< 伝道者の書 7 >

1 名は美膏に愈り 死る日は生るる日に愈る
Jina zuri ni bora kuliko manukato ya gharama, na siku ya kufa ni bora kuliko siku ya kuzaliwa.
2 哀傷の家に入は宴樂の家に入に愈る 其は一切の人の終かくのごとくなればなり 生る者またこれをその心にとむるあらん
Ni bora kwenda kwenye nyumba ya maombolezo kuliko nyumba ya karamu, kwa kuwa maombolezo huja kwa watu wote wakati wa mwisho wa uhai, kwa hiyo watu wanaoishi ni lazima waweke hili moyoni.
3 悲哀は嬉笑に愈る 其は面に憂色を帶るなれば心も善にむかへばなり
Huzuni ni bora kuliko kicheko, kwa kuwa baada ya uso wa huzuni huja furaha ya moyo.
4 賢き者の心は哀傷の家にあり 愚なる者の心は喜樂の家にあり
Moyo wa mwenye hekima uko katika nyumba ya maombolezo, lakini moyo wa wapumbavu uko katika nyumba ya karamu.
5 賢き者の勸責を聽は愚なる者の歌詠を聽に愈るなり
Ni bora kusikiliza maonyo ya mtu mwenye hekima kuliko kusikiliza wimbo wa wapumbavu.
6 愚なる者の笑は釜の下に焚る荊棘の聲のごとし是また空なり
Kwa kuwa kama mlio wa miiba chini ya chungu, ndivyo kilivyo kicheko cha wapumbavu. Huu pia ni mvuke.
7 賢き人も虐待る事によりて狂するに至るあり賄賂は人の心を壞なふ
kweli jeuri humfanya mtu mwenye hekima kuwa mpumbavu, na rusha huharibu moyo.
8 事の終はその始よりも善し 容忍心ある者は傲慢心ある者に勝る
Ni heri mwisho wa jambo kuliko mwanzo; na watu wenye uvumilivu ni bora kuliko wenye majivuno rohoni.
9 汝氣を急くして怒るなかれ 怒は愚なる者の胸にやどるなり
Usikasirike haraka rohoni mwako, kwa sababu hasira hukaa katika mioyo ya wapumbavu.
10 昔の今にまさるは何故ぞやと汝言なかれ 汝の斯る問をなすは是智慧よりいづる者にあらざるなり
Usiseme, “Kwa nini siku za zamani zilikuwa bora kuliko siku hizi?” Kwa kuwa sio kwa sababu ya hekima kwamba unauliza swali hili.
11 智慧の上に財產をかぬれば善し 然れば日を見る者等に利益おほかるべし
Hekima ni njema kama vitu vya thamani tunavyorithi kutoka kwa wazazi wetu. Inatoa faida kwa wale wanaoliona jua.
12 智慧も身の護庇となり銀子も身の護庇となる 然ど智惠はまたこれを有る者に生命を保しむ 是知識の殊勝たるところなり
Kwa kuwa hekima hutoa ulinzi kama vile fedha inavyoweza kutoa ulinzi, lakini faida ya maarifa ni kwamba hekima humpa uhai kwa yeyote aliye nayo.
13 汝神の作爲を考ふべし 神の曲たまひし者は誰かこれを直くすることを得ん
Tafakaria matendo ya Mungu: Ni nani awezaye kuimarisha chochote alichokipindisha?
14 幸福ある日には樂め 禍患ある日には考へよ 神はこの二者をあひ交錯て降したまふ 是は人をしてその後の事を知ることなからしめんためなり
Wakati nyakati vinakuwa njema, ishi kwa furaha katika hali hiyo, lakini wakati unapokuwa mbaya, tafakari hili: Mungu ameruhusu hali zote ziwepo, Kwa sababu hii, hakuna mwanadamu yeyote atakaye fahamu chochote kinacho kuja baada yake.
15 我この空の世にありて各樣の事を見たり 義人の義をおこなひて亡ぶるあり 惡人の惡をおこなひて長壽あり
Nimeona mambo mengi katika siku zangu za ubatili. Kuna watu wenye haki ambao wanaangamia licha ya kwamba wana haki, na kuna watu waovu wanaoishi maisha marefu licha ya kwamba ni waovu.
16 汝義に過るなかれまた賢に過るなかれ 汝なんぞ身を滅すべけんや
Usiwe mwenye haki katika macho yako mwenyewe. Kwa nini kujiharibu mwenyewe?
17 汝惡に過るなかれまた愚なる勿れ 汝なんぞ時いたらざるに死べけんや
Usiwe mwovu sana au mpumbavu. Kwa nini ufe kabla ya wakati wako?
18 汝此を執は善しまた彼にも手を放すなかれ 神を畏む者はこの一切の者の中より逃れ出るなり
Ni vyema kwamba ushike hekima hii, na kwamba usiache haki iende zake. Kwa kuwa mtu amchae Mungu atatimiza ahadi zake zote.
19 智慧の智者を幇くることは邑の豪雄者十人にまさるなり
Hekima ina nguvu ndani ya mwenye hekima, zaidi ya watawala kumi katika mji.
20 正義して善をおこなひ罪を犯すことなき人は世にあることなし
Hakuna mtu mwenye haki juu ya nchi anayefanya mema na hatendi dhambi.
21 人の言出す言詞には凡て心をとむる勿れ 恐くは汝の僕の汝を詛ふを聞こともあらん
Usisikilize kila neno linaongelewa, kwa sababu unaweza kusikia mtumishi wako anakulaani.
22 汝も屡人を詛ふことあるは汝の心に知ところなり
Vivyo hivyo unafahamu mwenyewe ndani ya moyo wako umewalaani wengine mara kadhaa.
23 我智慧をもてこの一切の事を試み我は智者とならんと謂たりしが遠くおよばざるなり
Haya yote nimeyathibitisha kwa hekima. Nikasema, “nitakuwa mwenye hekima,” lakini zaidi ambavyo ningekuwa.
24 事物の理は遠くして甚だ深し 誰かこれを究むることを得ん
Hekima i mbali na kina sana. Ni nani awezaye kuipata?
25 我は身をめぐらし心をもちひて物を知り事を探り 智慧と道理を索めんとし 又惡の愚たると愚癡の狂妄たるを知んとせり
Nikageuza moyo wangu kujifunza kuchunguza na kutafuta hekima na ufafanuzi wa ukweli, na kufahamu kwamba ubaya ni ujinga na kwamba upumbavu ni wazimu.
26 我了れり 婦人のその心羅と網のごとくその手縲絏のごとくなる者は是死よりも苦き者なり 神の悦びたまふ者は之を避ることを得ん罪人は之に執らるべし
Nikapata kufahamu kwamba uchungu kuliko kifo, ndivo alivyo mwanamke yeyote ambaye moyo wake umejaa mitego, na nyavu, na ambaye mikono yake ni minyororo. Yeyote ampendezaye Mungu ataponyoka kutoka kwake, lakini mwenye dhambi atachukuliwa naye.
27 傳道者言ふ 視よ我その數を知んとして一々に算へてつひに此事を了る
“Tafakari kile nilichovumbua,” asema Mwalimu. “Nimekuwa nikiongeza uvumbuzi mmoja hadi mwingine ili kwamba nipate ufafanuzi wa ukweli.
28 我なほ尋ねて得ざる者は是なり 我千人の中には一箇の男子を得たれども その數の中には一箇の女子をも得ざるなり
Hii ndiyo bado natafuta, lakini bado sijapata. Sikupata mwanamme mmoja mwenye haki miongoni mwa elfu, lakini sikupata mwanamke miongoni mwa wale wote.
29 我了れるところは唯是のみ 即ち神は人を正直者に造りたまひしに人衆多の計略を案出せしなり
Nimegundua hili: kwamba Mungu alimuumba binadamu akiwa mnyoofu, lakini wametoka katika hali ya unyofu wakitafuta magumu mengi.

< 伝道者の書 7 >