< 歴代誌Ⅰ 2 >
1 イスラエルの子らは次のとおりである。ルベン、シメオン、レビ、ユダ、イッサカル、ゼブルン、
Hawa ndio wana wa Israeli: Reubeni, Simioni, Lawi, Yuda, Isakari, Zebuloni,
2 ダン、ヨセフ、ベニヤミン、ナフタリ、ガド、アセル。
Dani, Yusufu, Benyamini, Naftali, Gadi, na Asheri.
3 ユダの子らはエル、オナン、シラである。この三人はカナンの女バテシュアがユダによって産んだ者である。ユダの長子エルは主の前に悪を行ったので、主は彼を殺された。
Wana wa Yuda walikuwa Eri, Onani, na Shela, ambao walizaliwa na binti wa Shua, Wakanaani. Eri, mzaliwa wa kwanza wa Yuda, alikuwa muovu katika macho ya Yahweh, na Yahweh akamwua.
4 ユダの嫁タマルはユダによってペレヅとゼラを産んだ。ユダの子らは合わせて五人である。
Tamari, mkwe wake, alimzalia Peresi na Zera. Yuda alikuwa na wana wa kiume wa tano.
Wana wa Peresi walikuwa Hesroni na Hamuli.
6 ゼラの子らはジムリ、エタン、ヘマン、カルコル、ダラで、合わせて五人である。
Wana wa Zera walikuwa Zimri, Ethani, Hemani, Kalikoli na Darda, wote kwa jumla ni watano.
7 カルミの子はアカル。アカルは奉納物について罪を犯し、イスラエルを悩ました者である。
Mwana wa Karmi alikuwa ni Akani, aliye leta taabu katika Israeli alipo iba kile kilicho hifadhiwa kwa ajili ya Mungu.
Mwana wa Ethani alikuwa Azaria.
9 ヘヅロンに生れた子らはエラメル、ラム、ケルバイである。
Wana wa Hezroni walikuwa ni Yerameeli, Ramu, na Kalebu.
10 ラムはアミナダブを生み、アミナダブはユダの子孫のつかさナションを生んだ。
Ramu akawa baba wa Aminadabu, na Aminadabu akawa baba wa Nashoni, kiongozi miongoni uzao wa Yuda.
11 ナションはサルマを生み、サルマはボアズを生み、
Nashoni akawa baba wa Salmoni, na Salmon akawa baba wa Boazi.
12 ボアズはオベデを生み、オベデはエッサイを生んだ。
Boazi akawa baba wa Obedi, na Obedi akawa baba wa Yese.
13 エッサイは長子エリアブ、次にアビナダブ、第三にシメア、
Yese akawa baba wa mzaliwa wake wa kwanza Eliabu, wa pili Abinadabu, wa tatu Shama.
Nethaneli wa nne, Radai wa tano.
Ozemu wa sita, na Daudi wa saba.
16 彼らの姉妹はゼルヤとアビガイルである。ゼルヤの産んだ子はアビシャイ、ヨアブ、アサヘルの三人である。
Dada zao walikuwa Seruya na Abigaili. Wana wa Seruya walikuwa Abishai, Yoabu, na Asaheli, jumla watatu.
17 アビガイルはアマサを産んだ。アマサの父はイシマエルびとエテルである。
Abigali akamzaa Amasa, ambaye baba yake alikuwa Yetheri Mwishmaeli.
18 ヘヅロンの子カレブはその妻アズバおよびエリオテによって子をもうけた。その子らはエシル、ショバブ、アルドンである。
Kalebu mwana wa Hesroni akawa baba wa watoto wa Azubu mkewe, na Yeriothi. Wanawe walikuwa Yesheri, Shobabu, na Ardoni.
19 カレブはアズバが死んだのでエフラタをめとった。エフラタはカレブによってホルを産んだ。
Azuba akafa, na Kalebu akamuoa Efrathi, aliye mzalia Huri.
Huri akawa baba wa Uri, na Uri akawa baba wa Besaleli.
21 そののちヘヅロンはギレアデの父マキルの娘の所にはいった。彼が彼女をめとったときは六十歳であった。彼女はヘヅロンによってセグブを産んだ。
Baadae Hesroni (alipo kuwa na miaka sitini) akamuoa binti wa Makiri, baba wa Gileadi. Akamzalia Segubu.
22 セグブはヤイルを生んだ。ヤイルはギレアデの地に二十三の町をもっていた。
Segubu akawa baba wa Yairi, aliye miliki miji ishirini na mitatu katika nchi ya Gileadi.
23 しかしゲシュルとアラムは彼らからハボテ・ヤイルおよびケナテとその村里など合わせて六十の町を取った。これらはみなギレアデの父マキルの子孫であった。
Geshuri na Aramu wakawapokonya miji ya Yairi na Kenathi, pamoja na miji sitini iliyo zunguka. Hawa wakazi wote walikuwa ni uzao wa Makiri, baba wa Gileadi.
24 ヘヅロンが死んだのち、カレブは父ヘヅロンの妻エフラタの所にはいった。彼女は彼にテコアの父アシュルを産んだ。
Baada ya kifo cha Hesroni, Kalebu akalala na Efrata, mke wa baba yake Hesroni. Akamzalia Ashuri, baba wa Tekoa.
25 ヘヅロンの長子エラメルの子らは長子ラム、次はブナ、オレン、オゼム、アヒヤである。
Wana wa Yerameeli, mzaliwa wa kwanza wa Hesroni, walikuwa ni Ramu mzaliwa wa kwanza, Buna, Oreni, Ozemu, na Ahiya.
26 エラメルはまたほかの妻をもっていた。名をアタラといって、オナムの母である。
Yerameeli alikuwa na mke mwingine, Jina lake lilikuwa Atara. Yeye alikuwa mama wa Onamu.
27 エラメルの長子ラムの子らはマアツ、ヤミン、エケルである。
Wana wa Ramu, mzaliwa wa kwanza wa Yerameeli, walikuwa Maasi, Yamini, na Ekeri.
28 オナムの子らはシャンマイとヤダである。シャンマイの子らはナダブとアビシュルである。
Wana wa Onamu walikuwa ni Shamai na Yada. Wana wa Shamai walikuwa ni Nadabu na Abishuri.
29 アビシュルの妻の名はアビハイルといって、アバンとモリデを産んだ。
Jina la mke wa Abishuri lilikuwa Abihaili, na akamzalia Abani na Molidi.
30 ナダブの子らはセレデとアッパイムである。セレデは子をもたずに死んだ。
Wana wa Nadabu walikuwa Seledi na Apaimu, lakini Seledi alikufa pasipo watoto.
31 アッパイムの子はイシ、イシの子はセシャン、セシャンの子はアヘライである。
Mwana wa Apaimu alikuwa Ishi. Mwana wa Ishi alikuwa Sheshani. Mwana wa Sheshani alikuwa Alai.
32 シャンマイの兄弟ヤダの子らはエテルとヨナタンである。エテルは子をもたずに死んだ。
Wana wa Yada, kaka yake Shamai, walikuwa Yetheri na Yonathani. Yetheri alikufa pasipo mtoto.
33 ヨナタンの子らはペレテとザザである。以上はエラメルの子孫である。
Wana wa Yonathani walikuwa Pelethi na Zaza. Hawa ndio uzao wa Yerameeli.
34 セシャンには男の子はなく、ただ女の子のみであったが、彼はヤルハと呼ぶエジプトびとの奴隷をもっていたので、
Sasa Sheshani hakuwa na watoto wa kiume, bali wa kike pekee. Sheshani alikuwa na mtumishi, wa Kimisri, ambaye jina lake lilikuwa Yariha.
35 セシャンは娘を奴隷ヤルハに与えてその妻とさせた。彼女はヤルハによってアッタイを産んだ。
Sheshani alimkabidhi binti yake kwa Yariha mtumishi wake kama mke wake. Akamzalia Atai.
36 アッタイはナタンを生み、ナタンはザバデを生み、
Atai akawa baba wa Nathani, na Nathani akawa baba wa Zabadi.
37 ザバデはエフラルを生み、エフラルはオベデを生み、
Zabadi akawa baba wa Efalali, na Afalali akawa baba wa Obedi.
38 オベデはエヒウを生み、エヒウはアザリヤを生み、
Obedi akawa baba wa Yehu, na Yehu akawa baba wa Azaria.
39 アザリヤはヘレヅを生み、ヘレヅはエレアサを生み、
Azaria akawa baba wa Helesi, na Helesi akawa baba wa Eleasa.
40 エレアサはシスマイを生み、シスマイはシャルムを生み、
Eleasa akawa baba wa Sismai, na Sismai akawa baba wa Shalumu.
41 シャルムはエカミヤを生み、エカミヤはエリシャマを生んだ。
Shalumu akawa baba wa Yekamia, na Yekamia akawa baba wa Elishama.
42 エラメルの兄弟であるカレブの子らは長子をマレシャといってジフの父である。マレシャの子はヘブロン。
Wana wa Kalebu, kaka yake Yerameeli, walikuwa ni Mesha mzaliwa wake wa kwanza, aliye kuwa baba wa Zifu. Mwanae wa pili, Maresha, allikuwa baba wa Hebroni.
43 ヘブロンの子らはコラ、タップア、レケム、シマである。
Wana wa Hebroni walikuwa Kora, Tapua, Rekemu, na Shema.
44 シマはラハムを生んだ。ラハムはヨルカムの父である。またレケムはシャンマイを生んだ。
Shema akawa baba wa Rahamu, baba wa Yorkeamu. Rekemu akawa baba wa Shamai.
45 シャンマイの子はマオン。マオンはベテヅルの父である。
Mwana wa Shamai alikuwa Maoni, na Maoni alikuwa baba wa Bethsuri.
46 カレブのそばめエパはハラン、モザ、ガゼズを産んだ。ハランはガゼズを生んだ。
Efa, suria wa Kalebu, alimza Harani, Mosa, na Gazezi. Harani akawa baba wa Gazezi.
47 エダイの子らはレゲム、ヨタム、ゲシャン、ペレテ、エパ、シャフである。
Wana wa Yadai walikuwa Regemu, Yothamu, Geshani, Peleti, Efa, na Shaafa.
48 カレブのそばめマアカはシベルとテルハナを産み、
Maaka, suria wa Kalebu, alimza Sheberi na Tirhana.
49 またマデマンナの父シャフおよびマクベナとギベアの父シワを産んだ。カレブの娘はアクサである。
Pia akamza Shaafu baba wa Madmana, Sheva baba wa Makbena na baba wa Gibea. Binti wa Kalebu alikuwa Aksa. Hawa walikuwa uzao wa Kalebu.
50 これらはカレブの子孫であった。エフラタの長子ホルの子らはキリアテ・ヤリムの父ショバル、
Hawa walikuwa wana wa Huri, mzaliwa wake wa kwanza kwa Efratha: Shobali baba wa Kiriath-Yearimu.
51 ベツレヘムの父サルマおよびベテガデルの父ハレフである。
Salma baba wa Bethlehemu, na Harefu baba wa Beth-gaderi.
52 キリアテ・ヤリムの父ショバル子らはハロエとメヌコテびとの半ばである。
Shobali baba wa kiriath-Yearimu alikuwa na uzao: Haroe, nusu ya watu Wamenuthite,
53 キリアテ・ヤリムの氏族はイテルびと、プテびと、シュマびと、ミシラびとであって、これらからザレアびとおよびエシタオルびとが出た。
na ukoo wa Kiriath-Yearimu: Waithri, Waputhi, Washumathi, na Wamishrai. Wasorathi na Waeshtaoli walitoka huku.
54 サルマの子らはベツレヘム、ネトパびと、アタロテ・ベテ・ヨアブ、マナハテびとの半ばおよびゾリびとである。
Ukoo wa Salma ulikuwa kama ufatao: Bethlehemu, Wanetofathi, Atroth-Beth-Yoabu, na nusu ya Wamenuhothi na Wazori,
55 またヤベヅに住んでいた書記の氏族テラテびと、シメアテびと、スカテびとである。これらはケニびとであってレカブの家の先祖ハマテから出た者である。
ukoo wa waandishi walio ishi Yabesi: Watirathi, Washimeathi, na Wasukathi. Hawa walikuwa Wakeni walio toka katika uzao wa Hamathi, babu wa Warekabu.