< 創世記 12 >
1 爰にヱホバ、アブラムに言たまひけるは汝の國を出で汝の親族に別れ汝の父の家を離れて我が汝に示さん其地に至れ
Kisha Yahwe akamwambia Abram, “Nenda utoke katika nchi yako, na toka kwa ndugu zako, na kwa jamaa za baba yako, uende katika nchi nitakayo kuonesha.
2 我汝を大なる國民と成し汝を祝み汝の名を大ならしめん汝は祉福の基となるべし
Nitakufanya uwe taifa kubwa, na nitakubariki na kulifanya jinalako kuwa kubwa, na utafanyika baraka.
3 我は汝を祝する者を祝し汝を詛ふ者を詛はん天下の諸の宗族汝によりて福禔を獲と
Nitawabariki wakubarikio, lakini asiye kuheshimu nita mlaani. Kupitia kwako familia zote za nchi zitabarikiwa.
4 アブラム乃ちヱホバの自己に言たまひし言に從て出たりロト彼と共に行りアブラムはハランを出たる時七十五歳なりき
Kwa hiyo Abram akaondoka kama vile Yahwe alivyo mwambia kufanya, na Lutu akaenda pamoja naye. Abram alikuwa na miaka sabini na mitano wakati alipotoka Harani.
5 アブラム其妻サライと其弟の子ロトおよび其集めたる總の所有とハランにて獲たる人衆を携へてカナンの地に往んとて出で遂にカナンの地に至れり
Abram akamchukua Sarai mkewe, Lutu, mtoto wa ndugu yake, na vyote walivyomiliki ambavyo wamevikusanya, na watu ambao wamewapata wakiwa huko Harani. Wakatoka kwenda katika nchi ya Kanaani, wakafika nchi ya Kanaani.
6 アブラム其地を經過てシケムの處に及びモレの橡樹に至れり其時にカナン人其地に住り
Abram akapitia katikati ya nchi hadi Shekemu, hadi mwaloni wa More. Wakati huo wakanaani waliishi katika nchi hiyo.
7 茲にヱホバ、アブラムに顯現れて我汝の苗裔に此地に與へんといひたまへり彼處にて彼己に顯現れたまひしヱホバに壇を築けり
Yahwe akamtokea Abram, na kusema, “Nitawapa uzao wako nchi hii.” Kwa hiyo Abram akamjengea madhabahu, Yahwe ambaye alimtokea.
8 彼其處よりベテルの東の山に移りて其天幕を張り西にベテル東にアイありき彼處にて彼ヱホバに壇を築きヱホバの名を龥り
Kutoka pale akaenda kwenye nchi ya mlima mashariki mwa Betheli, ambapo alipiga hema yake, magaribi kukiwa na Betheli na mashariki kukiwa na mji wa Ai. Akajenga madhabahu ya Yahwe pale na kuliitia jina la Yahwe.
Kisha Abram akaendelea kusafiri, akielekea upande wa Negebu.
10 茲に饑饉其地にありければアブラム、エジプトに寄寓らんとて彼處に下れり其は饑饉其地に甚しかりければなり
Kulikuwa na njaa katika nchi, kwa hiyo Abram akaenda kukaa Misri, kwa kuwa njaa ilikua kali katika nchi.
11 彼近く來りてエジプトに入んとする時其妻サライに言けるは視よ我汝を觀て美麗き婦人なるを知る
Wakati alipokaribia kuingia Misri, akamwambia Sarai mkewe, “tazama, najua kuwa wewe ni mwanamke mzuri.
12 是故にエジプト人汝を見る時是は彼の妻なりと言て我を殺さん然ど汝をば生存かん
Wamisri watakapokuona watasema, huyu ni mke wake, na wataniua mimi, lakini watakuacha wewe hai.
13 請ふ汝わが妹なりと言へ然ば我汝の故によりて安にしてわが命汝のために生存ん
Hivyo wewe sema kuwa ni dada yangu, ili kwamba niwe salama kwa sababu yako, na kumba maisha yangu yatasalimika kwa sababu yako.”
14 アブラム、エジプトに至りし時エジプト人此婦を見て甚だ美麗となせり
Ikawa kwamba Abram alipoingia Misri, Wamisri wakaona kwamba Sarai ni mzuri sana.
15 またパロの大臣等彼を視て彼をパロの前に譽めければ婦遂にパロの家に召入れられたり
Wakuu wa Farao wakamuona, na kumsifia kwa Farao, na huyu mwanamke akachukuliwa kupelekwa nyumbani mwa Farao.
16 是に於てパロ彼のために厚くアブラムを待ひてアブラム遂に羊牛僕婢牝牡の驢馬および駱駝を多く獲るに至れり
Farao akamtendea kwa wema Abram kwa ajili yake, na akampatia kondoo, maksai, punda waume watumishi wa kiume, watumishi wa kike, punda wake, na ngamia.
17 時にヱホバ、アブラムの妻サライの故によりて大なる災を以てパロと其家を惱したまへり
Kisha Yahwe akampiga Farao na nyumba yake kwa mapigo makuu kwa sababau ya Sarai, mke wa Abram.
18 パロ、アブラムを召て言けるは汝が我になしたる此事は何ぞや汝何故に彼が汝の妻なるを我に告ざりしや
Farao akamwita Abram na kusema, “Nini hiki ambacho umenifanyia? Kwa nini hukuniambia kuwa alikuwa mke wako?
19 汝何故に彼はわが妹なりといひしや我幾彼をわが妻にめとらんとせり然ば汝の妻は此にあり挈去るべしと
Kwa nini ulisema, 'ni dada yangu; na mimi nikamchukua kuwa mke wangu? Sasa kwa sababu hiyo huyu hapa mke wako. Mchukue na uende zako.”
20 パロ即ち彼の事を人々に命じければ彼と其妻および其有る諸の物を送りさらしめたり
Kisha Farao akatoa amri kwa watu wake kuhusiana naye, na wakamuondoa, yeye pamoja na mke wake na vyote alivyokuwa navyo.