< Yohana 15 >
1 Une nele usabibu ugwa lweli nu dada vango indemaji vaa usanbibu.
Mimi ni mzabibu wa huu kweli, na baba yangu ni mkulima wa mzabibu.
2 Hela ulusiamba lulegati ndiune ulusafi siwa hela usiamba ulusalu hola isehe ihuluhecha ili lupate uhuhola sana.
Kila tawi ndani yangu ambalo halizai tunda, na husafisha kila tawi ambalo huzaa tunda huliondoa ili kwamba liweze kuzaa zaidi.
3 Umwe lenu mvile vanonu msababu mvile vasuhwa uhuva nevile nevavulile.
Ninyi tayari mmekuwa safi kwa sababu ya ujumbe ambao nimekwisha waambia.
4 Mtame mgati ndione nayune netame gati ndiumwe kama ulusiambalulwa saluwesia uhu hola luene isio uhuva usanbibu nayumwe mnasitu uhutama igati ndiune.
Mkae ndani yangu, na mimi ndani yenu. Kama tawi lisivyoweza kuzaa peke yake lisipo kuwa katika mzabibu, kadhalika nayi, msipo kaa ndani yangu.
5 Une nele usanbibu umwe mlelusamba uveidumu mgati ndiumwe umnu uyu ihola isehe nyingi uhuva pasipo une samhaweze uhuvomba imbombo yuyoni.
Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi. Adumuye ndani yangu na mimi ndani yake, mtu huyu huzaa matunda mengi, kwa kuwa pasipo mimi hamuwezi kufanya jambo lolote.
6 Inave umnu yuyoni sivemo gati ndiune itagiwa kama ulusiamba nuhuuma avanu yavi kusanya amasamba nuhutaga humoto, nuhutehetela.
Ikiwa mtu yeyote hatasalia ndani yangu, atatupwa kama tawi na kukauka; watu hukusanya matawi na kuyatupa katika moto, na kuteketea.
7 Mnave mtama gati ndiune na kama amamenyu ya gitama gati ndiune dova lelioni ilimwinogwa numwe mvombeliwa.
Ikiwa mtadumu ndani yangu, na kama maneno yangu yakidumu ndani yenu, ombeni lolote mtakalo, nanyi mtafanyiwa.
8 Huele udada vango ihwinuliwa yamwi hola isehe nyini nuhuva vasiule vango.
Katika hili baba yangu ametukuzwa, kwamba mnazaa matunda mengi na kwamba ni wanafunzi wangu.
9 Kama udada vango umwa nganile une nayune nevaganile umwe; mdamage mlugano lwango.
Kama baba yangu alivyonipenda mimi, mimi pia nimewapenda ninyi; dumuni katika pendo langu.
10 Mnave mhwibata indagele chango mtama mlugano lwango kama umni batile indagelo icha dada yangu nuhutama mvugane wamwene.
Ikiwa mtashika amri zangu, mtadumu katika pendo langu kama nilivyo shika amri za baba yangu na kudumu katika pendo lake.
11 Nenchovile aga hulemwe ili uh hovuha hwenyo huve gati ndiune ili uhuhovona hwenyo hevombehe ehele kamilifu.
Nimesema mambo haya kwenu ili kwamba furaha yangu iwe ndani yenu na ili kwamba furaha yenu ifanyike kuwa timilifu.
12 Ulu lulu lagelo lwango uhuta mganane yumwe hwa yumwe kama umone vaganilune.
Hii ndiyo amri yangu, kwamba mpendane ninyi kwa ninyi kama nilivyo wapenda ninyi.
13 Hakuna umnu uvale nulugano ulu vaha hulihune ehumiee uvutamo uwa mwene hwa ajili ya lafiki avanine.
Hakuna mtu aliye na upendo mkuu kuliko huu, kwamba ayatoe maisha yake kwa ajiliya rafiki zake.
14 Umwe mlelafiki vango mnave mvomba aganihuvasuha.
Ninyi ni rafiki zangu ikiwa mtafanya yale niwaagizayo.
15 Sanihuve langa kama vatesiwa uhuva utesiwa sihwelewa hehuva utesiwa sihwelewa hehwo ivomba umbaha vamwene nevelangile kama malafiki uhuva nevavulile amambo goni aga uhuhuma hwa Dada.
Siwaiti watumwa, kwa kuwa mtumwa hajui kile afanyacho bwana wake. Nimewaita ninyi marafiki, kwa sababu nimewajulisheni mambo yote ambayo nimesikia kutoka kwa Baba.
16 Samwa njagule une bali une navachagiile umwe nuhwasuha mlute isehe nisehe chenyo chipate uhuhola isehe nesehe chenyo chipate uhu tama hela ehe mwinogwa uhudova hwa Dada mdove hulitawa ilengo ihuvapa.
Hamkunichagua mimi, bali mimi niliwachagua ninyi na kuwaweka mwende mazae matunda, na tunda lenu lipate kukaa. Hii liko hivi ili kwamba chochote muombacho kwa Baba kwa jina langu, atawapeni.
17 Amambo aga nihuvasuha hela mnu agana nage na vanine.
Mambo haya ninawaagiza, kwamba mpendane kila mtu na mwenzake.
18 Kama ehelunga hihuvakala lela welewe uhuta umwe mngalalile une kabula saheva kalalile umwe.
Kama ulimwengu utawachukia, mjuwe kwamba ulinichukia mimi kabla haujawachukia ninyi.
19 Inave mwale va helonga ehelunga hehale hihuvagana umwe leno uhusa sio mlevahelunga uhuva nava chagile uhuhuma mhe lunga ndi ehelunga hihuva kalalela.
Kama mngekuwa wa ulimwengu, ulimwengu ungewapenda kama wa kwao; Lakini kwa sababau ninyi sio wa ulimwengu na kwa sababu niliwachagua kutoka katika ulimwengu, ni kwa ajili hii ulimwengu huwachukia.
20 Kumbuha elimenyu elenavavulile uviteseha siwesia uhwa mbaha va mwene uhuva vanesiche une vihuvatesi nayumwe kama mwaibite amamenyu gango vahale vihwibata naga genyo.
Kumbukeni neno ambalo niliwaambia, 'Mtumwa si mkuu kuliko bwana wake.' Ikiwa walinitesa mimi, watawateseni ninyi pia; Kama walishika neno langu, wangelishika la kwenu pia.
21 Vavombiee amambo goni hulitawa iliango uhuva samhwelewa uveasuhile.
Watawatendeeni mambo haya yote kwa ajili ya jina langu kwa sababu hawamjui yule aliyenituma.
22 Kama nenga site uhwicha uhuva vula ndaleno, savavombile uvutulanongwa; lakini usehe ugu savahabeche uvutula nogwa wavene.
Kama nisingekuja na kuwaambia waambia, wasingalikuwa wamefanya dhambi; lakini sasa hawana udhuru kwa dhambi yao.
23 Uviihung'alalela une ihukala lela Udada pia.
Anichukiaye mimi humchukia Baba pia.
24 Nenave sanevombile embombo mvene ambapo asipali yumo uveavombile vahale viva nu vutula nongwa ule leno va vombile goni gavele vambwene nuhung'alalelaune nu Dada vango.
Ikiwa sijafanya kazi miongoni mwao ambayo hapana mmoja aliyeifanya, wangelikuwa hawana dhambi; lakini sasa wamefanya yote mawili wameona na wamenichukia mimi na Baba yangu.
25 Ele lihumla ili elimenyu letimela lelwo lesimbiwe hululagelo luavo: 'Vihungalalela une bila sababu.'
Hili linatokea ili kwamba neno litimie ambalo limeandikwa katika sheria yao: 'Wananichukia mimi bila sababu.'
26 Wakati ubembelesaji ichile uvepile nihusuha hulimwe uhuhuma hwa Dada, uyu vemepo uvalweli uvihuma hwa Dada ihusuhudela.
Wakati mfariji amekuja, ambaye nitamtuma kwenu kutoka kwa Baba, huyu ndiye, Roho wa kweli, ambaye anatokea kwa Baba, atanishuhudia.
27 Umwe pia mhusuhudela uhuva mvile pamoja nune tangu huvutengulilo.
Ninyi pia mnanishuhudia kwa sababu mmekuwa pamoja nami tangu mwanzo.