘의 왕을 삼노니
Basi Yehu akainuka na kwenda kwenye nyumba, na yule nabii akammiminia mafuta kwenye kichwa chake na kumwambia Yehu, “Yahwe, Mungu wa Israeli, anasema hivi: 'Nimekumiminia mafuta uwe mfalme juu ya watu wa Yahwe, juu ya Isaraeli.
7 너는 네 주 아합의 집을 치라 내가 나의 종 곧 선지자들의 피와 여호와의 종들의 피를 이세벨에게 갚아주리라
Wewe lazima uiue familia ya Ahabu bwana wako, ili niweze kulipiza kisasi cha damu ya watumishi wangu manabii, na damu ya watumishi wote wa Yahwe, ambao waliokuwa wameuawa kwa mkono wa Yezebeli.
8 아합의 온 집이 멸망하리니 이스라엘 중에 매인 자나 놓인 자나 아합에게 속한 모든 남자는 내가 다 멸절하되
Kwa kuwa nyumba yote ya Ahabu itaangamia, na nitamkatilia mbali kila mtoto wa kiume wa Ahabu, yeyote awe mtumwa au mtu huru.
9 아합의 집을 느밧의 아들 여로보암의 집과 같게 하며 또 아히야의 아들 바아사의 집과 같게 할지라
Nitaifanya nyumba ya Ahabu kama nyumba ya Yerobohamu mwana wa Nebati na kama nyumba ya Baasha mwana wa Ahiya.
10 이스르엘 지방에서 개들이 이세벨을 먹으리니 저를 장사할 사람이 없으리라 하셨느니라' 하고 곧 문을 열고 도망하니라
Mbwa watamla Yezebeli katika Yezreeli, na hakutakuwa na mtu wa kumzika.” Kisha nabii akafungua mlango na kukimbia.
11 예후가 나와서 그 주의 신복들에게 이르니 한 사람이 묻되 평안이뇨 그 미친 자가 무슨 까닭으로 그대에게 왔더뇨 대답하되 그대들이 그 사람과 그 말한 것을 알리라
Kisha Yehu akatoka kwenda kwa watumishi wa bwana wake, na mmoja akamwambia, “Je kila kitu kiko sawa? Kwa nini huyu mwenda wazimu amekuja kwako?” Yehu akawajibu, “Mnamjua huyo mtu na mambo asemayo.”
12 무리가 가로되 당치 않은 말이라 그대는 우리에게 이르라 대답하되 저가 이리 이리 내게 말하여 이르기를 여호와의 말씀이 내가 네게 기름을 부어 이스라엘 왕을 삼는다 하셨다 하더라
Wakasema, “Huo ni uongo. Tuambie.” Yehu akajibu, “Alisema hivi na vile juu yangu, na pia akasema, 'hivi ndivyo Yahwe asemavyo: Nimekumiminia mafuta kama mfalme juu ya Israeli.””
13 무리가 각각 자기의 옷을 급히 취하여 섬돌 위 곧 예후의 밑에 깔고 나팔을 불며 가로되 예후는 왕이라 하니라
Kisha kila mmoja wao akachukua vazi haraka na kuweka chini ya Yehu juu ya madaraja. Wakapiga baragumu na kusema, “Yehu ni mfalme.”
14 이에 님시의 손자 여호사밧의 아들 예후가 요람을 배반하였으니 곧 요람이 온 이스라엘로 더불어 아람 왕 하사엘을 인하여 길르앗 라못을 지키다가
Katika njia hii Yehu mwana wa Yehoshafati mwana wa Nimshi akafanya njama juu ya Yoramu. Basi Yoramu alikuwa akiilinda Ramothi Gileadi, yeye na Israeli yote, kwa sababu ya Hazaeli mfalme wa Shamu,
15 아람 왕 하사엘로 더불어 싸울 때에 아람 사람에게 상한 것을 치료하려 하여 이스르엘로 돌아왔던 때라 예후가 이르되 너희 뜻에 합당하거든 한 사람이라도 이 성에서 도망하여 이스르엘에 전하러 가지 못하게 하라 하니라
lakini mfalme Yoramu alikuwa amesharudi kwa Yezreeli ili kuponywa yale majeraha aliyokuwa ameyapewa na Washami, wakati akiwa anapigana dhidi ya Hazaeli mfalme wa Shamu. Yehu akawaambia watumishi wa Yoramu, “kama hili ndilo wazo lako, kisha usimwache mtu aondoke na kwenda nje ya mji, ili aende kupeleka habari hii Yezreeli.”
16 예후가 병거를 타고 이스르엘로 가니 요람이 거기 누웠음이라 유다왕 아하시야는 요람을 보러 내려 왔더라
Basi Yehu akaendesha gari la farasi mpaka Yezreeli; kwa kuwa Yoramu alikuwa amelala huko. Basi Ahazi mfalme wa Yuda alikuwa ameshuka chini kuonana na Yoramu.
17 이스르엘 망대에 파숫군 하나가 섰더니 예후의 무리의 오는 것을보고 가로되 내가 한 무리를 보나이다 요람이 가로되 한 사람을 말을 태워 보내어 맞아 평안이냐 묻게 하라
Mlinzi alikuwa amesimama juu ya mnara katika Yezreeli, akaliona lile kundi la Yehu alipokuwa akija kwa mbali kidogo; akasema, “Naona kundi la watu wanakuja.” Yoramu akasema, “Chukua mwendesha farasi, na umtume akakutane nao; mwambie aseme, “Je mnakuja kwa amani?””
18 한 사람이 말을 타고 가서 만나 가로되 왕의 말씀이 평안이냐 하시더이다 하매 예후가 가로되 평안이 네게 상관이 있느냐 내 뒤로 돌이키라 하니라 파숫군이 고하여 가로되 사자가 저희에게 갔으나 돌아오지 아니하나이다 하는지라
Hivyo mwendesha farasi akatoka kumlaki; akasema, “Mfalme asema hivi: Je mnakuja kwa amani?”' Basi Yehu akasema, “Wewe una nini na amani? Geuka na unifuate nyuma.” Kisha yule mlinzi akamwambia mfalme, Yule mjumbe ameshaonana nao, lakini anarudi.”
19 다시 한 사람을 말을 태워 보내었더니 저희에게 가서 가로되 왕의 말씀이 평안이냐 하시더이다 하매 예후가 가로되 평안이 네게 상관이 있느냐 내 뒤로 돌이키라 하니라
Kisha akapeleka mpanda farasi wa pili, ambaye alikuja kwao na kusema, “Mfalme asema hivi: 'Je mnakuja na amani?”' Yehu akajibu, “Wewe una nini na amani? Geuka na kunifuata nyuma.
20 파숫군이 또 고하여 가로되 저도 저희에게까지 갔으나 돌아오지 아니하고 그 병거 모는 것이 님시의 손자 예후의 모는 것 같이 미치게 모나이다
Tena yule mlinzi akatoa taarifa, “Amekwisha kuonana nao, lakini hatorudi. Kwa kuwa hilo gari la farasi limekuwa likiendeshwa ndivyo ambavyo Yehu mwana wa Nimshi aendeshavyo; anaendesha kwa kasi.”
21 요람이 가로되 메우라 하매 그 병거를 메운지라 이스라엘 왕 요람과 유다 왕 아하시야가 각각 그 병거를 타고 가서 예후를 맞을새 이스르엘 사람 나봇의 토지에서 만나매
Hivyo Yoramu akasema, “Andaa gari langu la farasi liwe tayari.” Wakaandaa gari lake la farasi, na Yoramu mfalme wa Israeli na Ahazi mfalme wa Yuda akaendesha, kila mmoja kwenye gari lake la farasi, kumlaki Yehu. Wakamkuta kwenye mali ya Nabothi Myezreeli.
22 요람이 예후를 보고 가로되 예후야 평안이냐 대답하되 네 어미 이세벨의 음행과 술수가 이렇게 많으니 어찌 평안이 있으랴
Wakati Yoramu alipomuona Yehu, alisema, “Je unakuja katika hali ya amani, Yehu?” Akajibu, “Amani gani hapo, wakati uzinzi wa ukahaba hufanywa na uchawi wa mama yako Yezebeli umejaa tele?”
23 요람이 곧 손을 돌이켜 도망하며 아하시야에게 이르되 아하시야여 반역이로다
Basi Yoramu akarudisha magari yake ya farasi na kukimbia na kumwambia Ahazia, “Kuna udanganyifu, Ahazia.
24 예후가 힘을 다하여 활을 당기어 요람의 두 팔 사이를 쏘니 살이 그 염통을 꿰뚫고 나오매 저가 병거 가운데 엎드러진지라
Ndipo Yehu akauvuta upinde wake kwa nguvu zake zote na kumpiga Yoramu kati ya mabega yake; mshale ukaenda kwenye moyo wake, akaanguka chini kwenye gari lake la farasi.
25 예후가 그 장관 빗갈에게 이르되 그 시체를 취하여 이스르엘 사람 나봇의 밭에 던지라 네가 기억하려니와 이전에 너와 내가 함께 타고 그 아비 아합을 좇았을 때에 여호와께서 이 아래 같이 저의 일을 예언하셨느니라
Ndipo Yehu akamwambia Bidkari nahodha wake, “Mchukue na mtupie kwenye shamba la Nabothi Myezreeni. Fikiria kuhusu vile ambavyo wewe na mimi tulivyoendesha pamoja baada ya Ahabu baba yake, Yahwe aliuweka juu unabii dhidi yake:
26 여호와께서 말씀하시기를 내가 어젯날에 나봇의 피와 그 아들들의 피를 분명히 보았노라 또 말씀하시기를 이 토지에서 네게 갚으리라 하셨으니 그런즉 여호와의 말씀대로 그 시체를 취하여 이 밭에 던질지니라
Jana niliona damu ya Nabothi na damu ya watoto wake - asema Yahwe - na nitahakikisha unalipia hili shamba - asema Yahwe. Sasa basi, mchukue na mtupe kwenye hili shamba, sawa sawa na neno la Yahwe.”
27 유다 왕 아하시야가 이를 보고 동산 정자 길로 도망하니 예후가 쫓아가며 이르되 저도 병거 가운데서 죽이라 하매 이블르암 가까운 구르 비탈에서 치니 저가 므깃도까지 도망하여 거기서 죽은지라
Wakati Ahazi yule mfalme wa Yuda alipoliona hili, akakimbia kwa njia ya Bethi Hagani. Lakini Yehu akamfuata, na kusema, “Muulie humo kwenye gari la farasi,” na wakampiga mahali pa kupandia Guri, karibu na Ebleamu. Ahazi akakimbilia Megido na kufia pale.
28 그 신복들이 저를 병거에 싣고 예루살렘에 이르러 다윗성에서 그 열조와 함께 그 묘실에 장사하니라
Watumishi wake wakaubeba mwili wake kwa magari ya farasi kwenda Yerusalemu na kumzika kwenye kaburi lake pamoja na baba zake katika mji wa Daudi.
29 아합의 아들 요람의 십 일년에 아하시야가 유다 왕이 되었었더라
Basi ilikuwa mwaka wa kumi na moja wa Yoramu mwana wa Ahabu huyo Ahazia akaanza kutawala juu ya Yuda.
30 예후가 이스르엘에 이르니 이세벨이 듣고 눈을 그리고 머리를 꾸미고 창에서 바라보다가
Wakati Yahu alipokuja kwa Yezebeli, Yezebeli akasikia juu ya hilo, akapaka wanja kwenye macho yake, akatengeneza nywele zake vizuri, na kuchungulia kwenye dirisha.
31 예후가 문에 들어오매 가로되 주인을 죽인 너 시므리여 평안하냐
Kadiri Yehu alipokuwa akiingia kwenye lango, akamwambia, “Je unakuja kwa amani, wewe Zimri, muuaji wa bwana wako?”
32 예후가 얼굴을 들어 창을 향하고 가로되 내 편이 될 자가 누구냐 누구냐 하니 두어 내시가 예후를 내다보는지라
Yehu akatazama juu ya dirisha na kusema, “Ni nani yuko upande wangu? Nani?” Matowashi wawili au watatu wakachungulia nje.
33 가로되 저를 내려던지라 하니 내려던지매 그 피가 담과 말에게 뛰더라 예후가 그 시체를 밟으니라
Basi Yehu aksema, “Mtupeni chini.” Hivyo wakamtupa Yezebeli chini, na damu yake nyingine ikamwagika kwenye ukuta na farasi, na Yehu akamkanyaga kanyaga chini ya miguu.
34 예후가 들어가서 먹고 마시고 가로되 가서 이 저주 받은 계집을 찾아 장사하라 저는 왕의 딸이니라 하매
Basi Yehu akaingia hiyo sehemu, akala na kunywa. Kisha akasema, “Mtazamani sasa huyu mwanamke aliyelaaniwa na kumzika, kwa kuwa ni binti wa mfalme.”
35 가서 장사하려 한즉 그 두골과 발과 손바닥 외에는 찾지 못한지라
Wakaenda kumzika, lakini hawakumkuta ila fuvu, miguu, na viganga vya mikono yake.
36 돌아와서 고한대 예후가 가로되 이는 여호와께서 그 종 디셉 사람 엘리야로 말씀하신바라 이르시기를 이스르엘 토지에서 개들이 이세벨의 고기를 먹을지라
Basi wakarudi na kumwambia Yehu. Akasema, “Hili ndilo neno la Yahwe ambalo ameliongea kupitia Eliya Mtishbi, likisema, 'Katika nchi Yezreeli mbwa ataula mwili wa Yezebeli,
37 그 시체가 이스르엘 토지에서 거름 같이 밭 면에 있으리니 이것이 이세벨이라고 가리켜 말하지 못하게 되리라 하셨느니라
na mwili wa Yezebeli utakuwa kama kinyesi juu ya uso wa mashamba katika nchi ya Yezreeli, kwa hiyo basi hakuna atakayeweza kusema, “Huyu ni Yezebeli.””

< 열왕기하 9 >