< 歴代誌Ⅱ 21 >

1 ヨシヤパテその先祖等とともに寝りてダビデの邑にその先祖等とともに葬られその子ヨラムこれに代て王となる
Yehoshafati akalala pamoja na babu zake na akizikwa pamoaja nao katika mji wa Daudi;
2 ヨシヤパテの子たるその兄弟はアザリヤ、ヱヒエル、ゼカリヤ、アザリヤ、ミカエルおよびシバテヤ是みなイスラエルの王ヨシヤパテの子なり
Yehoramu, mwanaye, akawa mfalme katika nafasi yake. Yehoramu alikuwa na ndugu, wana wa Yehoshafati: Azaria, Yerieli, Zekaria, Azaria, Mikaeli, na Shefatia. Wote hawa walikuwa wana wa Yehoshafati, mfalme wa Israeli.
3 その父彼らに金銀寶物の賜物を多く與へまたユダの守衛の邑々を與へけるが國はヨラムに與へたりヨラム長子なりければなり
Baba yao alikuwa amewapa zawadi kubwa ya fedha, dhahabu, na vitu vingine vya thamani, na miji yenye ngome katika Yuda, lakini kiti cha enzi alimpa Yehoramu, kwa sababu alikuwa mzaliwa wake wa kwanza.
4 ヨラムその父の位に登りて力つよくなりければその兄弟等をことごとく劍にかけて殺し又イスラエルの牧伯等數人を殺せり
Sasa Yehoramu alipokuwa ameinuka katika ufalme wa baba yake na kujiimarisha mwenyewe kama mfalme, akawaua ndugu zake wote kwa upanga, na pia viongizi wengine mbali mbali wa Israeli.
5 ヨラムは三十二歳の時位に即ヱルサレムにて八年の間世を治めたり
Yehoramu alikuwa na umri wa mika thelathini na mbili alipoanza kutawala, na akatawala kwa miaka minane katika Yerusalemu.
6 彼はアハブの家のなせるごとくイスラエルの王等の道にあゆめりアハブの女を妻となしたればなり斯かれヱホバの目に惡と觀たまふ事をなせしかども
Akatembea katika njia za wafalme wa Israeli, kama nyumba ya Ahabu ilivyokuwa ikifanya, kwa maana alikuwa na binti Ahabu kama mke wake, na akafanya yaliyo maovu katika macho ya Yahwe.
7 ヱホバ曩にダビデに契約をなし且彼とその子孫とに永遠に光明を與へんと言たまひし故によりてダビデの家を滅ぼすことを欲み給はざりき
Vile vile, Yahwe hakutaka kuiangamiza nyumba ya Daudi, kwa sababu ya agano ambalo alikuwa amefanya na Daudi; alikuwa ameahidi kwamba siku zote angetoa uzima kwa ajili yake na kwa ajili ya vizazi vyake.
8 ヨラムの世にエドム人叛きてユダの手に服せず自ら王を立たれば
Katika siku za Yehoramu, Edomu wakaasi wasiwe chini ya Yuda, na wakajisimamishia mfalme juu yao.
9 ヨラム其牧伯等および一切の戰車をしたがへて渉りゆき夜の中に起いでて自己を圍めるエドム人を撃ちその戰車の長等を撃り
Kisha Yeroboamu akavuka ng'ambo pamoja na maakida na magari yake yote. Ilikuwa usiku aliposimama na kupigana dhidi ya Waedomu ambao walikuwa wamemzunguka na maakida wa magari yake.
10 エドム人は斯叛きてユダの手に服せずなりしが今日まで然り此時にあたりてリブナもまた叛きてユダの手に服せずなりぬ是はヨラムその先祖の神ヱホバを棄たるに因てなり
Kwa hiyo Edomu iliasi kutoka kuwa chini ya Yuda mpaka leo. Libna pia aliasi wakati ule ule wasiwe chini yake. Kwa sababu Yehoramu alikuwa amemsahau Yahwe, Mungu wa babu zake.
11 彼またユダの山々に崇邱を作りてヱルサレムの民に姦淫をおこなはせユダを惑はせり
Zaidi ya hayo, Yehoramu pia alikuwa amezijenga sehemu zake za juu katika milma ya Yuda na akawafanya wakaaji wa Yuda kuishi kama makahaba, na akawaongoza Yuda katika upotevu.
12 時に預言者エリヤの書ヨラムの許に達せり其言に云く汝の先祖ダビデの神ヱホバかく言たまふ汝はその父ヨシヤパテの道にあゆまずまたユダの王アサの道にあゆまずして
Barua kutoka kwa nabii Eliya ikaja kwa Yerohamu. Ilisema, “Hivi ndivyo Yahwe, Mungu wa Daudi, babu yako, anasema: Kwa sababu hujatembea katika njia za Yehoshafafati, baba yako, wala katika njia za Asa, mfalme wa Yuda,
13 イスラエルの王等の道にあゆみユダの人とヱルサレムの民をしてアハブの家の姦淫をなせるごとくに姦淫を行はしめまた汝の父の家の者にて汝に愈れるところの汝の兄弟等を殺せり
bali umetembea katika njia za wafalme wa Israeli, na umewafanya Yuda na wakaaji wa Yerusalemu kuenenda kama kahaba, kama nyumba ya Ahabu walivyofanya—na kwa sababu pia umewaua ndugu zako katika familia ya baba yako kwa upanga, watu waliokuwa bora kuliko wewe mwenyewe—
14 故にヱホバ大なる災禍をもて汝の民汝の子女汝の妻等および汝の一切の所有を撃たまふべし
ona, Yahwe atawapiga watu wako na pigo kubwa, watoto wako, wake zako, na mali zako zote.
15 汝はまた臓腑の疾を得て大病になりその疾日々に重りて臓腑つひに墜んと
Wewe mwenyewe utakuwa na ugonjwa mwingi kwa sababu ya ugonjwa kataika katika utumbo wako, mpaka utumbo wako uanguke nje kwa sababu ya ugonjwa, siku baada ya siku.
16 即ちヱホバ、ヨラムを攻させんとてエテオピアに近きところのペリシテ人とアラビヤ人の心を振起したまひければ
Yahwe akaichochea roho ya Wafilisiti dhidi ya Yuda na ya Waarabu waliokuwa karibu na Waethipia.
17 彼らユダに攻のぼりて之を侵し王の家に在ところの貨財を盡く奪ひ取りまたヨウムの子等と妻等をも携へ去れり是をもてその末子ヱホアハズの外には一人も遺れる者なかりき
Wakaivamia Yuda, wakavamia katika nyumba ya mfalme. Pia wakawachukua wanaye na wake zake. Hakuna mwana aliyebakizwa kwa ajili yake ispokuwa, Yehoshafati, mwanaye mdogo.
18 此もろもろの事の後ヱホバ彼を撃て臓腑に愈ざる疾を生ぜしめたまひければ
Baada ya haya yote, Yahwe akampiga katika utumbo wake kwa ugonjwa usiopona.
19 月日を送り二年を經るにおよびてその臓腑疾のために墜ち重き病苦によりて死ねり民かれの先祖のために焚物をなせし如く彼のためには焚物をなさざりき
Ikawa wakati ulipofika, katika mwisho wa miaka miwili, kwamba utumbo wake ukaaanguka nje kwa sababu ya ugonjwa wake, na kwamba akafa kwa ugonjwa mkali. Watu wake hawakutengeneza moto kwa ajili ya heshima yake kama walivyokuwa wamefanyia babu zake.
20 彼は三十二歳の時位に即き八年の間ヱルサレムにて世を治めて終に薨去れり之を惜む者なかりき人衆これをダビデの邑に葬れり但し王等の墓にはあらず
Alikuwa ameanza kutawala alipokuwa na umrai wa miaka thelatahini na mbaili; akatawala katika Israeli kwa miaka minane, na alikufa bila kuaombolezwa. Wakamzika katika mji wa Daudi, lakini siyo katika makaburi ya kifalme.

< 歴代誌Ⅱ 21 >