< 詩篇 135 >

1 なんぢらヱホバを讃稱へよ ヱホバの名をほめたたへよ ヱホバの僕等ほめたたへよ
Msifuni Bwana. Lisifuni jina la Bwana, msifuni, enyi watumishi wa Bwana,
2 ヱホバの家われらの神のいへの大庭にたつものよ讃稱へよ
ninyi ambao mnatumika ndani ya nyumba ya Bwana, katika nyua za nyumba ya Mungu wetu.
3 ヱホバは恵ふかし なんぢらヱホバをほめたたへよ その聖名はうるはし讃うたへ
Msifuni Bwana, kwa kuwa Bwana ni mwema, liimbieni sifa jina lake, kwa maana hilo lapendeza.
4 そはヤハおのがためにヤコブをえらみイスラエルをえらみてその珍寳となしたまへり
Kwa maana Bwana amemchagua Yakobo kuwa wake mwenyewe, Israeli kuwa mali yake ya thamani.
5 われヱホバの大なるとわれらの主のもろもろの神にまされるとをしれり
Ninajua ya kuwa Bwana ni mkuu, kwamba Bwana wetu ni mkuu kuliko miungu yote.
6 ヱホバその聖旨にかなふことを天にも地にも海にも淵にもみなことごとく行ひ給ふなり
Bwana hufanya lolote apendalo, mbinguni na duniani, katika bahari na vilindi vyake vyote.
7 ヱホバは地のはてより霧をのぼらせ 雨のために電光をつくりその庫より風をいだしたまふ
Hufanya mawingu kupanda kutoka miisho ya dunia; hupeleka umeme wa radi pamoja na mvua na huleta upepo kutoka ghala zake.
8 ヱホバは人より畜類にいたるまでエジプトの首出をうちたまへり
Alimuua mzaliwa wa kwanza wa Misri, mzaliwa wa kwanza wa wanadamu na wanyama.
9 エジプトよヱホバはなんぢの中にしるしと奇しき事跡とをおくりて パロとその僕とに臨ませ給へり
Alipeleka ishara zake na maajabu katikati yako, ee Misri, dhidi ya Farao na watumishi wake wote.
10 ヱホバはおほくの國々をうち 又いきほひある王等をころし給へり
Aliyapiga mataifa mengi, na akaua wafalme wenye nguvu:
11 アモリ人のわうシホン、バシヤンの王オグならびにカナンの國々なり
Mfalme Sihoni na Waamori, Ogu mfalme wa Bashani na wafalme wote wa Kanaani:
12 かれらの地をゆづりとしその民イスフルの嗣業としてあたへ給へり
akatoa nchi yao kuwa urithi, urithi kwa watu wake Israeli.
13 ヱホバよなんぢの名はとこしへに絶ることなし ヱホバよなんぢの記念はよろづ世におよばん
Ee Bwana, jina lako ladumu milele, kumbukumbu za fahari zako, Ee Bwana, kwa vizazi vyote.
14 ヱホバはその民のために審判をなしその僕等にかかはれる聖意をかへたまふ可ればなり
Maana Bwana atawathibitisha watu wake, na kuwahurumia watumishi wake.
15 もろもろのくにの偶像はしろかねと金にして人の手のわざなり
Sanamu za mataifa ni fedha na dhahabu, zilizotengenezwa kwa mikono ya wanadamu.
16 そのぐうざうは口あれどいはず目あれど見ず
Zina vinywa, lakini haziwezi kusema, zina macho, lakini haziwezi kuona;
17 耳あれどきかず またその口に氣息あることなし
zina masikio, lakini haziwezi kusikia, wala hakuna pumzi katika vinywa vyao.
18 これを造るものと之によりたのむものとは皆これにひとしからん
Wale wanaozitengeneza watafanana nazo, vivyo hivyo wale wote wanaozitumainia.
19 イスラエルの家よヱホバをほめまつれ アロンのいへよヱホバをほめまつれ
Ee nyumba ya Israeli, msifuni Bwana; ee nyumba ya Aroni, msifuni Bwana;
20 レビの家よヱホバをほめまつれ ヱホバを畏るるものよヱホバをはめまつれ
ee nyumba ya Lawi, msifuni Bwana; ninyi mnaomcha, msifuni Bwana.
21 ヱルサレムにすみたまふヱホバはシオンにて讃まつるべきかな ヱホバをほめたたへよ
Msifuni Bwana kutoka Sayuni, msifuni yeye aishiye Yerusalemu. Msifuni Bwana.

< 詩篇 135 >