< ヨシュア記 22 >
1 茲にヨシユア、ルベン人ガド人およびマナセの支派の半を召て
Kwa wakati huo, Yoshua aliwaita Warubeni, Wagadi, na nusu ya kabila la Manase.
2 これに言けるは汝らはヱホバの僕モーセが汝らに命ぜし所をことごとく守り又わが汝らに命ぜし一切の事において我言に聽したがへり
Aliwaambia, “Mmefanya kila kitu ambacho Musa mtumishi wa Yahweh aliwaagiza ninyi. Mmeitii sauti yangu katika yote niliyowaagiza.
3 汝らは今日まで日ひさしく汝らの兄弟を離れずして汝らの神ヱホバの命令の言を守り來り
Bado hamjawaacha ndugu zenu hawa kwa siku zote hizi, mpaka siku hii ya leo. Na mmetimiza wajibu unaotakiwa na amri za Yahweh Mungu wenu.
4 今は已に汝らの神ヱホバなんぢらの兄弟に向に宣まひし如く安息を賜ふに至れり然ば汝ら身を轉らしヱホバの僕モーセが汝らに與へしヨルダンの彼方なる汝等の產業の地に歸りて自己の天幕にゆけ
Sasa Yahweh Mungu wenu amewapa pumziko ndugu zenu, kama alivyowaahidi. Hivyo basi, rudini na mwende katika hema zenu katika nchi mnayoimiliki, ambayo Musa mtumishi wa Yahweh aliwapeni katika upande mwingine wa Yordani.
5 只ヱホバの僕モーセが汝らに命じおきし誡命と律法とを善く謹しみて行ひ汝らの神ヱホバを愛しその一切の途に歩みその命令を守りて之に附したがひ心を盡し精神を盡して之に事ふべしと
Lakini zingatieni kuzishika amri na sheria ambazo Musa mtumishi wa Yahweh aliwaagiza ninyi, kumpenda Yahweh Mungu wenu, kutembea katika njia zake, kuzitunza amri zake, na kuambatana naye na kumwabudu yeye kwa moyo wenu wote na kwa roho zenu zote.
6 かくてヨシユア彼らを祝して去しめければ彼らはその天幕に往り
Basi Yoshua akawabariki na kisha akawaacha waende zao, nao wakarudi katika hema zao.
7 マナセの支派の半にはモーセ、バシヤンにて產業を與へおけりその他の半にはヨシユア、ヨルダンの此旁西の方にてその兄弟等の中に產業を與ふヨシユア彼らをその天幕に歸し遣るに當りて之を祝し
Na kwa nusu ya kabila la Manase, Musa alikuwa amewapa urithi katika Bashani, lakini kwa nusu ya kabila hilo, Yoshua aliwapa urithi karibu na ndugu zao katika nchi magharibi mwa Yordani. Yoshua aliwaaga waende katika hema zao; aliwabarikia,
8 之に告て言けるは汝ら衆多の貨財夥多しき家畜金銀銅鐵および夥多しき衣服をもちて汝らの天幕に歸り汝らの敵より獲たるその物を汝らの兄弟の中に分つべしと
na kisha akawaambia, “Rudini katika hema zenu mkiwa na pesa nyingi, na mkiwa na mifugo mingi, pamoja na na fedha, na dhahabu, na shaba na chuma, na nguo nyingi. Gawaneni na ndugu zenu nyara mlizochukua kutoka kwa maadui zenu.
9 爰にルベンの子孫ガドの子孫およびマナセの支派の半はヱホバのモーセによりて命じ給ひし所に循ひて己の所有の地すなはち已に獲たるギレアデの地に往んとてカナンの地のシロよりしてイスラエルの子孫に別れて歸りけるが
Hivyo, wazawa wa Rubeni, wazawa wa Gadi na nusu ya kabila la Manase walirudi nyumbani, waliwaacha watu wa Isaeli hapo Shilo, ambayo imo ndani ya nchi ya Kanaani. Waliondoka wakaenda katika mkoa wa Gileadi, katika nchi yao, ambayo wao wenyewe waliimiliki, katika utiifu wa amri za Yahweh, kwa mkono wa Musa.
10 ルベンの子孫ガドの子孫およびマナセの支派の半カナンの地のヨルダンの岸邊にいたるにおよびて彼處にてヨルダンの傍に一の壇を築けりその壇は大にして遥に見えわたる
Nao walipofika hapo Yordani iliyo katika nchi ya Kanaani, Warubeni na Wagadi na nusu ya kabila la Manase walijenga madhabahu karibu na Yordani, madhabahu kubwa na iliyotokeza na mashuhuri.
11 イスラエルの子孫はルベンの子孫ガドの子孫およびマナセの支派の半カナンの地の前の部にてヨルダンの岸邊イスラエルの子孫に屬する方にて一の壇を築けりと言を聞り
Watu wa Israeli walisikia habari hizo na wakaseam, “Tazama! Watu wa Rubeni, Gadi na nusu ya kabila la Manase wamejenga madhabahu mbele ya nchi ya Kanaani, huko Gelilothi, katika mkoa karibu na Yordani, katika upande ambao ni miliki ya watu wa Israeli.”
12 イスラエルの子孫これを聞と斉しくイスラエルの子孫の會衆ことごとくシロに集まりて彼らの所に攻のぼらんとす
Wakati watu wa Israeli waliposikia hivyo, kusanyiko lote la watu wa Israeli walikusanyika kwa pamoja huko Shilo ili wapande kupigana vita nao.
13 イスラエルの子孫すなはち祭司エレアザルの子ピハネスをギレアデの地に遣はしてルベンの子孫ガドの子孫およびマナセの支派の半の所に至らしめ
Kisha watu wa Israeli walituma wajumbe kwa Warubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase, katika nchi ya Gileadi. Walimtuma pia Finehasi mwana wa Eliezari, kuhani,
14 イスラエルの各々の支派の中より父祖の家の牧伯一人づつを擧て合せて十人の牧伯を之に伴なはしむ是みなイスラエルの家族の中にて父祖の家の長たる者なりき
na viongozi kumi pamoja naye, mmoja kutoka katika familia za mababa wa Israeli, na kila mmoja wao alikuwa ni kiongozi wa ukoo miongoni mwa watu wa Israeli.
15 彼らギレアデの地に往きルベンの子孫ガドの子孫およびマナセの支派の半にいたりて之に語りて言けらく
Walienda kwa watu wa Rubeni, Gadi, na nusu ya kabila la Manase, katika nchi ya Gileadi, na wakawaambia:
16 ヱホバの全會衆かく言ふ汝らイスラエルの神にむかひて愆を犯し今日すでに翻へりてヱホバに從がはざらんとし即ち己のために一の壇を築きて今日ヱホバに叛かんとするは何事ぞや
“Kusanyiko lote la Yahweh linasema kuwa, ' Ni jambo gani hili lisilo la uaminifu ambalo mmelitenda kinyume na Mungu wa Israeli, kwa kugeuka badala ya kumfuata Yahweh siku hii na kujijengea wenyewe madhabahu katika uasi kinyume na Yahweh katika siku hii?
17 ベオルの罪われらに足ざらんや之がためにヱホバの會衆に災禍くだりたりしかども我ら今日までも尚身を潔めてその罪を棄ざるなり
Je dhambi zetu huko Peori hazikututosha? Bado hata sasa hatujajitakasa wenyewe kwa dhambi hiyo. Kwa ajili ya dhambi ile lilikuja pigo kwa kusanyiko lote la Yahweh.
18 然るに汝らは今日ひるがへりてヱホバに從がはざらんとするや汝ら今日ヱホバに叛けば明日はヱホバ、イスラエルの全會衆を怒りたまふべし
Je, nanyi leo pia mwageuka na kuacha kumfuata Yahweh? Kama mtaasi kinyume na Yahweh leo, kesho atakuwa na hasira na kusanyiko lote la Israeli.
19 然ながら汝らの所有の地もし潔からずばヱホバの幕屋のたてるヱホバの產業の地に濟り來て我らの中にて所有を獲よ惟われらの神ヱホバの壇の外に壇を築きてヱホバに叛く勿れまた我らに悖るなかれ
Na kama nchi ambayo mnaimiliki imetiwa unajisi, basi mwaweza kuvuka katika nchi ambayo Sanduku la Yahweh lasimama na mjichukulie kwa ajili yenu umiliki miongoni mwetu. Hamtakiwi kuasi kinyume na Yahweh tu, wala kuasi kinyume chetu kwa kujenga madhabahu kwa ajili yenu wenyewe badala ya madhabahu ya Yahweh Mungu wa wetu.
20 ゼラの子アカン詛はれし物につきて愆を犯しつひにイスラエルの全會衆に震怒臨みしにあらずや且また其罪にて滅亡し者は彼人ひとりにはあらざりき
Je hakuwa Akani mwana wa Zera aliyeivunja imani kwa vitu vile ambavyo vilikuwa vimetunzwa kwa ajili ya Mungu? Na je ghadhabu ya Mungu haikushuka kwa watu wote wa Israeli? Mtu yule hakuangamia peke yake kwa uovu wake.
21 ルベンの子孫ガドの子孫およびマナセの支派の半答へてイスラエルの宗族の長等に言けるは
Kisha makabila ya Rubeni, Gadi na nusu ya kabila la Manase wakawajibu wazee wa koo za Israeli:
22 諸の神の神ヱホバ諸の神の神ヱホバ知しめすイスラエルも亦知んもし叛く事あるひはヱホバに罪を犯す事ならば汝今日我らを救ふなかれ
“Yahweh, Mungu Mwenye nguvu! Yahweh, Mungu Mwenye nguvu! Yeye anajua, na Israeli naijue yenyewe! Kama ilikuwa ni katika uasi au katika kuvunja imani kinyume na Yahweh, msituache hai katika siku hii ya leo
23 我らが壇を築きし事もし翻がへりてヱホバに從がはざらんが爲なるか又は其上に燔祭素祭を献げんが爲なるか又はその上に酬恩祭の犠牲を獻げんがためならばヱホバみづからその罪を問討したまへ
kwa ajili ya kujenga madhabahu ili tugeuka na kuacha kumfuata Yahweh. Kama tumejenga madhabahu hii ili kutoa juu yake sadaka ya kuteketezwa, sadaka ya nafaka, au sadaka ya amani, basi Yahweh na atuadhibu.
24 我等は遠き慮をもて故に斯なしたるなり即ち思ひけらく後の日にいたりて汝らの子孫われらの子孫に語りて言ならん汝らはイスラエルの神ヱホバと何の關係あらんや
La hasha, tulifanya hivyo kwa sababu ya hofu kwamba katika siku zijazo watoto wenu wanaweza kuwaambia watoto wetu, ' Mna nini ninyi na Yahweh, Mungu wa Israeli?
25 ルベンの子孫およびガドの子孫よヱホバ我らと汝らの間にヨルダンを界となしたまへり汝らはヱホバの中に分なしと斯いひてなんぢらの子孫われらの子孫としてヱホバを畏るることを息しめんと
Kwa kuwa Yahweh ameifanya Yordani kuwa mpaka kati yetu na ninyi. Ninyi watu wa Rubeni na watu wa Gadi, hamna kitu chochote naYahweh.' Na kwa hali hiyo, watoto wenu wanaweza kuwafanya watoto wetu waacha kumwabudu Yahweh.
26 是故に我ら言けらく我らいま一の壇を我らのために築かんと是燔祭のために非ずまた犠牲のために非ず
Basi tukasema, 'Hebu na tujenge sasa madhabahu, si kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa wala si kwa sadaka yoyote ile,
27 惟し之をして我らと汝らの間および我らの後の子孫の間に證とならしめて我ら燔祭犠牲および酬恩祭をもてヱホバの前にその職務をなさんがためなり然せば汝らの子孫後の日いたりて我らの子孫に汝らはヱホバの中に分なしと言こと無らん
ila iwe ni ushahidi kati yetu na ninyi, na kati ya kizazi chetu baada yetu, kwamba tutafanya ibada ya Yahweh mbele yake, pamoja na sadaka zetu za kuteketezwa na dhabihu zetu na sadaka zetu za amani, ili kwamba watoto wenu wasiweze kuwaambia watoto wetu katika siku zijazo kuwa, “Hamna sehemu katika Yahweh.”'
28 是をもて我ら言り彼らが我らまたは後の日に我らの子孫に然いはばその時我ら言ん我らの父祖の築きたりしヱホバの壇の模形を見よ是は燔祭のためにも非ずまた犠牲のためにもあらず我らと汝らとの間の證なり
Hivyo tukasema, 'kama hili litasemwa kwa kwetu au kwa watoto wetu katika siku zijazo, tutasema, “Tazama! Huu ni mfano wa madhabahu ya Yahweh, ambayo mababu zetu waliifanya, si kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa, wala si kwa dhabihu, bali kwa ajili ya ushahidi kati yetu ninyi.”
29 ヱホバに叛き翻へりて今日ヱホバに從がふことを息め我らの神ヱホバの幕屋の前にあるその祭壇の外に燔祭素祭犠牲などのために壇を築くことは我らの絶て爲ざる所なり
Na iwe mbali nasi kwamba tunataka kugeuka kinyume na Yahweh, na kuacha kumfuata yeye kwa kujenga madhabahu kwa ajili sadaka ya kuteketezwa, na kwa sadaka ya nafaka, au kwa dhabihu, badala ya madhabahu ya Yahweh Mungu wetu ambayo iko mbele ya hema la kukutania.'”
30 祭司ピネハスおよび會衆の長等即ち彼とともなるイスラエルの宗族の首等はルベンの子孫ガドの子孫およびマナセの子孫が述たる言を聞て善とせり
Finehasi kuhani na viongozi wa watu, ambao ni wakuu wa koo za Waisraeli ambao walikuwa pamoja naye, waliposikia maneno amabayo watu wa Rubeni, Gadi na nusu ya kabila la Manase, kwamba yalikuwa ni mazuri machoni pao.
31 祭司エレアザルの子ピネハスすなはちルベンの子孫ガドの子孫およびマナセの子孫に言けるは我ら今日ヱホバの我らの中に在すを知る其は汝らヱホバにむかひて此愆を犯さざればなり今なんぢらはイスラエルの子孫をヱホバの手より救ひいだせりと
Finehasi mwana wa Eliazeri kuhani aliwaambia watu wa Rubeni, Gadi na Manase, “Leo tumejua kwambaYahweh yuko miongoni mwetu, kwa kuwa hamjatenda uvunjaji wa imani kinyume naye. Sasa, mmewaokoa watu wa Israeli kutoka katika mkono wa Yahweh.”
32 祭司エレアザルの子ピネハスおよび牧伯等すなはちルベンの子孫およびガドの子孫に別れてギレアデの地よりカナンの地に歸りイスラエルの子孫にいたりて復命しけるに
Kisha Finehasi mwana wa Eliazeri kuhani, na viongozi walirudi kutoka kwa Warubeni na Wagadi, kutoka katika nchi ya Gileadi, na kurudi katika nchi ya Kanaani, kwa watu wa Israeli, na waliwaletea taarifa.
33 イスラエルの子孫これを善とせり而してイスラエルの子孫神を讃めルベンの子孫およびガドの子孫の住をる國を滅ぼしに攻上らんと重ねて言ざりき
Taarifa yao ilikuwa nzuri katika macho ya watu wa Israeli. Watu wa Israeli walimbarikia Mungu na hawakuendelea kusema tena juu ya kuinua vita dhidi ya Warubeni na Wagadi, ili kuiharibu nchi ambayo walikuwa wanaishi.
34 ルベンの子孫およびガドの子孫その壇をエド(證)と名けて云ふ是は我らの間にありてヱホバは神にいますとの證をなす者なりと
Warubeni na Wagadi waliita ile madhabahu “Ushahidi,” kwa kuwa walisema, “Ni ushahidi miongoni mwetu kuwa Yahweh ni Mungu.”