< ピリピ人への手紙 4 >

1 この故に我が愛するところ慕ふところの兄弟、われの喜悦われの冠冕たる愛する者よ、斯くのごとく主にありて堅く立て。
Kwa hiyo wapendwa wangu, ambao nawatamani, ambao ni furaha na taji yangu. Simameni imara katika Bwana, enyi rafiki wapendwa.
2 我ユウオデヤに勸めスントケに勸む、主にありて心を同じうせんことを。
Ninakusihi wewe Eudia, pia ninakusihi wewe Sintike, mrejeshe mahusiano ya amani kati yenu, kwa sababu ninyi, nyote wawili mliungana na Bwana.
3 また眞實に我と軛を共にする者よ、なんぢに求む。この二人の女を助けよ。彼らはクレメンス其のほか生命の書に名を録されたる我が同勞者と同じく、福音のために我とともに勤めたり。
Kwa kweli, niwasihi pia ninyi watenda kazi wenzangu, muwasaidie hawa wanawake kwa kuwa walitumika pamoja na mimi katika kueneza injili ya Bwana tukiwa na Kelementi pamoja na watumishi wengine wa Bwana, ambao majina yao yameandikwa katika kitabu cha uzima.
4 汝ら常に主にありて喜べ、我また言ふ、なんぢら喜べ。
katika Bwana siku zote. tena nitasema, furahini.
5 凡ての人に汝らの寛容を知らしめよ、主は近し。
Upole wenu na ujulikane kwa watu wote. Bwana yuko karibu.
6 何事をも思ひ煩ふな、ただ事ごとに祈をなし、願をなし、感謝して汝らの求を神に告げよ。
Msijisumbue kwa jambo lolote. Badala yake, fanyeni mambo yenu yote kwa njia ya kusali, kuomba na kushukuru. Na mahitaji yenu yajulikane kwa Mungu.
7 さらば凡て人の思にすぐる神の平安は、汝らの心と思とをキリスト・イエスによりて守らん。
Basi amani ya Bwana iliyo kuu kuliko ufahamu wote, italinda mioyo na mawazo yenu kwa msaad Kristo Yesu.
8 終に言はん、兄弟よ、凡そ眞なること、凡そ尊ぶべきこと、凡そ正しきこと、凡そ潔よきこと、凡そ愛すべきこと、凡そ令聞あること、如何なる徳いかなる譽にても、汝 等これを念へ。
Hatimaye, ndugu zangu; yatakafarini sana mambo yote yenye ukweli, heshima, haki, usafi, upendo, na yale yenye taarifa njema, yenye busara, pamoja na yale yanayohitaji kusifiwa.
9 なんぢら我に學びしところ、受けしところ、聞きしところ、見し所を皆おこなへ、さらば平和の神なんぢらと偕に在さん。
Yatekelezeni mambo yale mliojifunza, mliyopokea mliyoyasikia na yale mliyoyaona kwangu naye Baba yetu wa amani atakuwa nanyi.
10 汝らが我を思ふ心の今また萠したるを、われ主にありて甚く喜ぶ。汝らは固より我を思ひゐたるなれど、機を得ざりしなり。
Ninayo furaha kubwa sana juu yenu katika Bwana kwa kuwa ninyi mmeonyesha tena nia ya kujihusisha kwenu juu ya mahitaji yangu. Kwa kweli, hapo awali mlitamani kunijali kwa mahitaji yangu japo hamkupata fursa ya kunisaidia.
11 われ窮乏によりて之を言ふにあらず、我は如何なる状に居るとも、足ることを學びたればなり。
Sisemi hivyo ili kujipatia kitu kwa ajili ya mahitaji yangu. Kwani nimejifunza kuridhika katika hali zote.
12 我は卑賤にをる道を知り、富にをる道を知る。また飽くことにも、飢うることにも、富むことにも、乏しき事にも、一切の秘訣を得たり。
Nafahamu kuishi katika hali ya kupungukiwa na pia katika hali ya kuwa na vingi. Katika mazingira yote haya mimi nimejifunza siri ya namna ya kula wakati wa shibe na jinsi ya kula wakati wa njaa, yaani vingi na kuwa mhihtaji.
13 我を強くし給ふ者によりて、凡ての事をなし得るなり。
Ninaweza kufanya haya kwa kuwezeshwa na Yeye anitiaye nguvu.
14 されど汝らが我が患難に與りしは善き事なり。
Hata hivyo, mlifanya vyema kushiriki nami katika dhiki zangu.
15 ピリピ人よ、汝らも知る、わが汝らに福音を傳ふる始、マケドニヤを離れ去るとき、授受して我が事に與りしは、汝 等のみにして、他の教會には無かりき。
Ninyi wafilipi mnafahamu kwamba mwanzo wa injili nilipoondoka Makedonia, hakuna Kanisa lililoniwezesha katika mambo yanayohusu utoaji na kupokea isipokuwa ninyi pekee yenu.
16 汝らは我がテサロニケに居りし時に、一度ならず二度までも我が窮乏に物 贈れり。
Hata nilipokuwa Thesaslonika, ninyi mlinitumia msaada zaidi ya mara moja kwa ajili ya mahitaji yangu.
17 これ贈物を求むるにあらず、唯なんぢらの益となる實の繁からんことを求むるなり。
Simaanishi kwamba natafuta msaada. Bali nasema ili mpate matunda yaletayo faida kwenu.
18 我には凡ての物そなはりて餘あり、既にエパフロデトより汝らの贈物を受けたれば、飽き足れり。これは馨しき香にして神の享け給ふところ、喜びたまふ所の供物なり。
Nimepokea vitu vyote, na sasa nimejazwa na vitu vingi. Nimepokea vitu vyenu kutoka kwa Epafradito. Ni vitu vizuri vyenye kunukia mithiri ya manukato, vyenye kukubalika ambavyo vyote ni sadaka inayompendeza Mungu.
19 かくてわが神は己の富に隨ひ、キリスト・イエスによりて汝らの凡ての窮乏を榮光のうちに補ひ給はん。
Kwa ajili hiyo, Mungu wangu atawajazeni mahitaji yenu kwa utajiri wa utukufu wake katikaYesu Kristo.
20 願はくは榮光 世々 限りなく、我らの父なる神にあれ、アァメン。 (aiōn g165)
Sasa kwa Mungu na Baba yetu uwe utukufu milele na milele. Amina. (aiōn g165)
21 汝らキリスト・イエスに在りて聖徒おのおのに安否を問へ、我と偕にある兄弟たち汝らに安否を問ふ。
Salamu zangu zimfikie kila muumini katika Kristo Yesu. Wapendwa nilio nao hapa wanawasalimieni.
22 凡ての聖徒、殊にカイザルの家のもの、汝らに安否を問ふ。
Pia waumini wote hapa wanawasalimieni, hususani wale wa familia ya Kaisari.
23 願はくは主イエス・キリストの恩惠、なんぢらの靈と偕に在らんことを。
Na sasa neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe na roho zenu.

< ピリピ人への手紙 4 >