< ゼカリヤ書 8 >
Neno la Yahwe wa majeshi likanijia kusema,
2 萬軍のヱホバかく言たまふ我シオンのために甚だしく心を熱して妬く思ひ大なる忿怒を起して之がために妬く思ふ
“Yahwe wa majeshi asema hivi: Nina huzuni kwa ajili ya Sayuni kwa wivu mkuu na ninamaumivu kwa hasira nyingi!
3 ヱホバかく言たまふ今我シオンに歸れり我ヱルサレムの中に住んヱルサレムは誠實ある邑と稱へられ萬軍のヱホバの山は聖山と稱へらるべし
Yahwe wa majeshi asema hivi: Nitairudia Sayuni nami nitakaa kati ya Yerusalemu, kwa kuwa Yerusalemu itaitwa mji wa kweli na mlima wa Yahwe wa majeshi utaitwa Mlima Mtakatifu!
4 萬軍のヱホバかく言たまふヱルサレムの街衢には再び老たる男 老たる女坐せん皆年高くして各々杖を手に持べし
Yahwe wa majeshi asema hivi: Kwa mara nyingine tena kutakuwa na vikongwe katika mitaa ya Yerusalemu, na kila mtu ataitaji mkongojo mkononi mwake kwa vile alivyo mzee.
5 またその邑の街衢には男の兒 女の兒滿て街衢に遊び戯れん
Pia mitaa ya mji itajazwa na vijana wa kiume na kike wachezao.
6 萬軍のヱホバかく言たまふこの事其日には此民の遺餘者の目に奇といふとも我目に何の奇きこと有んや萬軍のヱホバこれを言ふ
Yahwe wa majeshi asema hivi: ikiwa jambo laonekana haliwezekani katika macho ya masalia ya watu hawa katika siku hizo, je haliwezekani pia machoni pangu? - asema Yahwe.
7 萬軍のヱホバかく言たまふ視よ我わが民を日の出る國より日の入る國より救ひ出し
Yahwe wa majeshi asema hivi: Tazama, nipo tayari kuwaokoa watu wangu kutoka nchi ya mawio na ya machweo ya jua!
8 かれらを携へ來りてヱルサレムの中に住しめん彼らは我民となり我は彼らの神となりて共に誠實と正義に居ん
Kwa maana nitawarudisha tena, nao wataishi ndani ya Yerusalemu, hivyo watakuwa watu wangu tena, nami nitakuwa Mungu wao katika kweli na utakatifu!
9 萬軍のヱホバかく言たまふ汝ら萬軍のヱホバの室なる殿を建んとて其基礎を置たる日に起りし預言者等の口の言詞を今日聞く者よ汝らの腕を強くせよ
Yahwe wa majeshi asema hivi: Ninyi mnaoendelea kusikia maneno yaleyale yaliyotoka katika vinywa vya manabii msingi wa nyumba yangu ulipowekwa - hii nyumba yangu, Yahwe wa majeshi: Itieni nguvu mikono yenu ili hekalu lijengwe.
10 此日の先には人も工の價を得ず獸畜も工の價を得ず出者も入者も仇の故をもて安然ならざりき即ち我人々をして互に相攻しめたり
Kwani kabla ya siku hizo hakuna mazao yaliyokusanywa na yeyote ndani yake, hakukuwa na faida siyo kwa mtu hata mnyama, na hakukuwa na amani kutoka kwa adui kwa kila aliyekwenda au kuja. Nilimfanya kila mtu kuwa kinyume cha mwenzake.
11 然れども今は我此民の遺餘者に對すること曩の日のごとくならずと萬軍のヱホバ言たまふ
Lakini sasa haitakuwa kama mwanzo, nitakuwa pamoja na masalia ya watu hawa - asema Yahwe wa majeshi.
12 即ち平安の種子あるべし葡萄の樹は果を結び地は産物を出し天は露を與へん我この民の遺餘者にこれを盡く獲さすべし
Kwani mbegu za amani zitapandwa; mzabibu unaokua utatoa matunda yake na nchi itatoa mazao yake; anga zitatoa umande, kwa maana nitawapa masalia ya watu hawa kumilki haya yote.
13 ユダの家およびイスラエルの家よ汝らが國々の中に呪詛となりしごとく此度は我なんぢらを救ふて祝言とならしめん懼るる勿れ汝らの腕を強くせよ
Ulikuwa mfano wa laana kwa mataifa mengine, enyi nyumba ya Yuda na nyumba ya Israeli. Hivyo nitawaokoa nanyi mtakuwa baraka. Msiogope; haya mikono yenu itiwe nguvu!
14 萬軍のヱホバかく言たまふ在昔汝らの先祖我を怒らせし時に我これに災禍を降さんと思ひて之を悔ざりき萬軍のヱホバこれを言ふ
Kwa maana Yahwe wa majeshi asema hivi: Kama nilivyopanga kuwatenda mabaya babu zenu walipochokoza hasira yangu - asema Yahwe wa majeshi - na wala sikujuta,
15 是のごとく我また今日ヱルサレムとユダの家に福祉を降さんと思ふ汝ら懼るる勿れ
ndivyo nitakavyoazimia kuutenda mema tena Yerusalemu na nyumba ya Yuda katika siku hizi! Msiogope!
16 汝らの爲べき事は是なり汝ら各たがひに眞實を言べし又汝等の門にて審判する時は眞實を執て平和の審判を爲べし
Haya ndiyo mambo mnayopaswa kufanya: Kasemeni kweli, kila mtu na jirani yake. Hukumuni kwa haki, usawa na amani katika malango yenu.
17 汝等すべて人の災害を心に圖る勿れ僞の誓を好む勿れ是等はみな我が惡む者なりとヱホバ言たまふ
Na asiwepo miongoni mwenu anayeazimu uovu moyoni mwake dhidi ya jirani yake, wala kuvutwa na viapo vya uongo; kwani haya yote ndiyo mambo ninayoyachukia! - asema Yahwe.”
Kisha neno la Yahwe wa majeshi likanijia kusema,
19 萬軍のヱホバかく言たまふ四月の斷食五月の斷食七月の斷食十月の斷食かへつてユダの家の宴樂となり欣喜となり佳節となるべし惟なんぢら眞實と平和を愛すべし
“Yahwe wa majeshi asema hivi: Mifungo ya mwezi wa nne, mwezi wa tano, mwezi wa saba na mwezi wa kumi itakuwa nyakati za furaha ya kila aina, kwa nyumba ya Yuda! Kwa hiyo pendeni kweli na amani!
20 萬軍のヱホバかく言たまふ國々の民および衆多の邑の居民來り就ん
Yahwe wa majeshi asema hivi: Watu watakuja tena, hata wanaoishi miji mingine.
21 即ちこの邑の居民往てかの邑の者に向ひ我儕すみやかに往てヱホバを和め萬軍のヱホバを求めんと言んに我も往べしと答へん
Watu wa mji mmoja watakwenda mji mwingine na kusema, “Haya twendeni haraka mbele ya Yahwe tukaombe na kumtafuta Yahwe wa majeshi! Sisi wenyewe tunakwenda pia.
22 衆多の民強き國民ヱルサレムに來りて萬軍のヱホバを求めヱホバを和めん
Watu wengi na mataifa yenye nguvu yatakuja kumtafuta Yahwe wa majeshi huko Yerusalemu na kuomba upendeleo kwa Yahwe!
23 萬軍のヱホバかく言たまふ其日には諸の國語の民十人にてユダヤ人一箇の裾を拉へん即ち之を拉へて言ん我ら汝らと與に往べし其は我ら神の汝らと偕にいますを聞たればなり
Yahwe wa majeshi asema hivi: Katika siku hizo watu kumi kutoka katika kila lugha na taifa watashika upindo wa kanzu zenu na kusema, “Haya sisi nasi tutakwenda pamoja nanyi, kwani tumesikia kwamba Mungu yu pamoja nayi!”