< ヨブ 記 4 >
Ndipo Elifazi Mtemani akajibu:
2 「もし人があなたにむかって意見を述べるならば、あなたは腹を立てるでしょうか。しかしだれが黙っておれましょう。
“Kama mtu akithubutu kuzungumza nawe, kutakukasirisha? Lakini ni nani awezaye kujizuia asiseme?
3 見よ、あなたは多くの人を教えさとし、衰えた手を強くした。
Fikiri jinsi ambavyo umewafundisha watu wengi, jinsi ambavyo umeitia nguvu mikono iliyokuwa dhaifu.
4 あなたの言葉はつまずく者をたすけ起し、かよわいひざを強くした。
Maneno yako yamewategemeza wale waliojikwaa; umeyatia nguvu magoti yaliyokuwa dhaifu.
5 ところが今、この事があなたに臨むと、あなたは耐え得ない。この事があなたに触れると、あなたはおじ惑う。
Lakini sasa hii taabu imekujia wewe, nawe unashuka moyo; imekupiga wewe, nawe unafadhaika.
6 あなたが神を恐れていることは、あなたのよりどころではないか。あなたの道の全きことは、あなたの望みではないか。
Je, kumcha Mungu kwako hakupaswi kuwa ndiyo matumaini yako na njia zako kutokuwa na lawama ndilo taraja lako?
7 考えてみよ、だれが罪のないのに、滅ぼされた者があるか。どこに正しい者で、断ち滅ぼされた者があるか。
“Fikiri sasa: Ni mtu yupi asiye na hatia ambaye aliwahi kuangamia? Ni wapi wanyofu waliwahi kuangamizwa?
8 わたしの見た所によれば、不義を耕し、害悪をまく者は、それを刈り取っている。
Kwa jinsi ambavyo mimi nimechunguza, wale walimao ubaya na wale hupanda uovu, huvuna hayo hayo hayo.
9 彼らは神のいぶきによって滅び、その怒りの息によって消えうせる。
Kwa pumzi ya Mungu huangamizwa; kwa mshindo wa hasira zake huangamia.
10 ししのほえる声、たけきししの声はともにやみ、若きししのきばは折られ、
Simba anaweza kunguruma na kukoroma, lakini bado meno ya simba mkubwa huvunjika.
11 雄じしは獲物を得ずに滅び、雌じしの子は散らされる。
Simba anaweza kuangamia kwa kukosa mawindo, nao wana wa simba jike hutawanyika.
12 さて、わたしに、言葉がひそかに臨んだ、わたしの耳はそのささやきを聞いた。
“Neno lililetwa kwangu kwa siri, masikio yangu yakasikia mnongʼono wake.
13 すなわち人の熟睡するころ、夜の幻によって思い乱れている時、
Katikati ya ndoto za kutia wasiwasi wakati wa usiku, hapo usingizi mzito uwapatapo wanadamu,
14 恐れがわたしに臨んだので、おののき、わたしの骨はことごとく震えた。
hofu na kutetemeka kulinishika na kufanya mifupa yangu yote itetemeke.
15 時に、霊があって、わたしの顔の前を過ぎたので、わたしの身の毛はよだった。
Kuna roho aliyepita mbele ya uso wangu, nazo nywele za mwili wangu zikasimama.
16 そのものは立ちどまったが、わたしはその姿を見わけることができなかった。一つのかたちが、わたしの目の前にあった。わたしは静かな声を聞いた、
Yule roho akasimama, lakini sikuweza kutambua kilikuwa kitu gani. Umbo fulani lilisimama mbele ya macho yangu, kukawa na ukimya kisha nikasikia sauti:
17 『人は神の前に正しくありえようか。人はその造り主の前に清くありえようか。
‘Je, binadamu aweza kuwa mwadilifu kuliko Mungu? Je, mtu aweza kuwa safi kuliko Muumba wake?
18 見よ、彼はそのしもべをさえ頼みとせず、その天使をも誤れる者とみなされる。
Kama Mungu hawaamini watumishi wake, kama yeye huwalaumu malaika zake kwa kukosea,
19 まして、泥の家に住む者、ちりをその基とする者、しみのようにつぶされる者。
ni mara ngapi zaidi wale waishio katika nyumba za udongo wa mfinyanzi, ambazo misingi yake ipo mavumbini, ambao wamepondwa kama nondo!
20 彼らは朝から夕までの間に打ち砕かれ、顧みる者もなく、永遠に滅びる。
Kati ya mawio na machweo huvunjwa vipande vipande; bila yeyote kutambua, huangamia milele.
21 もしその天幕の綱が彼らのうちに取り去られるなら、ついに悟ることもなく、死にうせるではないか』。
Je, kamba za hema yao hazikungʼolewa, hivyo hufa bila hekima?’